Why do men lie especially in relationships?

Pumpkin girl

Senior Member
Joined
Jun 24, 2026
Posts
148
Reaction score
385
Hello guys naamini mko poa, poleni na majukumu ya hapa na pale,… yakiwa yamebaki masaa kadhaa tuianze weekend nilihitaji tuzungumze hii issue japo kwa uchache, sijajua kama mshawahi kuidiscuss ila sio mbaya pia hata tukiirudia….,

Swali langu ni kwa wanaume hivi ni kwanini huwa mnadanganya kwenye mahusiano yenu? Ni kwamba mkisema ukweli mtapungukiwa kitu gani kwenu? Kuna visa kadhaa nishawahi kuvisoma, kusimuliwa na vingine nimevishuhudia kwa macho yangu kutoka kwangu, kwa marafiki na watu wangu wa karibu pia ikiwemo ndugu,, Kati ya visa vyoote hivyo Naomba nielezee vichache ambavyo vimenifanya mpka nianzishe hii mada….;

Nilikua na rafiki angu ambae aligeuka kuwa ndugu kabisa japo sio ndugu wa damu yeye alikua na mahusiano na mpenzi wake kwa mda mrefu zaidi ya mwaka na nusu na hayo mahusiano yalikua ni mahusiano hot kweli kweli na yeye alihisi amepata maana mwanaume alikua akimfanyia kila kitu anacho kihitaji plus ahadi za kuoana Kede kede pindi atakapo hitimu masomo yake, zawadi zilikua za kutosha simu ni 24/7 kwahiyo huyu rafiki angu hakuhisi dalili yoyote mbaya kwa huyo bby dady wake; shida ilianza Baada ya yeye kumaliza masomo na kumgusia huyo mwanaume suala la ndoa ili wajivinjari kwa uhuru mwanaume akaanza kujizungusha na kutoa sababu zisizo eleweka basi binti ndo kuanza kufuatilia taratibu akagundua mwanaume alikua mume wa mtu tena ndoa ya kanisani na anao watoto wa tatu, sasa nikaanza kujiuliza kwanini huyo mwanaume hakumuweka wazi mpenzi wake akaamua kumficha? Na pia vipi kwa mke wake alikua ana mdanganyaje mpka anaondoka kwenda kula raha na huyu rafiki angu? Kiukweli Nilikoswa majibu

Kisa cha pili nilikishuhudia kwa binamu yangu yeye alikua kaolewa tayali na ndoa yao ilikua nzuri isiyo na migogoro ( kwa nje ya ndani siyajui) walikua ni watu wenye furaha na mume wake alikua anafanya kazi ya kuendesha magari makubwa kwenda mikoa tofauti na hata nje ya Tz, bahati mbaya alipataga ajari akafariki siku ya msiba akatokea mwanamke mwingine akajitambulisha ni mke wa marehemu na cheti cha ndoa alikua nacho japo wao walifunga ndoa ya serikalini cha ajabu ni kwamba huyu binamu yangu hakujua kabisa kama mme wake alikua na ndoa nyingine na pia kwa siku walizokua wakikaa pamoja hakuweza kuona dalili yoyote ya usaliti

Visa ni vingi jamani na siwezi kuvielezea vyote ila naamini hata ninyi mshawahi kusimuliwa au kushuhudia kwa macho yenu na wengine mnayaishi haya maisha kila siku kwa wenza au wapenzi wenu;… sasa hebu wanaume mtueleze kwanini mnayafanya haya? Kwanini hamuwi wakweli kwa wenzenu na mnachagua kuwaumiza kihisia? Kama mapenzi yako yameisha kwa mtu na unaoa unapata furaha sehemu nyingine si unasema tu ukweli ili kila mtu aendelee na ratiba nyingine

Ya kwangu ni hayo kwa leo karibuni kwa maoni
 
Hivi wanawake hawadanganyi kwenye mahusiano.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom