Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 20,852
- 52,721
Kuna kosa ambalo vijana wengi huwa tunalifanya tunapoanza mahusiano.
Tunakutana na msichana leo, kesho tayari tunaanza kuishi kama mume na mke kiakili. Kila muda ni simu hasa nyakati za usiku,video calls, passwords za mitandao ya kijamii tunabadilishana,tunaanza na mipango ya majina ya watoto 😂, lakini ukichunguza misingi ya maisha yetu inakuwa bado haijasimama.
Huwa tunasahau ukweli mchungu unaosema mapenzi yanahitaji hisia, lakini maisha yanahitaji busara.
Funzo kwa vijana wenzangu, na hapa ndipo ambapo huwa tunaangukia pabaya.
Kwanza kama kijana unapaswa kuelewa
1. Usikimbilie kujenga matarajio makubwa kabla hamjaelewana kikamilifu na huyo msichana. Mara nyingi msichana anaweza kuonekana sahihi katika wiki chache za mwanzo, lakini tabia halisi hujitokeza baada ya muda mrefu kupita. Jifunze kuzungumza, kuelewa maadili ya huyo msichana, namna anavyoshughulikia hasira, fedha na changamoto za maisha.
Mvuto pekee hautengenezi mahusiano ya kudumu au ndoa yenye afya.
2. Linda faragha ya mahusiano yenu. Sio kila picha mnazotumiana au kupiga pamoja uiweke status WhatsApp, sio kila mazungumzo mnayozungumza uwashirikishe marafiki, na sio kila unapotokea ugomvi ugeuke mada ya mitandaoni, yaani kwa kifupi maisha ya ya mahusiano yasigeuke gumzo mitandaoni.
Mahusiano yenye tija hujengwa kwa uaminifu, sio kwa kutafuta attentions kutoka kwa watu wengine.
3. Zaidi ya yote, endelea kujenga maisha yako kwanza. Tafuta kazi, jifunze ujuzi, weka malengo, na jitahidi kupata utulivu wa kifedha. Mahusiano mazuri hayawezi kuchukua nafasi ya ndoto zako. Badala yake, yanapaswa kuwa sehemu inayokuongezea nguvu, sio kukurudisha nyuma.
4. Epuka mazoea yanayokufanya ujisahau wewe mwenyewe. Kwanza jijenge mwenyewe na jithamini mwenyewe. Mahusiano yasikufanye uache kufanya kazi zako, uache kujifunza stadi za maisha, furaha yako isimtegemee mtu.
Kumbuka mapenzi ya kweli hayakufungi lakini hukupa nafasi ya kukua.
Kumbuka, mbele kuna nafasi ya kukutana na mtu ambaye mtajenga uhusiano wenye mawasiliano ya wazi tangu mwanzo, kuheshimiana, kuwa na mipaka ya kila mmoja, na vilevile kusaidiana kujenga kesho iliyo bora.
Kijana, usiweke nguvu zako zote kwenye mwanzo wa mahusiano hadi ukasahau mwisho wa safari. Jenga kwanza tabia, malengo na misingi ya maisha.
Ukikutana na mtu sahihi, mtajenga pamoja sio mmoja kumbeba mwenzake akiwa bado hajajijenga.
Mapenzi yanaweza kuwa sehemu ya maisha yako, lakini yasigeuke kuwa maisha yako yote.