Nifa, dada yangu katika Uislam, NAKUPENDA sana ❤️🤍

Nifa, dada yangu katika Uislam, NAKUPENDA sana ❤️🤍

Hakuna msimamo mkali ktk uislam.
Kuna unafiki na uislam. Sasa inategenea wewe umebase wapi.
Wasiokuwa waislam wanawapenda waislam wa aina flani
Hijab ni utumwa tu wa kidini sheikh. Waislamu waweke kipaumbele kwenye haki tu
 
Hijab ni utumwa tu wa kidini sheikh. Waislamu waweke kipaumbele kwenye haki tu
Wazungu wanatembea na chupi tu huko kwao, lkn wewe unagharimika kununua nguo nyingi na chupi unaficha ndani. Kwanini usivae chupi ukatembea kariakoo kama wazungu. Gharama yote ya nini unatumia?
 
Mimi nitakumbushwa na wengine

Umeandika nakala ndefu kwa mtu ambaye kumbe hamujuwani kabisa!!!... haupo naye karibu wala hujui yake.. Unatumia vipicha.. Huyo si ana rap pia, amekuwa ana mavazi yake tanguuu hajawa alipofikia Now.. Andika yako basi uso we ufunze wengine.. Sio Nifa tu...
 
Mashallah. Lkn namuona live tiktok akiwa hajavaa hijab. Au Ai ile?
 
Unaweza kuvaa hijabu Matendo 0
Unaweza usivae hijabu Matendo 0
Unaweza kuvaa hijabu Matendo 100%🤝
Unaweza usivae hijabu matendo 100%

Mavazi cyo kipimo Cha Matendo ya mtu kwa mwenyezi Mungu

Mimi nimekaa Ulongoni B Kuna wanawake wa kisambaa na makabila mengine wanafunika mpaka macho lakini niliwala Tena wengine wakiwa KWENYE mfungo enzi hizo
Miaka ya nyuma .

Tusijiaminishe kana kwamba ukificha macho na mikono ndo mtakatitufu. na Matendo Yako ni mazuri si kweli

Unaweza ukavaa hijabu ukawa kafiri wa kutupwa na mwingine anaweza akavaa sket akawa na unafuu mkubwa kushinda mvaa hijabu huu ni utafti wangu nilioufanya kwa asilimia mia Moja.

Kuhusu nifa nadhani, ungemfuata Dm au ungemtumia mtu wake wa kalibu ,,inawezekana ana sababu zake labda ameambiwa na madaktri asivae kwa sababu za kiafya,,

Usimhukumu mtu au kumu attack Mt public kabla ya kupata mawazo yake.inawezekana ana hoja za msingi kuzidi ulichoandika hapa.
 
Isaya 46:9 – "Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi."
 
Unaweza kuvaa hijabu Matendo 0
Unaweza usivae hijabu Matendo 0
Unaweza kuvaa hijabu Matendo 100%🤝
Unaweza usivae hijabu matendo 100%

Mavazi cyo kipimo Cha Matendo ya mtu kwa mwenyezi Mungu

Mimi nimekaa Ulongoni B Kuna wanawake wa kisambaa na makabila mengine wanafunika mpaka macho lakini niliwala Tena wengine wakiwa KWENYE mfungo enzi hizo
Miaka ya nyuma .

Tusijiaminishe kana kwamba ukificha macho na mikono ndo mtakatitufu. na Matendo Yako ni mazuri si kweli

Unaweza ukavaa hijabu ukawa kafiri wa kutupwa na mwingine anaweza akavaa sket akawa na unafuu mkubwa kushinda mvaa hijabu huu ni utafti wangu nilioufanya kwa asilimia mia Moja.

Kuhusu nifa nadhani, ungemfuata Dm au ungemtumia mtu wake wa kalibu ,,inawezekana ana sababu zake labda ameambiwa na madaktri asivae kwa sababu za kiafya,,

Usimhukumu mtu au kumu attack Mt public kabla ya kupata mawazo yake.inawezekana ana hoja za msingi kuzidi ulichoandika hapa.
Unaweza kusoma kazi - 0
Unaweza usisome kazi - 0
Kama daktari kamwambia asivae Hijab, kwanini asimwambie abaki na nguo ya ndani tu?
 
Unaweza kuvaa hijabu Matendo 0
Unaweza usivae hijabu Matendo 0
Unaweza kuvaa hijabu Matendo 100%🤝
Unaweza usivae hijabu matendo 100%

Mavazi cyo kipimo Cha Matendo ya mtu kwa mwenyezi Mungu

Mimi nimekaa Ulongoni B Kuna wanawake wa kisambaa na makabila mengine wanafunika mpaka macho lakini niliwala Tena wengine wakiwa KWENYE mfungo enzi hizo
Miaka ya nyuma .

Tusijiaminishe kana kwamba ukificha macho na mikono ndo mtakatitufu. na Matendo Yako ni mazuri si kweli

Unaweza ukavaa hijabu ukawa kafiri wa kutupwa na mwingine anaweza akavaa sket akawa na unafuu mkubwa kushinda mvaa hijabu huu ni utafti wangu nilioufanya kwa asilimia mia Moja.

Kuhusu nifa nadhani, ungemfuata Dm au ungemtumia mtu wake wa kalibu ,,inawezekana ana sababu zake labda ameambiwa na madaktri asivae kwa sababu za kiafya,,

Usimhukumu mtu au kumu attack Mt public kabla ya kupata mawazo yake.inawezekana ana hoja za msingi kuzidi ulichoandika hapa.
Kwani hii attack? Kuna tusi hapa? Anapambana na Mange na maria Sarungi ashindwe kuvumilia hizi nasaha?
 
Kwani hii attack? Kuna tusi hapa? Anapambana na Mange na maria Sarungi ashindwe kuvumilia hizi nasaha?

Kama ni hvyo unamanisha wadada au wanawake ambao hawavai hijabu Matendo Yao ni ya ovyo ? Soma Uzi wake wote alafu unijibu?
 
Nimekuchagua wewe kukutumia ujumbe huu kwa sababu nakupenda sana, nakuheshimu na ninakutakia kheri duniani na Akhera.
Sina nia ya kukuhukumu, kukukosoa au kujiona bora kuliko wewe. Nimekuandikia kwa upendo wa dhati, kwa sababu ningependa kukuona ukiwa karibu zaidi na Allah na ukiwa sababu ya mabinti wengine kumkaribia Allah pia.

Nifa, dada yangu, kuna jambo ambalo nimeona ni vyema nikukumbushe kwa upendo kuhusu hijab yako.
Nakumbuka kwamba wakati ulipokuwa unapitia matatizo, ulikuwa ukivaa hijab. Sasa ninapoona umeiacha, nimeguswa na jambo hili na nikaona nikushirikishe nasaha hii kama ndugu yako katika Uislamu.

Dada yangu, usimkumbuke Allah wakati wa shida pekee, bali endelea kumtii wakati wa furaha, mafanikio na umaarufu pia. Allah ndiye Mola wetu wakati wa shida na wakati wa faraja. Yeye ndiye tunayemuomba tunapokuwa na matatizo, na ndiye tunayepaswa kumshukuru tunapopata neema.

Hijab si vazi la wakati wa matatizo pekee, bali ni sehemu ya utiifu wa mwanamke Muislamu kwa Allah. Allah anasema katika Qur’ani:

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ

“Na waambie wanawake Waumini wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika, na waangushe vifuniko vyao juu ya vifua vyao.”

(Surat An-Nūr 24:31)

Nifa, ninapokutazama kama msanii maarufu mwenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii, ninaona kwamba una nafasi kubwa ya kuleta athari nzuri katika jamii. Mabinti wengi wanakuangalia, wanakufuatilia na baadhi yao wanaweza kukuona kama mfano wa kuigwa. Hii ni nafasi ambayo unaweza kuitumia kueneza kheri na kuhamasisha wengine kumtii Allah.

Fikiria jinsi ambavyo kurudi kwako kuvaa hijab kwa imani na msimamo kunaweza kuwagusa mabinti wengi. Unaweza kuwaonyesha kwamba mwanamke anaweza kuwa msanii, kuwa na kipaji, kufanikiwa na kuwa maarufu huku akiendelea kushikamana na dini yake. Unaweza kuwa kioo chema kwa mabinti wanaotamani kufanikiwa bila kuacha maadili yao ya Kiislamu.

Huenda watu wengi wakakuheshimu zaidi kwa msimamo wako wa kidini, ingawa heshima ya kweli haitegemei mavazi pekee. Jambo muhimu zaidi ni kwamba utakuwa umechukua hatua ya kumtii Allah na kutumia nafasi yako ya umaarufu kwa jambo lenye manufaa.

Dada yangu Nifa, usiogope kwamba kuvaa hijab kutakupunguzia thamani au uwezo wako kama msanii. Thamani ya mwanadamu haipimwi kwa mavazi, umaarufu au idadi ya wafuasi alionao. Cha msingi ni kuwa na imani, tabia njema na kujitahidi kutekeleza wajibu wetu kwa Allah.

Pia, usisubiri uwe mkamilifu ndipo uvae hijab. Sisi sote tuna mapungufu na tunahitaji kujirekebisha kila siku. Unaweza kuanza leo kumtii Allah huku ukiendelea kujiboresha katika mambo mengine ya maisha yako. Usiruhusu makosa ya jana yakuzuie kufanya jambo jema leo.

Nifa, tukumbuke kwamba dunia ni ya muda. Uzuri, mali, umaarufu na vyeo vyote vina mwisho. Kuna kifo, kuna Siku ya Kiyama, kuna Pepo na kuna Moto. Haya si mambo ya kuyachukulia kwa mzaha, kwa sababu kila mmoja wetu atarudi kwa Muumba wake.

Allah anasema:

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ

“Kila nafsi itaonja mauti, na hakika mtalipwa ujira wenu kikamilifu Siku ya Kiyama.”

(Surat Āl ‘Imrān 3:185)

Dada yangu, siku moja kila mmoja wetu atasimama mbele ya Allah na kuwajibika kwa matendo yake. Wafuasi wetu, umaarufu wetu na sifa za watu haviwezi kuchukua nafasi ya matendo yetu mbele ya Allah. Kwa hiyo, tusiipe dunia nafasi kubwa kuliko Akhera, na tusiruhusu kutafuta kukubalika na watu kutufanye tusahau wajibu wetu kwa Muumba wetu.

Ninachokuomba kwa upendo ni kwamba ufikirie upya suala la hijab na urudi kuivaa kwa ajili ya Allah, si kwa ajili yangu, si kwa ajili ya watu, wala si kwa kutafuta sifa. Ifanye iwe sehemu ya safari yako ya kumkaribia Allah na ya kujiandaa kwa maisha ya Akhera.

Nifa, ujumbe huu unatoka moyoni mwangu. Nimekuchagua wewe kukukumbusha kwa sababu nakupenda sana na ninaamini kwamba unaweza kuwa sababu ya mabinti wengine kukumbuka wajibu wao kwa Allah. Sitaki uuchukulie kama lawama, bali kama nasaha kutoka kwa mtu anayekutakia mema.

Ikiwa kuna jambo linalokufanya ushindwe kuvaa hijab, usikate tamaa na usione kwamba umeshindwa kabisa. Tafuta msaada, jiimarishe kiimani na chukua hatua kwa moyo wa dhati. Mlango wa kurejea kwa Allah uko wazi, na rehema Zake ni kubwa.

Nifa, dunia itapita, umaarufu utapita, lakini maisha ya Akhera ndiyo ya kudumu. Tujitahidi kuishi kwa namna ambayo tutafurahi kukutana na Allah. Na kwa kuwa una ushawishi kwa watu wengi, tumia nafasi hiyo kueneza kheri, kuwa mfano wa tabia njema na kuwahamasisha wengine kumkumbuka Allah.

Nakuombea Allah akupe nguvu ya kusimama katika dini Yake, akuongoze katika yaliyo mema, akulinde na Moto, akujaalie kuingia Peponi kwa rehema Zake, na akufanye kioo chema kwa mabinti wa Kiislamu.

Allah akufungulie milango ya kheri duniani na Akhera, akuthibitishe katika imani na akufanye miongoni mwa waja Wake anaowapenda na kuwaridhia.

Nakupenda sana, Nifa, na ninakutakia yaliyo bora katika maisha haya na maisha yajayo. Allah akuongoze na akujalie mwisho mwema. Aamiin ya Rabbal-‘Aalamiin. 🤲🏽❤️
Niffer kama Wema ni watoto wa wazazi wenye dini mbili tofauti
Una uhakika gani ni ipi anayo fuata?
 
Niffer kama Wema ni watoto wa wazazi wenye dini mbili tofauti
Una uhakika gani ni ipi anayo fuata?
mwanamitandao maarufu Jenifer Bilikwija Jovin (Niffer) alichapisha video yake ya kwanza mitandaoni akiwa msikitini mnamo Desemba 4, 2025, mara baada ya kuachiwa huru gerezani.
 
Back
Top Bottom