Ni wangapi wanakumbuka jina la mwalimu wa darasa la kwanza?

Ni wangapi wanakumbuka jina la mwalimu wa darasa la kwanza?

Mwl. Namika na mapunda loop siji wasahau walikuwa wakali darasa zima tukiwaona tulikuwa tunahisi chui wameingia darasani
Huyo namika alinitandikaga viboko sijui Saba kisa nilishindwa kufungua adidas [emoji53][emoji53]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namkumbuka Mwl. Mgimwa alikuwa aunt yangu term ya kwanza tukapewa barua (report) kuwapelekea wazazi. Nikajikaza sijafungua ile barua kukaribia na home kuna roho ikanambia fungua nyingine inaniambia acha tabia mbaya....duh ile roho ya fungua ikashinda.... ile kufungua nakutana na ile maini ya jumla nakutana na "MTUNDU SANA WAZAZI MMTAZAME VIZURI".

Nilihuzunika sana kwa hiyo comment ya ticha Mgimwa.

Lkn kwenye ufaulu nikawa wa 2...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom