Ni wakati wa Rais Samia kuziangalia bidhaa zilizopanda bei kutokana na matamko ya kisiasa na kuumiza wananchi wa hali ya nchi

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,474
2,000
Nakumbuka mwaka 2016 bei ya sukari ilikuwa shilingi 1,800 kwa kilo. Bei ya mfuko wa cement ilikuwa 11,000 hadi 12,000. Bei ya mafuta ya kula nayo ilikuwa chini sana lakini baada ya kuwekwa zuio la kutoingiza hizo bidhaa bei ilipanda kwa zaidi ya 60% na imekataa kushuka licha ya kutangaziwa kuwa bei ingeshuka.

Natambua maamuzi ya kuzuia uingizaji wa hizo bidhaa ni kwa sababu ya kulinda viwanda vya ndani na pia kiuchumi importation inapunguza mzunguko wa hela ndani ya nchi. Lakini swala la kuzuia importation kwa sababu ya kulinda bidhaa au viwanda vya ndani wakati viwanda vya ndani havina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya ndani ni kuwaumiza walaji wa mwisho (final consumers). Nadhani maamuzi sahihi ni yale ya kupiga marufuku uagizwaji wa bidhaa ambazo hapa nchini zinatosheleza mahitaji ya walaji. Tokea bei ya sukari, cement na mafuta ivurugwe imekataa kushuka kabisa licha ya kuambiwa sijui kuna shehena zinapakuliwa bandarini.

Nakushauri na ninakuomba Rais wetu uliangalie kwa kina hili swala. Angalia kama viwanda vyetu vya ndani vina uwezo wa kuzalisha na kutosheleza mahitaji ya walaji, na kama utabaini havitoshelezi basi nakuomba urejeshe utaratibu uliokuwepo zamani kabla ya kuvurugwa ili uwaondolee mzigo wa gharama walaji wa mwisho. Kuna faida gani ya kulinda viwanda vya ndani wakati wananchi wa hali ya chini wanaumia? Kuna faida gani ya kulinda viwanda vya ndani wakati havina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya walaji? Viwanda vya ndani vilindwe lakini ule "upungufu" ujazilizwe kwa kuagiza nje. Yaani viwanda vya ndani vilindwe kwa kile kiasi kinachoweza kuzalisha. Kinachozalishwa nchini kinunuliwe chote kiishe na kinachopelea kiagizwe kutoka nje ili kuziba pengo, na sio viwanda vya ndani vilindwe kwa gharama za walaji wa mwisho. Not to protect domestic manufacturers at the expense of consumers. This is not fair at all.

Naomba nimalizie kwa kusema kwamba sipingani na maamuzi ya kulinda viwanda vya ndani, ninachoshauri ni kwamba upungufu uliosababisha bei kupanda ujazilizwe kwa kutumia utaratibu uliokuwepo zamani kabla ya bei kuvurugwa na kupanda jumla na kukataa kushuka hadi sasa licha ya ahadi ya kwamba bei ingeshuka.

Naomba kuwasilisha.
 
nygax

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,372
2,000
Jambo la msingi sana hilo mkuu. Maana huku kwetu Lita 20 ya mafuta ya kupikia inaenda mpaka 84,000/= (mafuta ambayo si alizeti)
 
PANAFRICA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
213
500
Naunga hoja mkono.
Mafuta ya petroli huku mikoani Lita ni shs 2350/kutoka shs1950 ya mwezi March
 
konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,474
2,000
Jambo la msingi sana hilo mkuu. Maana huku kwetu Lita 20 ya mafuta ya kupikia inaenda mpaka 84,000/= (mafuta ambayo si alizeti)
Mama aliangalie hili swala. Bei zilipanda ghafla kutokana na maamuzi ya kisiasa na wala hazikupanda kwa sababu ya principle za soko ya "demand and supply"
 
greenwoods

JF-Expert Member
Sep 21, 2020
667
1,000
Sio mnalialia utadhani mama hayo mafuta na sukari yapo kwenye mwili wake ndo ashushe bei kama mnavyotaka nyinyi. Je mmejaribu kuingia kwenye website za kenya au uganda mkaulizia bei ya hizo bidhaa kwa pesa zao then mkazi convert kwa tsh muone tofauti yake!!??.
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,948
2,000
Naunga hoja mkono.
Mafuta ya petroli huku mikoani Lita ni shs 2350/kutoka shs1950 ya mwezi March
Mkuu sehemu ambayo ki ukweli serikali hata ya awamu ya tano ilijitahidi sana ni kwenye upande wa mafuta ya petrol na diesel, kupanda hovyo hovyo, siku hizi bei elekezi hupangwa na ewura kila jtano ya kwanza ya kila mwezi!ndio maana siku hizi hutakuta utofauti mkubwa sana wa bei kati ya bei ya dar na huko kigoma.
 
konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,474
2,000
Sio mnalialia utadhani mama hayo mafuta na sukari yapo kwenye mwili wake ndo ashushe bei kama mnavyotaka nyinyi. Je mmejaribu kuingia kwenye website za kenya au uganda mkaulizia bei ya hizo bidhaa kwa pesa zao then mkazi convert kwa tsh muone tofauti yake!!??.
Nadhani hujasoma nilichoandika bali umekurupuka kucoment tu.
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,948
2,000
Mama aliangalie hili swala. Bei zilipanda ghafla kutokana na maamuzi ya kisiasa na wala hazikupanda kwa sababu ya principle za soko ya "demand and supply"
Kweli kwenye mafuta na sukari kilichotufikisha hapa ni mambo ya kisiasa tu!"maamuzi ya ki muhemuko" unajua kabisa viwanda vya ndani havitosherezi mahitaji unaanza kuleta masharti ya ajabu ajabu!!na vitisho, yaani tatizo la kiuchumi unataka kulimaliza kwa matamko mala ohoo, bei elekezi ni hii!!kweli?ma rc, dc nao wanaanza kucheza ngoma, hiyo kutafuta wafanya biashara wanaouza bei juu?!!wewe hujui nimeinunua kwa bei gani na wapi uje unipangie bei ya kuuza?siku zote bei ya kuuza inaongozwa na upatikanaji wa bidhaa husika sokoni.
 
Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
3,104
2,000
Mama aliangalie hili swala. Bei zilipanda ghafla kutokana na maamuzi ya kisiasa na wala hazikupanda kwa sababu ya principle za soko ya "demand and supply"
Mafuta ya kupikia yanaweza yakapanda zaidi, sababu ya poor planning.Mafuta yanayozalishwa ndani hayakidhi mahitaji wazalishaji waliomba kuagiza malighafi nje walikataliwa ila baadae wakakubaliwa baada ya uhaba mkubwa.

Mwezi wa 4 Kuna meli imeingia imeleta mafuta ghafi ya mawese(Crude Palm Oil) mpaka leo haijashusha mzigo ipo nje inasubiri na meli za petrol zinapewa kipaumbele kuliko mafuta ya kupikia wakati petrol tunakuwa na reserve hata ya wiki kadhaa nchini.
 
konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,474
2,000
Kweli kwenye mafuta na sukari kilichotufikisha hapa ni mambo ya kisiasa tu!"maamuzi ya ki muhemuko" unajua kabisa viwanda vya ndani havitosherezi mahitaji unaanza kuleta masharti ya ajabu ajabu!!na vitisho, yaani tatizo la kiuchumi unataka kulimaliza kwa matamko mala ohoo, bei elekezi ni hii!!kweli?ma rc, dc nao wanaanza kucheza ngoma, hiyo kutafuta wafanya biashara wanaouza bei juu?!!wewe hujui nimeinunua kwa bei gani na wapi uje unipangie bei ya kuuza?siku zote bei ya kuuza inaongozwa na upatikanaji wa bidhaa husika sokoni.
Kabisa mkuu. Kwa hiyo mama akiamua bei ya zamani inarudi. Kupanda kwa bei ya hizi bidhaa ni kwa kujitakia tu. Hakuna bei elekezi kwenye soko huria. Bei inapangwa na soko lenyewe.
 
greenwoods

JF-Expert Member
Sep 21, 2020
667
1,000
Basi labda tufanye kwamba haupo Tanzania.
Shida sio kuishi tz au kwa majirani ,suala lililopo sio kulinda viwanda vya ndani ila ukweli bei la soko la baadhi ya hizo bidha zimecheza ndo maana nikasema ukitaka kuona ukweli ingia kwenye web za kenya za kuuza baadhi ya hizo bidhaa utaona hazina tofauti sana na za kwetu mfano sukari inacheza kuanzia ksh 104 mp 116 kwa kg sawa na 2100 mpk 2800 tsh ukija kwenye mafuta ya kula nayo ni the same. Sasa leo ulitaka mama apange bei mnayotaka nyinyi ile za zamani maana yake afanye subsidy atoboke mfukoni kitu ambacho hawezi.
 
Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
3,104
2,000
Kweli kwenye mafuta na sukari kilichotufikisha hapa ni mambo ya kisiasa tu!"maamuzi ya ki muhemuko" unajua kabisa viwanda vya ndani havitosherezi mahitaji unaanza kuleta masharti ya ajabu ajabu!!na vitisho, yaani tatizo la kiuchumi unataka kulimaliza kwa matamko mala ohoo, bei elekezi ni hii!!kweli?ma rc, dc nao wanaanza kucheza ngoma, hiyo kutafuta wafanya biashara wanaouza bei juu?!!wewe hujui nimeinunua kwa bei gani na wapi uje unipangie bei ya kuuza?siku zote bei ya kuuza inaongozwa na upatikanaji wa bidhaa husika sokoni.
Wiki iliyopita kwenye nakala ya gazeti la Daily News bodi ya Sukari walitangaza tenda ili apatikane mtu wa kuagiza Industrial Sugar.
 
Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
3,104
2,000
Shida sio kuishi tz au kwa majirani ,swala lililopo sio kulinda viwanda vya ndani ila ukweli bei la soko la baadhi ya hizo bidha zimecheza ndo maana nikasema ukitaka kuona ukweli ingia kwenye web za kenya za kuuza baadhi ya hizo bidhaa utaona hazina tofauti sana na za kwetu mfano sukari inacheza kuanzia ksh 104 mp 116 kwa kg sawa na 2100 mpk 2800 tsh ukija kwenye mafuta ya kula nayo ni the same. Sasa leo ulitaka mama apange bei mnayotaka nyinyi ile za zamani maana yake afanye subsidy atoboke mfukoni kitu ambacho hawezi.
Kwa Mafuta ya kupikia Uganda Bei ipo chini, sababu kuna plantation za palm oil kwenye visiwa vya Kalangala ambapo huchukuliwa yakiwa ghafi na kwenda kutengenezwa kwenye Viwanda Jinja.

Mafuta ya kupikia kutoka Uganda mengi yanatumika Kanda ya Ziwa. Kama sikosei yanaitwa Mukwano ambacho ni kiwanda Cha urafiki Kati ya waganda na wachina.
Kipindi Cha nyuma Bukoba kulikuwa na Importer wa haya mafuta na sabuni kutoka Uganda.
 
konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,474
2,000
Shida sio kuishi tz au kwa majirani ,swala lililopo sio kulinda viwanda vya ndani ila ukweli bei la soko la baadhi ya hizo bidha zimecheza ndo maana nikasema ukitaka kuona ukweli ingia kwenye web za kenya za kuuza baadhi ya hizo bidhaa utaona hazina tofauti sana na za kwetu mfano sukari inacheza kuanzia ksh 104 mp 116 kwa kg sawa na 2100 mpk 2800 tsh ukija kwenye mafuta ya kula nayo ni the same. Sasa leo ulitaka mama apange bei mnayotaka nyinyi ile za zamani maana yake afanye subsidy atoboke mfukoni kitu ambacho hawezi.
Okay acha tu nikukumbushe japo najua unakumbuka ila tu umeamua kujitoa ufahamu. Iko hivi bei ya sukari kwa mfano ilikuwa 1,800 kwa kilo lakini Rais wetu Mungu amrehemu akatoa agizo la kupiga marufuku kuagizwa kwa sukari kutoka nje kwa madai ya kwamba sukari ile haikuwa salama kwa walaji na hapo hapo bei ya sukari ikapanda hadi 3,000 na zaidi kwa kilo. Tokea hapo sukari haijarudi kwenye ile bei iliyokuwa kabla ya tamko. Serikali ilianza kukimbizana na wafanyabiashara kwa madai ya kwamba wanaficha sukari ndio maana bei imepanda lakini sukari haikushuka bei hadi leo. So if you read between the lines you can see the reason behind for this price hike.
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,948
2,000
Sio mnalialia utadhani mama hayo mafuta na sukari yapo kwenye mwili wake ndo ashushe bei kama mnavyotaka nyinyi. Je mmejaribu kuingia kwenye website za kenya au uganda mkaulizia bei ya hizo bidhaa kwa pesa zao then mkazi convert kwa tsh muone tofauti yake!!??.
Kwa hiyo bei ya sukari/mafuta ya kenya ndio iwe hiyo hiyo Tz?bei za bidhaa zinatofautishwa kwa mambo mengi sana, bila kusahau uchumi wa nchi!mfano DRC, sukari kilo moja ni tsh.1900, mafuta ya petrol ni tsh.2000

Yaani kwa upande wa sukari na mafuta ya kula serikali ya awamu ya tano, ndio chanzo cha tatizo hilo!!uwezo wa tanzania kuzalisha sukari ni mdogo hivyo kuna kama metric tani laki 3, lazima kila mwaka ziagizwe nje, kwenye utoaji vibari ni shida mala wanataka bodi ya sukari ndio iagize, mala wanataka kulinda viwanda vya ndani!!hata hawaeleweki, tatizo linajitokeza ndio wanafanya maandalizi ya zima moto!!kwenye mafuta ya kula nako ni hivyo toka mwezi wa 11 mwaka jana ndio tatizo la mafuta lilianza hadi leo ni zaidi ya miezi 6, nini kimefanyika?!kila siku wanakwambia kuna meli zinashusha mafuta bandarini , mbona supply bado ni ndogo sokoni?

Anaibuka DC, eti anataka kutoa bei elekezi ya mafuta ya kula!huyo muuzaji hujui anayapata wapi na kwa bei gani unakuja kumwambia auze bei fulani?!! Mwaka jana wakati wa tatizo la cement , kuna sehemu niliipata kwa bei ya juu hadi inafika dukani kila mfuko uligharimu 17500.

Wanakuja dukani kamati ya ulinzi na usalama wanafoka ohhh mnawaonea wanyonge serikali hii haitakubali bei ya simenti ni 16500!!tu, nikawambia hilo haliwezekani nikawaonyesha documents na hapo nje wapambe kibao (wanyonge hao)na hapo karibia mji mzima hakuna cement

kesho njoo ofisini, nikaenda waliniambia ukweli tu kuwa hizi siasa ni hatari, wewe kauze bei yenye faida kwako.acheni soko liamue bei!!
 
Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
16,552
2,000
Sio mnalialia utadhani mama hayo mafuta na sukari yapo kwenye mwili wake ndo ashushe bei kama mnavyotaka nyinyi. Je mmejaribu kuingia kwenye website za kenya au uganda mkaulizia bei ya hizo bidhaa kwa pesa zao then mkazi convert kwa tsh muone tofauti yake!!??.
Rais wa nchi ni mmoja kati ya top policy makers. Foreign trade policies za hapa kwetu (ambazo zimebana zaidi importation ya bidhaa kama alizotaja mleta mada) zina impact kubwa kutokana na kuathiri supply na bei ya bidhaa za viwandani na mashambani.

Hivyo wewe kwakuwa huelewi kitu unakimbilia kuchangia mada kwa ushabiki wa kijiweni.

Inabidi uelewe kuwa matamko ya kisiasa ya athari katika nyanja mbalimbali ikiwemo za kiuchumi, kijamii n.k.

Pia unatakiwa ujue kuwa hizi policies huwa zinafanyiwa amendments kila baada ya muda ili kuangalia feasibility yake kuendana na wakati husika.
 
greenwoods

JF-Expert Member
Sep 21, 2020
667
1,000
Okay acha tu nikukumbushe japo najua unakumbuka ila tu umeamua kujitoa ufahamu. Iko hivi bei ya sukari kwa mfano ilikuwa 1,800 kwa kilo lakini Rais wetu Mungu amrehemu akatoa agizo la kupiga marufuku kuagizwa kwa sukari kutoka nje kwa madai ya kwamba sukari ile haikuwa salama kwa walaji na hapo hapo bei ya sukari ikapanda hadi 3,000 na zaidi kwa kilo. Tokea hapo sukari haijarudi kwenye ile bei iliyokuwa kabla ya tamko. Serikali ilianza kukimbizana na wafanyabiashara kwa madai ya kwamba wanaficha sukari ndio maana bei imepanda lakini sukari haikushuka bei. So if you read between the lines you can see the reason behind for this price hike.
Sawa mimi sijakataa ila tuu nikuambie kitu kimoja hawa wenye viwanda wikubwa si kenya si tz si ug eafrica kwa ujumla wana wasiliana kwa ukaribu sana kuhusu soko lipoje kwa muda gani, na wao wanaamua bei bidhaa yetu tuuze shilingi ngapi,kuna mwaka fulani nilikuwepo uganda kakira sugar walikuwa wanauza sukari bei juu kwa uganda ambapo kiwanda ndo kipo lakini south sudan ilikuwa inapatikana kwabei ndogo sana mpaka waganda wakawa wanenda kununua sudan waniuza tena nchini mwao kwa njia za panya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom