Kasi Kubwa ya Ujenzi Yapaisha Bei ya Saruji Nchini

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,051
49,735
Pamoja na kwamba mahitaji ya saruji Nchini ni kidogo kuliko uzalishaji Wetu ila bei ya saruji imekuwa ikipanda badala ya kushuka.

Kwa mujibu wa Viwanda vya saruji ni kwamba mahitaji ya ndani na Nje ya Nchi yameongezeka zaidi na kupelekwa bei kupanda.

Nini maoni yako?

====

1703666972729.png

Licha ya uzalishaji wa saruji kuwa zaidi ya mahitaji ya nchi, bei imeendelea kuwa juu, huku gharama za uzalishaji zikitajwa kuwa chanzo.

Kwa mujibu wa Serikali, uzalishaji wa saruji nchini umefikia tani milioni 11 kwa mwaka, huku mahitaji ya nchi yakiwa ni tani milioni 7.5 kwa mwaka.

Ongezeko hilo la uzalishaji limewafanya wanunuzi watarajie kupungua kwa bei ya bidhaa hiyo madukani, kama ilivyozoeleka katika bidhaa nyingine.

Hata hivyo, bei ya mfuko mmoja wa kilogramu 50 wa saruji imebaki kuwa Sh17,000 hadi Sh19,000 kwa muda mrefu wakati wazalishaji wakiendelea kusaka masoko ya nje ya nchi.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom