konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,666
- 8,582
Nakumbuka mwaka 2016 bei ya sukari ilikuwa shilingi 1,800 kwa kilo. Bei ya mfuko wa cement ilikuwa 11,000 hadi 12,000. Bei ya mafuta ya kula nayo ilikuwa chini sana lakini baada ya kuwekwa zuio la kutoingiza hizo bidhaa bei ilipanda kwa zaidi ya 60% na imekataa kushuka licha ya kutangaziwa kuwa bei ingeshuka.
Natambua maamuzi ya kuzuia uingizaji wa hizo bidhaa ni kwa sababu ya kulinda viwanda vya ndani na pia kiuchumi importation inapunguza mzunguko wa hela ndani ya nchi. Lakini swala la kuzuia importation kwa sababu ya kulinda bidhaa au viwanda vya ndani wakati viwanda vya ndani havina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya ndani ni kuwaumiza walaji wa mwisho (final consumers). Nadhani maamuzi sahihi ni yale ya kupiga marufuku uagizwaji wa bidhaa ambazo hapa nchini zinatosheleza mahitaji ya walaji. Tokea bei ya sukari, cement na mafuta ivurugwe imekataa kushuka kabisa licha ya kuambiwa sijui kuna shehena zinapakuliwa bandarini.
Nakushauri na ninakuomba Rais wetu uliangalie kwa kina hili swala. Angalia kama viwanda vyetu vya ndani vina uwezo wa kuzalisha na kutosheleza mahitaji ya walaji, na kama utabaini havitoshelezi basi nakuomba urejeshe utaratibu uliokuwepo zamani kabla ya kuvurugwa ili uwaondolee mzigo wa gharama walaji wa mwisho. Kuna faida gani ya kulinda viwanda vya ndani wakati wananchi wa hali ya chini wanaumia? Kuna faida gani ya kulinda viwanda vya ndani wakati havina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya walaji? Viwanda vya ndani vilindwe lakini ule "upungufu" ujazilizwe kwa kuagiza nje. Yaani viwanda vya ndani vilindwe kwa kile kiasi kinachoweza kuzalisha. Kinachozalishwa nchini kinunuliwe chote kiishe na kinachopelea kiagizwe kutoka nje ili kuziba pengo, na sio viwanda vya ndani vilindwe kwa gharama za walaji wa mwisho. Not to protect domestic manufacturers at the expense of consumers. This is not fair at all.
Naomba nimalizie kwa kusema kwamba sipingani na maamuzi ya kulinda viwanda vya ndani, ninachoshauri ni kwamba upungufu uliosababisha bei kupanda ujazilizwe kwa kutumia utaratibu uliokuwepo zamani kabla ya bei kuvurugwa na kupanda jumla na kukataa kushuka hadi sasa licha ya ahadi ya kwamba bei ingeshuka.
Naomba kuwasilisha.