Ni wakati wa Rais Samia kuziangalia bidhaa zilizopanda bei kutokana na matamko ya kisiasa na kuumiza wananchi wa hali ya nchi

Rais wa nchi ni mmoja kati ya top policy makers. Foreign trade policies za hapa kwetu (ambazo zimebana zaidi importation ya bidhaa kama alizotaja mleta mada) zina impact kubwa kutokana na kuathiri supply na bei ya bidhaa za viwandani na mashambani.

Hivi wewe kwakuwa huelewi kitu unakimbilia kuchangia mada ya kisomi kwa ushabiki wa kijiweni.

Inabidi uelewe kuwa matamko ya kisiasa ya athari katika nyanja mbalimbali ikiwemo za kiuchumi, kijamii n.k.

Pia unatakiwa ujue kuwa hizi policies huwa zinafanyiwa amendments kila baada ya muda ili kuangalia feasibility yake kuendana na wakati husika.
Nimemwambia jamaa hajasoma bandiko langu bali amekurupuka tu kucoment maana kwenye bandiko nimeelezea hatua kwa hatua hata layman anaweza kunielewa.
 
Wiki iliyopita kwenye nakala ya gazeti la Daily News bodi ya Sukari walitangaza tenda ili apatikane mtu wa kuagiza Industrial Sugar.
Sasa industrial sugar, ilikuwa inaingizwa na wenye viwanda wenyewe, ikaonekana kuna uhuni unafanyika, ok!kama wameona watangaze tenda sawa!!ila kwenye brown sugar huku ndio kuna shida, kwanza hizo tenda kuzipata ni shida, na kuna wazee wachache tu(wahindi)ndio wanazo hizo hata kama wanazidiwa lakini wamesha hodhi soko!!
Wanatengeneza upungufu ili bei ipande, na viwanda vya ndani wanapiga tu kelele kuwa hawana soko wakati uwezo wa kulisha soko hawana!!
 
Sawa mimi sijakataa ila tuu nikuambie kitu kimoja hawa wenye viwanda wikubwa si kenya si tz si ug eafrica kwa ujumla wana wasiliana kwa ukaribu sana kuhusu soko lipoje kwa muda gani, na wao wanaamua bei bidhaa yetu tuuze shilingi ngapi,kuna mwaka fulani nilikuwepo uganda kakira sugar walikuwa wanauza sukari bei juu kwa uganda ambapo kiwanda ndo kipo lakini south sudan ilikuwa inapatikana kwabei ndogo sana mpaka waganda wakawa wanenda kununua sudan waniuza tena nchini mwao kwa njia za panya.
Lakini unakubaliana nini kilikuwa chanzo cha bei kupanda? Kama bei itakataa kushuka kwa sababu soko la dunia limebadirika pia haijustfy kilichofanyika huko nyuma.
 
Sawa mimi sijakataa ila tuu nikuambie kitu kimoja hawa wenye viwanda wikubwa si kenya si tz si ug eafrica kwa ujumla wana wasiliana kwa ukaribu sana kuhusu soko lipoje kwa muda gani, na wao wanaamua bei bidhaa yetu tuuze shilingi ngapi,kuna mwaka fulani nilikuwepo uganda kakira sugar walikuwa wanauza sukari bei juu kwa uganda ambapo kiwanda ndo kipo lakini south sudan ilikuwa inapatikana kwabei ndogo sana mpaka waganda wakawa wanenda kununua sudan waniuza tena nchini mwao kwa njia za panya.
Sasa mkuu sukari ni tofauti kwani kwa tanzania kwa mwaka mahitaji ni kama tani 450, 000 lakini viwanda vya ndani uwezo wake ni kama tani 150, 000! tu!!hawawezi kuwa na nguvu ya kupanga bei ya soko, ndio maana miaka kama 7 nyuma viwanda vya ndani vilikuwa vinalia kukosa soko la sukari yao kutokana na bei kuwa kubwa kulinganisha na sukari ya nje, ni kweli kuna nyingine ilikuwa inaingizwa kwa magendo.ila kodi kubwa ni chanzo hasa cha bidhaa kutofautiana bei toka nchi moja na nyingine.
 
Sasa pengo la tani 300,000 linazibwaje? Sio ndio kusababisha kupanda kwa bei?
 
Yaani mambo mengine kweli, huwa yanaudhi sana...eti kulinda viwanda vya ndani... yaani kulinda uzembe na uroho wa wachache, kujitajirisha na kuumiza wananchi wasio na uwezo wa kuwa na viongozi, wenye uchungu wa kusemea.... yaani jamani tunaomba Mama yetu ikikupendeza, kwenye hali sema neno ili roho za watu wako zipone... kazi iendelee.
Jambo la msingi sana hilo mkuu. Maana huku kwetu Lita 20 ya mafuta ya kupikia inaenda mpaka 84,000/= (mafuta ambayo si alizeti)
 
Sio mnalialia utadhani mama hayo mafuta na sukari yapo kwenye mwili wake ndo ashushe bei kama mnavyotaka nyinyi. Je mmejaribu kuingia kwenye website za kenya au uganda mkaulizia bei ya hizo bidhaa kwa pesa zao then mkazi convert kwa tsh muone tofauti yake!!??.
Magufuli ndio chanzo cha yote ayo, anaingia yeye sukari bei kg tsh 1800/=, akaleta siasa zake sukari ikapanda na haikushuka Tena, ilibakia kutuma task force kuvamia magodown ya watu
 
Shida sio kuishi tz au kwa majirani ,swala lililopo sio kulinda viwanda vya ndani ila ukweli bei la soko la baadhi ya hizo bidha zimecheza ndo maana nikasema ukitaka kuona ukweli ingia kwenye web za kenya za kuuza baadhi ya hizo bidhaa utaona hazina tofauti sana na za kwetu mfano sukari inacheza kuanzia ksh 104 mp 116 kwa kg sawa na 2100 mpk 2800 tsh ukija kwenye mafuta ya kula nayo ni the same. Sasa leo ulitaka mama apange bei mnayotaka nyinyi ile za zamani maana yake afanye subsidy atoboke mfukoni kitu ambacho hawezi.
rubbish
 
Kwa Mafuta ya kupikia Uganda Bei ipo chini, sababu kuna plantation za palm oil kwenye visiwa vya Kalangala ambapo huchukuliwa yakiwa ghafi na kwenda kutengenezwa kwenye Viwanda Jinja.

Mafuta ya kupikia kutoka Uganda mengi yanatumika Kanda ya Ziwa. Kama sikosei yanaitwa Mukwano ambacho ni kiwanda Cha urafiki Kati ya waganda na wachina.
Kipindi Cha nyuma Bukoba kulikuwa na Importer wa haya mafuta na sabuni kutoka Uganda.
Na sisi tuemdeleze kwa kasi kilimo cha michikichi, sun flag, karanga na mazao mengine yanayoweza kuzalisha mafuta ya kula na kushawishi wawekezaji ujenzi wa viwanda vya kutosha kwenye uzalishaji wa mafuta haya.
 
Yaani mambo mengine kweli, huwa yanaudhi sana...eti kulinda viwanda vya ndani... yaani kulinda uzembe na uroho wa wachache, kujitajirisha na kuumiza wananchi wasio na uwezo wa kuwa na viongozi, wenye uchungu wa kusemea.... yaani jamani tunaomba Mama yetu ikikupendeza, kwenye hali sema neno ili roho za watu wako zipone... kazi iendelee.
Kulinda viwanda vya ndani ni jambo jema ila kuwe na mipaka. Sio kulinda kwa gharama za mlaji wa mwisho.
 
Na sisi tuemdeleze kwa kasi kilimo cha michikichi, sun flag, karanga na mazao mengine yanayoweza kuzalisha mafuta ya kula na kushawishi wawekezaji ujenzi wa viwanda vya kutosha kwenye uzalishaji wa mafuta haya.
Kabisa mkuu. Hii ni fursa pia kwa watanzania.
 
Sasa pengo la tani 300,000 linazibwaje? Sio ndio kusababisha kupanda kwa bei?
Ndio maana huo upungufu wa tani laki 3, kila mwaka lazima sukari hiyo iagizwe toka nje, na ni miaka yote hilo linafanyika, sasa tatizo la awamu ya tano, kulijaa ukiritimba kwenye utoaji vibali hivyo, wanavitoa sio kwa muda muafaka, ndio maana tatizo limekuwa likijirudia kila leo.
 
Back
Top Bottom