Huenda ipo siku nitakuja funguka kama mimi ni mtu wa aina gani, mikasa na visa nilivyopitia, nini maono yangu mara baada ya kupitia hayo, je nimewahi kuwaona majini kwa macho au kuongea nao, mimi ni mchawi au lah, imani yangu
nk
Hapo kutakuwa na funzo zito haswa kwa wale ambao hawajawahi hata kuuhisi uchawi na wale wenye kuujua watasisimkwa na mwili, maana kilichoshamiri leo ujue kiliimarishwa jana na kila kitu kina chanzo chake.
Kwa sasa tujikite katika mada husika.......pia namshukuru mkuu Mshana anavyoleta mada hizi na anafanya kazi kubwa.