Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,639
- 729,610
Ukiuliza hili swali wengi watakuambia usiku...lakini kiuhalisia ni kwamba wachawi huroga muda wowote katika mazingira yoyote na popote.Wale wa usiku ni wanga na washirikina tuu.
Mwanga kazi yake kubwa ni kufurahisha nafsi kwa kukuchezea na kukuchosha lakini hana madhara kivile.
Mshirikina ni mpiga dili na mfanyabiashara ni mtu wa kati huyu ndio mhusika mkuu wa kupeleka kwa wachawi zana za kufanyia madawa kama nywele damu, nguo, nyayo, kucha, viungo vya binadamu kulingana na mahitaji nk nk..
Mshirikina hana muda bali huangalia ni saa ngapi na sehemu gani sahihi ya kufanya yake ili apate alichokusudia (kumbuka mshirikina pia anaweza kuwa mwanga au mchawi )
Sasa basi mchawi yeye ndo yule anayejiita au kujifanya mganga wa kienyeji huyu anacheza na fani zote tatu uchawi ushirikina na ulozi.
Ni mchawi huyu huyu anayeweza kukuroga kwa kutumia ushirikina wake kisha akakutibu kwa kutumia uganga wake ni michezo tu ya kucheza na zana.
Mchawi na mshirikina huweza kufanya mambo yao popote na vile jinsi wapendavyo wao japo kupitia ushirikina hupata vitendea kazi na kupitia uchawi huweza kutoa tiba.
Mpiga zongo ni mchawi si mshirikina japo anatumia ushirikina kukupiga hilo zongo.
Ukikuta umewekewa madawa sehemu jua ni mchawi katumia ushirikina kufanya yake
Lakini usihadaike wala kubabaika siku hizi uchawi wa kweli unapotea kilichobaki ni stori na mazingaombwe.
Kitakachokuumiza ni imani yako na woga wako.Simama na Mungu wako utafunuliwa mengi.