Kwanza nikupe pole sana kwa haya unayopitia
Pili nikupongeze kwa ujasiri wa kuwa mkweli na muwazi mbele ya wote
Nianze kwa kusema kuwa Mungu anakupenda bado tena anakupenda sana
Kuna watu wanapitia vipindi vigumu sana kwa sasa kuliko wewe..wengine wako vitandani hospital na majumbani huku hata hela ya matibabu ikiwa ishu, kuna wengine hawana ajira na wana changamoto za ada kodi nk, kuna wengine wana changamoto za mahusiano na tatizo kubwa likiwa ni kipato
Mungu wetu ni mwema tena ni mwema sana kamwe hawezi kukupa majaribu kupita uwezo wako na kamwe hawezi kukufungia milango yote
Akifunga wa juu wa chini atakuachia wazi Akifunga wa kushoto wa kulia hataufunga....ukitulia na kumtegemea yeye atakuonyesha njia ya kutokea
KUHUSU NDUGU ZAKO:
Pamoja mimi
mshana jr kupewa majina yote mabaya yahusuyo nguvu za giza na pamoja na kuongelea kwa mapana yake ishu za wachawi na ushirikina lakini kamwe sitakushauri uende huko ...huko sio pa kwenda huko unaenda kutengeneza maagano na viapo vitakavyokutesa milele
Kuna kufungwa katika maisha kuna kuchezewa kwingi tu kuna kurogwa...lakini mpaka haya yatokee basi Mungu mwenyewe karuhusu kama iliyokuwa kwa Ayubu....hakuna jaribu lisilo na mwisho kwakuwa michezo yote ya mwanadamu ina kikomo chake na kiboko yake...Mungu mwenye enzi yote
Ushauri wangu;
Usiende popote usifanye chochote bali simama na Mungu wako Omba funga sali, hata kama utachekwa hata kama utadhihakiwa hata kama utatengwa na watu wa dunia hata kama utapoteza kila kitu...simama na imani yako na Mungu wako....Kutapambazuka tuu hata usiku uwe mrefu kiasi gani lakini Kutapambazuka
Usiende kwa waganga
Usiende kwa wasafisha nyota
Usiende kulewa pombe
Usitumie madawa ya kulevya
SIMAMA IMARA SIMAMA NA MUNGU WAKO faida yake utaiona