Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

na Happiness Katabazi

TUHUMA za ufisadi zilizosambazwa katika mtandao wa intaneti zikimlenga Spika wa Bunge, Samuel Sitta, zimesababisha Ofisi ya Bunge kuanzisha uchunguzi dhidi ya kiongozi huyo wa juu wa mamlaka hiyo ya dola.
Taarifa za kuanza kwa uchunguzi huo zilitangazwa na Katibu wa Bunge, Damian Foka wakati alipofanya mahojiano na gazeti hili, ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa Foka, madai ambayo atayafanyia uchunguzi ni yale yanayomhusisha Spika na tuhuma za kuwasilisha katika ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Bunge risiti za kughushi za matumizi yake.

“Ofisi za Bunge hazina taarifa za Spika kughushi risiti, nipeni muda niwasiliane na wakuu wa vitengo husika, ili tutafute ukweli kuhusu tuhuma hizo, na iwapo tutabaini lolote tutatoa majibu. Ile ni ofisi ya umma na mali zake zinatakiwa zitumike kwa matumizi yanayopaswa na si vinginevyo,” alisema Foka.

Pamoja na hilo, Foka alikiri madai yaliyoandikwa katika mtandao wa intaneti yanayoeleza kuwa, Sitta aliwasilisha risiti ya shilingi milioni mbili aliyonunulia dawa kutoka katika duka moja la dawa lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Aidha, alisema baada ya kuwasilisha risiti hiyo, alimwelekeza alete pia cheti cha daktari kilichokuwa kikionyesha kuwa alitakiwa kutumia dawa zenye gharama hizo kutokana na matatizo yake ya kiafya katika kipindi cha wiki moja.

“Ni kweli kuwa mwezi uliopita, Spika Sitta alilipwa shilingi milioni mbili katika kipindi cha wiki moja kwa ajili ya kununulia dawa katika duka la dawa la Oysterbay,” alisema Foka.

Alisema malipo hayo ni halali kwa sababu Ofisi ya Bunge ina taarifa kuhusu matatizo ya kiafya ya Spika Sitta ambayo hata hivyo hakutaka kuyaweka bayana kwa madai kuwa maradhi ya mtu ni siri yake na daktari wake.
Hata hivyo taarifa ambazo gazeti hili linazo zinaeleza kuwa, Spika amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya miguu ambayo kimsingi ndiyo aliyokuwa akiyatibu kupitia dawa alizonunua katika duka hilo la dawa.

Kuhusu madai kwamba Spika amekuwa akijihusisha katika matumizi mabaya yasiyotambulika kisheria na kikanuni kwa madaraka yake, ya magari mawili ya Bunge aliyopewa kwa shughuli zake binafsi, Foka alisema hana taarifa hizo na kuongeza kuwa uwezekano wa kuwepo kwa jambo hilo ni mdogo.

Wakati Foka akitoa taarifa hizo, maofisa kadhaa wa Bunge waliozungumza na Tanzania Daima wanaeleza kuwa, siku chache zilizopita ofisi ya Katibu wa Bunge ilipata kumhoji Sitta kuhusu kuwapo kwa madai hayo yanayomhusisha na matumizi yasiyofaa ya magari ya umma.

Foka pia alikanusha madai kwamba Ofisi ya Bunge imekuwa ikilipa gharama za umeme na maji kwa baadhi ya watu walio na uhusiano wa karibu na Spika, ambao kimsingi hawastahili kupata malipo hayo.

Pia alikanusha madai kuwa, kamati moja ya kudumu ya Bunge iligundua kuwepo mapungufu katika matumuzi ya fedha yaliyofanywa na Spika, lakini wajumbe wake walinyamazishwa na Sitta mwenyewe baada ya kuwatisha kuwa, iwapo wangeweka hadharani upungufu huo, wangekabiliwa na adhabu ya kunyimwa posho pamoja na kutopangiwa safari za nje.

Akizungumza madai kwamba Sitta amekuwa akilipwa kiasi kikubwa kwa ajili ya safari anazofanya ndani na nje ya nchi, na pia kujilimbikizia deni kubwa linalotajwa kufikia sh milioni 60, Foka alisema anachofahamu, Spika anasafiri nje na huwa analipiwa huduma ya maradhi na nusu ya asilimia 20 ya posho kama fedha za matumuzi na si zaidi ya hapo.

Naye Mkurugenzi wa Elimu ya Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge, Jose Mwakasyuka ambaye alikuwapo wakati Foka akihojiwa, alisema mali za Bunge zipo salama na kwamba tuhuma zinazoelekezwa sasa kwa Spika zina kila dalili ya kuwepo nia ya makusudi ya kumchafua.

“Hizi tuhuma ni za kupakana matope na kuchafuliana majina, kwani tuhuma zenyewe hazimtaji nani aliyezitoa. Nadhani kuna watu wanataka waandishi waache kuandika mambo ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya nchi na badala yake wajielekeze kwenye tuhuma dhidi ya viongozi,” alisema Mwakasyuka.

Hivi karibuni, Spika Sitta alizungumza na gazeti hili kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake na kueleza kuwa, hawezi kuzizungumzia kwa sababu zinatolewa na wahuni wenye lengo la kumchafulia jina lake mbele ya jamii.

Mbali ya hilo, Sitta alilielekeza Tanzania Daima kuwasiliana na maofisa wa Bunge ili kupata ukweli wote kuhusu madai hayo yaliyoandikwa katika mtandao mmoja wa intaneti.

Source: Tanzania Daima
 
jamani huu ni mkakati maalum wa kuchafuana hapa. Zengwe hili dhidi ya huyu mzee liliaza kupikwa tangu enzi ya hoja za Malima na Mengi. Kama mtakumbuka gazeti la Mwanahalisi liliandika habari za mkakati dhidi ya Sitta na huyu mzee akalipangua hili Jambo. Watu wale wale waliotaka kumtoa huyo mzee kwa sababu ya baadhi ya misimamo yake ndio hao hao wanalipika Jambo hili. Nina uhakika na Sitta mwenyewe anajua amejijengea maadui wengi ninavyo mfahamu mimi asingeweza kujiweka kwenye kikaango namana hiyo. NINAKUHAKIKISHIA ANAWAJUA.

Kuna watu hapa wanataka kuchanganya mambo ya nani kalala na nani na uongozi wa taifa. Kama huo ungekuwa ndio msingi wetu wa kuchagua viongozi kina Mzee Kawawa wasingekuwa wamepewa uongozi wa nchi hii kwa muda mrefu namna hiyo. Msekwa vipi yeye? wana JF tujadili mambo muhimu kwa taifa mambo ya ngono hapa ni RUBISH- Hao wenyewe wanao endeleza mambo ya ngono hapa tukifumua ya kwao watakuwa wapi. Wengine wamezaa mpaka na wafanyakazi wao wa ndani........... Ninaombeni tuache hili.

Kuna watu wengine hapa wana fananisha siasa za marekani na za Tanzania. wamarekani wanaojiuzulu ni wale walioulizwa na kukana hasa mbele ya kiapo kuwa hawakuhusika na mambo ya ngono! Wakati Bill Clinton anaingia madarakani kwa sababu alihusishwa na mambo mengi ya ngono mkewe aliulizwa na akasema kuwa ni kweli anamfahamu mume wake kuwa anapenda ngono lakani akawapa wamarekani changamoto kuwa " WANAMCHAGUA RAIS WA MAREKANI NA SIYO PAPA"
 
Naomba urudi usome tena magazeti ya leo na matumizi ya Sitta ya pesa zetu si kuchafuana kuna ukweli juu ya risit zake
 
JF Setting standars again,

I have no faith in the investigation

Kuhusu madai kwamba Spika amekuwa akijihusisha katika matumizi mabaya yasiyotambulika kisheria na kikanuni kwa madaraka yake, ya magari mawili ya Bunge aliyopewa kwa shughuli zake binafsi, Foka alisema hana taarifa hizo na kuongeza kuwa uwezekano wa kuwepo kwa jambo hilo ni mdogo.

Hawa watendaji wetu mbona wanakuwa kama punguani? Hivi mtu utasemaje huna taarifa lakini uwezekano wa accusations kuwa kweli ni mdogo?

Ukijua kuwa uwezekano wa taarifa kuwa kweli ni mdogo ina maana kwa njia moja au nyingine una taarifa zilizokusaidia kufikia hiyo conclusion.Na kama huna taarifa hutakiwi kusema kitu chochote kinachoweza kuwa intepreted kama una m favor au humpi favor speaker, unatakiwa kuwa neutral mpaka uchunguzi ukamilike.Ama sivyo ndiyo wanatupa mashaka wananchi kama uchunguzi utakuwa wa kina au utakuwa wa kumuosha tu speaker.Mi ningependekeza watu wa nje ya ofisi ya bunge, walio independent waje kuchunguza maana hawa watu hawawezi kum expose bosi wao.Tayari washaanza kutoa vi statement vilivyopinda.

Foka pia alikanusha madai kwamba Ofisi ya Bunge imekuwa ikilipa gharama za umeme na maji kwa baadhi ya watu walio na uhusiano wa karibu na Spika, ambao kimsingi hawastahili kupata malipo hayo.

Alikanushaje? Huwezi kukanusha kwa kutoa statements tu.Toa reasoning.Sema hatujawahi kupata ankara kutoka nyumba yoyote zaidi ya nyumba ya speaker na vitabu vyetu viko wazi kwa ukaguzi.Hapo tutaheshimu ukanushaji wako, lakini hii habari ya kukanusha tu hata Bill Clinton alikanusha "I did not have sexual relationship with that woman" baadaye akawa exposed.

Pia alikanusha madai kuwa, kamati moja ya kudumu ya Bunge iligundua kuwepo mapungufu katika matumuzi ya fedha yaliyofanywa na Spika, lakini wajumbe wake walinyamazishwa na Sitta mwenyewe baada ya kuwatisha kuwa, iwapo wangeweka hadharani upungufu huo, wangekabiliwa na adhabu ya kunyimwa posho pamoja na kutopangiwa safari za nje.

Sasa ofisi ya katibu wa bunge ndiyo imekuwa wasemaji wa wabunge? Hao wabunge wa hiyo kamati yenyewe wanasemaje? Mtu unakanusha tuhuma ambazo hazikuhusu wewe unajionyesha kabisa role yako ni kumkingia kifua Spika.

Naye Mkurugenzi wa Elimu ya Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge, Jose Mwakasyuka ambaye alikuwapo wakati Foka akihojiwa, alisema mali za Bunge zipo salama na kwamba tuhuma zinazoelekezwa sasa kwa Spika zina kila dalili ya kuwepo nia ya makusudi ya kumchafua.

Mnajichanganya zaidi, sasa kama mnajua hizi ni tuhuma za kumchafua kisiasa uchunguzi wa nini? Na uchunguzi unaweza kuwa wa haki kweli kama watu washaanza kuwa na bias hii ya kum favor speaker?

“Hizi tuhuma ni za kupakana matope na kuchafuliana majina, kwani tuhuma zenyewe hazimtaji nani aliyezitoa. Nadhani kuna watu wanataka waandishi waache kuandika mambo ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya nchi na badala yake wajielekeze kwenye tuhuma dhidi ya viongozi,” alisema Mwakasyuka.

Typical attention shifting spin, unataka kutoa attention kwenye issues na kuipeleka kwa mtu aliyezitoa.Dispute the issues.

Tota kulindana in play.Scratch my back I will scratch yours.Wanajua wako ofisi ya bunge na Spika atawakumbuika wakimprotect.

Hawako qualified kabisa kufanya uchunguzi.
 
Inaonesha bila shaka kuwa huko Tanzania hakuna ambaye si fisadi labda baba yangu tu.
Inabidi tusiangaliane machoni, tuangaliane mioyoni au la nchi inakwisha
 
Inaonesha bila shaka kuwa huko Tanzania hakuna ambaye si fisadi labda baba yangu tu.
Inabidi tusiangaliane machoni, tuangaliane mioyoni au la nchi inakwisha

Naturally, all human beings are selfish, hence uFisadi! Tena ukiwa na power ndio kabisaaa! Sasa, fight nature? MMh, well...you gotta put a hell of a fight!
 
Naturally, all human beings are selfish, hence uFisadi! Tena ukiwa na power ndio kabisaaa! Sasa, fight nature? MMh, well...you gotta put a hell of a fight!

So you DO endorse ufisadi right?

Kama watu wasingekuwa wana fight nature kuifanya i adapt tusingekuwa na ndege, television, umeme nk.

Argument ya "You can't fight nature is weak" indeed.
 
So you DO endorse ufisadi right?

Kama watu wasingekuwa wana fight nature kuifanya i adapt tusingekuwa na ndege, television, umeme nk.

Argument ya "You can't fight nature is weak" indeed.

And where did she say "You can't fight nature" ??

She was implying that the fight is a tough one and only those with strength will win.

I agree 100%
 
Note the first sentence is a question, followed by observations.In no part of the post did I say anybody said we can't fight nature.I just pointed out the self defeatist nature of the argument and the fact that most advancement are made by scaling the challenges.
 
cosign_3d_lg.gif
 
Tatizo la Tanzania inaelekea ni kubwa kuliko tunavyodhani. Kuna culture ya corruption kuanzia chini mpaka juu.

Ni watu wachache sana wanaofanya kazi serikalini na baadhi ya mashirika ya huduma ambao unaweza kusema hawana harufu ya corruption.

Labda na wengine wote tunaoshinda hapa JF tujiangalie mara mbili mbili, je tunatofauti na hao akina Sitta? Si ajabu na sisi kila siku tuna forge karatasi za malipo na documents zingine kwa nia ya kuiibia serikali au waajiri wetu.

Bila ya sisi pia kuchukia na kupinga uhalifu wa aina yoyote ile, haya mabadiliko tunayopigania, itatuchukua miaka mingi sana kuyafikia.

Miaka ya Nyerere, rushwa ilikuwa inachukiwa kuanzia chini mpaka juu. Mtu angeweza kumkana ndugu yake shauri kahusishwa na rushwa, lakini sasa wala rushwa ndio wajanja.
 
Tanzania hakuna "rule of law"

Kama walivyosema wasemaji hapo juu, it is human nature to be selfish, it is human nature to seek the easy way out, kwa hiyo kama kuna mihela ipo ofisini na hamna sheria za kumbana mfujaji wa mali za umma, au kama sheria zipo lakini kuna huku kulindana kama alikowekewa Sitta, watu wataendelea kukomba tu.

Tunahitaji misheria na mi watchdog na kuendeleza culture ya kuziheshimu hizo sheria.
 
Samweli unatuangusha Milioni mbili ni pesa nyingi sana kwa kigezo chochote kile iwe inatoa Serikali au unatoa mfukoni mwako,
Mbona tunakuamini sana? sasa mchezo gani umeanza?

Hata kama wanakusingizia kwa nini iwe wewe? Kwa nini wasimsingizie mwingine? Aaaaaa! hebu jisafishe bwana!!!
Hatutaki sisi kukusema vibaya ingawa tunajua ni juzi tu umetimiza miaka 40 ya ndoa yako na Dada Mage. Sasa tusiseme kuwa pesa ya kutimiza miaka 40 ya ndoa ndio hiyo unayosema ya dawa tusifike huko hebu jitetee mapema.
 
ndio mchezo wao hao,kila mtu akula pale alipo,mzee sita tupe mchanganuo wa hizo dawa au ulikuwa unatoa msaada nini
 
Hmm! Dawa za 2 mil, huh? I can come up with a few:
A) 2nd line ARVs for HIV
B) Chemotherapeutic agents for a cancer
None of the above are anything 2 b ashamed of so Bunge better tell us what they have been doing with OUR money!
I am sure he could afford 2 buy the drugs out of his own pocket if he wanted to! Kuna waTZ wanakufa kwa kushindwa kununua dawa kama Insulin wao wanaspend govt monies on fancy remedies.
Tut tut!!

C)XTB (extensive multi drug resistance TB) hii angekuwa amelazwa na isolated..sasa kama andunda tu inatutia shaka sana...
 
Samweli hatusemi ujibu kwenye JF, Jibu popote pale sisi tutakusikia vinginevyo subiri kuundiwa tume akina Mwakyembe watakuja na Tathmini za kukutaka upime uzito wa hoja na kisha kuamua cha kufanya,Hawatasema jiuzuru. Kumbuka mwenzio akinyolewa wewe tia maji, sasa hivi tunasafisha nchi kila jambo ambalo akili haikubali litawekwa hadharani lijadiliwe.
 
Back
Top Bottom