Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

MAMBO YA KATIBA YA UVCCMM

18. Ni mwiko kwa kiongozi:-
(1) Kutumia madaraka aliyopewa ama kwa ajili
ya manufaa yake binafsi au kwa
upendeleo, au kwa namna yoyote ambayo
ni kinyume cha lengo lililokusudiwa
madaraka hayo.
(2) Kupokea mapato ya kificho, kutoa au
kupokea rushwa, kushiriki katika mambo
yoyote ya magendo au mambo mengine
yaliyo kinyume cha lengo lililokusudiwa
madaraka hayo.
 
http://www.klhnews.com/index.php/headlines/agenda-21-yaundwa.php

Pamoja na mada hii kuwa tamu, hebu tujikumbushe hii habari ya Mwanakijiji hapa na kama JF nayo ni sehemu ya mkakati

husika.

http://www.klhnews.com/index.php/headlines/agenda-21-yaundwa.php

Agenda 21 yaundwa kumsafisha Lowassa

1 2 3 4 5 (4 votes) Written by Mwanakijiji
Saturday, 23 February 2008
Mtandao mpya wa wale waliojikuta wametupwa nje ya serikali na ambao wanajiandaa kujibu mapigo umeundwa. Habari za

kuaminika toka kwenye kuta na madirisha mbalimbali ya wahusika zinasema kuwa mtandao huo una lengo moja kubwa ambalo

ni kulipiza kisasi kwa yale yaliyotokea Dodoma wiki karibu mbili zilizopita. Haijulikani maana ya "Ajenda 21" nini.
Inadaiwa kuwa ni baadhi ya watu hawa hawa ndio waliohusika kwa namna moja katika jaribio lao lililoshindwa la

kuifuta Jambo Forum hewani. Vyanzo vya karibu na mitaa ya Magogoni Jijini Dar vinasema kuwa suala la Jambo Forums

lilileta mgawanyiko wa wazi na ililazimu "Ikulu" kuingilia kati na kuamuru mtandao huo uachiliwe kwani "unaisaidia

serikali na umekuwa ukiandika habari kwa usahihi zaidi kuliko vyombo vingi vya habari" kwa mujibu wa Ofisa mmoja

mfagizi katika jengo la Ikulu.

Mchunguzi wa KLH News aliyeko Arusha anaripoti kuwa mtandao huo ambao siyo tu una lengo la kujibu mapigo lakini pia

umedhamiria kurejesha na kuinua tena wasifu wa aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa. Mtandao huo ambao mkoani

Arusha unasadikiwa kuhusisha baadhi ya wafanya biashara inadaiwa umeandaa mapokezi makubwa kwa Bw. Lowassa ambaye

anatarajiwa kuelekea jimboni kwake siku ya Jumamosi kuzungumza na wananchi wake.

"Ni kweli watu kadhaa wanashirikiana kuandaa mapokezi hayo, lakini ni nani hasa siwezi kukuambia" alisema mjumbe

mmoja wa mtandao huo. Pamoja na ajenda yao hiyo mtandao huo una nguvu kubwa ya kiuchumi ambayo hailingani na mtandao

mwingine wowote na baadhi ya mashabiki wa JF na KLH wanaona kuwa wako njiani kuzidiwa nguvu mara milioni kadhaa.

Uchunguzi wa KLHN ambao umepenya kwenye kingo za nyumba na maofisi ya watu hao unaonesha kuwa mtandao huo unaundwa

na wanasiasa wa chama tawala ambao wamejikuta hawamo tena serikalini, wafanyabiashara maarufu, vyombo kadhaa vya

habari (ambavyo vingine vimeanza kuandika habari zinazotokana na "agenda" hiyo) na mashabiki wengine wakubwa wa

aliyekuwa Waziri Mkuu. Mmoja wapo wa watu watakaoshiriki katika kuandaa mapokezi hayo ya Lowassa ni mfanyabiashara

wa madini ya Tanzanite aliyewahi kutumikia kifungo kutokana na makosa ya ujambazi Bw. Justin Nyari. Bw. Nyari

baadaye aliweza kushinda rufaa yake kwenye Mahakama Kuu.

Wakati habari hii ya KLHN inaandikwa tayari Kikwete, Dk. Slaa, Mengi na Zitto walikwisha kuguswa na kuchafuliwa, sasa kaja

Mbowe na baadaye Sitta. Nakumbuka mtu mmoja alimwambia Mbowe, "nitakujibu kwa staili yangu" baada ya mtu huyo kuguswa na mapigo ya wabunge wa Chadema hasa siku ile ilipotolewa kwa mara ya kwanza orodha ya MAFISADI. Kwa wanaokumbuka orodha ile hata hapa JF ilitolewa ikiwa na majina manane (8) likiwamo jina la Kikwete lakini bila ya majina ya Lowassa, Karamagi na Rostam,katika kipindi ambacho BoT (EPA) na Richmond na TICS zilikua zimepamba moto.

SINA hakika na hii hapa ya web ya Chadema

http://www.chadema.net/habari/2007/orodha1/ukurasa2.php

Majina hayo ya kina EL, Karamagi na RA ambayo yaliongezwa baadaye, yaliwakera wahusika. Sina hakika kama hili lilikua BAHATI MBAYA katika maandalizi ya orodha kwani wananchi waliwajua hawa kuwa ndio vinara wa UFISADI.

Ndipo mtu mmoja akawaambia watu, "atajibu kiaana" na kwamba hana haraka na hilo, kwani ni SUALA LA MUDA TU.

Kabla sijahoji USAHIHI wa TAARIFA ya SITTA na kwamba pamoja na kuwa HOJA ya SITTA ni sehemu ya mapambano yetu ya kuhakikisha
nchi inakua SAFI, kuna maswali ya kujiuliza, maswali ambayo nilijiuliza alipoanza kushambuliwa Slaa, Zitto na hata Mengi.

-Nilitoa mfano wa polisi (SITTA,SLAA, ZITTO, KILANGO, MWAKYEMBE, MENGI,MBOWE) ambaye 'tunamtuhumu' kwamba hana maadili ambaye AMESHIKA SILAHA na mbele yetu tuna MAJAMBAZI (LOWASSA, ROSTAM, KARAMAGI, CHENGE) yenye silaha yanaua WATANZANIA WENZETU, sasa tutaanza kumshughulikia huyo POLISI kwanza!!? ama tutampa nafasi ayadhibiti majambazi?!!!

Hapa lazima tuzingatia kipindi tulichonacho, kwamba sasa ndicho ambacho wanaibuka watu wanaojifanya wana uchungu na nchi, watu ambao awali hawakua wenzetu kabisa, sasa wametoka nje eti ndio wanaona maovu, kuzuia wasishughulikiwe ama kuwatisha POLISI wetu wasipambane nao. KWanza tujue kwamba polisi (WAZALENDO) tulionao ni wachache mno na hawana SILAHA (uwezo) na vyombo vya usafiri (MEDIA) vilivyopo ni vichache (JF, MWANAHALISI, RAIAMWEMA, THISDAY, KLHN) na tunapoanza kugeukana na kugeuza mashambulizi upande wetu, tunampa adui nafasi ya kushinda VITA tuliyoisimamia kwa urahisi mkubwa na baadaye, majambazi hayo yatarudi na kutushughulikia wenyewe (kama walivyowakamata MAC na Mike), watafungia magazeti na mitandao yote na ikibidi wataua watu na NAWAHAKIKISHIA hawatafanya makosa tena ya KUJIAMINI MNO na kutudharau tena (kusema kelele za chura) kama walivyofanya kwa RICHMOND na EPA, sasa wameshajua JF, Mwanahalisi, Thisday, RaiaMwema ni kiboko kwa hiyo wameingia kwa KASI, NGUVU, ARI na PESA 'mpya' na ndugu zangu HISTORIA ITATUHUKUMU, MUNGU ATATULAANI kwa kusema, "Muliniomba nafasi nikawapa, nikawachanganya, mukaichezea kwa kugombana wenyewe kwa wenyewe tena hadharani". Tumeingiliwa ndani ya nyumba, sasa tunagombana wenyewe na wezi WANAPETA. Tumebadili mwelekeo, sasa FISADI ni MBOWE NA SITTA huku kwa upande mwingine LOWASSA (akifananishwa na Ali Hassan Mwinyi), KARAMAGI, ROSTAM (akifafanishwa na Amir Jamal) ni MASHUJAA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WALAANI MAFISADI NA MAKUWADI WAO


ORODHA YA KWANZA YA LIST OF SHAME kama ilivyowekwa hapa JF.

________________________________________
ORODHA YA MAFISADI
(LIST OF SHAME)

KANUNI/ VIGEZO VILIVYOTUMIKA

A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi ambao

kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa

Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma wamefanya

maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/au taasisi za

kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu

katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya

Watanzania.

MISINGI YA KISHERIA/KISIASA YA ORODHA YA MAFISADI

A. KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sura ya 2 ya Sheria za Tanzania imeweka ‘Malengo Muhimu na Misingi

ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali’ kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:
(a) Kwamba “wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa

wananchi….”;

(b) Kwamba “lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi”; na

(c) Kwamba “Serikali itawajibika kwa wananchi….”
(d) ….”

Katika kutekeleza malengo na misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali iliyotajwa, “… Mamlaka ya Nchi na vyombo

vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
(a) …
(b) Kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;

(c) Kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba wa Taifa unaendelezwa,

unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;

(d) Kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
(e) …
(f) …
(g) …
(h) Kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;

(i) Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye

jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;

(j) Kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za

uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
(k) ….”

Ibara ya 7(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeamuru kuwa “… Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote na mamlaka

yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na

jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii …” ya Katiba. Katiba pia

imewapa viongozi wa umma “… wajibu wa kufuata na kuitii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano.” Aidha,

viongozi wa umma wamepewa “… wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali

yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi….” Vile vile viongozi wote wa umma “watatakiwa na sheria kutunza vizuri

mali ya Mamlaka ya Nchi nay a pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa taifa

kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”

Licha ya masharti ya kikatiba yaliyotajwa hapo juu, viongozi wa umma waliotajwa katika Orodha hii ya Mafisadi

walikuwa wanabanwa na masharti ya sheria nyingine za nchi yetu kama ifuatavyo:

B. SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA, 1995

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili

na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya

Serikali na katika sekta ya umma. Katika kutekeleza wajibu wake, Rais anatakiwa kuweka taratibu thabiti za maadili

katika utumishi wa umma ambazo:

(a) Zitahakikisha kwamba kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na wajibu

wake kama kiongozi wa umma;
(b) …

(c) Zitaweka taratibu za wazi za maadili kuhusu migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wa kuchaguliwa na wa

kuteuliwa;

(d) Zitapunguza uwezekano wa migongano inayotokana na maslahi binafsi kuingiliana na shughuli za umma za viongozi wa

umma na kuweka taratibu za utatuzi wa migongano hiyo inapotokea.

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma:
(a) kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na

watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali;

(b) kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha

shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na haitatosheleza kwao

kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu;

(c) kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya

umma;

(d) kuhusiana na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na

maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya;

(e) kuhusiana na maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma watapanga masuala yao kwa

namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo

inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma;

(f) kuhusiana na zawadi, viongozi wa umma hawatadai au kupokea manufaa ya kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo ndogo,

ukarimu wa jadi/takrima au manufaa mengine yenye thamani ishara, isipokuwa tu kama manufaa hayo yatatokana na

mkataba au mali ya kiongozi wa umma;

(g) kuhusiana na upendeleo, viongozi wa umma hawatatumia vyeo vyao rasmi katika kusaidia taasisi au watu binafsi

katika mahusiano yao na serikali iwapo kufanya hivyo kutasababisha upendeleo kwa mtu yeyote;
(h) …
(i) Kuhusiana na mali ya serikali ambayo viongozi wa umma hawatatumia ama moja kwa moja ama kisiri siri, au kuruhusu

kutumiwa kwa mali ya serikali ya aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mali ya serikali iliyokodishwa kwa ajili ya

kumnufaisha kiongozi wa umma;

(j) Kuhusiana na ajira baada ya utumishi wa umma, viongozi wa umma hawatafanya vitendo vitakavyoshusha hadhi na

heshima ya utumishi wa umma baada ya kuondoka katika utumishi ili kupunguza uwezekano wa matarajio ya ajira kuleta

migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wanapokuwa katika utumishi wa umma; kupata upendeleo baada ya kuondoka

katika utumishi wa umma; kutumia taarifa zinazopatikana kutokana na utumishi wa umma kwa maslahi binafsi; na kutumia

utumishi wa umma kwa ajili ya kupatia nafasi za ajira nje ya utumishi wa umma.

VIONGOZI WA UMMA WALIOKO KATIKA ORODHA HII WAMEKIUKA NA/AU KUVUNJA MASHARTI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO NA

SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KAMA IFUATAVYO:

A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

1. DR. DAUDI T.S. BALALI

Dr. Daudi Balali amekuwa na bado ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997. Katika kipindi hicho cha miaka

kumi, Gavana Balali amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

(i) Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, ameruhusu na/au

kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufikia Shilingi 522, 459, 255,000 katika ujenzi wa

majengo ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyoko barabara ya Mirambo, Dar es Salaam na Gulioni, Zanzibar. Aidha taarifa

kutoka vyanzo vingine zinaonyesha kwamba mwaka 1998 kampuni ya Skanska Jensen ya Sweden ilituhumiwa kutoa hongo ya

Dola za Marekani milioni 5 kwa Gavana Balali tuhuma zilizopelekea kampuni hiyo kupigwa marufuku kushiriki tenda ya

ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, katika mazingira yanayoashiria ufisadi mkubwa, kampuni ya Group 5 ya Afrika ya

Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Skanska Jensen ilipewa tenda ya kujenga majengo hayo ya Benki Kuu;

(ii) Kufuatana na barua iliyotajwa katika aya ya (i) hapo juu, Gavana Balali aliidhinisha na/au kuruhusu na/au

kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 118,396,460.36 zilizopelekwa katika akaunti isiyojulikana ya Benki ya Nedbank

Ltd. ya Afrika Kusini kama malipo ya madeni ya kampuni muflisi ya Meremeta Ltd. iliyokuwa inachimba dhahabu katika

eneo la Buhemba wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara. Kwa miaka mingi Serikali ilikuwa ikitoa taarifa za uongo kwamba

Meremeta Ltd. ilikuwa ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa

ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Hata hivyo, nakala ya usajili iliyotolewa na Msajili wa

Makampuni wa Uingereza na Wales inaonyesha kwamba kampuni hiyo iliandikishwa nchini Uingereza tarehe 19 Agosti 1997

na ilifilisiwa huko huko Uingereza tarehe 10 Januari 2006. Aidha, taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

(BRELA) ya tarehe 31 Mei 2005 inaonyesha kwamba Meremeta Ltd. ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania

kama tawi tarehe 3 Oktoba, 1997. Vile vile taarifa hiyo inaonyesha kwamba hisa 50 za Meremeta Ltd. zilikuwa

zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini na hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na

Serikali ya Tanzania kwa kupitia kwa Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha. Inajulikana vile vile kwamba Gavana

Balali aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Meremeta Ltd. kati ya mwaka 2004 na 2005. Hata hivyo, kuna

utata mkubwa juu ya nani ni mmiliki hasa wa Meremeta Ltd. kwa kuwa taarifa ya BRELA inaonyesha pia kwamba makampuni

mawili ya Kiingereza – London Law Services Ltd. na London Law Secretarial Ltd. – nayo yanamiliki hisa moja moja za

Meremeta Ltd. Makampuni hayo yanatumia anwani moja iliyoko 84 Temple Chambers, Temple Avenue, jijini London.

Haijulikani ni kwanini Gavana Balali aliruhusu fedha za umma kutumika kulipia madeni yote ya kampuni ambayo Serikali

ilikuwa inamiliki hisa 50 tu wakati makampuni mengine ya kigeni yalikuwa yanamiliki hisa 52. Na kama ilivyosema

barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, uhalali wa Serikali kulipa madeni ya Meremeta Ltd. kwa Nedbank Ltd. badala ya

kuiacha benki hiyo kudai malipo hayo kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na wadeni wengine haujulikani;

(iii) Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu, Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia

malipo ya Dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kampuni ya Tangold Ltd. Katika hotuba yake Bungeni ya tarehe 27 Juni

2007, Waziri wa Madini na Nishati Mheshimiwa Nazir Karamagi alidai kwamba “… mali na madeni ya MEREMETA

yamehamishiwa kwenye kampuni mpya ya TANGOLD ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.” Hata hivyo,

barua ya BRELA ya tarehe 4 Julai 2007 inatamka wazi kwamba “Tangold Limited ni kampuni ya kigeni iliyosajiliwa kwa

mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Mauritius, na baadae kuandikishwa nchini Tanzania kama tawi la kampuni ya kigeni.”

Barua hiyo inaongeza kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania mnamo tarehe 20 Februari 2006

na kwamba Katiba ya kampuni hiyo haikuonyesha “majina ya wanahisa wa kampuni na mgawanyo wa hisa.” Barua hiyo ya

BRELA inaonyesha kwamba wakurugenzi wa Tangold Limited ni pamoja na Gavana Balali, Gray S. Mgonja ambaye ni Katibu

Mkuu Wizara ya Fedha, Andrew J. Chenge ambaye ni Waziri wa sasa wa Miundo Mbinu, Patrick W.R. Rutabanzibwa ambaye ni

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Vincent F. Mrisho ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha fomu Na. 1F

inayohusu usajili wa kampuni za kigeni iliyowasilishwa BRELA na mawakili wa Tangold Limited na kusainiwa na Gavana

Balali tarehe 20 Mei 2005 inaonyesha kwamba kampuni hii imetokea “Jamhuri ya Mauritius” na anwani yake iko Suite

520, Barkly Wharf, Le Caudan, Waterfront, Port Louis, Mauritius. Hivyo ndivyo kinavyoonyesha cheti cha usajili

kilichotolewa na Msajili wa Makampuni wa Jamhuri ya Mauritius mnamo tarehe 5 Aprili 2005 na pia leseni ya biashara

iliyotolewa kwa Tangold Ltd. Port Louis nchini Mauritius tarehe 8 Aprili 2005. nyaraka hizi pia zinaonyesha kwamba

Tangold Limited ni kampuni binafsi (private company limited by shares). Kuna utata zaidi kwani kifungu cha 7(e) cha

Katiba ya Tangold Ltd. kinaruhusu hisa za wanaomiliki kampuni hiyo binafsi kuhamisha hisa zao kwa wanandoa, baba,

mama, watoto, wajukuu au wakwe zao wa kike au wa kiume! Sasa kama ni kweli kwamba Tangold Ltd. inamilikiwa na

Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja, je nani ni mke au mume au baba au mama au motto au mjukuu au mkwe wa

kike au wa kiume wa Serikali ya Tanzania ambaye anaweza kuhamishiwa hisa za kampuni hiyo? Katika barua yake ya

ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alidai kwamba Ofisi yake ilishindwa kuelewa uhalali wa malipo ya dola za Marekani

13,340,168.37 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Tangold Limited;

(iv) Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia mkopo usio na riba wa Dola za Marekani 5,512,398.55

kwa kampuni ya Mwananchi Gold Co. Ltd. kati ya mwaka 2004 na tarehe 30 Juni 2006. Kati ya fedha hizo, deni la dola

2,807,920 limedhaminiwa kwa dhahabu ghafi ambayo ingenunuliwa kutokana na fedha za mkopo zilizotolewa na Benki Kuu

yenyewe! Kwa maana rahisi ni kwamba kampuni ya Mwananchi Gold haijatoa dhamana yoyote inayoeleweka kwa mabilioni ya

shilingi ilizokopeshwa na Benki Kuu chini ya Gavana Balali. Kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, hadi kufikia

mwezi Desemba 2006 Mwananchi Gold Co. Ltd. ilikuwa imeshindwa kulipa hata riba ya mkopo huo kwa kiasi cha dola za

Marekani 62,847.91. “Katika mazingira haya”, inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, “hatukuweza kujiridhisha

kwamba deni la dola la Marekani 5512398.55 inalodaiwa (Mwananchi Gold Co. Ltd.) hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006

linaweza kulipika.” Je, ni kampuni gani hii iliyopewa mamilioni ya fedha za umma katika fedha za kigeni bila kudaiwa

riba au kupewa kipindi maalumu cha kulipa mkopo huo? Kufuatana na taarifa za BRELA, Mwananchi Gold Co. Ltd. ni

kampuni binafsi ambayo wanahisa wake ni Benki Kuu ya Tanzania yenye hisa 500, Shirika la Maendeleo la Taifa (hisa

500), Mwananchi Trust Co. Ltd. (hisa 1,123) na Chimera Co. Ltd. (hisa 500). Kampuni hii ilisajiliwa kama kampuni

binafsi tarehe 12 Desemba 2002. Mawakili wake ni kampuni ya mawakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Associates

ikiwashirikisha aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wakati huo marehemu Francis L. Nyalali, Waziri Mkuu wa zamani Joseph

Sinde Warioba na aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa R. Mahalu. Wakurugenzi wa Mwananchi Gold

ni Joseph Sinde Warioba, Gavana Daudi Balali, Col. J. Simbakalia, Vulfrida Grace Mahalu, Yusuf H. Mushi na raia

wawili wa Italia, Paolo Cesari na Patrizio Magrini. Vulfrida Mahalu ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa kampuni binafsi ya VMB

Holdings (1996) Ltd. na pia ni mke wa Profesa Mahalu ambaye kwa sasa anakabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi

kutokana na madai ya wizi wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Serikali wakati akiwa balozi wa Tanzania nchini

Italia! Kanali Simbakalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Taifa na Yusuf Mushi ni Mkurugenzi

Mtendaji wa kampuni binafsi ya Business Machines Consultants (T) Ltd;

(v) Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya shilingi 131,950,750,000 kwa watu

wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. Vile vile Gavana Balali anadaiwa kuidhinisha malipo ya

shilingi bilioni 4,228,658,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. “Katika mazingira

haya”, inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, “hatukuridhika na uhalali wa hasara ya

shillingi bilioni 131.9 zinazoonekana katika taarifa za fedha hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006….” Kwa mantiki hiyo,

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu aliiasa Benki Kuu kuanzisha uchunguzi wa malipo yaliyosababisha hasara ya shilingi

131,950,750,000 na shilingi 4,228,658,000 zilizolipwa kama malipo ya madeni ya nje. Waziri wa Fedha Zakia Meghji

mwenyewe amekiri kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma katika akaunti za malipo ya madeni ya nje katika barua

yake kwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). IMF yenyewe katika taarifa kwa vyombo vya habari ya

tarehe 27 Juni 2007 imetamka kwamba “Serikali (ya Tanzania) imekwisha kusimamisha malipo kutoka akaunti hiyo hadi

uchunguzi huo utakapokamilika.” Wakati Serikali ikitoa taarifa hizi kwa IMF imekataa kata kata kutoa taarifa hizi

kwa umma wa Watanzania wala wawakilishi wao Bungeni.

2. ANDREW J. CHENGE

Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya sasa ya Rais

Jakaya Mrisho Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka yote kumi ya

utawala wa Rais Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo, Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa “mshauri wa Serikali ya Jamhuri

ya Muungano juu ya mambo ya sheria na … aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo

yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria….” Katika kipindi

hicho cha miaka kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
(i) Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola

za Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
(ii) Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri

Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa katika sehemu

inayomhusu Gavana Balali;
(iii) Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa

Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya kimataifa

ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake Bungeni tarehe 6 Novemba

2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha

miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya

shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi

bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William

Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega

ulipofunguliwa hadi mwaka huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani

bilioni 2.614 wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge

angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa

linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.

3. BASIL P. MRAMBA

Mheshimiwa Basil Mramba ni Mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Rombo na Waziri wa Viwanda na Biashara na kwa miaka kumi

ya utawala wa Rais Mkapa alikuwa ndiye Waziri wa Fedha. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Mheshimiwa Mramba

amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

(i) Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government

Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu.

Chini ya mkataba wake na Serikali ya Tanzania, Kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba

inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu. Kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu,

katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart (Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi

wa mahesabu ya makampuni ya dhahabu, ijapokuwa “hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu

ukaguzi uliofanywa katika mwaka 2005/06”! Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alisema katika barua yake kwamba

“hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni

ya ushindani.”
(ii) Vile vile kuna taarifa za kuwepo kwa rushwa na/au ufisadi mkubwa kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex

Stewart Assayers. Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya

Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye jina la Bwana Basil ambaye ana wadhifa wa Waziri katika serikali ya

Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye kampuni hiyo

na kuwa analipwa na kampuni hiyo. Kwa mujibu wa Flores, hakuwezi kukawa na ushahidi wowote kuthibitisha kwamba

‘Bwana Basil’ anapokea malipo kutoka kwa Alex Stewart kwa vile malipo yote kwake yamekuwa yakifanyika nje ya nchi.

Kwa kadri tunavyofahamu, mtu pekee aliyekuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Tatu na ambaye pia ni waziri katika

Serikali ya Awamu ya Nne na ambaye ana jina la ‘Basil’ ni Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba. Tumemtaka Waziri wa

Fedha kutupatia nakala ya Mkataba kati ya Benki Kuu na Alex Stewart, na kuwataka Mheshimiwa Basil Mramba na Erwin

Flores walete maelezo yao kwetu kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka, Haki na Kinga za Bunge ya mwaka 1988 kwa barua yetu

ya tarehe 18 Julai 2007 ili waweze kujibu tuhuma hizi. Bado tunasubiri majibu hayo.
(iii) Mheshimiwa Mramba amehusishwa pia na ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za umma na uuzaji holela wa

rasilmali za taifa letu. Kashfa hizo ni pamoja ni ununuzi wa rada ya kijeshi, ununuzi wa ndege ya Rais, na

ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na National Microfinance Bank (NMB).

4. GRAY S. MGONJA

Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania

na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa

kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya

Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma

katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.

5. PATRICK W.R. RUTABANZIBWA

Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati mikataba mibovu ya

madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Kwa sasa Bwana Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na

vile vile Mkurugenzi wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited. Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina katika maelezo

yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna mgongano mkubwa kati maslahi yake binafsi kama Mkurugenzi

wa kampuni binafsi iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa kuyalinda akiwa kama

kiongozi wa umma.

6. NIMROD ELIREHEMA MKONO

Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa kampuni ya mawakili ya Mkono &

Company Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali inaainisha kuwa Benki

Kuu imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia ambapo Benki Kuu

inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates wamekwishalipwa

shilingi 8,128,375,237 kwa fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia

13.5 ya deni lote inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa

kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.

Lakini hoja nyingine ya kimsingi ni kama malipo haya kwa mawakili yanaruhusiwa chini ya Kanuni za Malipo ya Mawakili

na Uamuzi ya Gharama za Kesi za mwaka 1991, Tangazo la Serikali Na. 515 la mwaka 1991 (Advocates’ Remuneration and

Taxation of Costs Rules, 1991). Kanuni hizi zimeweka kiwango cha malipo ya mawakili katika kesi ambazo fedha

inayodaiwa ni zaidi ya Shilingi milioni 10 kuwa ni asilimia tatu. Kwa kufuata masharti ya sheria hii ya malipo ya

mawakili, kampuni ya Mkono & Co. Advocates ilipaswa kulipwa Shilingi bilioni 1.8.

Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu

wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd.,

Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana

na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme’ iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati

Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo

kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: “Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni

vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye

makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa

kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD.,

AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)

Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: “Mheshimiwa Spika, ni

vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa

haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati

(permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa

Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa. Nimrod Mkono

alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya Marcus Ltd., makampuni

ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya utaratibu wa DCP.”

7. BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza

kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na

anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba

wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa

familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya

Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa

asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa

zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya

kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa

Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili

wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na

bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu

ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa

kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa

hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa

mkataba.

8. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais,

Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994

hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini,

Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya

kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia

wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni

ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa

Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa

nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya

miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza

eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao

wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute

Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao

ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.

Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama

Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha

wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining

Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na

kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya

kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni

ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni

moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

C. SHERIA YA UDHIBITI WA MAKOSA YA KUHUJUMU UCHUMI, 1984
D. SHERIA YA KUZUIA RUSHWA, 1971 na/au SHERIA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, 2007
 
.......simpendi Sitta kwasababu ya

Mabovu yake (Kuanzia Ustawishaji Dododma na TIC)
Kujiona yeyeni Bora Kuliko wenzake
Ubabe wake nknk nk nk nk

Kwanini, hapo mwanzo nilisema hii Hoja IENDE KWENYE VIBWEKA/VITUKO VYA WAKUBWA.................ni kwa sababu....irregardless ya Agenda 21

........mtu unaingia JF vuuu...............mara ooohhh Spika anatumia Millioni 5 katika safari zake za ndani.......mara ohhh akienda Safari zake za nje anatumia Millioni 15........mara oooohhh sijui alikopa wapi na mara alikopa wapi.............halafu Hoja yake imekuja kumezwa sasa na vimada wake so and so....wanatumia magari ya serikali fulani fulani (yakatajwa)

1.Kuna Miiko ya Viongozi (nashukuru kuna mjumbe mmoja hapo juu ameweka baadhi)
2.Kuna Mapato na matumizi ya viongozi ambayo yako clearly defined

Mtoa mada agekuja na kwa kusema Spika akisafiri safari za ndani/Nje anatakiwa kutumia Kiasi X yeye akatumia X+.......hapo ningemuelewa...and there must be a justification kwa matumizi hayo

Kwa std tulizo jiwekea hapa JF ya kujadili akina Mar Chifupa (RIP), Mengi, Mbowe na wengineo kuhus affairs zao ndio maana nili-conclude kuwa hiii mada inafaa kuwa hapa ilipo.

Pengine tukiipata HIYO MVUA.........wengine tunasubiri hiyo mvua.....kwani hatuwi disguised na just a tone la mvua.
 
Yaani ina maana hata Mh. Cheyo naye alikubali kulamba huo uchafu? Maana naamini yeye alikuwa Mwenyekiti wa hiyo Kamati kama sitakuwa nime-overlook.
 
jamani haya yote ni sehemu ya mapambano ya kifikra na tuelewe kabisa kuwa katika mapambano haya yasiyo na sheria basi kila silaha inaonekana kutumiwa! Tatizo ninaloliona ni watu kuanza kutumia "nuclear option" ili siyo tu kushinda vita bali pia kumuangamiza adui yao.

Lowassa, Karamagi, na Msabaha na baada ya muda si mrefu Hosea na Mwanyika wote waliangushwa/wataangushwa kutokana na kazi zao; kwambe wameshindwa kutelekeza wajibu wao. Hakuangushwa mtu kwa sababu ya alilala na nani, na hakuangushwa mtu kwa sababu ya ana vimada wangapi. Kama tunataka kuzungumzia maadili ya ngono hili ni jambo muhimu na even kabla ya hili nilishaanza kuandika makala kuhusu "ufisadi wa ngono, nao ni ufisadi". Hili tunaweza kulizungumza lakini tukianza kurusha majina, tujue kabisa "kipimo kile kile tupimiacho, ndicho kitakachotumiwa dhidi yetu au dhidi ya rafiki zetu".

Tusijefurahia mkuki kwa nguruwe lakini siku ukigeuzwa kuwa ni kwa binadamu watu tuanze kubadilisha principles.

Sasa ukisoma habari nyingine kule kwenye KLH News jinsi "Lowassa alivyozidiwa Kete" utaona ni kwanini kuna watu wana kisasi na spika.

Kwa hiyo badala ya kudandia tu, tukumbuke kuwa kuna watu wanaweza kuja na madazi mazito ilimradi wafanye damage hata kama madai hayo si ya kweli; kama yule jamaa aliyedai kuwa Mbowe ni mbakaji watoto na ana kesi kadhaa mahakamana "tangu miaka ya tisini" na hadi hivi sasa jamaa huyo ameshindwa kuwa muungwana na kuiondoa na kuomba radhi.

Na kama kuna mtu anafikiria haya mambo yanamlenga Sitta tu afikirie tena, wenye kuleta habari hii wana target zao na hapo kwa Sitta siyo mwisho.

Hata hiyvo kama nilivyozungumza wakati ya mada ile ya "picha" kuwa viongozi wenyewe wasipokemeana wakidhani wanaumbuana wajue kabisa kuwa kikigeuzwa upande wao wasilie faulu!
 
Mkuu halisi

Umesomeka Mkuu!

Nafikiri wakati mwingine ni kukumbushana, make ukiwa Vitani na Risasi zinatoka kila upande unaweza kusahau kama mwenzako ametangulia.
 
mhh ,minjemba hii hata haya hawana ,hao wote watatu wa wawizi inakuwaje?.kwa nini tusimwambie mwenye mzigo wake unamalizwa.Ahh lakini ya nini we acha tunyamaze tu, maana ufisadi wa huyo mwenye mzigo wake naye hatuujui labda na yeye ana play boy wake maana hawa wenzetu kwa sababu ya mihela ya bure wanaishi kama wazungu,kila mtu kivyake,mpaka watoto wao huwezi kuamini wanavyoishi ukibahatika kuokota jamani umeukata.
tutaishia kusema tu hatuwawezi,wenyewe wanaitana mashujaa, sasa sisi ninani kwao.
NAOMBA NIJIBU HAYO UNAYOSEMA NIKWELI? MAANA HAINGII AKILINI KAMA SUGAR DADY HUYU ANAFANANA NA HAYO UNAYOTUPA.HALAFU UNASEMA HILO NI TONE LA MAJI TU 'INATISHA! IKIWA KATIKA KIKOMBE CHA KAHAWA ITAKUWAJE.
HE HAYA KWAHERI
TUMUACHIE MUNGU SIJUI ITAKUWAJE SIKU MTU APATE MSHTUKO WA MOYO YUPO NYUMBA NDOGO.

SEFF
 
TUHUMA za ufisadi zilizosambazwa katika mtandao wa intaneti zikimlenga Spika wa Bunge, Samuel Sitta, zimesababisha Ofisi ya Bunge kuanzisha uchunguzi dhidi ya kiongozi huyo wa juu wa mamlaka hiyo ya dola.
Taarifa za kuanza kwa uchunguzi huo zilitangazwa na Katibu wa Bunge, Damian Foka wakati alipofanya mahojiano na gazeti hili, ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa Foka, madai ambayo atayafanyia uchunguzi ni yale yanayomhusisha Spika na tuhuma za kuwasilisha katika ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Bunge risiti za kughushi za matumizi yake.

“Ofisi za Bunge hazina taarifa za Spika kughushi risiti, nipeni muda niwasiliane na wakuu wa vitengo husika, ili tutafute ukweli kuhusu tuhuma hizo, na iwapo tutabaini lolote tutatoa majibu. Ile ni ofisi ya umma na mali zake zinatakiwa zitumike kwa matumizi yanayopaswa na si vinginevyo,” alisema Foka.

Pamoja na hilo, Foka alikiri madai yaliyoandikwa katika mtandao wa intaneti yanayoeleza kuwa, Sitta aliwasilisha risiti ya shilingi milioni mbili aliyonunulia dawa kutoka katika duka moja la dawa lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Aidha, alisema baada ya kuwasilisha risiti hiyo, alimwelekeza alete pia cheti cha daktari kilichokuwa kikionyesha kuwa alitakiwa kutumia dawa zenye gharama hizo kutokana na matatizo yake ya kiafya katika kipindi cha wiki moja.

“Ni kweli kuwa mwezi uliopita, Spika Sitta alilipwa shilingi milioni mbili katika kipindi cha wiki moja kwa ajili ya kununulia dawa katika duka la dawa la Oysterbay,” alisema Foka.

Alisema malipo hayo ni halali kwa sababu Ofisi ya Bunge ina taarifa kuhusu matatizo ya kiafya ya Spika Sitta ambayo hata hivyo hakutaka kuyaweka bayana kwa madai kuwa maradhi ya mtu ni siri yake na daktari wake.

Hata hivyo taarifa ambazo gazeti hili linazo zinaeleza kuwa, Spika amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya miguu ambayo kimsingi ndiyo aliyokuwa akiyatibu kupitia dawa alizonunua katika duka hilo la dawa.

Kuhusu madai kwamba Spika amekuwa akijihusisha katika matumizi mabaya yasiyotambulika kisheria na kikanuni kwa madaraka yake, ya magari mawili ya Bunge aliyopewa kwa shughuli zake binafsi, Foka alisema hana taarifa hizo na kuongeza kuwa uwezekano wa kuwepo kwa jambo hilo ni mdogo.

Wakati Foka akitoa taarifa hizo, maofisa kadhaa wa Bunge waliozungumza na Tanzania Daima wanaeleza kuwa, siku chache zilizopita ofisi ya Katibu wa Bunge ilipata kumhoji Sitta kuhusu kuwapo kwa madai hayo yanayomhusisha na matumizi yasiyofaa ya magari ya umma.

Foka pia alikanusha madai kwamba Ofisi ya Bunge imekuwa ikilipa gharama za umeme na maji kwa baadhi ya watu walio na uhusiano wa karibu na Spika, ambao kimsingi hawastahili kupata malipo hayo.

Pia alikanusha madai kuwa, kamati moja ya kudumu ya Bunge iligundua kuwepo mapungufu katika matumuzi ya fedha yaliyofanywa na Spika, lakini wajumbe wake walinyamazishwa na Sitta mwenyewe baada ya kuwatisha kuwa, iwapo wangeweka hadharani upungufu huo, wangekabiliwa na adhabu ya kunyimwa posho pamoja na kutopangiwa safari za nje.

Akizungumza madai kwamba Sitta amekuwa akilipwa kiasi kikubwa kwa ajili ya safari anazofanya ndani na nje ya nchi, na pia kujilimbikizia deni kubwa linalotajwa kufikia sh milioni 60, Foka alisema anachofahamu, Spika anasafiri nje na huwa analipiwa huduma ya maradhi na nusu ya asilimia 20 ya posho kama fedha za matumuzi na si zaidi ya hapo.

Naye Mkurugenzi wa Elimu ya Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge, Jose Mwakasyuka ambaye alikuwapo wakati Foka akihojiwa, alisema mali za Bunge zipo salama na kwamba tuhuma zinazoelekezwa sasa kwa Spika zina kila dalili ya kuwepo nia ya makusudi ya kumchafua.

“Hizi tuhuma ni za kupakana matope na kuchafuliana majina, kwani tuhuma zenyewe hazimtaji nani aliyezitoa. Nadhani kuna watu wanataka waandishi waache kuandika mambo ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya nchi na badala yake wajielekeze kwenye tuhuma dhidi ya viongozi,” alisema Mwakasyuka.

Hivi karibuni, Spika Sitta alizungumza na gazeti hili kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake na kueleza kuwa, hawezi kuzizungumzia kwa sababu zinatolewa na wahuni wenye lengo la kumchafulia jina lake mbele ya jamii.

Mbali ya hilo, Sitta alilielekeza Tanzania Daima kuwasiliana na maofisa wa Bunge ili kupata ukweli wote kuhusu madai hayo yaliyoandikwa katika mtandao mmoja wa intaneti

SOURCE: TANZANIA DAIMA
 
Hivi huyu Sitta hajajua kwamba JF ndiyo kombora la kuangusha vigogo. Sasa achukulie mzaha haya yanayojadiliwa hapa kama atapona. Ukiingia kwa kashafa ni kashfa hizohizo zitakazokutimua!
 
Hmm! Dawa za 2 mil, huh? I can come up with a few:
A) 2nd line ARVs for HIV
B) Chemotherapeutic agents for a cancer
None of the above are anything 2 b ashamed of so Bunge better tell us what they have been doing with OUR money!
I am sure he could afford 2 buy the drugs out of his own pocket if he wanted to! Kuna waTZ wanakufa kwa kushindwa kununua dawa kama Insulin wao wanaspend govt monies on fancy remedies.
Tut tut!!
 
Hivi huyu Sitta hajajua kwamba JF ndiyo kombora la kuangusha vigogo. Sasa achukulie mzaha haya yanayojadiliwa hapa kama atapona. Ukiingia kwa kashafa ni kashfa hizohizo zitakazokutimua!
sita his days are countable now.anaandamwa na dhambi ya usaliti na siku moja itantoa nje ya ukumbi.
 
..Samuel Sitta ameoza tangu zamani sana alipokuwa DG wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu Dodoma, maarufu kama CDA. Pengine hata kabla ya hapo.

..Hizi taarifa za ngono zilikuwepo tangu akiwa waziri ktk serikali ya Kambarage.

..Nilifikiri kwamba kwasababu ya uzee na umri basi atakuwa amepumzika ngono.
 
Back
Top Bottom