Kweli hawa viongozi wetu hawana uchungu na kodi zetu, hiyo nyumba ina nini hasa? Na kama unaworthy 10ml kwa nini wanunue na thamani tena za ml 200!?
Namna hii hatuendi popote
Kwenye hii topic sijatia neno... Labda tuangalie kwa ufupi tu...
Nyumba ya zamani ambayo imegeuzwa kuwa Club ni hii hapa:
Na nyumba mpya inayolipiwa $8,000 kwa mwezi ni hii hapa:
Inaonekana kuna mgongano kati ufahamu na hapa ndipo tunapokwama katika kujadili ,ila ndi mjadiliano.
Hao akina Kikwete akina Sita Lipumba ,yako mambo ya kusemwa kwao na ni pale wanapozungumza ndio unaweza kuvaana nao ,kama tunavyomuona Sitta akikingia ubavu wanaoulizwa masuala ya papo kwa pao.
Hapa kunajadiliwa viwango vya mishahara katika vyeo vya kiserikali na si vinginevyo ,mfumo mzima wa mishahara ya serikali na viwango vyake ndio lengo kuu ,katika kuvijadili ,aidha hili halimhusi Kikwete wala Sita au Lipumba na wengine tele.
Vyeo na kima cha mshahara haviendani na hali ya WaTanzania walio wengi ,na hawa tunaowataja wameyakuta na wanayaendeleza pengine na kuyazidisha ,sasa faida ya majadala sio kwenda nao mbali sana ,kinachotakikana ni kujenga hoja nzito ambayo itakubalika kwa wadau ambao ni wananchi wapiga kura.Na nini wanatakiwa wafanye.
Pengine tukaona kwa upigaji kura itatuchukua muda mrefu kusahihisha na kuuondoa ufisadi huu kutokana na ukiritimba wa CCM (Hapa hakuna Kikwete hiki Chama kipo zaidi ya miaka 50 wanapokezana vijiti),nini kifanyike ?
Ni kuushawishi umma wa WaTanzania kuingia mabarabarani kupinga mishahara hii mikubwa ya aina yake ,hii ni kazi ya vyama vya upinzani ,labda hilo itaonekana ni kutaka kuleta fujo.Ila ni njia muhimu kwa siku hizi katika ulimwengu wanyonge kupinga au kuipinga Serikali kutokana na ubadhirifu unaovuka mipaka.
Jengine ni kufanya tathmini kwa nchi majirani hata za Ulaya namna watu kama hawa wanavyolipwa ,ikiwezekana tutafute mshauri muelekezi wa kutufanyia na kutuondolea mirija hii.Ila hili nalo litakuwa la ajabu.
La mwisho ambalo linaweza kuzua mvutano ni kwa upande wa vyama vya upinzani ambacho kitaweza kubeba jukumu la kubadilisha na kupitia upya mfumo wa kiwango cha lala salama kinachotumiwa na Sulatani CCM kulipa wafuasi wake wa ngazi za juu kuwarubuni ili ifanye itakavyo kama tunavyoona ,ukienda mabenki wanakwapua kwa ajili ya Uchaguzi ,wakienda kwenye vyombo vya dola tunaona vinavyotumika,wakienda mahakamani hata kama wanamakosa wanaibuka videdea ,bungeni wabunge wanaunga mkono na Spika anashangalia.
Ingawa bado fedha hio ukiibadilisha kwa dola si pesa kitu labda ile ya raisi kidogo inatia homa na akimaliza utamu wa Uraisi anafungiwa nyingine.Hata hivyo inabidi kwanza tujue International salari inasemaje ,sio tunakwenda mbio tu kama tunaozungumzia private busness,mnaweza mkapanga mkakuta Mkuu wa mkoa inabidi apokee laki moja.
...Kaka upo right !!!hizi biashara ya the bucket stops with people TZ hai-aplyy hata siku moja.kwa sababu hakuna DEMOKRASIA.
wangapi wanakufa kwa kukosa dawa?matibabu?polisi akikaa kwenye nyumba ya mabati no one talks about hadhi and dignity of our constitution's guards.lakini hiyo minjemba inayotuibia kila siku mnataka iwe na hadhi.kwa lipi la maana wanalolifanya?!hizo nyumba zote mbili,ya zamani na mpya in zaidi ya mara 10 ya ile ya mtanzania wa kawaida.zinatosha!mnataka waishi kama wako DC?!kwa lipi,kwa kipi?!we are soo proud of nothing.the day we learn to be humble may be things will change.
Mkuu kwa kurekebisha taarifa, hiyo nyumba ya juu haikuwa nyumba ya spika, nyumba aliyokua anakaa Msekwa na kuuziwa ipo mtaa wa Bongoyo. Hiyo nyumba inayooneshwa hapo alikua anakaa General Frish, ipo Haile selasie rd, opposite Jackies Pub na aliuziwa General kama wengine.
Ili kuwa fair, tunaomba na picha za mahekalu ya waziri mkuu, chief secretary na makamu wa rais. Kumlinganisha spika na nyumba za fullusuti za polisi tutakua hatumtendei haki na ni kupersonalize issue na haitatusaidia kitu in the long run.
...Kaka upo right !!!
---Hii Kusema Spika anastahiki hadhi Fulani wakati Waalimu,..Polisi..Madaktari nao wanastahiki lkn Hawapati....Tuache Ujinga wa Kusema eti Sheria Inaruhusu....
kama SPIKA amekuwa Front kupambana na UFISADI ...na Anajua Hali Halisi ya watanzania Alikuwa hana haja ya Kukataa Nyumba aliyopewa Kuishi...Angeweza Kuhitaji Marekebisho Kadhaa tu..
Kwa Kitendo hiki Spika Haguswi na Shida za Wananchi...Bunge Letu Limejaa MAFISADI...!!!
waseme wengine ni haki yao akisema Sheikh Yahya ni ulozi, nyie m-vipi?Shekh tia bidii ramli zako za ulozi, ipo siku moto utakuwakia
Shekh tia bidii ramli zako za ulozi, ipo siku moto utakuwakia
Wakuu heshima sana na huu mjadala ni very educative, kuna mengi sana hapa yamesemwa ambayo ni valid na hayakwepeki, ni muhimu sana hii debate ikapanuliwa katika sekta nyingi za serikali yetu ukianzia na ofisi ya rais hadi chini,
- Pamoja na kwamba Spika indiviually hana makosa kisheria kwa kuishi kwenye hii nyumba, ni kweli he is obligated kuangalia matumizi ya ofisi yake, kwa sababu hata Obama alipoingia amebadili mengi sana ya matumizi ya ofisi yake ili kupunguza matumizi ambayo yako okayed na sheria.
- Bunge letu lianze kujiangalia upya, kama kweli linaishi within our national financial means maana reading between the lines hii thread inaonekana kuna some financial abuse huko kwa visingizio vya sheria na hili ni kwa wabunge wote kuanzia CCM na hata Upinzani,
- Kamati ya bunge ya mahesabu ianzishe utaratibu wa kuweka wazi matumizi ya ofisi mbali mbali za serikali na hasa mishahara ya maofisa wa serikali, I mean mimi sikujua kwamba tuna wananchi wanaolipwa mpaka Shillingi Millioni 18, garademiti that is 18,000 USD are you kidding me or what hivi unajua what it takes kwa US government kukulipa hela kama hizo tena monthly?
I mean nilitaka kuu'dissmis huu mjadala, kwa sababu ya kukosekana kwa facts, lakini damn this is a valid national debate Tanzania tunakuwaje na maofisa wa serikali wanaoweza kulipwa US Dollars 18,000 kwa mwezi hela za kodi za wananchi? That is insane, sasa hawa wabunge wanafanya nini huko bungeni zaidi ya kwenda kukusanya pay day tu, yes hili la nyumba ya Spika ingawa halina anything to do na yeye binafsi as a leader kisheria, lakini ni justified tena 100% kulijadili as a starting point against matumizi mbaya ya hela za kodi za wananchi.
Respect.
Kamanda FMEs!
Kwanini katika kupunguza matumizi na kuleta mantiki tusiamue kupunguza matumizi kwa viongozi wote wa umma kuanzia Rais, Makamu, Majaji, Wakuu wa majeshi, vyombo vya umma, Wabunge n.k Hiyo ndiyo movement ya kuungwa mkono; lakini hii ya kuchagua mtu mmoja tu...
Wakati wanafunzi wa Chuo Kikuu walipoandamana kwenda Ikulu ya Nyerere mwanzoni mwa miaka ya 70 kupinga kulazimishwa kuingia JKT na wakidai kuwa kama wataenda JKT basi muda watakaokuwa kule walipwa kama watumishi wa umma, Nyerere aliamuru mishahara ya watumishi wote ikatwe kwani inaonekana ni anasa. Na mishahara yote ikakatwa ili kupunguza hisia kuwa kuna watu wanaishi kifahari mno kutokana na mishahara yao.
Kama tunataka kumkatia "Spita" matumizi ili kuonesha kuwa tunajali hali ya maisha ya watu na kuleta nidhamu ya fedha.. tukate matumizi ya serikali nzima. Lakini ili tujue tunachokata ni kiasi gani hatuna budi kujua viongozi wengine wote wanalipwa kiasi gani, mapango, na pecks nyingine.
Hapa tuwaangalie viongozi wafuatao tu na mtu yeyote mwenye data atumwagie hapa:
Rais
Makamu wa Rais
Waziri Mkuu
Rais wa Zanzibar
Spika na Naibu wake
Mawaziri
Manaibu Waziri
Wakuu wa Majeshi (JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa, Magereza n.k)
Wabunge wote
Wakurugenzi wa taasisi za umma wanaoteuliwa
wanalipwa mshahara wa kiasi gani?
Je wanalipwa posho ya kiasi gani kwa safari ya ndani au ya nje?
Je mawaziri wanapopangishwa nyumba huwa wanalipa kiasi gani?
Pecks zao nyingine ni zipi?
Mkuu, nilichounga mkono kwa Yahya Husein ni uhuru wake wa kutoa maoni kama watanzania wengine, hayo mengine ni yake mwenyewe usinihusishe nayo, Nabii wangu mm ni Muhammad (s.a.w), ambaye ndo kigezo kwangu, Upo!!Huyu Sheikh ndo Nabii wa akina JUNIUS!!!
Kwanza huyu sheikh anaShirki ambayo katika dini ya kiislamu haitakiwi. Pili nilimuona LIVE siku hiyo kupitia kwa Msaidizi wake ALIUUNGA MKONO WARAKA HUO!
Sasa huyo mwandishi na bwana Junius sijui wanataka kupindisha nini hapa,
Kuchanganya Mahakama ya Kadhi na WARAKA ni sawa na kuchanganya maji na Chuma ukitegemea vita ungana!!
Hata Bakwata wameunga mkono WARAKA huo!
Mkuu, nilichounga mkono kwa Yahya Husein ni uhuru wake wa kutoa maoni kama watanzania wengine, hayo mengine ni yake mwenyewe usinihusishe nayo, Nabii wangu mm ni Muhammad (s.a.w), ambaye ndo kigezo kwangu, Upo!!
Wakuu,
Naomba tuangalie yafuatayo kabla ya kuhitimisha :
Nafasi ya nyumba ...yaani ipo kwenye kiwanja chenye ukubwa kiasi gani. Kwa kutizama picha hiyo nyumba imejengwa karibu sana na ukuta, haina nafasi mbele sijui kwa nyuma.
Nyumba ina accessories muhimu kama Swimming pool na ya ukubwa gani?, Jakuzi? au (ndo mojawapo ya iliyonunuliwa na Million 200).
Nyumba ina ka kiwanja cha basket au ina Gym?
Angalia mengineo, ipo close na bahari au eneo lisilo na nyumba karibu na hapo kuwa na hewa safi.
Nyumba ambayo ina sifa nilizotaja hapo juu ninayojua ililipiwa kodi ya Dollar 6000 tena ilikuwa kampuni inamkodishia Expatriate wa ngazi ya juu.
Uzoefu wangu unaniambia kuwa kati ya nyumba NNE ninazozijua ambazo wamepangiwa washkaji zangu wa kigeni kwenye eneo la Masaki bei ni USD 3000 mpaka 5000 USD.
Jamani sijaona zaidi ya USD 6000. Sasa hii mi sijui. Halafu pia kupangisha nyumba kwa THIRD PARTY WAS UNPROFESSIONAL kwa nchi kama Tanzania (sector ya agency ni changa), kwasababu for sure Margin inaongezeka. Ninaamini wafanyakazi wa Bunge wana uzoefu...
Ila kabla ya kuingia NDANI naweza kusema HAPO VALUE FOR MONEY HAMNA.
Asanteni