Sura-ya-Kwanza
JF-Expert Member
- Nov 17, 2007
- 568
- 12
Hapa ndipo tutakapo zikumbuka nyumba za serikali, hiyo Government Agency ya serikali ilitakiwa kuanza mkakati wa kubomoa nyumba za zamani na kujenga Maflay ambayo yangeweza kuweka wafanyakazi wengi zaidi na kutengeneza mazingira ya maeneo hayo, na pale wafanyakazi wa serikali wakiamua kuka katika nyumba zao, basi hizoi nyumba zingepangishwa kwa mtu yoyote, mradi pesa ya muhusika, kuhusu viongozi wanao stahili nyumba za serikali kutokana na nafasi zao basi wangelazimishwa kuka katika nyumba stahili ambazo zinamilikiwa na serikali, kama Mkuu wa jeshi, polisi, Mkuu wa Chuo Kikuu, Spika, Raisi , makamu wa Raisi, Waziri Mkuu etc au wafanye study wa nchi zingine wanavyo wapatia nyumba viongozi husika, au hiyo housing allowance. Na kwa kweli kiongozi atakaye shinda uchaguzi mwaka 2010 itabidi afanye mkakati huo wa kuona njia iliyo bora ya serikali kuwa na nyumba stahili kwa baadhi ya watumishi wake au ndio system ya Chuo kikuu ya Housing allowance ya 1m ni ipi inafaa? kuwapa mtaji zaidi hao government agency au tupeane mkononi kila mtu akajenge nyumba yake kwa kutumia hiyo housing allowance.
Masikini hajijui. Tukishaanza kujitambua kuwa sisi ni masikini basi hapo ndiyo tu-discuss maendeleo! Kwa sasa tunampigia ng'ombe filimbi!
Spika Sitta aandamwa
na Mwandishi Wetu
- Sasa ahusishwa kwa matumizi makubwa
Spika ana stahili zake kama Spika, hivyo kulipiwa kodi ya pango kwa dola 8,000 kwa mwezi na samani zake za ndani kugharimu zaidi ya sh mil 200 si jambo la ajabu. Ni kiongozi mwenye hadhi hiyo. Rais anajua, ndiye anayeidhinisha stahili zote za Spika. Hivyo hakuna jambo la ajabu hapo, alisema Shellukindo.
Chanzo: Tanzania Daima
Bomba sana, leo nimetembelea bandara ya Mtwara iliyotelekezwa. Hii bandari ingetumika kidogo tu inge-turn around kabisa maisha ya hawa wamakonde hapa, lakini wapi bana!!
Lakini maisha magumu sana hapa, hotel sh 60,000, ugali/chips/wali kuku 8000-Mtwara!!
Anyway achana na hizi habari wewe, mada hapa ni Spika Sitta-sasa mambo ya Mtwara unayaleta ya nini hapa.
Unaambiwa Spika kupangishiwa nyumba ya dola 8,000, thamani za dola 200,000, benzi ya dola 300,000 katika nchi ambayo asilimia zaidi ya 50 ya wananchi wake wanapata chini ya dola 1 kwa siku ni UFISADI ULIOTUKUKA, mimi nakubali wewe unasemaji? Changia mada hii usilete longolongo!
Mbona Adam Sapi Mkwawa alikuwa anakaa nyumba ya kawaida tu relatively speaking pale nyuma ya ubalozi wa Marekani wa zamani (Laibon) na alikuwa Spika mzuri tu?
how much does it cost to buy spika's house i thought 100 - 200million u get very classic house tena dodoma. this is how our leaders are very illiterate. why do they simple buy a house for him! wameshatumia zaidi ya million210 but still they dont have spika's house. wanatucheze 2010 we have to show them they way. huyu spika siamatoka tabora hadhi upi apewe mtu watabora huu. ile nyumba ya serikali tena ilipewa bure kwa nini isimtoshe hamna akili kabisa huyu mzee kwani hakukata .......
Yaani, kama analipiwa dola 8000 kwa miezi 18 iliyobakia na exchange rateya 1200 tsh.. ina maana hadi ikiisha miezi hiyo itakuwa imegharimu 172.8 milioni. Ukiongeza na hizo za samani, ni 372.8.
Je tunaweza kujenga nyumba ya serikali ambayo itatumiwa na maspika wote wa sasa na hao wajao na ikawa na hadhi ya Spika. If we can't.. then we more than screwed!
8,000 x 12 x 5 = usd 480,000 in five years only housing; kweli masikini hajijui kuwa ni masikini; hata akili haifanyi kazi. Hata Raisi hana akili![/QUOTE]
Mkuu hapo mmmh, Heri mimi sijaesema aaaahh aahaha aaaaha.
Kwa mtazamo wangu nafikiri Raisi ana akili ila busara ndo MPATUPU. Watu wanaomzunguka ni bure kabisa. Huwezi kufanya hivi vitu kama huna 10% kickbacks, hapa kuna samsing'