Ni taratibu gani za kuuza kiwanja kilichowekwa kama dhamana zinazotakiwa kufuata baada ya mkopaji kushindwa kulipa deni?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,256
2,000
Naomba kuuliza iwapo mtu amekopa fedha na akaweka kiwanja kama dhamana na kukawa na mkataba wa maandishi kuwa akishindwa kulipa deni basi kiwanja alichoweka Kama dhamana kitachukuliwa na kuwa mali ya mkopeshaji na ambachi atakiuza ili kulipia deni.

Kwa mfano,hata kama mkataba unamruhusu mkopeshaji kuchukua kiwanja husika kama mali yake ili aweze kukiuza kurudisha hela yake,ni lazima apate kibali cha mahakama?

Pia, kwa wanaofanya biashara hii ya kukopesha kama watu binafsi na bila kusajiliwa na bila kulipa kodi ya serikali,wana uhalal kisheriai wa kuchukua dhamana ya mkopaji na kuiza ili kufidia deni?

Na mamlaka za utoaji wa hati zinatakiwa kupata/kupewa document gani ili kubadilisha umiliki wa kiwanja kwa mtu alieshindwa kulipa deni?

Je, mamlaka zitatumia mkataba wa kukopeshana tu kuhamisha umiliki?

Nini nafasi ya mdaiwa katika jambo hili?

Je, ni lazima nae ahusishwe?

Kama mdaiwa amegoma kuhusishwa,mkopeshaji anatakiwa afanye nini ili aweze kuuza kiwanja kihalali?

Na mbali na hati za viwanja,hali ikoje kwa vitu kama kadi za vyombo vya moto(gari,pikipiki,n.k) vilivyowekwa kama dhamana?
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
24,156
2,000
Kwa mujibu wa sheria za Ardhi ni marufuku kutwaa ardhi au nyumba ya mtu bila amri ya mahakama
Benki itakupa notisi,itakupeleka mahakamani kukushitaki,ukishindwa kesi,mahakama itaamuru mali yako iuzwe
Ni kinyume cha sheria kuweka dhamana ya ardhi nyumba bila ya kumsainisha mke na mume,endapo mume hana mke itabidi aape kwanza(affidavit) kwamba hana mke
Ni kinyume cha sheria za JMT kuanzisha biashara ya kukopesha bila ya kibali cha BoT
 
King999

JF-Expert Member
Aug 15, 2019
1,517

hapa ndo sintofahamu inapoanzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abdallahkova

JF-Expert Member
Apr 19, 2017
1,138
2,000
Kwa mujibu wa sheria za Ardhi ni marufuku kutwaa ardhi au nyumba ya mtu bila amri ya mahakama
Benki itakupa notisi,itakupeleka mahakamani kukushitaki,ukishindwa kesi,mahakama itaamuru mali yako iuzwe
Ni kinyume cha sheria kuweka dhamana ya ardhi nyumba bila ya kumsainisha mke na mume,endapo mume hana mke itabidi aape kwanza(affidavit) kwamba hana mke
Ni kinyume cha sheria za JMT kuanzisha biashara ya kukopesha bila ya kibali cha BoT
Hakuna sheria inasema hivo .bank inafata sheria za bot .mkopaji ukivunja mkataba unaletewa notice ya siku 60 yakulipa deni lote .usipolipa anaandikiwa dalali barua yakukusanya deni. Dalali anakuletea notice tena yasiku 7 .usikupo lipa anakutoa Kwenye gazeti kwa siku 7 tena .kisha anauza dhamana. Inshu yamahakama landa mdaiwa akafungue kesi apewe zuio na mahakama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
24,156
2,000
Hakuna sheria inasema hivo .bank inafata sheria za bot .mkopaji ukivunja mkataba unaletewa notice ya siku 60 yakulipa deni lote .usipolipa anaandikiwa dalali barua yakukusanya deni. Dalali anakuletea notice tena yasiku 7 .usikupo lipa anakutoa Kwenye gazeti kwa siku 7 tena .kisha anauza dhamana. Inshu yamahakama landa mdaiwa akafungue kesi apewe zuio na mahakama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Zingeuzwa nyumba nyingi sana kama ni hivyo ulivyoandika
Jaribu kuputia sheria ya ardhi,Tanzania huwezi piga mnada ardhi bila ya ruhusa ya mahakama
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom