Ukishindwa kulipa mkopo, Bank hairuhusiwi kisheria kuuza mali ambazo hazikua sehemu ya makubaliano ya dhamana ya kuchukulia mkopo

Apr 26, 2022
64
100
Ukishindwa kulipa mkopo, kuna njia nyingi za benki ku recover (kujilipa) hela yao. Mojawapo ni kuuza mali uliyoweka kama dhamana (security).

Sasa ikitokea benki wameamua kuuza mali yako ili kulipa deni la mkopo uliochukua kwao, mojawapo ya masharti ni kwamba, wanatakiwa kuuza ile mali tu mliyokubaliana itumike kama dhamana kwenye makubaliano yenu ya mkopo (loan/facility agreement).

Kama bank wakiuza mali yako uliyoweka dhamana ikawa bahati mbaya haijatosha kumaliza deni wanalokudai, hawaruhusiwi kurudi tena Mahakamani kuomba kukamata na kupiga mnada mali zako zingine ili kumalizia deni la mkopo lililobaki.

Mali ambazo sio sehemu ya makubaliano ya kuchukulia mkopo, haziwezi kupigwa mnada na benki ili kumalizia deni la mkopo.

Haya ninayosema ni kwa mujibu wa maamuzi mbalimbali ya Mahakama ya Tanzania, ikiwemo uamuzi wa Mahakama Kuu, kwenye kesi ya REHEMA JOHN MUSH dhidi ya NATIONAL MICROFINANCE BANK (NMB), RUFAA YA MADAI NAMBA 79 YA MWAKA 2022. (Mbele ya Mheshimiwa Jaji Kakolaki).

(Ikumbukwe kwamba, maamuzi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa NI SHERIA nchini Tanzania, kama tu hayajatenguliwa na Mahakama yenye Mamlaka kwenye kesi nyingine).

Kitu kingine benki (mkopeshaji) anatakiwa kutoa notice kabla ya kupiga mnada mali yako. Swali, hiyo notice inatakiwa iwe siku ngapi na nini matokeo au madhara ikiwa benki watauza tu bila kukupa au kutoa notice?

Elimu hii ya sheria bure imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke - 0754575246 (WhatsApp) zakariamaseke@gmail.com
(Advocate Candidate).
 
Back
Top Bottom