Kenya: Ajiua baada ya kushindwa kulipa deni la 520000/=

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
MWANAUME wa miaka 40, mkazi wa Kijiji cha Manyata katika Kaunti ya Murang’a, anadaiwa kujitoa uhai kwa ajili ya kukwepa deni la Ksh 30, 000 ambayo ni sawa na Sh 520, 000 za Tanzania ambalo linadaiwa kuwa ni rushwa kwa polisi wa Kituo cha Sabasaba.

===
Mwanaume wa miaka 40, mkazi wa Kijiji cha Manyata katika Kaunti ya Murang’a, anadaiwa kujitoa uhai kukwepa deni la Sh30, 000 (sawa na Sh520, 000 za Tanzania) ambalo linadaiwa kuwa rushwa kwa polisi wa Kituo cha Sabasaba.

Kwa mujibu wa msemaji wa kamati ya marafiki kuhusu maziko ya ndugu huyo aliyejulikana na kwa jina la Joseph Murigi, imeelezwa kuwa polisi hao walikuwa wakimdai hongo, ili wasimshtaki kwa hatia ya kupiga picha za ‘aibu’ mitandaoni.

“Murigi alikuwa na kashfa fulani kutoka kwa mpenzi wake. Picha za aibu za mpenzi huyo zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii na akaorodheshwa kama mshukiwa mkuu,” amesema James Guchu ambaye ni msemaji wa kamati hiyo.

Guchu aliongeza kuwa, baada ya mwanamke huyo kuripoti katika kituo cha polisi cha Sabasaba, Murigi alianza kutafutwa ili atiwe mbaroni.

“Polisi walifanikiwa kumkamata na kumfikisha kituoni kwao hapo Sabasaba, ambapo kesi iliandaliwa kienyeji na hivyo kukutwa na hatia. Aliamriwa kulipa faini ya Sh30, 000; ambazo zilikuwa zikabidhiwe kwa mkuu wa kituo,” amesema.

Kwa kuwa marehemu hakuwa na pesa hizo, inadaiwa kwamba baadhi ya marafiki na familia kwa pamoja tulichangishana fedha ya haraka na kufanikiwa kupata Sh15, 000.

“Murigi aliachiwa kwa dhamana hata hivyo alitakiwa kumalizia pesa iliyokuwa imebaki kabla ya Agosti 7, 2023. Hata hivyo, marehemu alisisitiza kuwa, hakuhusika katika kusambaza picha hizo na kwamba ametiwa hatiani bila ushahidi wa kumhusisha kutolewa,” amesema Guchu.

Kwa upande wake, Evanson Njogu ambaye ni baba wa marehemu, ameiambia Taifa Leo Dijitali, kwamba alipigiwa simu na maofisa wa polisi wa Nanyuki Agosti 10, mwaka huu; akielezwa kuwa mwanae alikuwa amejinyonga.

Kuhusiana na deni la polisi, Njogu amesema kuwa anaelewa juu ya sakata hilo la mwanane kutuhumiwa kusambaza picha za mpenzi wake kama ilivyoripotiwa na polisi lakini pia anafahamu juu ya hiyo faini, huku akisema: “mimi mwenyewe ndiye nilikabidhi maafisa hao hizo pesa.”

Hata hivyo, amesema kwamba sakata hiyo ilimsababishia mwanae msongo wa mawazo, ambapo anadhani ndiyo chanzo cha yeye kusafiri kwenda Nanyuki ili akajitoe uhai wake.

Amesema, “Alikuwa ameapa kutoroka ili asikamatwe tena huku akitafuta pesa zilizosalia za hongo ya polisi hao.”

Kwa mujibu wa Njogu, mwanae alikuwa akifanya kazi kama karani katika kampuni moja Maragua na kukimbia kwake ili asikamatwe na askari ilikuwa sawa na kuacha kazi.

Familia ya marehemu inawalaumu polisi wa Sabasaba kwa maafa ya mtoto wao, wakiwasema kama ni wenye tamaa na wabinafsi.

Alipotafutwa ili kuthibitisha au kukana tuhuma hizo, Naibu Kamishna wa Polisi Murang’a Kusini, Gitonga Murungi, amekataa kuongea na vyombo vya habari kuhusu suala hilo.

“Sasa tunamtaka Mbunge wetu, Mary wa Maua na viongozi wengine wote wa Kaunti hii waungane kukemea ukatili huu wa maafisa wa polisi. Hii tamaa ya hongo na kupiganisha jamii ili wapate vya haramu imekuwa janga,” amesema Kasisi Simon Njoroge wa Kanisa la Mwito wa Israeli, Murang’a.
 
Back
Top Bottom