Mnada wa benki baada ya kuuzwa mali yako unaweza kubatilishwa kwa mambo mawili makuu

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,562
MNADA WA BENKI BAADA YA KUUZWA MALI YAKO UNAWEZA KUBATILISHWA KWA MAMBO MAWILI MAKUU.

Na Bashir Yakub, WAKILI
+255714047241.

Kushindwa kulipa deni hakuhalalishi ukiukaji wa haki za msingi za mkopaji. Mkopaji pamoja na kuwa ameshindwa kulipa deni kwasababu zozote zile bado analindwa na sheria katika haki alizonazo.

Kuanzia kushindwa kufanya marejesho mpaka kuuza mali ya mdeni kwa nnada kuna taratibu za kisheiria lazima zifuatwe.

Kwanza lazima iwe ni kweli kashindwa kufanya marejesho na yuko nje ya muda, notisi ya siku 60 ya kushindwa kufanya marejesho(default notice), matangazo ya kuuza(public advertisement), notisi ya siku 14 ya kuuza, matangazo ya mnada siku ya mnada, kuhakikisha mali inauzwa bei nzuri ya soko, mnunuzi kulipa 25% siku ya mnada na kumalizia 75% baada ya siku 14, kama kuna fedha imebaki baada ya mauzo(chenji) kumrudishia mliyeuza mali yake, nk,nk.

Hizi ni taratibu kwa mujibu Sheria ya Ardhi Sura ya 113, Sheria ya Madalali (wa Minada) Sura ya 227, Sheria ya Mikataba Sura ya 345, Sheria ya Rehani(The Motgage Financing Special Provision Act, No.17/2008.

Moja ya maeneo ambayo Mahakama ya rufaa imeweka wazi kuwa yanabatilisha mnada ni rushwaCorruption) na nia ovu(collusion) katika uuzaji wa mali ya mkopaji.

Nia ovu ni pamoja na njama na udanganyifu katika mchakato mzima wa mnada.

Ikiwa nyumba yako, kiwanja chako kimeuzwa na haya yalitokea basi unayo haki ya kutafuta msaada wa mahakama ili mnada uweze kubatilishwa.

Zipo baadhi ya taasisi za fedha pamoja na madalali wasio waaminifu hujiingiza katika matendo hayo mabaya na kuuza mali za mdeni kwa hila. Hawa wanakuwa wamekosea na huo mnada unatakiwa uhesabike batili.

Mahakama ya rufaa imeyasema haya katika mashauri mengi ikiwemo THE NATIONAL BANK OF COMMERCE vs DAR ES SALAAM EDUCATION & STATIONERY (1995)TLR 292, MAIMUNA K
MUSA SAGAMIKO vs AFRICAN BANKING COOPERATION, LAND CASE No.193/2015, JM HAULIERS LTD vs ACCESS MICROFINANCE BANK , CIVIL APPEAL No.274/2021 na nyingine nyingi.

Muhimu ni kuwa hata kama mdaiwa ameshindwa kulipa deni lazima sheria zifuatwe katika kumalizana naye.

Kwahiyo yule ambaye anahisi kuonewa anayo haki ya wazi kushitaki akiomba kubatilishwa mnada.
 
Mfano mtumishi wa umma amechukua mkopo benki kwa dhamana ya ajira yani mwajiri marejesho ni ndani ya miaka mitano. Mwajiri kaamua kusitisha mkataba kabla mwajiriwa haja-clear deni.

Je kisheria benki ina haki ya kumdai mwajiriwa au mwajiri aliyedhamini mkopo.
 
Ikitokea mdaiwa akapata hela wakati mnada unaendelea ila bado haujahitimishwa, anaweza kwenda kuusimamisha?
 
Bunge ndio linacover deni, hata Tundu Lisu alipovuliwa ubunge akuwahi kuulizwa deni mpaka pale Rais alipotowa Amri Lisu alipwe haki zake ndio ofisi ya bunge ikakata na madeni yake ya benki.

Lisu asingelipwa haki zake na hilo deni hasingelipa.
Sheria ya Ndoa ya 1971 inampa ruhusa Mke Kukopa kwa Jina la Mume... Mke kakopa kisha ndoa ikavunjika kabla hajaCLEAR deni! Nani wa kubeba hilo deni?
 
Nadhani kuna some amendment hasa kwenye sheria ya Ardhi ni lazima wenzake wote wahusike kabla ya kufanya chochote.

Wife wangu alikuwa na plot yake binafsi mkoani, alipotaka kuuza ilibidi kuna form kwa Advocate Mimi nilikwenda kujaza na kusaini kwamba nalidhia plot hiyo kuuzwa, licha kwamba ni Mali yake binafsi.
 
Mfano mtumishi wa umma amechukua mkopo benki kwa dhamana ya ajira yani mwajiri marejesho ni ndani ya miaka mitano. Mwajiri kaamua kusitisha mkataba kabla mwajiriwa haja-clear deni.

Je kisheria benki ina haki ya kumdai mwajiriwa au mwajiri aliyedhamini mkopo.
Ndo maana ya kua na bima ya mkopo kwa mtumishi,kabla ya kulipwa pesa yote uliomba kukopa huwa wanakata % kadhaa kulingana na mkopo uliomba hii itafidia ukiwa utapatwa na kifo au kufukuzwa kazi nk
 
Back
Top Bottom