Mnada wa Benki baada ya kuuzwa mali yako unaweza kubatilishwa kwa mambo mawili makuu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Kushindwa kulipa deni hakuhalalishi ukiukaji wa haki za msingi za mkopaji. Mkopaji pamoja na kuwa ameshindwa kulipa deni kwasababu zozote zile bado analindwa na sheria katika haki alizonazo.

Kuanzia kushindwa kufanya marejesho mpaka kuuza mali ya mdeni kwa nnada kuna taratibu za kisheiria lazima zifuatwe.

Kwanza lazima iwe ni kweli kashindwa kufanya marejesho na yuko nje ya muda, notisi ya siku 60 ya kushindwa kufanya marejesho(default notice), matangazo ya kuuza(public advertisement), notisi ya siku 14 ya kuuza, matangazo ya mnada siku ya mnada, kuhakikisha mali inauzwa bei nzuri ya soko, mnunuzi kulipa 25% siku ya mnada na kumalizia 75% baada ya siku 14, kama kuna fedha imebaki baada ya mauzo(chenji) kumrudishia mliyeuza mali yake, nk,nk.

Hizi ni taratibu kwa mujibu Sheria ya Ardhi Sura ya 113, Sheria ya Madalali (wa Minada) Sura ya 227, Sheria ya Mikataba Sura ya 345, Sheria ya Rehani(The Motgage Financing Special Provision Act, No.17/2008.

Moja ya maeneo ambayo Mahakama ya rufaa imeweka wazi kuwa yanabatilisha mnada ni rushwaCorruption) na nia ovu(collusion) katika uuzaji wa mali ya mkopaji.

Nia ovu ni pamoja na njama na udanganyifu katika mchakato mzima wa mnada.

Ikiwa nyumba yako, kiwanja chako kimeuzwa na haya yalitokea basi unayo haki ya kutafuta msaada wa mahakama ili mnada uweze kubatilishwa.

Zipo baadhi ya taasisi za fedha pamoja na madalali wasio waaminifu hujiingiza katika matendo hayo mabaya na kuuza mali za mdeni kwa hila. Hawa wanakuwa wamekosea na huo mnada unatakiwa uhesabike batili.

Mahakama ya rufaa imeyasema haya katika mashauri mengi ikiwemo THE NATIONAL BANK OF COMMERCE vs DAR ES SALAAM EDUCATION & STATIONERY (1995)TLR 292, MAIMUNA K
MUSA SAGAMIKO vs AFRICAN BANKING COOPERATION, LAND CASE No.193/2015, JM HAULIERS LTD vs ACCESS MICROFINANCE BANK , CIVIL APPEAL No.274/2021 na nyingine nyingi.

Muhimu ni kuwa hata kama mdaiwa ameshindwa kulipa deni lazima sheria zifuatwe katika kumalizana naye.

Kwahiyo yule ambaye anahisi kuonewa anayo haki ya wazi kushitaki akiomba kubatilishwa mnada.

Andiko la: Bashir Yakub, WAKILI +255714047241.
 
Baada ya Mahakama kunirudishia aridhi yangu,Wale wote walio shiriki kwenye udanganyifu huo lazima niwaburuze Mahakama ya Jinai nikiwa na team ya Wataalamu wa Jinai; DCI pamoja na DPP nyuma yangu! hapo hachomoki Mtu hata Kama Wana mkwanja kiasi gani!!
 
Back
Top Bottom