Ni sawa dalali kufanya kazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa?

Hujaeleweka mkuu.

Yaani jamaa anafanya kazi kwa mkuu wa mkoa ila baadae akiwa nje ya ofisi anafanya kazi ya udalali?

Au ni dalali ila kazi hiyo anaifanyia kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa? (Kwamba amepanga chumba hapo au anakaa kabisa ofisi ya mkuu wa mkoa akifanya shughuli zake za udalali?

Kama suala ni ishu ya kwanza. Ni sahihi kwa mtumishi wa umma kuwa na kazi ya ngongeza nje ya kazi yake rasmi.
 
Kwa taratibu na sheria za kazi si sahihi kabisa! Kibongobongo na kula kwa urefu wa kamba haina noma kabisa
Sio sahihi kivipi, udalali wa gari ni kazi ya part time ambayo dalali anaiganya kwa simu tu huku akiwa anafanya kazi nyingine, na ni kazi halali
Sio sahihi kwa nini?
 
Sema ni mstari mwembamba sana unamtenganisha Dalali na Tapeli...,
Kua dalali kunakaribisha janja janja, Uongo, ambavyo ni vitu tofauti na utumishi....
Otherwise SIONI kosa.
Mimi kazi yangu inanohisha na madalali wa magari mara nyingi, madalali matapeli ni wachache sana, actually sijawahi kukutana hata na mmoja
Hata kama wapo hakuna kazi ambayo haina watu wabaya
 
Huyo ni consultant.... Ukiiweka hivyo inakuwa poa...lakini ukisema dalali ndio inaleta ukakasi na itamletea shida..udalali no ujanja ujanja atajikuta anakesi kibao na kaz kwisha
 
Sentesi tata hiyo.


Je dalali ni mtumishi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa baada ya kazi anajishughulisha na udalali?

Je Kuna dalali wa mtaani anafanya kazi za udalali kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa?

Hueleweki.
 
Back
Top Bottom