Ni sahihi kujenga kwenye kiwanja cha mkeo?

Ni sahihi kujenga kwenye kiwanja cha mkeo?

Kama mume anaogopa kutendwa akijwnga kiwanja cha mkewe

Kwa nini mke asiogope kutendwa kwa kubadili ownership

Kwanza kwa nini abadili??????

Kwa mtazamo wa aina hii ndoa ni ngumu sana aisee......

Hizi ndoa za siku hizi sijui zinaumwa nini walah...... wanandoa wakishakuwa na hofu za namna hii kunakuwa na ufa usioonekana, wa kimya kimya


Hilo la mke na mume kila mtu kufanya yake ndani ya ndoa siliafiki hata siku moja. Bado ushauri wa Eli79 nauona umetulia. Kingine ni mke kukubali kubadili ownership bila kurudishiwa pesa ili wajenge pamoja kwenye Kiwanja chao.


Au mie ndio nina mtazamo wa kizamani?????
 
Habar za muda na wakati.kama huuu ndugu msomaji.
Leo napenda unipe uzur, ubaya, tahadhar au chochote ktk hili.
mke wangu anakiwanja ambacho alikinunua kabla hatujawa pamoja na sasa nipo nae anataka tujenge kwenye kiwanja chake mi nimegoma sijakubaliana na hili.
vp wadau hili linakaaje?

Ngoja akunyime kile kitu anacho wewe huna kwa muda wa mieizi 3 utaenda kujenga tu wala hutakumbuka kuja kuuliza hapa tena.
 
Jenga tu kwani uwoga wa nini? Kama ni mke wako na ikitokea mkaachana si kuna sheria za nchi ambazo zinaamua ya kwamba mali ni 50/50 sasa wasi wasi wako ni nini?
Maadamu mmeoana kisheria Kiwanja chake ni chako pia hivyo hakuna kitu anachoweza kukufanya angalau kisheria!

Yaaani yaani narudia Bora kusomesha mchumba kuliko kujenga kwenye hicho kiwanja ushauri wa Buuure kabisa bora mkabadili jina mkaandika la mtoto wenu ndiyo ujenge mimi wife ana kiwanja huu ni mwaka wa saba majirani wanalima huko maharagwe siwezi jenga kabisa hawa watu ni hatari bora kuishi nao kwa akili.
 
Badilisha jina la kiwanja kwanza,andika la kwenu wote kisha ndo mjenge...
 
Si mtazamo wa kizamani hata kidogo, hivyo ndivyo inatakiwa iwe lakini ukiangalia hali halisi ya ndoa hizi za miaka hii wengi wameshalizwa na kubaki na majuto mjukuu. Hivyo ni vizuri kuchukua tahadhari.

Kama mume anaogopa kutendwa akijwnga kiwanja cha mkewe

Kwa nini mke asiogope kutendwa kwa kubadili ownership

Kwanza kwa nini abadili??????

Kwa mtazamo wa aina hii ndoa ni ngumu sana aisee......

Hizi ndoa za siku hizi sijui zinaumwa nini walah...... wanandoa wakishakuwa na hofu za namna hii kunakuwa na ufa usioonekana, wa kimya kimya





Au mie ndio nina mtazamo wa kizamani?????
 
Achana na Mawazo ta kitoto. Jenga nyumba, muishi kwa amani. Mbona hujiamini? Kwani mkiachana ndo we utakufa? Wangapi wamekufa bila nyumba? Kwani mkeo hata mkiachana ukamuachia hiyo nyumba atafaidi mini cha ziada sana zaidi ta kuacha kumbukumbu yako kwake? Think positive kijana 1+1=2 ndo maisha ya Leo. Badilikeni jamani. Mi ni kidume usijefikiri ni mwanamke

Ahaaa ok kumbe ni Kidume maana nimeshangaa sana ingekuwa Dume ningepanic ila umeongea kufuatana na mawazo ya Halmashauri ya akili jinsi ilivyo mkuu ni hivi wewe ni kichwa lazma ufanye maamuzi kiume kama mkeo ana kiwanja anataka mjenge usikatae nunua wewe jenga mshirikishe then kile chake wekeni nyumba ya pili andikeni jina la mtoto weka mpangaji ila eti mimi nimelala kwenye kiwanja cha mke wangu sitakaa nipate usingizi.
 
Binafsi, Nmepewa Kiwanja na Mama Mzazi Maeneo ya Kimara. Lakini kutokana na wenzetu kuumbiwa Roho tofauti na Ss akina Adam, nilikaa siku Moja nikawaza na kuwazua kuwa Je!, siku ambayo Leo au Kesho Sipo, Je Mke wangu atakuwa Salama na Hiyo Property Niliyojenga kwenye Kiwanja nilicho pewa na Mama!? Nikasitisha wazo la Kujenga hapo, nikasema hicho kiwanja nitampatia Mwanangu(Mjukuu wake) Baadae atakapo anza kujitegemea. Nikaenda nikanunua Plot Kinyerezi nikajenga huko.

Kwani wanawake wanatabia ya Kubadilika badilika kama Kinyonga wanapo udhiana wao kwa wao. Anaweza akaudhiana na Mkwe wake akakimbilia kwenda kupokonya alichowagea hata kama ni Miaka mingapi iliyopita.
 
.....Aha ha ha! Baharia muoga siku zote huogopa kuogelea kwenye maji yenye kina kirefu. I don't see the logic here.

Mimi nilianza kujenga nyumba kabla hatujaoana, wife nae alikuwa na kiwanja kabla hatujaoana baada ya kuoana na kuwa na familia tumejenga nyumba kwenye kiwanja cha wife kwahiyo sasa hivi tunasema tuna nyumba 2. Usiwe muoga katika kufanya jambo la maendeleo kwa familia yako kutokana na ubinafsi, uoga na uchoyo wako.

Tusiwe wabinafsi, kwani tunavyojenga kinafswenye viwanja vyetu wanaume lengo ni baadae tukiachana tuwanyanyase wenzetu? Mpende mke wako na mwanao kama yupo na naamini mmeoana ili muishi pamoja, hata siku moja usiwaze kuhusu kuachana.

Naamini Mungu akikupa mke, akipanga mje kuachana basi atakupa uwezo zaidi wa kutafuta mali nyingine tofauti na hiyo nyumba.

kwenye furaha kwani kuna matatizo sheikh?...hakuna! matatizo huanza kunapokuwa na mafarakano. nyumba unayojenga wewe mwanaume wala hauwezi kumnyanyasia mkeo hata mkifarakana kwa sababu inaeleweka wazi kwamba ikilazimu kuachana MTAGAWANA, hata kama mwenzio amechangia sifuri wala huwezi kumnyanyasa sheria inamlinda. sasa ndugu yetu hapo kakuta mwanamke anamiliki kiwanja kabla ya kumwoa, hiyo ni mali ya binafsi wala haina uhusiano na familia, mkifarakana mwenzio ana hati we una maneno...utaramba chumvi!
 
Hahhahahaaa.nimecheka sana hii jama.duh!eti chukua nyumba yako.lol

Ndo manake, Nyie Ke Sijui huwa mna matatizo gani... Yani mkishika vichenji huwa mnakuwaga na dharau kweli
Tena hasa ukigundua unamzidi Me kipato ndo kabisaa...!

Nasema hivyo kwasababu nimeshuhudia!
:confused2:
 
Wanaume bana
Ingekuwa kiwanja chake mkewe angehangaika heacen n earth wajenge

Ila cha mkewe full kumtisha...... insecurity kibaaaao

Hebu acheni ubinafsi

Mnawavunja mioyo wake zenu wanaojitoa kwa ajili yenu kwa hali na mali... maana hapo mke anajua kumbe mwenzangu yupo mguu nje mguu ndani

Tatizo sio ubinafsi elewa bibie, Tatizo ni dharau pindi likitokea la kutokea..
Kwanza ukijenga kwenye kiwanja cha mwanamke mtu unakuwa hujiamini, Kunamaamuzi magumu na kauli kama mwanaume utashindwa kuzitoa kwa kuhofia kuvuruga..!

Alafu kingine wanawake wa siku hizi ni mmekuwa tofauti kabisa na zamani, yaani ni mmekuwa majehuri, Viburi na Majivuno ndo mana huwa tunaweka Precaution mbele.
 
Maana wanaosema wabadilishe jina au arudiahe nusu fedha ina maana wanaumw nsio hawatengenezI mabalaa ndani ya Ndoa??!!

Ndio wabadilishe tittle deed hiyo kurudishiana nusu ni fair arrangement pia inaonesha mume anathamini mchango na jitihada za mkewe. . . .na appreciation kuwa "it worths the struggle" mke ana hiari ya kupokea au kukataa au akapokea na kusema hii tuanzie msingi. . . . . .

Mabalaa yako mengi pamoja na mmoja kufariki hivi akifa mke wakati all documents ziko kwa jina lake halafu familia yake ikaja kusema nyumba ilikuwa ya mtoto wao hilo sio balaa. . . . .??!!! Muanze mvutano na vikao visivyo mbele wala nyuma kujadili jambo ambalo uliliona kabisa linakuja. . . . .

Ni bora kuishi uhalisia kuliko kiweka kila kitu in the name of love. . . . .

Sheria iliwekwa kuzingatia yote haya na kama kweli mmekubaliana kuishi wote ina ugumu gani kuweka mambo kisheria kwa faida yenu na watoto???!!!
 
Binafsi, Nmepewa Kiwanja na Mama Mzazi Maeneo ya Kimara. Lakini kutokana na wenzetu kuumbiwa Roho tofauti na Ss akina Adam, nilikaa siku Moja nikawaza na kuwazua kuwa Je!, siku ambayo Leo au Kesho Sipo, Je Mke wangu atakuwa Salama na Hiyo Property Niliyojenga kwenye Kiwanja nilicho pewa na Mama!? Nikasitisha wazo la Kujenga hapo, nikasema hicho kiwanja nitampatia Mwanangu(Mjukuu wake) Baadae atakapo anza kujitegemea. Nikaenda nikanunua Plot Kinyerezi nikajenga huko.

Kwani wanawake wanatabia ya Kubadilika badilika kama Kinyonga wanapo udhiana wao kwa wao. Anaweza akaudhiana na Mkwe wake akakimbilia kwenda kupokonya alichowagea hata kama ni Miaka mingapi iliyopita.


Alikupa kiwanja au alikuruhusu kujenga katika eneo lake huyo mama yako??!!
 
Tatizo sio ubinafsi elewa bibie, Tatizo ni dharau pindi likitokea la kutokea..
Kwanza ukijenga kwenye kiwanja cha mwanamke mtu unakuwa hujiamini, Kunamaamuzi magumu na kauli kama mwanaume utashindwa kuzitoa kwa kuhofia kuvuruga..!

Alafu kingine wanawake wa siku hizi ni mmekuwa tofauti kabisa na zamani, yaani ni mmekuwa majehuri, Viburi na Majivuno ndo mana huwa tunaweka Precaution mbele.


Yaani ukijenga katika kiwanja ndio unakuwa hujiamini??!!!
Mkeo arudi tisa usiku ushindwe kuhoji sababu umejenga kiwanjani kwake??!!!

Hebu funguka ni kama sikusomi hivi. . .,. .
 
Akushauri kuwa katika maisha cha mke ni cha kwake, chako ndio chenu. Kwa hiyo kama unataka kummwogezea hela ajenge sawa, lakini mali hiyo itabaki yake. Huwezi kumshinda popote ikitokea mkatofautiana. Inategemea na tabia yake lakini wanawake wote wanana tabia moja kuhusu mali. Mie nilimwogezea wa kwangu hela kama robo tatu ya ujenzi alipomaliza kaka akaomba kukaa kwa muda sasa mwaka wa 15. Nikimuiza akapange ili ipangishwe anasema hawezi kumfukuza kaka yake. Ndivyo walivyo. Ukimfungulia mradi unakuwa wake na hutaona hata mia kutoka kwake. Hiyari ni ya kwako.
 
Yaani ukijenga katika kiwanja ndio unakuwa hujiamini??!!!
Mkeo arudi tisa usiku ushindwe kuhoji sababu umejenga kiwanjani kwake??!!!

Hebu funguka ni kama sikusomi hivi. . .,. .

Mfano mzuri ni huku ninapoishi..,

Kunajamaa flani alijenga kwenye sehemu ya mkewe kipindi alipokuwa kzini,.. Sasa ikaja kutokea zogo kazini akatimuliwa so akawa yuko home tu hana hili wala lile pesa hana wala yani kawa zero.
Sasa mke kawa Jeuri balaa, kila siku vurugu mechi..., Jamaa ilimbidi awe mpoleee kwa kushindwa kujiamini na mkimya lakini mke hakukoma akawa anatoka nje ya ndoa.

Ivi nnavyoandika huu uzi jamaa now kawa mlevi wa GONGO kwa mawazo na vitimbwi vya mkewe.
Kuna siku alijaribu kum-command mkewe la la la laaa mamaa alicharuka huyoo balaa.

Sasa niambie kuna kujiamini huko.

Kujenga kiwanja cha mwanamke sikatai lakini hakikisha mwanaume unakuwa na Makazi uliyoyaandaa wewe kama wewe kwanza ikishindikana kabisa japo hata kiwanja.

Wanawake wa sikuhizi hamtabiriki.
 
Ahaaa ok kumbe ni Kidume maana nimeshangaa sana ingekuwa Dume ningepanic ila umeongea kufuatana na mawazo ya Halmashauri ya akili jinsi ilivyo mkuu ni hivi wewe ni kichwa lazma ufanye maamuzi kiume kama mkeo ana kiwanja anataka mjenge usikatae nunua wewe jenga mshirikishe then kile chake wekeni nyumba ya pili andikeni jina la mtoto weka mpangaji ila eti mimi nimelala kwenye kiwanja cha mke wangu sitakaa nipate usingizi.

Mkuu nimecheka kidogo hapaa...
KunaMijamaa yani huwa hata aibu haina unakuta ipo kwenye nyumba/vyumba vya kupanga vya wake zao alafu haina wasiwasi imerelax kabisaa...
 
Dini yangu imenionya mara nyingi sana kuhusu mwanamke na tabia zake TAFADHALI usijalibu hata kufikilia kujenga kwenye hicho kiwanja
 
Back
Top Bottom