Ni sahihi kujenga kwenye kiwanja cha mkeo?

Ni sahihi kujenga kwenye kiwanja cha mkeo?

Kiwanja kipo eneo gan??...kama kipo eneo zuri zaidi jengeni tu alaf andikishen majina ya watoto kama mnao.

Ila kama kipo eneo la kawaida,uzeni kanunue kingne kwa hela ya pamoja then angushen mjengo
 
Mi najua mkishaoana hakuna mali ya mme wala mke. ni mali zenu wote. Mali za familia. Ndio maana hata ikitokea bahati mbaya mkaachana... sheria huwa wazi.... Mnagawana kwa usawa.

Sasa hii biashara mi nijenge yetu afu nikupe hela ukajenge yako... what the hell?? si bora nikuache na likiwanja lako ujipepee??

Anyway, kwa mfano uliyotoa... well.. I rest my case!

Na mkiamua kuna mali mnaweza kupeana binafsi
 
Hahahaa, umri tu ukikua utajua! Cha mwanaume cha familia, cha mwanamke cha mwanamke, akili ya kuambiwa changanya na yako! MAULA huyo mwanamke alinunua kiwanja kwa njia anazozijua, kabla ya mahusiano na wewe, hatuombei mabaya, lakini kuepusha migogoro tafuteni kiwanja kingine mjenge, kuwa naye wazi kabisa kwamba kuna leo na kesho, licha ya nyie kufarakana mmoja wenu anaweza kuondoka duniani akaacha migogoro! NUNUA UWANJA USINING'INIE KWENYE MGONGO WA MWANAMKE!

kwer kabisa vp kama alinunuliwa na mwanaume b4 ya mm
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wewe jenga alafu siku analeta jamaa anamgonga ukushuhudia then uone kati yako na yeye nani ataondoka kwenye nyumba na virago vyake
 
Si kuna 50/50 mkitimuana jenga tu, ila in case of mila na desturi kikwetu ni nonsense!!
 
Kwangu mimi sion kama ni sahihi jipange ununue chako au mnunue kingine pamoja hicho kiwekeni kama asset tu.yasije yakakukuta usimwamini MTU hasa kwenye mkwanja........
 
Mwee.. Mimi ni mwanamke, nashauri ujenge kwa kiwanja chako hata kama mtasaidiana. Majoritu ya ke ni shidaaaaaaaaa, usije ukalia na nyumba haihamishiki. Jitutumue ununue chako.
 
Sasa hilo si suala dogo tu la kubadilisha umiliki kwa kuongeza jina lako kwenye 'title deed' then mnakuwa washirika. Kama ukiona hilo mkeo halitaki basi jua kuna mbinu chafu nyuma ya pazia. Hivyo suluhu ya kueleweka tafuteni kiwanja kingine cha kununua pamoja na mjenge hapo.
 
.....Aha ha ha! Baharia muoga siku zote huogopa kuogelea kwenye maji yenye kina kirefu. I don't see the logic here.

Mimi nilianza kujenga nyumba kabla hatujaoana, wife nae alikuwa na kiwanja kabla hatujaoana baada ya kuoana na kuwa na familia tumejenga nyumba kwenye kiwanja cha wife kwahiyo sasa hivi tunasema tuna nyumba 2. Usiwe muoga katika kufanya jambo la maendeleo kwa familia yako kutokana na ubinafsi, uoga na uchoyo wako.

Tusiwe wabinafsi, kwani tunavyojenga kinafswenye viwanja vyetu wanaume lengo ni baadae tukiachana tuwanyanyase wenzetu? Mpende mke wako na mwanao kama yupo na naamini mmeoana ili muishi pamoja, hata siku moja usiwaze kuhusu kuachana.

Naamini Mungu akikupa mke, akipanga mje kuachana basi atakupa uwezo zaidi wa kutafuta mali nyingine tofauti na hiyo nyumba.
 
Siyo vibaya ila iwe kwa makubaliano ya kimaandishi kwa kufuata utaratibu sahihi. Ili baadae usije patwa ba majuto ya kusema ningejua hata nisingejenga.
 
Cc BAK eli79

.....Aha ha ha! Baharia muoga siku zote huogopa kuogelea kwenye maji yenye kina kirefu. I don't see the logic here.

Mimi nilianza kujenga nyumba kabla hatujaoana, wife nae alikuwa na kiwanja kabla hatujaoana baada ya kuoana na kuwa na familia tumejenga nyumba kwahiyo sasa hivi tunasema tuna nyumba 2. Usiwe muoga katika kufanya jambo la maendeleo kwa familia yako.

Tusiwe wabinafsi, kwani tunavyojenga kwenye viwanja vyetu wanaume lengo ni baadae tukiachana tuwanyanyase wenzetu? Mpende mke wako na mwanao kama yupo na naamini mmeoana ili muishi pamoja, hata siku moja usiwaze kuhusu kuachana.

Naamini Mungu akikupa mke, akipanga mje kuachana basi atakupa uwezo zaidi wa kutafuta mali nyingine tofauti na hiyo nyumba.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu BADILI TABIA mie ningependa sana kuona mtazamo kama huu katika ndoa nyingi, lakini ukweli ni kwamba balaa linapoingia ndani ya ndoa kuna baadhi hugeuka na kuwa kama wanyama mpaka mtu unashangaa duh! Huyu kweli ndiye mume/mke wangu kweli!? Mbona ana roho mbaya kiasi hiki? Ni bora kuchukua tahadhari mapema badala ya kumuamini mtu 110% halafu akakutenda ukabaki na majuto mjukuu.

Last edited by a moderator:
Sasa kama ndoa ndio zinaenda kwa style ya kujihami inabidi huyu mwanaume anunue kiwanja chake ajenge kwa nguvu zake wahamiw

Mke ajikusanye kwa nguvu zakw ajenge

Maana wanaosema wabadilishe jina au arudiahe nusu fedha ina maana wanaumw nsio hawatengenezI mabalaa ndani ya ndoa???

Kila mtu ahangaikie lake halafu waone kama watasonga mbele

  • Thanks
Reactions: BAK
Usije ukajaribu kwa lugha nzuri unayopewa sasa siku atapokuwa ameungana na ndugu zake anadai kiwanja chake hutaamini huyo aleyekuwa akikushawishi kwa lugha ya upole
 
Hilo la mke na mume kila mtu kufanya yake ndani ya ndoa siliafiki hata siku moja. Bado ushauri wa Eli79 nauona umetulia. Kingine ni mke kukubali kubadili ownership bila kurudishiwa pesa ili wajenge pamoja kwenye Kiwanja chao.

Back
Top Bottom