Ni sababu ipi muhimu sisi wazazi tunakuwa na mtoto zaidi ya mmoja?

Chance ndoto

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
2,990
7,100
Habari za muda huu ndugu zangu. Nimekaa, nikafikiria, Mimi ni mzazi wa mtoto mmoja wa kike.

Sasa issue kubwa nataka kufahamu nimeona kama nimeridhika au sina sababu maalumu ya kuongeza mtoto. Najiweza sana kiuchumi, mimi kijana mdogo ila mwanangu yupo anaishi na mama yake Uingereza (Mama mtanzania age 27) nilimpeleka mwenyewe. Anajiweza. Na pia sipo nae kimahusiano kwa sasa ila nina mtunza huyu binti.

(Nia nikutoa point za uchumi na uhusiano). Sasa sina Wazo lolote la kuongeza mtoto, yaani nina mapenzi yaliyopitiliza kwa huyu niliye nae.

Wazee sababu ipi inafanya mtu awe na watoto zaidi ya mmoja au wengine kupitiliza hadi watano. Nini sababu?

Au huwaga ni bahati mbaya tu, mimba hiyo?
 
Mkuu,

Mimi ni kama wewe, nilipata mmoja tu nikaridhika.

Kama unapenda dunia iendelee kuwa na watu, unatakiwa angalau kuwa na watoto wawili.

Actually kimahesabu ya takwimu tunatakiwa kuwa na average ya watoto 2.1, hii ndiyo replacement rate.

Ukiwa na mtoto mmoja wewe, na dunia nzima ikiwa na mtoto mmoja average, maana yake kizazi kinachofuata kitakuwa nusu ya kizazi hiki, na kinachokifuatia kitakuwa nusu ya hiki, mpaka kizazi kitaisha.
 
Ukweli lazima mpewe, mkimeza mkitema shauri zenu
Aah, wewe unaweza kuona ukweli kumbe unatuletea shombo tu.

Mtu kauliza swali, hajakuuliza wewe.

Anapata michango ya watu wengine kumjibu.

Wewe kinachokuuma nini?

Kama hupendi hiyo mada kwa nini usiiruke tu uende kwenye mada unazopenda?

Ulitaka kumzalia mtoa mada mtoto wa pili akakukatalia, ndiyo maana unatuletea kisirani chako hapa?

Au uko mwezini unasumbuliwa na hormones?
 
Kwahiyo ndugu yangu, unaniambia tuzae kwaajili hiyo ya takwimu, au watu huongeza sababu ya takwimu
Hapana,

Zaa unavyotaka. Au usizae unavyotaka.

Huo ni uamuzi wako.

Mimi ninachosema ni kwamba, moja ya hasara na matatizo ya kuzaa mtoto mmoja mmoja ni kwamba, watu wote wakizaa hivyo, idadi ya watu kwa kizazi itapungua kwa nusu kila kizazi, mpaka kizazi kitoweke kabisa.

Sijakwambia uzae au usizae vyovyote, siwezi kukupangia hilo jambo ambalo ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu kuamua uzae au usizae unavyotaka.
 
Mkuu,

Mimi ni kama wewe, nilipata mmoja tu nikaridhika.

Kama unapenda dunia iendelee kuwa na watu, unatakiwa angalau kuwa na watoto wawili.

Actually kimahesabu ya takwimu tunatakiwa kuwa na average ya watoto 2.1, hii ndiyo replacement rate.

Ukiwa na mtoto mmoja wewe, na dunia nzima ikiwa na mtoto mmoja average, maana yake kizazi kinachofuata kitakuwa nusu ya kizazi hiki, na kinachokifuatia kitakuwa nusu ya hiki, mpaka kizazi kitaisha.
Mwishowe tutakuwa na idadi kubwa ya wazee kuliko vijana
 
Mwishowe tutakuwa na idadi kubwa ya wazee kuliko vijana

Inaweza kufikia mpaka nchi kuishiwa na watu kabisa.

Hili tatizo linaonekana kama utani, ila South Korea wanalipitia sasa hivi.

Kuna kampuni ya ujenzi ya South Korea inatoa fedha kiasi cha US dollar 75,000 kwa kila mfanyakazi ambaye amepata mtoto ndani ya miaka miwili iliyopita, au atakayepata mtoto.

Hii ni kupambana na "population decline" huko South Korea.

Watu wamegoma kuzaana.

Mtihani ni kwamba, inaonekana kuwa kadiri nchi zinavyopata maendeleo ya kiuchumi na watu kuelimika, na maisha kupanda gharama, watu wanaamua kuzaa watoto wachache zaidi.

Kama una uwezo na afya na Mali zaa ligezo uwe na nguvu za kuwahudumia na kulea
Mkuu,

Unawezaje kumshauri mtu azae wakati yeye mwenyewe kashaonesha hana interest na idadi ya watoto, yeye anataka mtoto mmoja ampe quality nzuri ya maisha, hataki quantity, anataka quality.

Hataki juwa na watoto wengi wanaogombea kupata attentionbya baba, anataka mtoto mmoja atakayempa attention yote.

Sasa hapo unamshauri vipi azae watoto zaidi?
 
Mkuu,

Mimi ni kama wewe, nilipata mmoja tu nikaridhika.

Kama unapenda dunia iendelee kuwa na watu, unatakiwa angalau kuwa na watoto wawili.

Actually kimahesabu ya takwimu tunatakiwa kuwa na average ya watoto 2.1, hii ndiyo replacement rate.

Ukiwa na mtoto mmoja wewe, na dunia nzima ikiwa na mtoto mmoja average, maana yake kizazi kinachofuata kitakuwa nusu ya kizazi hiki, na kinachokifuatia kitakuwa nusu ya hiki, mpaka kizazi kitaisha.
Hizi sasa fix mkuu. Huwezi sema watakuwa nusu maana ukumbuke pia tutakuwa na huduma bora hivyo watu wataishi longaaaa
 
Back
Top Bottom