Wanaume wengi hufa kabla ya wakati wao kwa sababu ya laana kutoka kwa wazazi

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,099
22,537
INTRODUCTON.

Salaam, Shalom!!

(Kutoka 20:12) says: WAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO, ILI SIKU ZAKO ZIKAWE NYINGI KATIKA NCHI UPEWAYO NA BWANA MUNGU WAKO.

Leo naandika mada hii nikiwa na Sina furaha sababu Mimi Rabbon pia ni Mwanaume.

Wanaume tulipoambiwa tuishi Kwa akili na wake zetu, au na wanawake ,Kuna Siri imejificha nyuma, ipi hiyo?

Under Ceteris peribus, while other factors remain constant,

Ni Kweli, wanaume wengi huoa wake wanaowazidi umri hivyo wengi wanapotangulia kufariki ndugu na jamaa hutoa sababu hii, lakini Si Kweli, IPO sababu zaidi ya hiyo.

Wanawake ujiwauliza watakwambia wti Kwa Sababu wao hawatunzi jambo moyoni na hulia machozi sana ndo sababu ya kuishi maisha marefu.

Wanasayansi wengine hudai kuwa sababu wanawake wao Wana matiti ambayo hutunza maziwa ambayo ni chakula kinachowapa kusurvive muda mrefu, hapo ni Kweli Kwa kiasi fulani, bt si sababu kuu.

Wanaume wenzangu tujiulize inakuwaje mwanamke anazaa Kwa uchungu hadi watoto 14, na wote tunajua shughuli pevu ya kuzaa mtoto ilivyo, lakini mwanamke huyo huyo utaondoka na kumwacha duniani, nini sababu? Tatizo ni LAANA hii nitakayoiongelea leo.

Dunia nzima imeweka mfumo thabiti kwamba Mali anazomiliki mwanamke ni zake pekeake, lakini Mali anazomiliki mwanamume ni za wote, Kuna kitu hapo kimejificha ambacho wanaume Bado hawajakijua kinachopelekea kuchomoka duniani mapema.

Namwongelea Mwanaume anayehangaisha KICHWA usiku na mchana kutafuta riziki ya familia na hapumziki, nini kinachomwondoa mapema?

Namwongelea Mwanaume anayevuja JASHO, anamhudumia mkewe na hawara na machangudoa na anamudu wote kuwapa mahitaji yao, kwanini anawahi kuchomoka duniani mapema?

Namwongelea Mwanaume aliyeokoka mwenye baba na mama wa kiroho, anawatunza wazazi wake wa kiroho, lakini Bado anawahi kuchomoka duniani kabla ya siku zake, nini chanzo?

Naongea na Mwanaume unayeacha Kodi ya meza Kila siku, unajibana Ili familia yako isonge, kwanini bado huna maisha marefu, ipi sababu, ni hii:

LAANA YA WAZAZI NI CHANZO KIKUU CHA WANAUME WENGI KUFA MAPEMA KABLA YA WAKATI WAO.

Wanaume wengi tumelisahau hili.

Kwani hamkusoma maandiko katika Amri ya Mungu isemayo,

"Waheshimu baba Yako na mama Yako, Ili siku zako zipate kuwa nyingi katika Nchi upewayo na BWANA Mungu wako"

Pia hamkusoma kuwa,

" Baba na mama (Wazazi) ni miungu wa Dunia hii?

Watu wengi hasa vijana na wanaume huangaika sana na hukumbwa na mabalaa na kufungwa vipato vyao duniani bila kujua Chanzo ni LAANA ya wazazi!!

Wakati ukiacha Kodi ya meza Kwa mke wako, atahakikisha anatenga kiasi kidogo kidogo Kila siku, Kisha hukituma Kwa mama yake mzazi.

Mzazi wa mke wako ambaye mara nyingi ni mwanamke sababu mzazi wa kiume mara nyingi anakuwa ameshaiaga Dunia, mzazi yule wa kike, huipokea sadaka Ile na kumwombea baraka aliyeitoa ambaye ni mwanae wa kike, baraka hizo hazitakufikia wewe Mwanaume sababu nawe unao wazazi wako kijijini hawana hata mia mbovu😭

Wazazi wako ewe Mwanaume wanaweza kata hata mwaka hujawatumia chochote kuwatunza, wanaishi nyumba chakavu wanalala chini, hata godoro hamna, wewe umehangaikia familia Yako wanakula na kulala vizuri, unamsahau baba na mama Yako!!

Ikitokea umeenda kijijini, utamwita pembeni mama na kumshikisha bulungutu la pesa, Kisha baba unampa pesa kiduchu ilhali ndo anajukumu kutunza familia.

Wazazi wako wanaposikia umenunua gari Kwa ajili ya mkeo kutembelea na wakisikia umejenga ukweni kwa mkeo, kinachotokea huwa wanahuzunika😭

Mama anashika tumbo na kumlilia Mungu, baba hushika kiuno na kulia, Kila Mmoja sirini Kwa wakati wake.

Ugumu wa maisha wanaume wengi tunaoupitia mijini, chanzo kikuu ni LAANA ya wazazi.

Mwaka mzima unaisha hujapeleka Kwa wazazi hata mia mbovu, lakini unapata pesa ya kuhonga MAKAHABA. LAANA inakunyemelea......

Unapomuhonga kahaba, yeye huchukua pesa hiyo na kutumia pesa kiasi Kwa wazazi wake, Kwa maana ingine, pesa yako inatumika kuwa baraka kwa mwanamke while wewe hupati kiasi cha kuchota baraka za wazazi walokuzaa.

Na wanawake ni Wachache sana ambao huwakumbusha waume zao kuwatumia chochote wazazi wa waume zao.

Mwanaume mwenzangu, hasa vijana ambao hamjaoa bado, msisubiri kupata KICHAA kitokanacho na LAANA ya wazazi wanapohuzunika Kwa ajili yetu. Msisubiri kupelekwa kijijini mkiwa katika majeneza.



Na hii ndo OCTOBER 2023, Wenzetu wa mikoa ya kaskazini wanajipanga kwenda Kwa wazazi wao kushukuru kana kwamba huko ndo pekee palipo na wazazi, msijesema sikuwaambia!!!


SOLUTION.
1. Hakikisha unatunza Kwa Siri chochote kitu, unatumia Kwa wazazi wako kimya kimya, sababu najua wake zenu wengi Wana gubu na wasingependa mbarikiwe.

2. Pata muda wa kuongea nao hata Kwa simu na uwashirikishe changamoto unazopitia, ukijua kuwa hao ni miungu wa Dunia hii.

Wazazi wanapokuhuzunikia Kwa kutowajali wazazi, humpa KIBALI shetani kukushambulia Kwa mapigo na LAANA mbalimbali!!

3. Tafuta muda ukatubu, wajengee wazazi wako nyumba nzuri, watumie zawadi, nenda kusali lakini jua miungu mwenye FUNGUO za maisha Yako duniani ni wazazi,

4. Ishi na mke wako Kwa Akili sana, hakikisha unamzidi akili na Maarifa.

5. Jipange kidogo kidogo uweze kurudi kuwaona hata mara Moja Kwa mwaka angalau.

6. Ikiwa umelelewa na mzazi mmoja, mtafute mzazi wako wa pili msamehe, tapika Sumu yote ulolishwa na mzazi alikulea, hakikisha unawatunza wote sawa sawa. UTABARIKIWA!! Siku zako zitakuwa nyingi katika Nchi upewayo na BWANA Mungu wako. Amen.

Ningeongea zaidi bt inatosha Kwa sasa!!!

Karibuni Kwa shuhuda na MAONI 🙏.
 
Ndugu Mimi Hadi machozi yananilenga,

Kuna wazazi vijijini wanahudumiwa na tasaf, wengine wanaishi kama hawakuzaa watoto.

Watoto wao wapo mijini wanakula Bata na malaya,

LAANA inawafuata,

Wakatubu.

Amen
itabd tujue maana ya laana kwanza
 
Yote ya juu hayanihusu kabisa wala familia yangu kwa ujumla
Ila hiyo ya suluhisho yote ndio ya kwetu sasa
Na ndio tunafanya kwa pamoja ndugu wote labda ndio maana mambo yanaenda vizuri
Wazazi ni Baraka kubwa sana na ni lazima waangaliwe kama walivyotuangalia

Ila kwa kuwahi kufa labda ni matabaka na matabaka
Sidhani kama ni laana maana wazungu wanawakimbia wazazi wao wakiwa na miaka 18 ila wanaishi mpaka 90
Ila Wazazi wana part yao katika maisha yetu na kama maisha yanakuendea kombo jitafakari sana
 
Umeandika vyema.
Jambo la msingi nililoliona kwenye bandiko lako ni ulivyowakumbusha vijana/wanaume kuwakumbuka wazazi na kuwahudumia👍👍

Ila kufa mapema hilo bado ni fumbo, sidhani kama linahusiana kwa namna yoyote na kutokuwajali wazazi.
Kuna jamaa yangu alikuwa rafiki haswa, alikuwa anawajali sana wazazi wake....cha kusikitisha jamaa alikufa akiwa mdogo kabisa(42yrs Old) na alipata ajali alipokuwa njiani kutoka Dar kwenda kumchukua mama yake mgonjwa kumleta mjini kwa matibabu.

All n all itoshe tu kusema wanaume kufa mapema inaweza kuwa ni tuzo ya kazi nzuri aliyofanya...maana maisha marefu kwa mwanaume inamaanisha mateso zaidi.
ieleweke marehemu hajui chochote, aliyeishi muda mfupi na aliyeishi miaka 120 wote ni sawa baada ya kufa.
 
Umeandika vyema.
Jambo la msingi nililoliona kwenye bandiko lako ni vijana/wanaume kuwakumbuka wazazi na kuwahudumia👍👍

Ila kufa mapema hilo bado ni fumbo, kuna jamaa yangu alikuwa rafiki haswa, alikuwa anawajali haswa wazazi wake....cha kusikitisha jamaa alikufa akiwa mdogo kabisa(42yrs Old) na alipata ajali alipokuwa njiani kutoka Dar kwenda kumchukua mama yake mgonjwa kumleta mjini kwa maribabu.

All n all itoshe tu kusema wanaume kufa mapema inaweza kuwa ni tunzo ya kazi nzuri aliyofanya...maana maisha marefu kwa mwanaume inamaanisha mateso zaidi.
ieleweke marehemu hajui chochote, aliyeishi muda mfupi na aliyeishi miaka 120 wote ni sawa baada ya kufa.
Ngoja niedit na na kuongeza, ceteris peribus,

Other factors remain the same. LAANA ya wazazi iwe one of the factors.
 
Kuwahudumia wazee ni jambo muhimu mno, ila kuhusu laana hizo ni propaganda tu hazina uhalisia, kufa mapema kwa wanaume kuna sababu lukuki za kimazingira hasa kwenye nchi zetu za ulimwengu wa tatu.
Under Ceteris peribus!!

Sababu za vifo vya wanaume ni nyingi na vinasababishwa na mengi,

Lakini Leo tuongelee, LAANA ya wazazi kama chanzo mojawapo muhimu kichangiacho vifo na mkwamo Kwa vijana na wanaume wengi.
 
Under Ceteris peribus!!

Sababu za vifo vya wanaume ni nyingi na vinasababishwa na mengi,

Lakini Leo tuongelee, LAANA ya wazazi kama chanzo mojawapo muhimu kicganguacho vifo na mkwamo Kwa vijana wengi.
Mkuu kile kitendo ya mzazi kutamka maneno mabaya kama unavyoita laana , wewe ukiamini haya maneno na ukawa na mashaka yatakutokea kama yalivyo , hiyo ni law of attraction na maumbile yanavyofanya kazi kulingana na fikra zetu.

Bila hata laana mambo yako yana weza kwama sana , kutokana na unavyofikiri na kuchukua maamuzi na hata mda mwingne hisia zako zinaweza kuathiri matokeo.

Jinsi tulivyo ni matokea ya fikra zetu hasi au chanya .

Ukijenga fikra wanaume tunakufa mapema kwa sababu hatusaidii wazazi ,utakufa kweli kwa fikra hizo ukienda kinyume.

Na sio kwa sababu eti umepata laana kutoka kwa wazazi.

Katika kitu cha kuchunga sana ili kupata matokeo chanya kwa yale tunayotarajia ni kuchunga fikra zisiharibiwe.

Kwa sababu kanuni inasema fikra ikiharibika, hisia na mienendo na matokea huwa hasi .

Ndio maana matajiri hupenda kuweka makazi yao mbali na maskini na watu wenye fikra duni ili kulinda fikra zao kwa sababu fikra chanya ndio hazina.
 
Back
Top Bottom