PiedPiper77
Senior Member
- Jan 8, 2025
- 180
- 223
.CHAUMMA INA UMA.
Kuna baadhi ya wanasiasa wanajidanganya na wengine kudanganywa kuwa CHAUMMA inaweza kuwa tishio kwa chama tawala leo au kesho, hii naomba wasahau kabisa.
Kwa taarifa tu, Vyama vyote vilivyoanzishwa kama matokeo ya migogoro havijawahi kufanya vizuri popote duniani tujiulize CHAUMMA itakuja na maajabu gani?
Kwa hapa Tanzania labda niwape mfano mdogo wa hii ACT Wazalendo ya Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe baada ya kugombana na Freeman Mbowe akaamua kuanzisha chama Cha ACT WAZALENDO ambayo mpaka leo bara haikuwahi kuamka ukiachilia Zanzibar ya Hayati Maalim Seifu.
Kitendo hiki cha waasi toka CHADEMA almaarufu kama G55 baada ya mgogoro wa Kukosa fursa za Ubunge wa viti maalum na Uongozi ndani ya CHADEMA na kukimbilia CHAUMMA ili kuzipata fursa hizo ni ishara tosha kuwa G55 nia yao ni wao kwanza na Watanzania watajijua wenyewe.
Jambo zuri ni kwamba Watanzania wengi bado wanaamini si CHAUMMA Wala ACT WAZALENDO wanaweza kuwa mbadala wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwani ni vyama ambavyo CCM inavilea kama GSM anavyozilea baadhi ya timu za Ligi kuu hapa Tanzania na ndio maana timu hizo hazijawahi kuifunga yanga.