Jamani naomba kuwauliza swali linalonitatiza sana. Miaka ile ya themanini wakati mi niko mdogo kule Kinondoni kulikuwa na tajiri mmoja mwenye magari mengi aina ya scania 111, jamaa mwenyewe alikuwa anaitwa MWANAMBOKA na mascania yake tulikuwa tunayaita mascania ya Mwanamboka. Huyu jamaa ni maarufu sana Kinondoni pale, sasa miaka ya 2000's akaja akajitokeza binti mmoja anayeitwa KHADIJA MWANAMBOKA, sasa nauliza huyu Khadija Mwanamboka ni mwanawe au ni ndugu au ni jina tu limefanana? Maana huyu Khadija anaonekana ni mwarabu na yule mzee mwenyewe kama jina lake linavyoonyesha ni mswahili ila sijui ni wa mkoa gani wala kabila gani.Kwa anayemfahamu vizuri huyu jamaa na maisha yake tubadilishane mawazo si vibaya tukajikumbusha mambo yaliyokuwa yakituburudisha zamani jamani. Hivyo jamani kwa yeyote yule mwenye kumjua huyu mzee atupe historia yake na ya familia yake mana alikuwa maarufu na tajiri sana enzi hizo dsm.
Khadija si mtoto wa kuzaliwa na Mwanamboka. Mwananamboka alikuwa akiwalea watoto wa ndugu zake. Hadija amesoma Kinondoni Muslim na kaka zake Saad, Nassoro na wengine.
kuna wakati ilivumishwa kuwa yale malori yalikuwa ni ya Salim Ahmed Salim. pengine kweli. who knows?
Watu mnazo data karibu mtamzidi hata DR SLAA?
mambo bado mambo bado mambo dadooooooo
Ndie mwanae, sijui kivipi ila wanaukooo! HAPANA CHEZEYA KHADIJA MWANAMBOKA TANGU AKIWA DANCER BILLS YA ENZI HIZOOOO NA KUNDI LAO LA MADUUU WESTERNIZED!!!!!!! Kila mtoto wa kino alikuwa anataka kuwa dancer na yeye ili atingishe kama kina dada Khadija!!!!!!!!! AGE IS A THIEF!!!!!!!!!! Enzi hizo za Mzee Ruta PAPA Diamond Sounds, Muzee ya Silent Inn!!!!!!!!!!! Akamshusha Defao LIVE!!!!!!!!!!! Bwana asifiwe sana Mzee wetu wa ukweeee! UMENIKUMBUSHA MBALI SANAAA KWENYE REDE ZA PEKU PEKU NDANI YA PICHU YA TAIWAN!!!!!!!!!! Kumbe nazeeka sasa!!!!
ahahahahahhahahhah LARA aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa !kitu cha igongwe social hall unakikumbuka?lang'ata je?
hunters club pale ubungo?
kitu ilikuwa inapigwa YEKE YEKE TUMORO YEKE YEKE!Vitunguu vinanukiaaa aaaaah,vitunguu vinanukiaa jammaaaee, shemeji naye anataka nimpevituz,
yekeke mshua yekeyeke,yekeke mshua yekeyeke....
hahahahahaha. Ulposepa ndo palinoga zaidi.. Ulikosa uhondo
Huyu Saad Ally alishajitoa,mwenye Mwanamboka Hauliers anaitwa Salum mwenye kufanana na Madiluu sytem.