SoC02 Ni namna gani tutaipiku Uchina katika Science na teknolojia, na kuwa wawekezaji wakubwa na wauzaji wa teknolojia kote duniani

Stories of Change - 2022 Competition

manofpeople18

New Member
Jul 19, 2013
1
0
UTANGULIZI
Ndugu msomaji wa makalia hii, nilicho kiandika hapo juu, kuhusu jinsi nchi yangu pendwa, Tanzania inaweza kuipita Uchina katika technologia Miaka ijayo, kama Tuu tutaamua kuwekeza katika Elimu yetu kwa kiwango cha mapinduzi.

Pia hili lilikua ni ndoto kwa Uchina miaka ya 60's kuipiku marekani katika science na technologia, ila kwa sasa sio ndoto tena tunashuhudia kwa macho yetu jinsi Uchina inavyo songa kuiacha Marekani nyuma mpaka kufiakia katikati ya mwaka 2030 uchina ndo itakua nchi yenye nguvu duniani katika nyanja zote inakadiriwa na wataalamu wa Tafiti.

NINI KIFANYIKE?

TUFUMUE MFUMO WETU WA ELIMU NCHINI


Hili liendane sambamba na kubadilisha mitaala ya Elimu ya nchi yetu (Tanzania curriculum) hapa tukubaliane kwamba katika mfumo wetu wa Elimu wa sasa umepitwa na wakati, Mfumo huu wa Elimu sio kwamba ni mbaya la hasha, ila ni kwamba nyakati tulizo nazo sasa haziendani na mtaala huu wa miaka ya 60's.

Mtaala huu ulitufaa sana Baada ya uhuru kwani Vision ya Mtaala huu ilihimiza lengo la Elimu ya Tanzania ni kumuandaa kijana kua Mzalendo kwa nchi yake, Umoja na mshikamano katika jamii.

Lakini kwa sasa kuna kila sababu ya kuongeza jambo lingine kijana pia awe m'bobevu katika science na technologia ili aweze kuisaidia nchi katika kipindi hiki cha dunia ya ushindani katika science.

Mfano china wao wameingiza science na technologia katika Mitaala yao kama tegemeo la nchi, na wanahimiza kila kijana Asome vyema ili aweze kuisaidia nchi yake kuvuka vikwazo vya dunia hii mtambuka. Uzalendo ni Elimu, na ujuzi katika science na technologia kulisaidia taifa.

YAFUATAYO NI MAMBO YA KUWEKA KATIKA MTAALA WETU MPYA WA ELIMU NCHINI TANZANIA. (Kwa maoni yangu)

(i) Masomo ya science yaanze kufundishwa shule ya Msingi la 1-7 (practically),na hii isiwe kuchanganywa kama somo moja (Stadi za kazi) hapa yawe masomo ya science kama ilivyo Secondary school, na Maabara ziwepo, hii ina maana gani, kwa maoni yangu tunapoteza wana science wakubwa, na wataalamu mbali mbali kwa kuchelewa kuwagundu na kuwaendeleza, sasa tukiwa na hizi Maabara shule za msingi itasaidia kwani watoto hua kayika kipindi cha udadisi na udhubutu zaidi wanapokua chini ya miaka 18, hapa hua na uwezo mkubwa wa kuelewa mambo, kujaribu na hamu ya kufanikisha mambo na kuyashuhudia, Mtaala mpya uwape nafasi hiyo.

Mfano nchini china wanafanya hivi na ndo maana wamefaniliwa sana katika science na ugunduzi. Pichani ni chapisho kutoka google ikionyesha wanafunzi wa primary school huko Uchina wakifanyika practical ya ICT na engineering, na Watanzania wakiwa katika mafunzo ya maudhui katika shule tofauti nchini.

View attachment 2336483
Screenshot_2022-08-27-16-09-47-88_680d03679600f7af0b4c700c6b270fe7.jpg
(ii) Somo la uzalendo lishikanishwe sambamba na Elimu ya science na technologia, wenzetu wa Cuba na Uchina wamefanikiwa sana kwenye hili, mfano Cuba wao wameweka kwenye mitaala yao kijana wa kicuba asome atumie ujuzi wake wa science katika kulisaidia taifa lake, na hili ndo zao la madakitari wengi wa Cuba wenye uwezo mkubwa duniani.

(iii) Kuwe na vyuo Vikuu vichache kwa ajili ya kuzalisha administrative wachache, yaani maofisa, na Vyuo vya VETA vingi kwa ajili ya kuzalisha Wataalamu wengi ili kurekebisha mlinganyo wa shughuli kwani sasa wasimamizi ni wengi kuliko wafanyaji kazi wataalamu.

Wenzetu china licha ya kua na wanafunzi zaidi ya million 200 wa Elimu ya primary, namba ya wanafunzi katika vyuo Vikuu na Ufundi ilikua ni million 33 mwaka 2010-2020.

(iv) Kuwe na Elimu ya mwendelezo kwa Waalimu wote nchini haswa hawa wa science ambao sasa watakua kwanzia primary school (career development) hii itasaidia waalimu kuwa competitive na kuendana na mabadiliko ya science na technologia kwa wakati wote.

(v) Elimu ya watu wazima iwe practical oriented yaani Elimu ya watu wazima ielekezwe zaidi katika vyuo vya Ufundi VETA, ili kuwajengea uwezo na kuwa wazalishaji mapema, kujikwamua kimaisha baada ya kuhitimu, hii itapunguza dependency kwenye ajira za serekali na watajiajiri wenyewe.

(vi) mfumo wa utambuzi wa uwezo wa wanafunzi darasani yaani alama za ufaulu, zitambulike kisheria na sio kubadilishwa kila mara hii inaondoa upimaji mzuri kwa wanafunzi kulinganisha na muda kuweza tambua ni awamu ipi walifanya vizuri kuliko nyingine, napendekeza ili kupata wanafunzi cream, na ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi vyuo vikuu alama za ufaulukwa Grade ziwe hivi A 100-85 B 84-75 C 74-61 D 60-49 F 48-0. Hii ni kwa Mujibu wa maoni yangu.

(vii) Sera ya Elimu, pamoja na vision ya Elimu vyote viwe katika katiba, na sio chini ya Waziri wa Elimu kwani tunaamini mawaziri wengine hawatokani na wafanyakazi katika wizara ya Elimu hivyo wakiachiwa nafasi kubwa kama hii ya kuamua sera ya Elimu kunaweza kuja kufanyika makosa makubwa na yakaligarimu Taifa, sera ya elimu tuonaomba iwe yajieleza katika katiba.

(viii) Wakati, au kila ikihitajika kufanya mabadiliko katika sera ya elimu au jambo lolote katika Elimu, tunaomba waalimu wanaofindisha madarasani ndo waulizwe na sio viongozi walio wahi kua waalimu na wadau wa elimu pekee, tunapendekeza waalimu wapewe vishikwambi kwa ajili ya kufanyia kazi zao za kila siku, Ambavyo pia vitatumia katika maswala ya research kuhusu mfumo wa elimu n.k

NINI KIFANYIKE KWA WAALIMU ILI KUAMSHA ARI YA KAZI YA MWALIMU MWENYEWE NA JAMII KWA UJUMLA.

1. Waalimu wajengewe nyumba za makazi maeneo ambayo hawana mfano kama maeneo ya mjini ambapo makazi hua changamoto wapangishiwe nyumba, kama haiwezekani wapewe hela ya kodi katika mishahara yao,waalimu wengi wanatumbukia katika lindi la umasikini kutokana na kodi kubwa za mijini.

2. Wafanyakazi wa serekali wapewe mikopo nafuu ya serekali yenye nafuu ya riba na mashariti rafiki, hii itasaidia kupunguza riba kubwa kwnye mishahara ya Wafanyakazi na kurudisha hari ya kazi.

3. Waalimu walipwe posho kama baadhi ya kada, Kwani waalimu wengi wako kando ya nchi kwenye mazingira magumu, lakini pia kwa kuwa waalimu ni walenzi mara nyingine hutumia fedha za mishara yao kutatua changamoto za wateja wao (wanafunzi) hivyo waalimu nao walipwe posho kwani nao wanadili na jamii wakati wote kama wabunge na hata zaidi.

4. Waalimu wenye juhudi na maarifa wanapewa nishani na Mweshimiwa Raisi ambaye ni mwajiri kwa wale walio perform vizuri na mwajiri akawatambua washindanishwe na wapewe nishani, Elimu ni kazi mahisusi na UTI wa mgongo wa Taifa lolote, kwa mfano hapa tulipo ni zao la elimu yetu tusitafute mchawi.

5. Waalimu wawe na bima ya maisha ya matibabu hata baada ya kustaafu hii ni heshima kwa mwalimu na alile liyendea taifa

6. Waalimu wapewe usafiri kwa kutengewa fungu wanunuliwe staff bus kila shule inawezekana nashauri lifanyike.

7. Waalimu wapewe mafunzo na zana za kisasa za kufundishia, kama projector, laptop tupunguze matumizi ya chaki hii itapunguza garama kwa serekali lakini itapunguza matatizo ya kiafya kwa waalimu na wanafunzi.

KWA JAMII
Jamii ipewe elimu na ushauri juu ya Elimu thamani ya elimu na Waalimu kwao na watoto wao na taifa kwa ujumla na mchango wa mwalimu kwa Taifa ili kuipa dhamani tena elimu na waalimu kama zamani wanachi washauriwe kutoa ushirikiano katika juhidi za serekali katika uboreshaji wa elimu nchini.

Conclusion
Elimu ya nchi ndo huakisi na kutafsiri jamii na Taifa la sasa na lijalo tujali Elimu yetu kujenga taifa letu, kwa Kuweka mitaala ya kisasa na itayo toa majibu ya changamoto za leo na kesho.

Wako katika ujenzi wa Taifa
manofpeople18
Screenshot_2022-08-27-16-06-51-13_680d03679600f7af0b4c700c6b270fe7.jpg
Screenshot_2022-08-27-16-09-47-88_680d03679600f7af0b4c700c6b270fe7.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_2022-08-27-16-03-26-77_680d03679600f7af0b4c700c6b270fe7.jpg
    Screenshot_2022-08-27-16-03-26-77_680d03679600f7af0b4c700c6b270fe7.jpg
    60.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom