Ni mwaka sasa bila Baba yetu mpenzi! (special for Madame B)

Ni mwaka sasa bila Baba yetu mpenzi! (special for Madame B)

Poleni sana,mdogo wangu Madame B pamoja na Kijino,Mungu awatie faraja.Ni safari yetu,baba alitutangulia na sisi tutamfuata muda wetu ukifika!
 
Last edited by a moderator:
Mpendwa, misa Jumapili tutasoma.
Asante amu.

tupo pamoja ningekuwa huko tungejumuika pamoja.Wape hi madogo wote na mzee wa ''aunt mbona hunibakshii''?
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana Madame B na Kijino + wafiwa wote...

Msimba ni jambo gumu kulieleza kwa maneno ya kawaida...Tunahitaji neema ya Mungu kuukabili!!





RIP Baba!
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana,mdogo wangu Madame B pamoja na Kijino,Mungu awatie faraja.Ni safari yetu,baba alitutangulia na sisi tutamfuata muda wetu ukifika!

Asante sana kaka kipenzi sungura1980.
Hakika ni kweli usemayo.
Njia yetu ni moja, tujitayarishe kurejea kwa Mola, muda na siku yoyote.
Baba yetu ametangulia, sisi tupo nyuma yake.
Cha umuhimu ni kuyaenzi yale mazuri aliyotuachia.
Nami naendelea vizuri.
Asante kaka, tuko pamoja.
 
Last edited by a moderator:
tupo pamoja ningekuwa huko tungejumuika pamoja.Wape hi madogo wote na mzee wa ''aunt mbona hunibakshii''?

Hahaha!
Usijali mdogo wangu,
anakusalimia, anakuulizia afu.
Ila usiwe na shaka, waweza kumuombea hata huko uliko mpendwa.
Najua umuhimu wako mdogo wangu.
Asante sana.
Salamu zimefika.
 
hata mimi nitakufa.
baba yake madame B alifariki.
Kila mtu atakufa.
TUACHE UBABE,UMIMI,MAJIVUNO,UKATIRI,UHASAMA,UCHOYO MAANA WOTE TUTAKUFA NA ROHO PEKEE ITABAKI HUKU MWILI UNAOTUPA UBABE,UKATIRI,UMIMI NK UTATEKETEA NA HATUTAKUWA NA UWEZO WA KUFANYA HAYO.
tupendane,tuwe wapole,wakalimu,wastaarabu nk.
POLE SANA MADAME B.
 
Poleni sana Madame B na Kijino + wafiwa wote...

Msiba ni jambo gumu kulieleza kwa maneno ya kawaida...Tunahitaji neema ya Mungu kuukabili!!





RIP Baba!


Asante sana mpendwa wangu na Kaka yangu mkubwa Dark City.
Kiukweli msiba ni fumbo gumu sana lisilo na jibu lenye uhakika, kwani huweza kumkumba mzima na kumuacha yule aliye mahututi...ni Neema za Mungu peke yake ndizo zenye kuweza kutuinua.
Kila mja ataiacha Dunia, hivyo ni vema kuishi kwa upendo na utashi ili tuweze kukabili yale yajayo.
Asante sana mpendwa, tuko pamoja kwenye maombi.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Madame B na Kijino.
Ulikuwa msiba wetu sote, na hakika tunaendelea kumkumbuka mzazi wetu.
Cha msingi ni kuendelea kumwombea.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Madame B
apumzike kwa amani mzee wenu apumzike pia baba yangu miaka 12 sasa

Pole sana mpenzi kwa kuondokewa na yule mumpendae.
Asante sana Elizabeth Dominic,
Laiti tungekuwa tunajua muda na siku ya kifo, tungejiandaa mapema, ila Mungu katufumba mno.
Ila, tuishi kwa kumpendeza yeye ili tupate mavuno mema kule tunakoenda.
Pole sana mpendwa.
Asante sana kipenzi.
Tuko pamoja katika maombi ya pamoja ya kuwaombea wapendwa wazazi wetu.
 
Last edited by a moderator:
hata mimi nitakufa.
baba yake madame B alifariki.
Kila mtu atakufa.
TUACHE UBABE,UMIMI,MAJIVUNO,UKATIRI,UHASAMA,UCHOYO MAANA WOTE TUTAKUFA NA ROHO PEKEE ITABAKI HUKU MWILI UNAOTUPA UBABE,UKATIRI,UMIMI NK UTATEKETEA NA HATUTAKUWA NA UWEZO WA KUFANYA HAYO.
tupendane,tuwe wapole,wakalimu,wastaarabu nk.
POLE SANA MADAME B.

Asante sana mdogo wangu Mshinga.
Miili yetu hii si mali kitu...roho mbaya na kila aina ya maovu yatubidi tuepukane nayo ili tuweze kujitengenezea maisha mazuri kule tuendako.
Kila nafsi itaonja mauti, na pia tukumbuke sisi ni mavumbi hvo kurejea mavumbini ni haki yetu sote.
Tutengeneze njia safi mapema, ili tuweze kufika kwa Baba yetu salama.
Asante Mshinga, tuko pamoja katika maombi.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Madame B na Kijino.
Ulikuwa msiba wetu sote, na hakika tunaendelea kumkumbuka mzazi wetu.
Cha msingi ni kuendelea kumwombea.

Asante sana kaka PakaJimmy.
Nikikumbuka jinsi wenzangu mlivonifariji, sina pa kuanzia.
Sikuwa na cha kuwalipa, ila Neema na Baraka za Mungu hakika ziliwaangaza tangu mwanzo mpaka mwisho wa maombolezo.
Msiba wa mtu unayempenda, unauma sana kaka hasa pale anapobaki kama mzazi pekee anayewaongoza.
Asante kaka, tuzidi kumuombea mpendwa Baba yetu.
Nawashukuru kwa kweli.
PakaJimmy, kule Amboni, Chumvini...nilipoumia, nililia na mengi.
Ila yote yamepita.
Asante sana.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom