Himidini
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 5,534
- 4,193
- Thread starter
- #81
Poleni muluofiwa
Hayo ni majaaliwa
Ni vyema kivumiliwa
Sote tutaelekea
Ni kweli mulimpenda
Kwa mazuri alotenda
Kwa molawe amekwenda
Dua tunamuombea
Mola ampe mazuri
Amundoshee shari
Kwa mola wetu kahari
Mikono tunanyanyua
Nasi tuliobakia
Tumuabudu jalia
Kwani dunia ni njia
Na sote tutajifia
Tuyapunguze maasi
Tumuabudu mkwasi
Kwani pia hata sisi
Mauti yatungojea
Siku yetu itafika
Ya kuenda kwa rabuka
Mauti yatatudaka
Wala hatutokimbia
^^
Swadata Mahirtwahir,
Kifo hakina rafiki,
Kifo hakizoeleki,
Kifo hakikwepeki,
Kifo safari ya sokoni,
Kila mja anae safiri,
Lazima apite sokoni,
Akanunue kitu fulani,
Tuonyeshane mapenzi,
Dunia tu wasafiri.
^^