Ni mwaka sasa bila Baba yetu mpenzi! (special for Madame B)

Ni mwaka sasa bila Baba yetu mpenzi! (special for Madame B)

1061443ny0m7963kn.gif

...najua inatia uchungu sana pale mauti yanapomkuta mzazi mmoja mpweke na pekee ambae nae alipoteza mkewe kwa kifo cha ghafla!!!

Nakukumbuka sana baba yangu, kwa maana uliondoka tukiwa bado twakuhitaji.
...ulitupenda sana, ulitujali sana,na hilo kila mtu alilijua...

Twajua kizuri hakidumu, ila kwa mapenzi ya Mungu.
Kimwili hauko nasi, ila kiroho tutaishi nawe mpaka siku tutakayokutana.

Uliishi nasi kwa upendo ambao tulijivunia kupata Baba mwema kama wewe.
Siwezi kueleza...uchungu umenijaa moyoni.

Baba na Mama, tutawakumbuka daima.
Mema yenu mliyotuachia bado twayaendeleza.

Madame B, Kijino, ShemmySeanP & Nanah.
Asante kipenzi Himidini.

780662ommatxbjxq.gif
 
Pole sana @ Madam B,,, Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali mema peponi amen.
 
Madame B and Kijino:


Samuel 1; 26


-"I grieve for you, ... my brother; dear and delightful you were to me; your love for me was wonderful, surpassing the love of women."
Also it is written,

The joyful in in the sight of God is death of his Saints.

RIP our Daddy.

Asante mpendwa Mount Kibo...
Nashukuru kwa ujumbe wako..na faraja yako.
Asante sana.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana.

Ni vigumu kumsahau mpendwa wako ata ipite milioni miaka.

Cha muhimu ni kumuombea baba ili azidi kupumzika huko aliko.
 

pole sana Madame B
tuzidi kumuombea baba
apumzike kwa amani!!

...Amina.
Inatia uchungu pale mzazi mmoja pekee mliebaki nae anapopatwa na mauti.
...hakuna wa kucheka nae, wala kufurahi nae milele kwa mtu uliyezoea kumwita Baba.
Ila ni lazima maandiko yatimie..."Kila Nafsi Itaonja Mauti".
Asante sana mpendwa Passion Lady...tuko pamoja.
 
Last edited by a moderator:
Pole Madame B and Co.... Tulihuzunika pamoja tutafurahi pamoja!!!

Ni kweli mpendwa HuntersQ...
Kuzaliwa..sote twafurahi.
Kifo..sote twahuzunika.
Ipo siku ya kulia na kucheka kwa kila kiumbe kilichozaliwa na mwanamke.
Asante sana mkuu HuntersQ, tuko pamoja kwenye maombi.
 
Last edited by a moderator:
Poleni muluofiwa
Hayo ni majaaliwa
Ni vyema kivumiliwa
Sote tutaelekea

Ni kweli mulimpenda
Kwa mazuri alotenda
Kwa molawe amekwenda
Dua tunamuombea

Mola ampe mazuri
Amundoshee shari
Kwa mola wetu kahari
Mikono tunanyanyua

Nasi tuliobakia
Tumuabudu jalia
Kwani dunia ni njia
Na sote tutajifia

Tuyapunguze maasi
Tumuabudu mkwasi
Kwani pia hata sisi
Mauti yatungojea

Siku yetu itafika
Ya kuenda kwa rabuka
Mauti yatatudaka
Wala hatutokimbia

Mpendwa mahirtwahir...asante sana sana kwa ujumbe wako mzuri na wenye kutufariji.
Sote kwake tutarejea...sisi tu mavumbi, na mavumbini tutarejea.
Muhimu ni kuomba Dua ili tuepukane na madhila ya huko tuendako.
Asante sana mkuu.
Tuko pamoja.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana.

Ni vigumu kumsahau mpendwa wako ata ipite milioni miaka.

Cha muhimu ni kumuombea baba ili azidi kupumzika huko aliko.

Ni kweli mpenzi, hata ipite miaka mingapi, kumbukumbu haitoweza kufutika...
Japo tumepewa sehemu ndogo ya kusahau, lakini haitoweza kuubadili ukweli.
Asante sana Angel Nylon...tuzidi kumuombea baba yetu.
Asante.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana.

Ni vigumu kumsahau mpendwa wako ata ipite milioni miaka.

Cha muhimu ni kumuombea baba ili azidi kupumzika huko aliko.

Ni kweli mpenzi, hata ipite miaka mingapi, kumbukumbu haitoweza kufutika...
Japo tumepewa sehemu ndogo ya kusahau, lakini haitoweza kuubadili ukweli.
Asante sana Angel Nylon...tuzidi kumuombea baba yetu.
Asante.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom