Ni Mungu gani anaesaidia mtu Mzinifu na anaezaa nje bila ya Ndoa?

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Kwenye pitapita zangu mtandaoni nikakutana na Demu analalamika kuachwa na Jamaa baada ya kupewa Kibendi.

Kama unavyojua penye watu hapakosi neno, basi watu wakaanza kutiririka kumpa pole na kumwambia yule Dada kuwa Mungu atamsaidia na mtoto wake.

Watu wengine wakawa wanamwambia wanamuombea kwa Mungu apate kipato kikubwa baada ya kupigwa chini na jamaa yake.

Swali langu kwenu wenye Dini, hivi ni kweli dua zinaweza kujibiwa kwa mtu kama huyu aliezini na kukimbiwa na jamaa?

WENYE IMANI NAOMBA MNIJIBU.
 
Kuna vitu viwili hapo

Dua ndio inaweza jibiwa haina kifungo

Pili, kuhusu mwanaume kulaaniwa eti kafanya kitu kibaya kumuacha hapo hawapo sahihi huo uhusiano hautambuliki kidini hapa kama unalazimisha kurasimisha kwa Mungu hapa mwanaume hana kosa, kosa Lake kudhini tu.
 
Kuzaa ndani ya ndoa ndo huwa kuna kuwaje kuwaje? Ufafanuzi wa hili kwanza then ntajibu hoja yako?

Au niliweke hivi "mtoto wa ndani ya ndoa ni yupi"?
 
Kwenye pitapita zangu mtandaoni nikakutana na Demu analalamika kuachwa na Jamaa baada ya kupewa Kibendi.

Kama unavyojua penye watu hapakosi neno, basi watu wakaanza kutiririka kumpa pole na kumwambia yule Dada kuwa Mungu atamsaidia na mtoto wake.

Watu wengine wakawa wanamwambia wanamuombea kwa Mungu apate kipato kikubwa baada ya kupigwa chini na jamaa yake.

Swali langu kwenu wenye Dini, hivi ni kweli dua zinaweza kujibiwa kwa mtu kama huyu aliezini na kukimbiwa na jamaa?

WENYE IMANI NAOMBA MNIJIBU.
Kwani kwa uelewa wako Mungu anasaidia watu gani
 
Back
Top Bottom