Watoto waliozaliwa nje ya ndoa wana haki ya kurithi

Apr 26, 2022
64
100
KESI NYINGINE AMBAYO MAHAKAMA ILISEMA WATOTO WALIOZALIWA NJE YA NDOA WANA HAKI YA KURITHI:

Leo tunasoma kesi ya ELIZABETH MOHAMED v. ADOLF JOHN MAGESA ADMINISTRATION APPEAL (RUFAA YA MIRATHI) NO.14 OF 2011

Haya ni baadhi ya maswali machache ambayo utapata majibu yake ndani ya hii kesi.👇

1: Je, mtu anaweza kufunga ndoa inayoruhusu kuoa mke mmoja tu, na baadaye akaoa tena mke au wanawake wengine wakati bado ndoa yake ya kwanza ipo na inaendelea?

2: Je ndoa ya Kikristo nayo ni ndoa ya mke mmoja inayotambulika kwenye Sheria ya Ndoa au ni vitu viwili tofauti?

3: Je, ukifunga ndoa ya Kikristo, sheria inakukataza kuoa tena mwanamke au wanawake wengine? Kwa lugha nyingine, je sheria inakulazimisha kushika mafundisho ya dini yako?

4: Je, ukifunga ndoa ya Kiislam, tayari (automatic) unakuwa umeruhusiwa kisheria kuoa wanawake wengi (wanne) kama ukitaka?

5: Au je, ukifunga ndoa ya Kiislam ina maana huwezi kuoa wanawake zaidi ya wanne? Je sheria inakulazimisha kushika mafundisho ya Qur'an?

6: Sheria gani itatumika kugawa mirathi kwa Mkristo akifa bila kuacha wosia? Je Wakristo wana sheria za mirathi kama Waislam?

Mwandishi: Zakaria Maseke.
(Advocate Pending Admission).
(0754575246 - WhatsApp).
zakariamaseke@gmail.com

FACTS (Story ya kesi iko hivi): 👇

-Marehemu, John Cosmas Magesa, alikuwa anafanya kazi ya utabibu (medical officer).
-Alifunga ndoa ya Kikristo na Juliana Gerald, mwaka 1988.
-Ndoa yao ilibarikiwa kupata watoto wawili (Adolf John na Anna John).

-Lakini huyu mwanamume, kabla hajafa alikuwa anaishi na wanawake wengine wawili, mmoja anaitwa Elizabeth Mohamed, ambaye hadi alifunga naye ndoa ya kimila, akalipa mahari Shilingi 300,000/=, wakazaa naye watoto watatu

-Mwingine alikuwa anaitwa Pendo Zablon.

-Hivyo marehemu alikuwa na wake watatu, wa ndoa mmoja na wengine wawili pamoja na watoto watano jumla

-BAADAYE HUYU MWANAUME AKAFA BILA KUACHA WOSIA.

-Adolph kijana wa marehemu, akafungua mirathi Mahakama ya Mwanzo, akaomba na akateuliwa kuwa msimamizi wa mirathi)
-Akawekewa pingamizi na mwanamke mwingine kwa jina Elizabeth.

-Mgogoro ulikuwa ni je, hawa watoto watatu ambao marehemu alizaa na yule mwanamke mwingine (Elizabeth Mohamed) wanastahili kurithi mali za baba yao?

-Mahakama ya Mwanzo iliamua kwamba, wale watoto watatu ambao huyu mwanamke alizaa na marehemu John Cosmas wanastahili kurithi mirathi ya baba yao).

-Adolph kijana wa marehemu akakata rufaa Mahakama ya Wilaya.

-Kwenye rufaa, Mahakama ya Wilaya ikatengua maamuzi ya Mahakama ya Mwanzo, ikasema hawastahili.

-Mahakama ya Wilaya ikasema hivi, *“ikiwa huyu mwanamke na marehemu walikuwa na mahusiano ya kimapenzi, wale watoto watatu waliozaa walizaliwa kwenye mahusiano ya uzinzi na hivyo hawawezi kurithi kwenye mirathi ya upande wa baba.”

-Pia Mahakama ya Wilaya ikasema, “amri ya Mahakama ya Mwanzo ya kumkaribisha huyu mwanamke na watoto wake haramu kushiriki matunda ya mirathi ya marehemu iwekwe kando.”

-Mwanamke, Elizabeth Mohammed, akakata rufaa Mahakama kuu.

SASA TUKO MAHAKAMA KUU.

Elizabeth ametinga Mahakama Kuu, analalamika kwamba, Mahakama ya Wilaya ilikosea kuamua kwamba, watoto aliozaa na marehemu walikuwa haramu hivyo hawana haki ya kurithi.

-Kumbuka mgogoro Mahakamani sio uhalali wa ndoa ya pili aliyofunga marehemu, ila ni uhalali wa watoto waliopatikana kwenye hiyo ndoa ya pili.

-Wakili wa huyu Mwanamke akaiambia Mahakama kwamba, irejee maamuzi yake kwenye kesi nyingine ya Chacha Malima dhidi ya Mwita Kitogo ya mwaka 1986, ukurasa wa 119 ambapo Mheshimiwa Jaji Katiti kwenye hiyo kesi, alizungumzia jinsi ya kuhalalisha mtoto haramu.

-Jaji Katiti alisema, kwa mujibu wa vifungu vya 181A and B vya sheria ya kimila, (the Customary Law (Declaration) order 1963), kuna njia mbili ambazo zinaweza kutumika kumhalalisha mtoto haramu.

-Ambapo baba wa mtoto (kibayolojia) aliyetajwa na mama au ambaye anakubalika kama baba kwa asili, ndo anaweza kumhalalisha mtoto:-

1: Moja, ama kwa kumuoa mama wa mtoto (by either marrying the mother).
2: Au, pili bila kumuoa mama wa mtoto ila kwa kulipa shilingi 100 (or without marrying the child’s mother by paying T.shs 100/=)

(Usishtuke hizi ni sheria za zamani sana na hii kesi ni ya mwaka 2011, kabla hiyo dhana ya mtoto haramu haijapigwa marufuku na Mahakama nchini. Mi nakuelezea kesi husika kama ilivyokuwa)

-Tuendeleee.

-Kwa kifupi Mahakama ikasema, vitu vya kuzingatia ili kuamua haki ya mtoto kurithi ni ama, marehemu awe ni baba kibayolojia (biological farther) au anayekubalika kuwa baba wa mtoto (or acceptably father of the child).

-Na kwenye hii kesi, vyote viwili vilikuwepo, maana marehemu alikuwa baba mzazi (kibayolojia) wa wale watoto watatu aliozaa na Elizabeth Mohamed.

-Na hata Adolf, kijana wa marehemu anakubali hilo kwa maelezo yake aliyotoa Mahakamani ambapo alisema, “Marehemu alikuwa na miji mitatu, mkubwa ukiwa Magu. Katika mji wa katikati kuna watoto lakini sipaswi kuwaweka katika faili hili kwa kuogopa kutenda dhambi kushuhudia watoto wa nje ya Ndoa.”

-Adolf alichokuwa anapinga ni uhalali wa ndoa ya marehemu baba yake na hao wanawake wengine.

-Anasema, kwa sababu baba yake alikuwa Mkristo na alikufa na kuzikwa Kikristo, hiyo ndoa yake ya pili sio halali, hivyo hata hao watoto waliopatikana huko ni haramu.

- Kabla ya kuendelea kuamua kuhusu uhalali au uharamu wa watoto ambao Elizabeth Mohammed alizaa na marehemu, Jaji akaanza kwanza na hoja ya ndoa kati ya marehemu na huyu mwanamke.

-Akaanza kuichambua sheria ya ndoa, akasema “kwa mujibu wa kifungu cha 38, kifungu kidogo cha kwanza, aya c (Section 38(1) c) of the Law of Marriage Act [Cap 29 R.E. 2002] (sasa hivi ni R.E 2019),

Shughuli yoyote yenye mwelekeo wa kuwa ndoa ni batili kama, mmoja wa wahusika ana ndoa nyingine. (a ceremony purporting to be a marriage is a nullity if either party is incompetent to marry by reason of an existing marriage).

Section 15(1) ya sheria hiyo hiyo inasema, hakuna mtu ambaye ameoa kwa aina ya ndoa inayoruhusu mwanamke mmoja tu, atakayeruhusiwa kufunga ndoa nyingine tena (no man while married by monogamous marriage, shall contract another marriage).

-Kijana wa marehemu anadai kwamba hiyo ndoa nyingine kati ya marehemu na Elizabeth Mohammed ni batili kwa sababu bado kulikuwa na ndoa nyingine inayoendelea kati ya baba yake na mama yake (Juliana Gerald - mke wa kwanza).

-Na mke wa kwanza Juliana Gerald (mama yake Adolf) alishuhudia mbele ya Mahakama ya Mwanzo akidai alikuwa mke halali wa marehemu, lakini hakutoa ushahidi wowote kama vile cheti cha ndoa au kithibitisho chochote n.k, ili Mahakama ijue kama aina ya ndoa waliyofunga ni ile inayoruhusu mwanamke mmoja tu (monogamous) na hivyo kumzuia mwanaume asioe tena?

-Jaji akasema, ingawa hoja hii haikupingwa Mahakamani, lakini kukosekana kwa huo ushahidi, na ukizingatia mwenzi mmoja wa ndoa ni marehemu hawezi kuja kutoa ushahidi, basi haikuwa sahihi kwa kitendo cha Mahakama ya Wilaya kubatilisha maamuzi ya Mahakama ya Mwanzo na kutamka kuwa ndoa kati ya marehemu na Elizabeth Mohammed ni batili.

-Jaji akaendelea kusema, haitoshi tu Juliana kuiambia Mahakama kwa mdomo kwamba aliolewa na marehemu kwa ndoa ya Kikristo, BILA KUFAFANUA KAMA NDOA YAKE NA MAREHEMU ILIKUWA YA MKE MMOJA TU (monogamous marriage) au la, au JE NDOA YA KIKRISTO NA NDOA YA MKE MMOJA ni kitu kile kile? (Whether Christian Marriage is the same thing as Monogamous marriage contemplated under the provisions of Section 15(1) of the LMA)?

-Jaji akaendelea kusema, Ingawa mgogoro sio ndoa kati ya marehemu na Elizabeth Mohammed kwamba ilikuwa halali kisheria au la, au je kwamba marehemu angeweza kuoa mke mwingine wakati kuna ndoa ya kwanza ya Kikristo kati yake na Juliana Gerald? (Issue haikuwa hiyo).

-Ila mgogoro ni kuhusu hawa watoto marehemu aliozaa na Elizabeth Mohammed, je wana haki ya kurithi mali za marehemu?

-Mahakama ikasema, ingawa huo ndo mgogoro hapa, lakini bado ilikuwa ni muhimu kwa Mahakama ya Mwanzo kuchunguza (status ya) mahusiano ya marehemu na hawa wanawake wawili, ili iweze kuamua vizuri hadhi (status) ya wale watoto wa marehemu kwenye mirathi ya baba yao.

-“Tuchukulie kwa mfano, kwamba marehemu alikuwa na ndoa ya Kikristo inayoendea na Juliana Gerald, swali linalofuata ni je, hiyo tu inaweza kuwa sababu tosha ya kubatilisha ndoa yake ya pili (ya kimila) na Elizabeth Mohammed, hivyo kufanya watoto aliozaa naye wawe haramu?” Aliuliza Mheshimiwa Jaji.

- “Kama nilivyokwisha sema, hoja ya ndoa ya Kikristo na Juliana sio mgogoro kwenye hii kesi, lakini hadi kufikia hapa, nalazimika awali ya yote, ku deal (kushughulika) na hii hoja, ambayo kwa mawazo yangu, hupelekea mkanganyiko mkubwa sana katika mahakama zetu.” Alisema Mheshimiwa Jaji.

-“Pili, nitajadili hoja ya watoto wanaozaliwa katika mahusiano kama hayo aliyokuwa nayo marehemu na Elizabeth Mohammed.”

Jaji akaendelea kusema, “kuoa kwa kulingana na imani ya dini ya mtu ni suala la kiimani zaidi kuliko kisheria… Na masuala ya imani au dini yanalindwa na Katiba, lakini yako nje ya Mamlaka ya Mahakama.”

-Mfano, Mahakama haiwezi kumuuliza mtu kwa nini ameamua kubadili dini au kwa nini hashiki maagizo fulani ya dini yake.

-Ibara ya 19(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa mtu haki na uhuru wa kuchagua kwenye masuala ya dini, ikiwemo kubadili dini n.k

- “Ibara hiyo ya 19(1) inahusisha pia na haki ya kuchagua kushika au kutoshika baadhi ya maagizo au maagizo yote ya dini.”

-Mfano Muislam ana uhuru na haki ya kuchagua kutii au kutotii utaratibu wa kuswali swala tano kwa siku, na maamuzi yake hayawezi kuhojiwa katika Mahakama yoyote, kwa sababu uhuru na haki yake vinalindwa Kikatiba. (Lakini hana huo uhuru au haki kwenye Qur'an).

-Vivyo hivyo, Mkristo, mfano marehemu John Cosmas Magesa kwenye hii kesi, alikuwa na haki na uhuru Kikatiba, wa kufata au kutofata kanuni ya mume mmoja - mke mmoja (had the right and freedom under the Constitution of this country to observe or not to observe the Canon norm of one man one wife).

-Huo uhuru hauwezi kuhojiwa Mahakamani.

-Lakini, huo uhuru haupo kwenye Biblia.

-Mahakama Kuu ikasema, “Kuna kifungu kwenye Biblia, ambapo Yesu aliulizwa na Mafarisayo awaambie kama, sheria yao inaruhusu kumpa talaka mwanamke?”

-Yesu alijibu kwa kuwauliza swali, “Musa aliwaamuru nini?” Waliposema, “Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.”

- Yesu akawaambia, “Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe…”

-Baadae jioni walipokuwa nyumbani, wanafunzi wa Yesu wakamwuliza habari ya neno hilo.

Yesu Akawaambia, kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake, na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.

-Jaji akataja kwamba hayo maneno ameyatoa Marko 10:2-12.

-Kwa hiyo kwa mujibu wa Biblia, kitendo cha marehemu kumuoa Elizabeth, ilikuwa ni uzinzi, lakini haiko hivyo kwenye hii Mahakama.

-Uamuzi wa marehemu kutofata hiyo sheria au huo utaratibu ungeweza tu kuhojiwa au kulalamikiwa na Juliana Gerald (mke wake) ambaye ndiye walikuwa na mkataba wa ndoa, na eneo sahihi lingekuwa kwenye MAHAKAMA YA KANISA.

-Vinginevyo, Juliana akitaka kulalamika mbele ya Mahakama ya kisheria, basi lazima atoe cheti cha ndoa, kuthibitisha kwamba, ndoa yao haikuwa tu ya Kikristo, ila pia ya mke mmoja tu. (Upon producing a certificate of marriage certifying that their marriage was not only a Christian, but also a monogamous marriage).

-Lakini kama marehemu alimuoa Juliana ndoa ya Kikristo, na kama ndoa ya Kikristo inakataza kufunga ndoa ya pili wakati bado ile ya kwanza haijavunjika, hilo ni suala la kuamuliwa na Mahakama za Kanisa.

-Jaji akaendelea kukazia hii hoja, akasema “Imekuwa kawaida kwa mahakama zetu, zinapokutana na kesi inayohusu ndoa, zinachukulia kwamba, ikiwa watu wameoana ndoa ya Kikristo basi lazima itakuwa ya mke mmoja tu (that where the parties are married according to Christian rites, the marriage must be monogamous).

- Na ikiwa watu wameoana ndoa ya Kiislam, ndoa yao lazima itakuwa ya wanawake wengi (and where parties are married in accordance with Islamic law, their marriage must be polygamous one).

-Hiyo haiko hivyo wakati wote, (that is not always the case and courts should never make findings on assumption where there are specific prescribed procedures for proving the alleged facts).

-Mahakama zisiwe zinatoa maamuzi kwa kudhani/kukisisia pale kunapokuwa na hatua maalum zilizowekwa kisheria za kuthibitisha hoja zinazodaiwa.

-Kisheria, hadhi na uwepo wa ndoa vinaweza tu kuthibitishwa kwa kutoa Mahakamani cheti cha ndoa au kupitia kutoa ushahidi wa ndoa kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 55(a) cha Sheria ya Ndoa.

-Kisheria, ndoa ya Kikristo na ndoa ya mke mmoja haimaanishi ni kitu kimoja. (In law Christian marriages & monogamous marriages are not necessarily the same thing.

-Jaji akasema, Mahakama katika nchi hii hazina mamlaka ya kuhoji migogoro ya ndoa za Kikristo, kufanya hivyo kutaibua hoja ya kutii na kutotii maagizo ya dini.

-Mfano, sio wajibu wa Mahakama hii kumuuliza mwanamume Mkristo, kwa nini ameshindwa kufata kanuni inayomtaka mwanamume kuoa mke mmoja tu? Hili ni suala la kidini, ambalo linaweza tu kusikilizwa na Mahakama za Kanisa.

-Mahakama zijikite tu kuamua ndoa ambazo zimefungwa kwa mujibu wa sheria ya ndoa, bila kujali ni za Kikristo au sio.

Mwisho, Jaji akamalizia hii hoja kwa kusema kwamba, njia pekee iliyopo ya kuhoji kukosa utii kwa marehemu juu ya dini yake, itakuwa ni siku ya UFUFUO, mbele ya Mwenyezi Mungu.

-TURUDI KWENYE MGOGORO WA KESI SASA

-Baada ya hayo, Jaji akaja sasa kuamua suala ambalo ndo mgogoro hasa kwenye hii kesi.

-Mgogoro ni je, watoto wa Elizabeth Mohammed wanastahili kurithi kwenye mirathi ya marehemu baba yao?

-Mahakama ilirejea kesi au maamuzi ya zamani (yaliyotangulia kutolewa na Mahakama) ambayo yalikataza watoto waliozaliwa nje ya ndoa kurithi, kama vile maamuzi ya Mahakama ya Rufani, kwenye kesi ya Violet Ishengoma Kahangwa and Jovin Mutabuzi v. The Administrator General and Mrs. Eudokia Kahangwa, kesi ya mwaka 1990

-Jaji akasema, hadhani kama maamuzi kwenye hiyo kesi bado ni sheria nzuri kwa Tanzania leo hii. Hasa baada ya kutungwa kwa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, kifungu cha 5, 9 na 10.

-Kwa sababu wakati maamuzi hayo yanafanyika Sheria ya Mtoto ya mwaka, 2009 haikuwepo.

-Pia maamuzi hayo yalijikita (walitumia) sana kwenye sheria za kimila za Wahaya, ambazo zilikuwa zinakataza watoto haramu kurithi, ambayo ndio sheria pia iliyotumika mwaka 2010, na Mahakama ya Wilaya kwenye hii kesi kuwakataa wale watoto wa Elizabeth wasirithi.

-Mahakama ikasema, sheria ya kimila ya Wahaya kwa wakati huo haikuwa kwa kweli inapingana na sheria za Tanzania, za wakati huo.

-Lakini kwa sasa, sheria kama hizo zinazokataa watoto waliozaliwa nje ya ndoa kurithi zinapingana na Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, hasa kifungu cha tano.

-Hivyo, Mahakama ikasema sheria ya Kimila ya Wahaya iliyotumika kwenye hii kesi na Mahakama ya Wilaya kuwakatalia watoto waliozaliwa nje ya ndoa wasirithi haifai, kwanza inambambika mtoto dhambi ambayo hakushiriki kuifanya.

-Mahakama ikasema kwa sasa, ni ubaguzi na kinyume cha ubinadamu kumuita, haramu, mtoto ambaye amezaliwa na wazazi ambao hawajaoana, ambapo kimsingi inamaanisha sio mtoto halali kisheria. (It is discriminative and inhumane to call a child born of parents who are not married to each other an illegitimate child which in essence means that he/she is an unlawful child.

-Mahusiano ya wazazi yanaweza kuwa haramu au sio halali kisheria, kulingana na kanuni za jamii au dini husika, LAKINI KILICHOPATIKANA katika muungano huo, yaani binadamu aliyezaliwa kama matokeo ya mahusiano hayo, hawezi kwa maana yoyote kisheria kuwa sio halali katika taifa lisilo na mfungamano wa itikadi kama la kwetu. (The association of the parents may be illegitimate or unlawfully according to the norms of a given society and/or religion but the product of such association, that is a human being born as a result of such association cannot by any legal definition be illegal and/ or unlawful in a secular state like ours.

-Bahati nzuri, watunga sheria wa nchi hii waliligundua hilo kosa la ukoloni, na wakafuta huko kukataliwa kwa kutunga Sheria ya mtoto (the Law of Child Act, 2009).

-Utangulizi wa sheria hiyo unasema, ilitungwa kutekeleza (it was enacted to give effect) mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia na kusaini.

-Kifungu cha 5(2) cha sheria hiyo (ya mtoto) kinapiga marufuku ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya mtoto.

-Kifungu cha 10 cha sheria hiyo hiyo kinampa mtoto haki ya kunufaika na mali ya mzazi wake.

-Kifungu cha 9 cha sheria hiyo hiyo kinampa mzazi wajibu wa kumtunza mtoto wakati wa uhai wake. Na kuna ushahidi kwamba marehemu alitimiza wajibu wake kwa kuwatunza watoto wake, wakiwemo wale watatu wa Elizabeth.

-Adolf, Kijana wa marehemu aliendelea kushikilia hoja yake kwamba, watoto watatu wa Elizabeth hawana haki ya kurithi kwa sababu, Mkristo hawezi kuoa mke mwingine, wakati ndoa yake ya kwanza bado ipo.

-Mahakama ikasema hata ndoa ya huyu kijana na mama yake (Juliana-mke wa kwanza) pia haiko wazi, maana cheti cha ndoa hakikuonekana.

-Mwisho, Mahakama ikaamua kwamba, hawa watoto watatu wa Elizabeth wanastahili kurithi.

-Mahakama ikakubali rufaa ya Elizabeth Mohammed, na kuamuru watoto wake waingizwe kweny orodha ya warithi wa marehemu John Cosmas Magesa.

-Mwisho Mahakama ikahama kwenye hiyo hoja, ikaendelea kutafuta sheria gani itumike kugawa mirathi ya marehemu kwenye hii kesi.

-Marehemu hakuacha wosia.

-Wakatumia sheria ya serikali (Indian Succession Act) maana Wakristo hawana Sheria maalum za mirathi kama Waislam.

Uchambuzi wa kesi hii umeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke - Advocate/Wakili.
(0754575246)
(0746575259 - WhatsApp).
(zakariamaseke@gmail.com)

Mungu akubariki.

-Unaweza kusambaza hii kesi ila usibadili yaliyomo.
-Hizi kesi zipo mtandaoni ukitaka kujiridhisha au kusoma mwenyewe, ila kwa kiingereza. Ingia website inaitwa (Tanzlii).

-Kind regards-
 
Safi sana kwa uchambuzi wakili. Ninaomba nakala au link ya kesi hiyo.
 
Ukristo na Uislam ni falsafa ambazo hazitakiwi kabisa kuingilia sheria zetu. Ni falsafa zilizotawala zama za kale za ujima na ni falasafa za watu wa Mashariki ya Kati.

Tatizo moja kubwa sana ni kwamba falsafa hizi huingizwa kwenye vichwa vya waTanzania kuanzia utotoni wakati ambapo hawajitambui. Wakati sheria ya nchi huanza kufundishwa vyuoni tu. Kwenye ngazi za chini za shule za msingi sheria haifundishwi.

Hivyo waTanzania wengi sana kwa kuwa hawafiki vyuoni (na hata wale wachache wanaofika vyuoni wengi wao hawasomei sheria) hawajui sheria za nchi, bali wanajua sheria za Ukristo na Uislam. Hili ni tatizo kubwa sana katika jamii maana waTanzania wengi wanadhani sheria za Ukristo na Uislam ndo sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom