Ni muda sasa tunatakiwa kuwa na sheria inayomtaka Rais kuendeleza alichokiacha mtangulizi wake na sio kuendesha nchi kwa maono yake

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
May 10, 2013
740
855
Katika mamia ya sheria nilizowahi kuzisoma hapa nchini Tanzania sijwahi kukutana na sheria inayomtaka Rais kuendeleza kile alichokianzisha mtangulizi wake, na badala yake nchi huwa ikiendeshwa kwa maono ya Rais aliyeoko madarakani.Tuna ushaidi kwa namna gani nchi imekuwa ikipoteza mamia ya pesa kutokana na kutokuwa na sheria kama hii.

Mfano wakati wa uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kuliibuliwa mamia ya miradi mikubwa na midogo na kabla ya kumaliza ukamilishaji wa miradi hiyo tarehe 17/03/2021 tukatangaziwa kuwa nchi imepoteza Rais kwa ugonjwa wa umeme wa moyo, watu wengi wakaingiwa na hofu ya kuwa je Rais anayekuwa anaweza kweli kumalizia ile miradi? na hii inakuja kutokana na kutokuwa na sheria, palekuwa miradi mikubwa kama Mwalimu Nyerere kule Rufiji, ufufuaji wa shirika la ndege kwa kununua ndege, mradi wa ujenzi wa reli ya treni ya kisasa n.k.

Nipende kumpongeza Raisi wa sasa kwa maono yake binafsi ya kuendeleza hii miradi ambayo ilitumia mamilioni ya pesa za ndani na mikopo kwani maono yake na uzalendo wake ndivyo vimemshinikiza kuendeleza kwani hakuna sheria inayomshikiza kuiendeleza.Imagine asingeendeleza tungekuwa tumepoteza mapesa mangapi?. Ni muda sasa kuletwa kwa sheria inayomtaka Raisi kuendeleza na kutekeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake.

''Sheria bora ndizo zinazo determine mustakabali wa nchi husika''

Pia soma Hivi kuna Sheria inayolinda miradi iliyoanzishwa na Rais John Magufuli?
 
Naunga mkono hoja, hata kama hakuna sheria rasmi, nchi inaendeshwa kwa katiba, sheria, taratibu na kanuni, miradi yote ya maendeleo ina
mikataba, na kuna
kipengele cha continuity anapopokea ofisi, Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?
P
Madaraka na nguvu zote za serikali (Rais) zinatoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba.
Sasa wale wanaompa madaraka na nguvu wakishindwa kumdhibiti halafu wakalalamika tuwaweke kwenye kundi la watu gani kiakili?
Msingi wa umasikini wa taifa umejengeka hapa.
 
Katika mamia ya sheria nilizowahi kuzisoma hapa nchini Tanzania sijwahi kukutana na sheria inayomtaka Rais kuendeleza kile alichokianzisha mtangulizi wake, na badala yake nchi huwa ikiendeshwa kwa maono ya Rais aliyeoko madarakani.Tuna ushaidi kwa namna gani nchi imekuwa ikipoteza mamia ya pesa kutokana na kutokuwa na sheria kama hii.

Mfano wakati wa uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kuliibuliwa mamia ya miradi mikubwa na midogo na kabla ya kumaliza ukamilishaji wa miradi hiyo tarehe 17/03/2021 tukatangaziwa kuwa nchi imepoteza Rais kwa ugonjwa wa umeme wa moyo, watu wengi wakaingiwa na hofu ya kuwa je Rais anayekuwa anaweza kweli kumalizia ile miradi? na hii inakuja kutokana na kutokuwa na sheria, palekuwa miradi mikubwa kama Mwalimu Nyerere kule Rufiji, ufufuaji wa shirika la ndege kwa kununua ndege, mradi wa ujenzi wa reli ya treni ya kisasa n.k.

Nipende kumpongeza Raisi wa sasa kwa maono yake binafsi ya kuendeleza hii miradi ambayo ilitumia mamilioni ya pesa za ndani na mikopo kwani maono yake na uzalendo wake ndivyo vimemshinikiza kuendeleza kwani hakuna sheria inayomshikiza kuiendeleza.Imagine asingeendeleza tungekuwa tumepoteza mapesa mangapi?. Ni muda sasa kuletwa kwa sheria inayomtaka Raisi kuendeleza na kutekeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake.

''Sheria bora ndizo zinazo determine mustakabali wa nchi husika''

Pia soma Hivi kuna Sheria inayolinda miradi iliyoanzishwa na Rais John Magufuli?
CHa muhimu siyo kuendeleza ya mtangulizi wake maana mengine yanaweza kuwa mtangulizi alikosea na alifanya kwa utashi wake na si maslahi ya nchi, cha msingi kuwe na vision kama nchi na maraisi wote waifuate hiyo vision kama mabadiliko basi yapitishwe bungeni
 
Mi sikubaliani.

Nnaona rais acha aendelee kuwa rais. Mfalme haswaa kwa wakati wake.

Acha atoe maamuzi na ayafanyie kazi. Na ndio atayafanyia kazi kikamilifu na kwa raha..... no kwa FURAHA.

Tatizo tutalitengeneza, rais hatakuwa 'responsible' na mradi wowote maana hayakuwa maoni yake wala.

Halafuu hii 'trend' ya kutaka kuwaondoa binadamu (atapatia na kukosea pia) lakini mwisho wa siku ni mtu fulani mwenye mamlaka na kuweka mifumo. Basi ndio mwisho wa siku mtakataa rais kuwa mwanadamu mtataka awe AI tu ndio rais.

Chagueni hamuwataki wanadamu mnataka mashine au?
 
Mada nzuri mno,nchi inahitaji TAASISI IMARA ZENYE KUJITEGEMEA kisheria,taasisi hizi zitatuletea utawala bora na SIO mihemko ya mpangaji mkuu wa magogoni,BUNGE huru litunge sheria,UTAWALA watekeleze hizi sheria na JUDICIARY watafsiri hizi sheria, uzuri wa kuwa na taasisi imara ni pamoja na HAKI ya kuwajibika kisheria,mfano mmoja tu;mahabusu anapofia kituo cha police au suspect anapokufa kwenye mapambano na police,police hapa wanakua ni suspects pia, hawawezi kujichunguza, ila tukiwa na IPID kisheria,hawa wana uwezo wa kuchunguza na kutoa uamuzi ulio neutral, pia wana uwezo wa to arrest na kumfikisha mahakamani police
 
Back
Top Bottom