Kiongozi asiye na dira huishia kuendesha nchi kupitia mashinikizo

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,755
Tumekuwa na ombwe kubwa la uongozi wa nchi yetu tangu awamu ya sita ichukue hatamu.

Kuhamisha wamaasai kutoka Loliondo ili kuwakabidhi Waarabu kipande cha ardhi kumezalisha shinikizo la jumuiya za utetezi wa Haki za binadamu.

Rais anayeshikiza kumtoa Spika madarakani kwa kutoa maoni yake juu ya kasi yake ya kuliingiza Taifa kwenye mikopo mikubwa isiyovumilika, inetuletea matanga mapya ya bunge lisilo hai kufa tena.

Mkataba wa Hovyo wa DPW umetuzalia shinikizo la wananchi kudai Tanganyika yao baada ya kugundulika kuwa mkataba huo unainyonga Tanzania Bara kwa 100%.

Wananchi wanashinikiza serikali kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya ya Wananchi.

Serikali inashinikiza Bunge kupitisha sheria za hovyo ikiwemo ya kinga jinai kwa maafisa wa Usalama wa Taifa.

Ikulu kushinikiza ripoti ya CAG kutojadiliwa Bungeni ili kuwalinda viongozi waandamizi dhidi ya ufisadi mkubwa wanaoendelea kuufanya Kila upande ni shinikizo juu ya shinikizo.

Rais anayesimama kujibu hoja ngumu kwa kusema ameamua kunyamaza kimya ni wazi amekosa mwelekeo na hana dira ya wapi anaipeleka nchi.

Kila leo tunaona bora jana. Kiongozi aina hiyo hafai kuaminiwa kushika hatamu za nchi. 2025 ipo mlangoni.
 
Back
Top Bottom