Ni kweli mchumba hasomeshwi?

Ni kweli mchumba hasomeshwi?

Mkuu mimi nilijipa moyo kama wewe lakini leo nakumbuka maneno niliyoyaona kuwa ni kejeli toka kwa wadau humu JF nikasinga kuhudumia dem wangu aliyekuwa ccp na nikaenda mbali zaidi kwa kumpeleka mdogo wake shule baada ya kuona kashindwa kutokana na familia yake kukosa pesa. Mkuu katafute uzi huu humu JF "MCHUMBA KAENDA CCP" halafu upitie taratibu then nitafute nitakupa somo hata kwa simu mimi nitakupigia tu nikueleza kijana mwenzangu.
NEVER TAKE A GIRL TO SCHOOL NOR COLLEGE FOR THE SAKE OF MARRIAGE.

Never without a signed agreement!
 
Anasomeshwa lakini lazima kuwe na mkataba ambao utasimamiwa na lawyer i.e. notary public ili kuahakikisha kama mkataba ukivunjwa basi pesa inarudishwa na ka-interest kidogo. Na ni gharama zote kuanzia accommodation, meals, books, stationery, transport, clothing, research, etc. Huyo mchumba akikataa ku-sign hiyo contract basi ujue hapo hamna kitu. Ila mke wa ndoa ndio wa kusomesha kwa sababu tayari unaye na elimu yake ni guaranteed kunufaisha familia yako.
Nimekuelewa sana ndg.
Nashkuru sana kwa ushauri mxuri.
 
Tatizo majukumu ya mzaz anapewa Mpenz yani mtu ankula Ada halafu anakuomba Umlipie haha? Si Ubwege huo
 
Anasomeshwa lakini lazima kuwe na mkataba ambao utasimamiwa na lawyer i.e. notary public ili kuahakikisha kama mkataba ukivunjwa basi pesa inarudishwa na ka-interest kidogo. Na ni gharama zote kuanzia accommodation, meals, books, stationery, transport, clothing, research, etc. Huyo mchumba akikataa ku-sign hiyo contract basi ujue hapo hamna kitu. Ila mke wa ndoa ndio wa kusomesha kwa sababu tayari unaye na elimu yake ni guaranteed kunufaisha familia yako.
 
aaaah hata akitokea yule siwezi kumuacha nitachepuka nae tu kwa siri asijue lakini kumuacha hapana, namuonea huruma mkaka wa watu

kumbe unamwonea huruma na sio kumpenda? !!!! usiwe na mtu kwa ajili ya huruma itafika siku atajuta kuzaliwa
 
si kweli mbona mie nasomeshwa na mchumba'ngu na sina mawazo ya kumuacha labda kama ulikuwa unapenda msaada wake na si mwenyewe

aaaah hata akitokea yule siwezi kumuacha nitachepuka nae tu kwa siri asijue lakini kumuacha hapana, namuonea huruma mkaka wa watu
Et utachepuka kwa siri.... Ha haaa...
siko nae sababu ya kumuonea huruma nadhani nampenda sana sana ndo maana namuonea huruma.
happymsafi mi pia nasomesha.... Isije ikawa niwewe
 
Oa kwanza ndio umsomeshe,
Kasheshe ipo kama kana miaka 15 unakasomesha ili kakue wakati unasubiri kukaoa.
 
Usijaribu kabisa uta baki na manyoya tu na mfano hai mchizi amesomsha tena secondary kwa ridhaa ya wazazi kabisa mwisho wa siku harusi kubwa na msela mwingine
 
Mepenzi ni ugonjwa hatari sana kaka, unajua tena ukizama ni ngumu kutoka...
Zuia kuzama mapema
1467725625547.jpg
 
Kama unania ya kumsomeaha n kumsaidia assume unamsomesha yatima ili usitegemee chochote kwake, kama memsaidia tu, tatizo watu huwa na high expectations matokeo yake vitu vikiwa tofaut ni stress tu mwishowe uchiz au kujiua
 
Mkuu usijaribu, labda muwe marafiki kwanza mpaka hapo atakapomaliza.

Mimi ilishanitokea nilikuwa nasaidia gharama pale nilipoweza. Alikuwa anasoma mkoa na mm Niko mkoa mwingine. Mawasiliano yalikuwa mazuri tu.

Alipobakisha miezi minne tu kumaliza kimbembe kikaanza, mzee naambiwa mm Na we basi, hatuwezi kuendelea kama zamani.

Trust me, hao watu akili zao huwa za mkumbo na hubadilika muda wowote, hawajali wala, hasa kama mko mbali
 
Lakini pia Mtoa mada mbona watonesha watu majeraha walikuwa wameshasahau?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom