Ni kweli mchumba hasomeshwi?

tatizo elimu ni kitu ambacho mtu akishakipata hakiondoki kichwani wala huwezi kumnyang'anya. Ingekuwa inawezekana ungefuta kichwani vyote alivyosoma abaki kama awali ila uwezo huo haupo. Utachukua vyeti na ataenda kuchukua certified copies na atatumia kama kawaida. Inauma sana mkuu
Unabaki navyo kama kumbukumbu tu kama dr.slaa alivyobaki na kadi ya ccm
 
Ole wenu nyie vijana na wanaume mnaojifanya mnajua kupenda na kuwagharamia mabinti kwa madai eti ni wachumba wenu hali ya kuwa makwao hamfahamiki. Mwisho mnakijikuta mnawatunzia wenzenu. Hakuna swala bila ya udhu.
 
Me wangu nimemsomesha mwenyewe na hivi sasa tuna watoto 3 ana kazi nzuri na maisha yanaenda fureeesh.....natafuta mchepuko nao niupekeke shule, kama pesa iko hata ikikuacha haina shida si umemtengenezea life yake? Tenda wema kimbia.
 
Mkuu mimi nilijipa moyo kama wewe lakini leo nakumbuka maneno niliyoyaona kuwa ni kejeli toka kwa wadau humu JF nikasinga kuhudumia dem wangu aliyekuwa ccp na nikaenda mbali zaidi kwa kumpeleka mdogo wake shule baada ya kuona kashindwa kutokana na familia yake kukosa pesa. Mkuu katafute uzi huu humu JF "MCHUMBA KAENDA CCP" halafu upitie taratibu then nitafute nitakupa somo hata kwa simu mimi nitakupigia tu nikueleza kijana mwenzangu.
NEVER TAKE A GIRL TO SCHOOL NOR COLLEGE FOR THE SAKE OF MARRIAGE.
Mkuu mi naona nikikutafuta utaniongezea stress..Hiki kikombe ngoja nikikabiri tu..Thanx btw
 
Utamkumbuka chris brown na lil wayne walivyoimba these girls ain't loyal... Kipindi hicho mtoto ndio kamaliza research *****!!! Full Nyodo huku akikwambia we sio type yakeee mxieeeewwww!!!
 
Napanga kuwaletea mrejesho wa nguvu kuhusu haya mambo ila bado naumia kwanza nikipoa nitawaletea. Ila kwa kifupi "usithubutu kumsonesha mchumba vinginevyo ufanye hivyo kwa moyo mweupe kama unachangia kapu la kanisa na utabarikiwa mbali na hapo utakuja kufa kwa presha siku huyo mchumba atakapokupiga chini na kukuambia piga gharama zako ulizonipa nitakulipa"
Ila kugonga ruksa?
 
si kweli mbona mie nasomeshwa na mchumba'ngu na sina mawazo ya kumuacha labda kama ulikuwa unapenda msaada wake na si mwenyewe
 
Salaam ndugu zangu,

Upo usemi usemao mchumba hasomeshwi.

Kila uchao na uchwao kumekuwa na vilio vingi kwa vijana wa kiume waliojitolea kuwasomesha wachumba zao kabla ya kufunga ndoa ila baadae huambulia maumivu makali baada ya kusalitiwa au kutelekezwa kabisa.

b0ebdcbdc1b43490d203752fefb2ed20.jpg

Tatizo ni nini hasa mpaka nyinyi akina dada kufikia maamuzi hayo?

Kijana wa kiume yakikukuta haya utafanyaje?

Naomba kila mmoja atoe yake ya moyoni au ushuhuda kuhusu jambo hili.

Nawasilisha.
Ni kweli mchumba hasomeshwi kwa sababu!

Jukumu la kusomesha ni la mzazi ,mlezi au ndugu wa mhusika!

Ukisha anza kumsomesha mpenzi moja kwa moja umechukua majukumu ya watu nilio wataja hapo juu!

Hivyo utakuwa huna tofauti na hao watu hapo juu!

Kimsingi watu nilio wataja hapo juu kama ndugu,wazazi na walezi hawana uwezo wa kulala nae au kutembea na binti yao na hata wakifanya hivyo ni laana!

Hivyo basi kwakuwa wewe umegeuka Baba na mama au walezi wake hatoweza kutembea na wewe itambidi atafute mtu mwingine!

Ndio maana wengi walio fanya majukumu hayo ya wazazi waliachwa na si bahati mbaya bali ndio taratibu!

Hivyo kama una hela za kusomesha basi msomeshi ndugu yako na si mtu unaye taka kulala nae.
 
SIO WOTE WANAKUJA KUOTA MAPEMBE...SASA KWA MFANO KAMA SINA WAZAZI TANGU UDOGONI NASAIDIWA TU THEN NIMEKOSA ADA YA KUJIUNGA CHUO JAPO NKAPATA KADIPLOMA,NAKUTANA NA MWANAUME ANANIHITAJI KIMAHUSIANO SERIOUS NA NAMWAMBIA UKWELI NNA SHIDA NA NAPENDA KUTIMIZA NDOTO ZANGU NAOMBA UWE SEHEMU YA MSAADA KWANGU...HALAF YE ANANIJIBU "POLE BBY,MUNGU ATAKUSAIDIA...BASI JITAHIDI KUTAFUTA MSAADA HIVOHIVO UENDE CHUO..BLAH BLAH BLAH!!!
HIVI MNAELEWA MAANA YA NENO NAKUPENDA AU MNALITAMKA TU?WHY MNAGERALIZE ISHU YA MMOJA KUWA WOTE WAKO HIVO?
 
Ni kweli mchumba hasomeshwi kwa sababu!

Jukumu la kusomesha ni la mzazi ,mlezi au ndugu wa mhusika!

Ukisha anza kumsomesha mpenzi moja kwa moja umechukua majukumu ya watu nilio wataja hapo juu!

Hivyo utakuwa huna tofauti na hao watu hapo juu!

Kimsingi watu nilio wataja hapo juu kama ndugu,wazazi na walezi hawana uwezo wa kulala nae au kutembea na binti yao na hata wakifanya hivyo ni laana!

Hivyo basi kwakuwa wewe umegeuka Baba na mama au walezi wake hatoweza kutembea na wewe itambidi atafute mtu mwingine!

Ndio maana wengi walio fanya majukumu hayo ya wazazi waliachwa na si bahati mbaya bali ndio taratibu!

Hivyo kama una hela za kusomesha basi msomeshi ndugu yako na si mtu unaye taka kulala nae.

loya hahahahah ndio maana hata mke akisomeshwa anaanza kudharahau kumbe ni laana lol
 
Salaam ndugu zangu,

Upo usemi usemao mchumba hasomeshwi.

Kila uchao na uchwao kumekuwa na vilio vingi kwa vijana wa kiume waliojitolea kuwasomesha wachumba zao kabla ya kufunga ndoa ila baadae huambulia maumivu makali baada ya kusalitiwa au kutelekezwa kabisa.

b0ebdcbdc1b43490d203752fefb2ed20.jpg

Tatizo ni nini hasa mpaka nyinyi akina dada kufikia maamuzi hayo?

Kijana wa kiume yakikukuta haya utafanyaje?

Naomba kila mmoja atoe yake ya moyoni au ushuhuda kuhusu jambo hili.

Nawasilisha.

Anasomeshwa lakini lazima kuwe na mkataba ambao utasimamiwa na lawyer i.e. notary public ili kuahakikisha kama mkataba ukivunjwa basi pesa inarudishwa na ka-interest kidogo. Na ni gharama zote kuanzia accommodation, meals, books, stationery, transport, clothing, research, etc. Huyo mchumba akikataa ku-sign hiyo contract basi ujue hapo hamna kitu. Ila mke wa ndoa ndio wa kusomesha kwa sababu tayari unaye na elimu yake ni guaranteed kunufaisha familia yako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom