Ni kweli mchumba hasomeshwi?

Amoxlin

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,782
4,108
Salaam ndugu zangu,

Upo usemi usemao mchumba hasomeshwi.

Kila uchao na uchwao kumekuwa na vilio vingi kwa vijana wa kiume waliojitolea kuwasomesha wachumba zao kabla ya kufunga ndoa ila baadae huambulia maumivu makali baada ya kusalitiwa au kutelekezwa kabisa.

b0ebdcbdc1b43490d203752fefb2ed20.jpg


Tatizo ni nini hasa mpaka nyinyi akina dada kufikia maamuzi hayo?

Kijana wa kiume yakikukuta haya utafanyaje?

Naomba kila mmoja atoe yake ya moyoni au ushuhuda kuhusu jambo hili.

Nawasilisha.
 
Kumsomesha mchumba ni kujitakia maumivu ya moyo tu aisee.

Kuna kademu kangu kamoja ka msingi huko kalifeligi form 4 jamaa akafanya makeke akakapeleka chuo kakamaliza IFM kwa ahadi kuwa atakaoa.

Baadaye jamaa alikaoa bana, wamekaa miaka kama minne hivi ndoa ikawa chungu balaa, kila mmoja mjuaji, kidemu kila mtu anajigegedea, hata mie nimegegedako mara kibao tu.

Ni aibu aisee, kama unataka maisha mazuri na future nzuri tafuta tu aliyesomeshwa na wazazi wake, anakuaga na discpline ya maisha, hawa wa kusomeshwa hawa headache tupu.

Nimeshuhudia zaidi ya watu wanne wakisomesha wachumba wao, lakini mwisho wa siku wanaishia kulia tu aiseee.

Mchumba asomeshwi aisee, utakuja lia, bora usomeshe hata mdogo wako wa kike ipo siku atakusalimia kwa kukupigia magoti sio mchumba aiseee.
 
Labda alimuhudimia akifikiri kashapata mke, na huku aliacha kuendelea kumpaga sera tamu akazidiwa.au pia ilimpa bichwa na kumsema na vineno neno vidogo dogo ambavyo hakumbuki na hajui vinauzi sana.

Au msichana alikuwa tapeli aliyepata buzi laini akamtafuna haswa, huku pembeni analiwa na ampendaye.
 
Napanga kuwaletea mrejesho wa nguvu kuhusu haya mambo ila bado naumia kwanza nikipoa nitawaletea. Ila kwa kifupi "usithubutu kumsonesha mchumba vinginevyo ufanye hivyo kwa moyo mweupe kama unachangia kapu la kanisa na utabarikiwa mbali na hapo utakuja kufa kwa presha siku huyo mchumba atakapokupiga chini na kukuambia piga gharama zako ulizonipa nitakulipa"
 
Mkuu choga pole sana hawa watu hawadhaminiki ila malipo hapa hapa duniani atapata kile anachostahili nawe utapata unachostahili
 
Kuna kabinti nakasomesha jamani.. Nikiona story kama hizi napatwa na wasiwasi kweli..Bora ziwe za uongo aisee
Mkuu mimi nilijipa moyo kama wewe lakini leo nakumbuka maneno niliyoyaona kuwa ni kejeli toka kwa wadau humu JF nikasinga kuhudumia dem wangu aliyekuwa ccp na nikaenda mbali zaidi kwa kumpeleka mdogo wake shule baada ya kuona kashindwa kutokana na familia yake kukosa pesa. Mkuu katafute uzi huu humu JF "MCHUMBA KAENDA CCP" halafu upitie taratibu then nitafute nitakupa somo hata kwa simu mimi nitakupigia tu nikueleza kijana mwenzangu.
NEVER TAKE A GIRL TO SCHOOL NOR COLLEGE FOR THE SAKE OF MARRIAGE.
 
Tunakosea kwa kujifanya tunaoa mke kumbe tunaoa elimu kwa hiyo akija anayetaka kuoa mke anabeba tu.Kwanini usimuoe kwanza alafu ndo umsomeshe?
Wengine wanataka wakishaoa tu wanaanzisha familia hivyo wanaamua kumaliza suala la shule kwanza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom