Ni kuhusu lile Jambazi la Arusha .....

under_score

Senior Member
Nov 2, 2011
190
45
habari za kazi wakuu ?

Kuna tetesi nilizopata hivi punde kuwa lile jambazi sugu lililoua polisi pamoja na kumjeruhi vibaya kwa risasi mkuu mmoja wa polisi huko jijini Arusha takribani wiki mbili zilizopita hatimaye limekamatwa maeneo ya Monduli na kuuwawa na polisi hivi leo, kwa mdau yeyote wa Arusha mwenye taarifa rasmi tunaomba atujuze habari hii ....
 
Kama kweli, kazi nzuri, lakini kuna mijambazi mingine imetuibia miaka nenda rudi halafu inalindwa na hao hao polisi miaka nenda rudi.
 
Hivi unaijua Polisi ya Tz wewe?...... ili kujisafisha na kuonekana wanafanya kazi...wanaweza kufanya chochote hata kutoa taarifa za uongo....
 
Hivi unaijua Polisi ya Tz wewe?...... ili kujisafisha na kuonekana wanafanya kazi...wanaweza kufanya chochote hata kutoa taarifa za uongo....

Ni kweli mkuu wanaweza kumbambikizia raia mwema wakamuua halafu wakasema ni lile jambazi
 
Ni kweli sasa hivi nimepita maeneo ya Polisi kituo kikuu na kuna watu wengi mno, katika kuuliza wamedai kua ni kweli lile jambazi sugu lililokua linatafutwa hatimaye limeuwawa na sasa ninavyoongea watu wanaelekea maeneo ya hospitali ya Mount Meru Mochwari kulihakiki. Welldone jeshi la polisi.
 
hivi unaijua polisi ya tz wewe?...... Ili kujisafisha na kuonekana wanafanya kazi...wanaweza kufanya chochote hata kutoa taarifa za uongo....

si hivyo tu wanaweza
hata kuua raia wa
kawaida baada ya kumkwapulia mali zake
na kumzingizia ujambazi
kama zombie alivyofanya
 
I wish na Mafisadi sugu wangekuwa wanauliwa hivyo kama Majambazi sugu.
 
Polisi wa tanzania, ukiuwa wa kikosini, lazima na wewe uuawe, wanakuwa na hasira na huwezi kujikwamua.
 
Inabidi watu wafatilie ndo huyo au kama alivyofanya zombe kwa wafanyabiashara wa madini wa mahenge? Wasiwe wameua mdokozi wakasema ndo yeye jambazi,mpaka tuakikishe kama ndo lenyewe
 
habari za kazi wakuu ?

Kuna tetesi nilizopata hivi punde kuwa lile jambazi sugu lililoua polisi pamoja na kumjeruhi vibaya kwa risasi mkuu mmoja wa polisi huko jijini Arusha takribani wiki mbili zilizopita hatimaye limekamatwa maeneo ya Monduli na kuuwawa na polisi hivi leo, kwa mdau yeyote wa Arusha mwenye taarifa rasmi tunaomba atujuze habari hii ....

Mbona tena kuna risasi zilikuwa zinarindima jana saa nne usiku maeneo ya Kwa Mrombo? Ni ujambazi tena?
 
habari za kazi wakuu ?

Kuna tetesi nilizopata hivi punde kuwa lile jambazi sugu lililoua polisi pamoja na kumjeruhi vibaya kwa risasi mkuu mmoja wa polisi huko jijini Arusha takribani wiki mbili zilizopita hatimaye limekamatwa maeneo ya Monduli na kuuwawa na polisi hivi leo, kwa mdau yeyote wa Arusha mwenye taarifa rasmi tunaomba atujuze habari hii ....

kama wanaweza kwanini wasimkamate akiwa hai, ili haki itendeke na tusikie ana yepi ya kusema.
My take: Jamaa watakuwa wameua raia mwema, ili kujisafisha kwenye umma, urongo? Why, kila jambazi sugu liuwawe ilhali wahalifu wengine wanakamatwa. I smell something fishy...
 
Well done jeshi la polisi kama ni kweli. Na je hawa walioandikwa lini nao wanashughulikiwa lini?

Attachments

  • mwananchi paper.jpg
    mwananchi paper.jpg
    146.2 KB · Views: 815
Police wa bongo wanajuana na majambazi na wezi wa aina zote! Wanawakamataga only ikitokea kusalitiana au kuhatarisha kazi zao kama issue itaenda kombo!

Hebu fikiria hii; Siku moja tulikuwa Lumumba Street kuremba gari, kwa bahati mbaya mwenzangu akahisi kaibiwa bastola kumbe aliisahau kwenye gari ingine nyumbani, tilipanic ikabidi tuwaulize wale vijana kama wameiona wakakataa, uamuzi ukawa kwenda msimbazi police!
Kufika pale tukaeleza shida yetu then wakamtia ndani jamaa kwa uzembe which i think it was correct!

Bt cha ajabu baada ya muda walinirudia mm wakanambia hio bastola haijaibiwa bwana mtakua lazima mmeisahau mahali hebu pigeni simu nyumabani wapekue kila kona inawezekana ipo huko.

Kwa haraka niliwaza hawa jamaa wanauhakika gani kama haijaibiwa wakati cc ndio wahusika na imeibiwa Lumumba?
Ukichunguza sana utagundua kwamba hawa watu wanamtandao mitaani ya wahalifu kila kona, na kitu kikiibiwa smwhere lazima watajua haraka hata kabla ya kutoa mguu ofisini, mitandao yao hii ndio pia ni informers wa matukio yote ya uhalifu.

Hata gari tuliibiwa pia police walijua fika lipo kimara na linabadilishwa no na rangi, wakasema tukate kitu kidogo wakalifuatilie tukakata mara ya kwanza, ya pili tukaona wanatufanya ATM tukawaambia watupe ripoti tu tuka claim bima vile ubabaishaji ulizidi.

Hii ndio bongo mtu anakula mahali pa kazi , tatizo tu hawa ndugu zetu kazi yao ni muhimu na nyeti kuliko kula kwa kuuza twiga huko ngorongoro.
 
kama wanaweza kwanini wasimkamate akiwa hai, ili haki itendeke na tusikie ana yepi ya kusema.
My take: Jamaa watakuwa wameua raia mwema, ili kujisafisha kwenye umma, urongo? Why, kila jambazi sugu liuwawe ilhali wahalifu wengine wanakamatwa. I smell something fishy...

Na yawezekana pia hilo jambazi lilikuwa ni "mshirika" wao hao mapolisi mkuu, and so wamefanya kuliua haraka ili siri zao zisije julikana, maana kwa mujibu wa redio mbao ilisemekana kwamba kumbe siku ile ya tukio wale jamaa (mapolisi) walikua wameenda kule nyumbani kwa jambazi wakavutie chao!
 
Back
Top Bottom