Sikujua kichaa anayelala nje ya jengo langu ni mpelelezi anayemtafuta gaidi wa Kizungu niliyemuoa bila mimi kujua ni gaidi

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
323
906
SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳🔥
Sehemu ya Kwanza ( 1 )
***************

KILA Mtu
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

Ilikuwa takribani siku nne zimekatika tangu nianze kumuona mwanaume kichaa nje ya jumba langu akiwa ameketi na makorokoro yake, siku ya kwanza niliogopa kidogo kwani alilala hapo na makorokoro yake mpaka kukakucha, siku ya pili pia alifanya hivyo lakini siku ya tatu nilianza kumuhisi vibaya maana vichaa wengi wamekuwa wakitumiwa na majambazi katika kazi zao atakuja karibu na nyumba yako atapiga kambi wewe utajua ni kichaa kumbe ni msoma ramani. Basi nikataka kwenda kunfukuza lakini roho yangu ilisita kwa woga kwani sura yake ilikuwa inatisha vibaya mno, rundo la nywele chafu lilijikusanya kichwani mwake na isitoshe alikuwa anavuta mamisokoto sijui ni bangi au ni gonzo mwenzenu nikajihami hata kumsogelea.

Basi bwana usiku wa siku hiyo kulinyesha mvua kubwa sana, mvua ilipokatika nikatoka nje na tochi kuzunguka nyumba yangu niangalie usalama maana sikuwa na mlinzi bali nilikuwa naishi mimi tu na mke wangu Clara ambaye ni mzungu, naye tulikutana tu hotelini miezi miwili iliyopita nikiwa kwenye safari zangu za kikazi nikamtongoza akaubali basi nikamkaribisha kwangu na mabegi yake niishi naye wakati tukiendelea kufanya mchakato wa kwenda kutambulishana kwa wazazi. Sikukagua mabegi yake kwani sisi waafrika mila zetu ni mwiko kukagua mabegi ya mgeni japo yalikuwa chumbani kwangu.

Basi bwana wakati nazunguka nyumba yangu huku nikitembeza mwanga wa tochi huku na kule ghafla nikamuona yule kichaa akiwa amekaa palepale anapopenda kukaa na alikuwa amenyeshewa na mvua vibaya mno, nikasema potelea mbali hata awe jambazi siwezi kuruhusu binadamu mwenzangu ateseke vile mimi nimelala ndani, kama anaiba aibe tu, mali hizi ni za kutafuta na tutaziacha duniani. Kwanza angekuwa jambazi asingekubali anyeshewe vile yule ni mwendawazimu" Nilijisemea nafsini mwangu na kwa huruma nikaenda kumchukua, lakini kuna kibegi chake chakavu na kilikuwa kimeloana sana aliking'ang'ania licha ya kumtaka akitupe lakini alikataa katakata, nikaona kubishana na chizi ni kujipa kazi nikamchukua vile vile na kibegi chake, nilienda kumuogesha vizuri bila kujali kwani wote ni wanaume, nilimpa nguo zangu safi avae usiku ule kisha nikamuonyesha chumba alale, aliingia chumbani na hakutaka kuachia kibegi chake nilijiuliza "Kwani hicho kibegi kina nini mbona huyu kichaa hataki kukiachia" nilijiuliza sana lakini mwisho niliona ni tabia ya vichaa kung'ang'ania vitu wanavyovipenda.

Basi nilipohakikisha yule kichaa Kalala na mimi nikarudi chumbani kwangu alipo Clara mke wangu ambapo alikuwa amelala tangu mchana, nilipoingia chumbani nikamkuta anajiandaa maana kuna baadhi ya siku alikuwa akitoka usiku kwa madai ya kwamba anaenda kumpa kampani rafiki yake wa kike kule hotelini asibaki mpweke nami sikuwa namkatalia maana huyo rafiki yake ambaye walikuwa wanakaa naye hotelini ndiye aliyeniruhusu niishi naye na hata siku nilipotoka safarini na Clara tulikuja na rafiki yake lakini yeye alifikia hoteli ya mtaa wapili na kwangu. Alidai ana mtu wake mara kwa mara anamtembelea hivyo anataka amkute hotelini na si kwa mtu.

Basi Clara alipoondoka usiku ule nikabaki na maswali kichwani mwangu." Huyu mwanamke licha ya mvua yote hii kunyesha lakini hajaona haja ya kulala hivi ni kweli huwa anaenda kwa rafiki yake? Na begi lake dogo kabeba mbona hili kubwa limetiwa kufuli kuna nini ndani yake? Mh🤔 huku kukaribisha watu usiowafahamu vizuri ndani na mabegi huku hapana?" Niliwaza kisha nikaenda kuchukua plaizi ili nivunje lile kufuli nione ndani ya begi kuna nini halafu nirudishie kufuli kitaalam maana kazi hizo niliziweza.

Basi nikahangaika na kufuli mpaka likachomoka. Nikaanza kufungua nzipu taratibu huku mikono ikinitetemeka, ile natupia macho ndani ya begi😳 ghafla moyo wangu ulipasuka paaa mithili ya ukuni mkavu baada ya kuona slaha kali za kivita ambazo toka nizaliwe sijawahi kuziona. Macho yalinitoka 😳 kama dudumizi lilikabwa na kiazi cha moto kooni, ghafla uso wote ukaloa jasho licha ya chumba changu kuwa na kiyoyozi.. haraka nika.....

Niliyenda kuchukua plaizi ili nivunje lile kufuli kwenye begi la Clara ili nione ndani ya begi kuna nini halafu nirudishie kufuli la watu kitaalam maana kazi hizo niliziweza. Basi nikahangaika na kufuli mpaka likachomoka. Nikaanza kufungua nzipu taratibu huku mikono ikinitetemeka mithili ya mtu aliyeshika kambale ambaye bado yupo hai, basi ile tu natupia macho ndani ya begi😳 ghafla moyo wangu ulipasuka paaa mithili ya ukuni mkavu baada ya kuona slaha kali za kivita ambazo toka nizaliwe sijawahi kuziona. Macho yalinitoka 😳 kama dudumizi lilikabwa na kiazi cha moto kooni, ghafla uso wote ukaloa jasho licha ya chumba changu kuwa na kiyoyozi.. haraka nikaanza taratibu za kulirudishia lile kufuli kwa utaalam zaidi lakini wakati huo mtungo wa mawazo yalikuwa yakipenyeza kichwani kwangu sio kawaida.

"Mh huyu mwanamke anafanya kazi gani, mbona ana silaha kali hivi? au ni jambazi lakini mbona ni mpole vile na sura yake imejaa utashi wa kimahaba kiasi kile, hapana pengine kuna mtu anamtumia lakini jambazi hawezi kuwa na sura tamu kiasi kile" Niliongea mwenyewe kimoyomoyo na kujijibu mwenyewe kiufupi nilikuwa nimepagawa. "Lakini pengine huyu Clara ni jambazi nisijipe moyo kwa upole wake na mapenzi anayonipa kitandani nikamuona ni mwema laaaa hasha ! Hata simba ni hatari sana lakini kwenye mapenzi anatulia kama maji mtungini, hapa nisijipe moyo Brighton nimeangukia kwenye penzi la jambazi yani nimeyakanyaga kama sio kuyatimba" nilijisemea baada ya kumaliza kurudishia kufuli kwenye lile begi.

Nikakaa kitandani kisha nikavuta pumnzi ndefu na kushusha huku mkono ukiwa shavuni kwa mawazo "Mh na huyu kichaa ni kichaa kweli au geresha, kichaa gani anakubali kuogeshwa na apewe nguo nyingine avae bila kuleta utata wowote, sasa mbona na kile kibegi chake chakavu kilichonyeshewa na mvua ameking'ang'ania? kina nini ndani yake? Mbona sura yake ni kama mzungu chotara?

Kuna kitu si bure🤔 huenda ikawa huyu kichaa ni mpelelezi maana ndio kawaida yao unalikuta jitu linajidai chizi kumbe lipo kazini usione minywele ile ukasema chizi hapana ni askari wa usalama aliambiwa afuge manywele na mandevu maana kuna kazi anatakiwa kupewa miaka miwili badae hivyo anatakiwa awe katika muonekano wa kichaa. Inawezekana kabisa na huyu ni mpelelezi, anampeleleza Clara. Jamani Bryhton mimi si nitaambiwa nashirikiana na Clara wakati sijawahi kuiba hata kuku?" Niliwaza huku moyo ukinidunda vibaya mno.

Basi usiku huo wa manane nikatoka chumbani kwangu taratibu kwa mwendo wa kinyonga, nikaenda kusimama mlangoni mwa yule kichaa na kuaikilizia, nilimsikia akkoroma hapo nikabaini Kalala, basi nikajaribu kufungua mlango ajabu mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani na funguo, kidogo nikashangaa na kujiuliza " kichaa gani anafunga mlango kwa ndani au kuna taarifa gani anaficha zisijulikane?" Hapo nikagundua yule si kichaa bali ni mtu maalum katika kitengo maalumu. Basi nikajiongeza kuchungulia ndani kupitia tobo la kuingizia funguo.

Kumbe alifunga mlango na kutoa funguo mlangoni, hapo nikasema yes acha nikachukue funguo ya ziada nifungue taratibu mlango wa huyu kichaa, nichukue kile kibegi nione ndani yake kuna nini ili kujihakikishia kwamba naishi na watu wa aina gani ndani ya nyumba yangu. Nikafanya hivyo hatimaye nikafanikiwa kuingia ndani ya chumba kile..... Jamani Nyieeee..... Nyiee acheni tu kwani baada ya kuzama ndani haraka nika.

" Mh kichaa gani anaetambua kwamba muda wa kulala mlango unatakiwa ufungwe kwa ndania? 🤔Hapana huyu si kichaa bali kuna kitu au ama taarifa anaficha zisijulikane?" Niliwaza na hapo nikagundua yule si kichaa bali ni mtu maalum katika kitengo maalumu na kujifanya kote ni kichaa si kichaa bali pale yupo kazini. Basi mimi nikajiongeza kuchungulia ndani kupitia tobo la kuingizia funguo. Kumbe alifunga mlango na kutoa funguo mlangoni, hapo nikasema yes acha nikachukue funguo ya ziada nifungue taratibu mlango wa huyu kichaa, nichukue kile kibegi nione ndani yake kuna nini ili kujihakikishia kwamba naishi na watu wa aina gani ndani ya nyumba yangu.

Nikafanya hivyo hatimaye nikafanikiwa kuingia ndani ya chumba kile, huku nikitetemeka. Mara ghafla akaacha kukoroma😳 haraka nikakichukua kile kibegi na kutoka nacho nje taratibu kisha nikasimama pale mlangoni kwa muda kidogo nikisikilizia kama ataamka ama laa, mara akaanza tena kukoroma, taratibu nikaufunga ule mlango kwa nje na funguo. Haraka nikaelekea chumbani na kile kibegi chakavu ambacho hata mtoto wa fukara hawezi kubebea madaftari maana kilichakaa mno.

Basi nilipofika chumbani nikaketi Kitandani na kukifungua kile kibegi, kwanza nilikuta mfuko wa plastick uliofungwa, hapo nikagundua mfuko ule ni kwaajili ya kuzuia mvua isiloanishe vitu vilivyopo ndani yake. Nikautoa ule mfuko nje na kuufungua, kwanza nilishangaa 😳 kukuta simu na vitabu viwili, kimoja likiwa ni cha katiba ya America. Nikaikagua ile simu ilikuwa na paswed na iliwekwa vibration, bado tomaso nikaendelea kukagua zaidi ndani ya kile kitabu cha katiba, nilikuta picha ya yule kichaa akiwa amevalia gwanda la Marekani lenye nyota tano, na alikuwa nazifu huwezi kumdhania.

Tomaso niliendelea kukagua huku mikono ikinitetemeka mithili ya mgonjwa wa degedege, nikakuta vitambulisho vingi, usalama wa Taifa na vitengo vingi ambavyo yule kichaa alipitia akiwa kama mtumishi Marekani, nikakuta pasport ya kusafiria na nakala kadhaa. "Mh Mungu wangu yani vitu vyote hivi muhimu asiwe na hata bastola ya kumlinda je akivamiwa maana vyote ni Orginal na sio copy🤔 au bastola kaitoa akaweka uvunguni? Inawezekana" Niliwaza huku nikiendelea kupekua pekua.

Na ndipo ghafla😳 nikakutana na picha ya Clara imewekewa X na kwa nyuma iliandikwa "most wanted" yani anatafutwa kwa udi na uvumba, pia nikaona karatasi inayomuelezea Clara, macho yalinikodoka 😳 huku nikisoma, looo kumbe Clara ni jambazi kuu lililoua mamia ya watu nnchini Marekani yeye na mwenzake, pia akavunja mabenki mengi na kuiba pesa nyingi lakini haitoshi akamuua mtoto wa mbunge wa jimbo la California na ndipo akamua kutoroka yeye na mwenzake na inasemekana walitoroka na silaha kali walizoziiba kwenye kambi ya jeshi la kimarekani, Dah hakika nilikosa nguvu maana ni dhahiri zile silaha kwenye begi la Clara ndizo zilizoibiwa kwenye kambi ya jeshi la kimarekani.

"Mh Bryhton mie sasa nimeingia mkenge huku kushobokea wazungu hovyo na kukaribisha watu nisiowafahamu kwa undani nyumbani kwangu sasa kumeniweka pabaya sijui nifanyaje?🤔" Niliwaza na hapo nikaamua nirudishe taratibu vitu vya yule kichaa chumbani kwake maana alionekana ni mtu hatari sana, kabla sijaamka kitandani pale nilipoketi ili nirudishe vitu vya watu mara 😳 nikamsikia akiongea kwa jazba chumbani kwake tena kwa kingereza "aaaa! Nimeibiwa aaaa hapana haiwezekani" aliongea mwenyewe huku akifungua ule mlango wa chumba chake kwa ufunguo kwani alikuwa na funguo yake tofauti na ile yangu ya ziada niliyotumia kwenda kuchukua kibegi chake ili nimpekue.

Wakati anafungua mlango wake, haraka nikakitupia kile kibegi uvunguni kwangu huku nikitetemeka mpaka meno. Mara nikamsikia akitembea kwenye korido ya kuja chumbani kwangu. Mweee! Mweee ! Mweee Nilizidi kutetemeka na kuhisi haja kubwa ghafla, mara mlango wa chumba changu ukagongwa 😳 hapo nika...

Acheni nirudi maana ingekuwa ni wewe tayari ungeshajinyea walahi?
Unajua nini kiliendelea hakikisha unapomaliza kusoma unalike na kucoment ili usipitwe na moto huu🔥🔥🔥🔥🔥

Muendelezo soma: Sikujua kichaa anayelala nje ya jengo langu ni mpelelezi anayemtafuta gaidi wa Kizungu niliyemuoa bila mimi kujua ni gaidi
 
Sehemu ya Pili

Wakati nataka kurudisha kile kibeki chakavu cha yule kichaa chumbani kwake baada ya kugundua sio kichaa bali ni usalama wa taifa tena la Marekani na pia kibegi kile kilikuwa na nyaraka muhimu ambazo hazitakiwi kuonwa na raia yeyote isipokuwa yeye tu, kwa bahati mbaya ile nanyanyuka kitandani kwangu nilipoketi ili nirudishe mara 😳 nikamsikia anafungua mlango wa chumba chake😳 haraka nikakitupia kile kibegi uvunguni kwangu huku nikitetemeka mpaka meno. Punde nikamsikia tena akitembea kwenye korido ya kuja chumbani kwangu. Mweee! Mweee ! Mweee Nilizidi kutetemeka na kuhisi haja kubwa ya ghafla, mara mlango wa chumba changu ukagongwa 😳 hapo nika na hapo nikajisogeza mpaka mlangoni huku nikitetemea kwa woga, nikaishika kitasa na kufungua mlango, ile nafungua mlango tu ghafala nikashtukia nimenyooshewa bastola🥹 nilinyoosha mikono juu🙌 ishara ya kujisalimisha.

"Kabla sijakumwaga ubongo nataka kibegi changu nahesabu mpaka tatu nakumwaga ubongo" aliongea kwa lugha ya kingereza huku uso wake ukiwa umegubikwa na jazanda la hasira, wakati huo akiwa ameninyooshea bastola yake kichwani, nilishindwa nimjibu nini kwamba ninacho ama laa na nikisema ninacho itakuwaje?" Niliwaza huku midomo yangu ikinitetemeka na kuloa jasho kwa woga. Mara akaanza kuhesabu " one..... Two.... Kabla hajasema three " nikapayuka " Usiniue mkuu kibegi ninacho mi..." Kabla sijamalizia sentensi yangu nilishtukia 😳 teke nzito la tumbo nikaangukia kitandani, alinifuata na kuninyonga tai kwa nguvu mpaka macho yakaanza kuona giza kwa jinsi alivyonikaba. "Onyesha kilipo kibegi changu " aliongea kwa hasira sana. "Kipo uvunguni bosi" nilimwambia na hapo akaniachia kisha akaingia uvunguni na kutoa kile kibegi.

"Sikiliza wewe si kila unamuona anaokota Makopo huko barabarani ni chizi wengine tupo kwa ajili ya kuwalinda nyie rahia na mali zenu dhidi ya majambazi yaliyokubuhu tunayoyatafuta. Hivi unajua unaishi na jambazi la kimataifa humu ndani kwako?" Aliniuliza . "Hapana mkuu" nilijibu huku nikitetemeka. "Inawezekana kweli hujui kwasababu nilianza kukuchunguza toka mwanzo unaanza kumtongoza binti huyu ulionekana hujui chochote kuhusu yeye na nia yako kwake ilikuwa ni upendo tu lakini ukweli ni kwamba binti unaeishi naye ni nyamera, kaiba silaha kwenye kambi ya jeshi la kimarekani zenye thamani ya bilioni 10 za kimarekani, kavunja mabenki na kuua mamia ya watu. Sasa usogope mimi nitaendelea kujifanya kichaa lakini kubali nisaidiane na wewe kuchunguza kuwa huwa akitoka usiku anaenda wapi na silaha kapeleka wapi maana anaonekana anashirikiana na mtandao mkubwa sana" aliniambia. "Sawa mkuu naahidi nitakupa ushirikiano" nilijibu kisha tukashikana mikono na hapo akatoka chumbani kwangu na kurudi chumbani kwake bila kujua begi la silaha lipo palepale chumbani kwangu.

Asubuhi Clara alirudi na kunikuta nimekaa na yule kichaa sebuleni tunakunywa chai, Clara alinikumbatia na kunibu lipsi mbele ya yule kichaa, jamani Clara alikuwa na lips tamu laini unaweza kuhisi matukio ya ujambazi anasingiziwa . "I love baby nilikumiss sana" aliniambia Clara kisha akamgeukia yule kichaa "Na huyu si yule kichaa anaekaaga pale nje umeamua ukae nae humu ndani" aliniuliza "Ndio nimeona nimsaidie maana pale ananyeshewa tu na mvua hasa msimu huu wa mvua. Hivyo sio vizuri kulala ndani huku mwenzetu anateseka na mvua nje sisi ni binadamu haya majumba tutayaacha hapa duniani." Nilimwambia. " Hapo tu ndio napokupendea mr. Braiton una roho ya huruma na kujali wengine. Basi mimi nipo chumbani" aliniambia kisha akaelekea chumbani. Hazikupita hata dakika ngapi akaniita chumbani tena kwa jazba sana, nikanyanyuka na kumuacha yule kichaa pale sebuleni kisha nikaelekea chumbani. "Mbona kama begi langu limefunguliwa" aliniuliza "Jamani mpenzi kwani huoni kufuli limefungwa?" Nilimwambia "acha ubishi mimi kufuli langu likiwa limefunguliwa najua sema ukweli" kabla sijajibu nikashtukia 😳amechomoa bastola yake kibindoni na kunishika tai, macho yake ya kizungu yaliyofanana na ya paka aliyatoa kwa hasira huku akiwa ameniwekea bastola kwenye paji la uso. "Sema ukweli bila kudanganya mimi kukuua sioni tabu hata kama nakupenda" pale nikaona nikileta mzaha nauliwa kweli, sasa kama mtu kaua mamia ya watu sembuse mimi nzi mmoja? Nikamwambia ni mimi. "Ok sasa kwasababu ushaona kila kitu utashirikiana na mimi kwenye kazi zangu, na ole wako ulete kamdomo kako, maisha yako utayapoteza usione nilivyo mrembo hivi mimi ni zaidi ya shetani" alisema Clara. Daaa nikaishiwa pozi, kichaa anataka nisaidiane naye kwenye upelelezi dhidi ya Clara huku Clara naye anataka nishiriane naye kwenye ujambazi, nitajigawa vipi mimi? Nyieee...nyieeee acheni tu.
Nilimuahidi Clara tukiwa pale chumbani kwamba nitashirikiana naye kwenye kazi yake ya ujambazi kama alivyotaka, nia yangu ilikuwa ni kuinusuru roho yangu dhidi ya kifo kwani chumbani tulikuwa wawili tu na isitoshe alikuwa amenikaba tai kwa mkono mmoja huku mkono mwingine ukiwa umeshikilia bastola ambayo aliiweka kwenye paji langu la uso😣. Basi bwana baada ya kukubali akaniachia kisha akanibusu mdomoni😘 "Natumaini hutaniangusha mpenzi" aliniambia huku akinitazama kwa macho yake legevu ambayo akimtazama nayo muuza duka lazima azidishe chenchi. "Sitakuangusha mpenzi niamini" nilimjibu "Basi sawa kaendelee na ratiba zako acha mimi nilale maana usiku kuna Casino tunatakiwa tukalivamie, pia na wewe inatakiwa upate muda wa kulala maana tutaenda wote" aliniambia, nikakubaliana naye kisha nikatoka nnje na kumuacha alale.

Nikatoka nje nilipofika sebuleni nikamshika mkono kichaa na kumtoa nje mpaka kwenye garden ya nyumba yangu ambapo tulikaa chini ya mti wenye hewa safi ili tuongee kwani wakati natoka chumbani alionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua kilichoendelea kati yangu na Clara chumbani. "Enhee🤔nipe kaifa huyo nyamera anasemaje?" Aliwahi na swali. "Aah unajua lile begi la slaa ambazo ulikuwa unasema ni za kambi ya jeshi la Marekani lipo ndani...." Kabla sijaendelea kuongea akaninyamazisha kwanza kisha akaingiza mkono wake kwenye kibegi chake chakavu na kutoa notebook kisha akasahihisha na sijui alikuwa anasahihisha vitu gani. "Enhee endelea" akaniambia. "Sasa mimi lile begi kila siku nilikuwa naona linatiwa kufuli jana usiku nikapata mashaka na kuamua kulifungua nione kilichopo ndani yake lisije likawa lina madawa ya kulevya mke nikakamatwa nayo, sasa kwenye kufungua ndipo nikakutana na hizo silaha, niliogopa sana na kurudishia kufuli vizuri lakini licha ya kufanya hivyo bado amegundua begi lake limefunguliwa na maamuzi yake ni kwamba kwasababu nimezijua siri zake niungane naye katika kazi yake ya ujambazi na leo hii usiku tunaenda kuvamia kwenye Casino" nilimwambia.

"Kwanza nashukuru sana nimejua pahala silaha za kambi ya jeshi zilipo😋 lakini pili nimesikitika 😔 kusikia Clara siku hizi anaiba kwenye makasino tena ya kitanzania, inamana madola yote aliyopata kwa kuvunja mabenki ya kimarekani amepeleka wapi? Ama kweli pesa ya wizi haidumu hilo nimeamini kwani watu aliowaibia na kuwafilisi walikuwa ni mabilionea wakubwa sana Marekani, alivamia nyumba ya mtoto wa mbunge wa jimbo la California akamteka na kumlazimisha atoe pesa zote bank kupitia simu baada ya hapo akampeleka kwenye msitu uliopo Mexco hela zote akahamisha kwenye account yake yani ni mabilioni ya madola kisha wakamuacha huko msituni wakiwa wamemfunga, kwa pesa alizokomba Marekani nilitegemea kumuona ni bonge la trilionea, any way we ingia naye kazini halafu utanijuza kila kinachoendelea ukirudi, pia usijali kuna fungu lako kubwa tu" kichaa aliniambia. Tukamaliza maongezi yetu na sijui ni kitu gani kiliniambia nigeuke nyuma 😳ghafla nikashangaa kumuona Clara akiwa amesimama nyuma yetu, na sijui alifika pale saa ngapi kwani sisi tulikuwa tunaongea kwa kuinamishiana vichwa. Sijui kama aliyasikia maongezi yetu yote ama laa ndio alifika mwishoni ambapo hakuna ukakasi na ninapoweza kumdanganya kwa kutunga hoja🙆🏼‍♂️

Je Clara aligundua chochote ama hajagundua na kama kagundua itakuwaje? Nyiee...Nyieee acheni tu maana mwenzenu hapa utumbo unanicheza cheza kwa woga sijui kagundua ama hajagundua? Usipite bila kulike na kucomenti fanya ku share kabisa mnasemaje wadau💥
..ITAENDELEA......


Muendelezo soma: Sikujua kichaa anayelala nje ya jengo langu ni mpelelezi anayemtafuta gaidi wa Kizungu niliyemuoa bila mimi kujua ni gaidi
 
Sehemu ya Tatu

Tukamaliza maongezi yetu mimi na yule kichaa mpelelezi, na sijui ni kitu gani kikaniambia nigeuke nyuma😳 ghafla nikashangaa kumuona Clara amesimama nyuma yetu, na sijui alifika pable saa ngapi maana wakati naongea na yule kichaa tulikuwa tunaongea kwa kuinamishiana vichwa chini, hivyo umakini wetu ulikuwa kwenye maongezi na wala si kutazama pembeni ama nyuma, sasa , sijui kama aliyasikia maongezi yetu yote ama ndio alifika na kuyakutia mwishoni maana tulikuwa tunamsema yeye. Nilimtazama usoni alikuwa anatabasamu🙂, "Vipi naona unaongea na kichaa sasa mnaelewana kweli au ndio lugha mgongano" aliniuliza Clara huku akiwa ametabasamu. "Kwani umesikia chochote tulichoongea?" Niliuliza kwa kujihami ili nijue kama alisikia yale maongezi ama laa. "Akuu mimi ndio nimekuja sasa hivi nikamsikia huyu chizi wako akikuambia usijali kuna fungu lako kubwa tu, sasa ndio nikanyamaza kimya ili nijue ni fungu gani hilo ambalo chizi anataka akupe ili nicheke mimi maana yeye mwenyewe hapo alipo hajiwezi anaishi kwa kudra za mwenyezi Mungu😂" alisema Clara kisha akacheka ishara ya kumdharau yule kichaa bila kujua ni askari upelelezi. "Kwani alikua anakumbiaje?" Clara aliniuliza huku akiendelea kucheka.

"Aah unajua mara nyingi napenda kuongea na watu kama hawa kwasababu miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nafanya kazi kwenye hospitali ya vichaa kama daktari katika kitengo cha saikolojia, hivyo kama mgonjwa ni mtulivu na anaweza kuongea basi ninaweza kuongea naye na kupitia maongezi yake nikagundua ni kitu gani kilimsababishia augue ukichaa. Sasa uliponikuta namuhoji huyu kwa umakini nilitaka nijue ni kitu gani kilimpelekea awe hivi maana siwezi kuishi na mtu kwenye nyumba yangu halafu anaugua wendawazimu je tukinyongwa usiku ? Sasa ndio akawa ananihadithia kwamba kuna bosi alimpa mzigo wa milioni tisini asafirishe, akaambiwa ule mzigo ukifika ana fungu lake kubwa tu, lakini kwa bahati mbaya akiwa njiani akatekwa na mzigo ukaibiwa hali iliyomfanya awehukwe na akili maana bosi mwenyewe ni katili na asingemuelewa" Nilimwambia Clara mada ya uongo kabisa ili asihisi vibaya kwenye ile kauli ya mwisho ambayo alisikia kichaa aliniambia fungu lako lipo tena kubwa tu.

Clara akamwangalia yule kichaa usoni kwa sekunde kadhaa mara nikashtukia amemuwa kofi la ngumu lilloweka alama ya vidole shavuni kwake. "Wewe sema ukweli ni kweli ulipoteza mzigo au ni danganya toto unamdanganya mume wangu ili upate sehemu ya kulala na kula?" Clara alimuuliza yule kichaa kwa kumfokea. "Ni kweli nilipoteza mzigo dada😞" kichaa alijibu kinyonge yani kama sio askari mpelelezi vile. Clara akataka kumuwasha kofi la pili, kwa haraka nikauahika mkono wake na kumzuia "Usimpige bwana kwani kakosa nini si amesema ukweli wake basi muache" nilimwambia. "Usimtetee huyu mume wangu wengine wanajitia vichaa kumbe ni vibaka ila kama umemwamini tutaishi naye" alisema Clara. "Huyu hana shida hapa amekutana na mtaalam wa saikolojia" Nilimwambia Clara kisha akaketi kando yangu na kumfukuza yule kichaa " Hebu toka hapa huoni mabosi zako tunaongea unataka usikie nini unachokielewa wewe muone vile midevu hiyo kama beberu la mbuzi" Clara alimwambia yule kichaa, taratibu alinyanyuka na kuondoka pale tulipoketi, moyoni niliumia sana😔 wakati anaondoka kama mbwa aliyefukuzwa kwa jirani akila makombo. Akilini nikawaza sasa kwanini asilianzishe hapa hapa kama ni silaha anazotafuta zipo ndani, kama ni Clara huyu hapa kwanini asilianzishe" nikawaza lakini nikakumbuka aliniambia anafuatilia vitu vitatu kwanza Clara apatikane, pili slaa za kambi ya jeshi na tatu mtandao wa ujambazi ambao Clara anashirikiana nao, sasa vimepatikana viwili bado cha tatu na ndio maana amekuwa mpole kwa kila kitu.

Basi bwana sasa wakati tumekaa na Clara pekee yetu mara akapigiwa simu 📱na rafiki yake wakawa wanaongea kwa muda kidogo alipokata simu Clara akaniambia "rafiki yangu kanipigia simu kwamba ameenda kusoma ramani kwenye kasino la kigamboni akapata fununu kwamba leo usiku askari wa Tz watakuwa doria, hivyo tumepanga leo tusitoke atakuja na wenzake watatu hapa kuna mpango tunataka tuusuke wa kwenda kuvamia meli kubwa ya mizigo maana hata hivyo macasino hayana hela" alisema Clara. "Anhaa🤔 kwahiyo hao wenzake watatu atakaokuja nao ni wawapi maana mimi siwajui" Nilimwambia. "Ni wenzetu wa kiume tuliotoka nao Marekani" alisema Clara akilini nikapata jibu kwamba ule mtandao unaofanya kazi na Clara ambao kichaa mpelelezi anautafuta huenda ukawa ni huo. "Sawa basi mimi nawakaribisha bila neno wala shaka wawe na amani kabisa" nilimwambia Clara. " Sawa basi acha mi nikaoge nilale vizuri maana nina uchovu wa kazi ya jana maana wa kuja ni mpaka saa mbili usiku" alisema Clara kisha tukaagana kwa mabusu 🥰 yeye akaenda ndani mimi nikabaki nje.

Alivyoingia ndani tu nikamfuata kichaa mpelelezi na kumtoa nje ya geti na kumuelezea kila kitu. "Halooo wamenasa leo lazima niliamshe maana hao wanaokuja kama wapo watatu na Clara na rafiki yake wawili basi mtandao wao wote umekamilika maana wapo watano" alisema kichaa mpelelezi. "Sasa mkuu utawaweza wote hao?" Niliuliza kwa mashaka kwasababu mwenyewe alikuwa amedhoofu afya yake. "Ebwanaee mimi ndio Mr. Michael Miguel hapo wakumuogopa ni Clara tu maana ndiye mkuu wao na ndiye mzoefu kwenye mapigano ila kufa kupona nitapambana naye" alisema kichaa.
Moyoni nikajisemea mamaweeeeeee nimekaribisha vita ya kimarekani ndani kwangu sijui itakuwaje? Jamani nyieee...

Tulikaa sebulenj majira ya saa mbili kasorobo usiku tukiangalia runinga huku tukiendelea kuwasubiri wagenj wa Clara wafike. Pale sebuleni mimi na Clara tulikaa kochi la peke yetu huku tukiwa tukiwa tumekumbatiana kimahaba, mr. Michael ama kichaa mpelelezi alikaa kochi la peke yake huku akiwa ameikazia macho Tv akiangalia movie ya kikorea ambayo ilikuwa na ngumi balaa, "Sasa huyu chizi naye anaelewa chochote hapo kwenye movie😂 maana ameikazia macho Tv kama vile anaelewa chochote hebu atoke hapa asije akapandisha midadi akaanza kutupiga kama hao wavietinam wanavyochezea kipondo cha wakorea" Clara alitaka kumfukuza mr. Michael pale sebuleni.

"Achana naye bwana hawezi kufanya hivyo unavyomfikiria" Nilimtuliza Clara, mara tukasikia honi getini. "Waoo wageni wangu hao hebu nipishe nikawafungulie geti?" Aliniambia Clara huku akijitoa kwenye mwili wangu na kutoka nje, pale sebuleni akaniacha na Mr. Michael ama kichaa mpelelezi. "Halafu we Braiton unaonekana unampenda huyu mwanamke, acha kuleta mapenzi kwenye misheni hatari kama hii, yani wewe hujui hapo ulikuwa umemkumbatia mtu hatari zaidi ya sumu ya mamba, shauri yako nikiona na wewe unaleta mzaha nakuchanganya kwenye kipigo nitakachotoa leo" aliniambia Mr. Michael kwa kunong'ona, mara mlango ukafunguliwa Mr. Michael akaacha kuongea.

Waliingia wanaume wanne wakiume😂 yani wakiume waliojaza miili yao kama vile wapiganaji wa miereka, waliongozana na Clara pamoja na rafiki yake. Wakakaa kwenye kochi. "Wewe Michael hebu toka hapa sebuleni kwani huoni wageni" Clara alimfukuza kichaa pale sebuleni ingawa kulikuwa na sehemu nyingi za kukaa" Mr Michael akanyanyuka kwenye kochi na kuingia kwenye chumba chake ambacho kilikuwa karibu na pale sebuleni hivyo chochote ambacho kingeongelewa angeweza kusikia.

Basi bwana, wageni walikuja na pombe za gharama, pamoja na mapochopocho, minyama ya kuku, mipiza yani walijiandaa kwa kula bata bila kujua wapo vitani, walianza kujimiminia pombe na kuanza kunywa, "My honey mbona wewe humimini pombe kwenye glass" aliniuliza Clara. "Aah mimi nina dozi yani mnanitamanisha kweli ila tu sina bahati kwasababu nina dozi" nilimwambia Clara. "Mh mbona sasa hukuniambia kama unaumwa mpenzi" aliniuliza Clara " aah mambo mengi na sijui niljisahau vipi kukuambia" nilidanganya kwasababu nilijua muda wowote kitimu timu kinaweza kuanza sasa na mimi nikikutwa nimelewa naweza kuchanganywa kwenye kisago.

"Basi kula nyama sisi acha tuenjoy" aliniambia Clara moyoni nikasema nyama tena acha nile nishibe ili cha mtema kuni kikifika nikutwe nimeshiba, basi tulikula wakanywa na kusaza, "sasa jamani tusikilizane kwa makini" alianza kuongea mwanaume mmoja mwenye kifua kikubwa na kigumu ambacho unaweza kuvunjia tofali la block juu ya kifua hicho likavunjika. wote tukakaa kimya kumsikiliza, "Jumatatu tunaenda kuvamia meli kubwa ya mizigo bandarini, tutawateka manahodha na kuwaua kisha tutaigeuza meli na tutaelekea ukanda wa nchi za magharibi ambapo tutaenda kuuza mizigo huko" aliongea yule njemba huku kimia kikiwa kimetawala, mara😳kichaa akafungua mlango wake na kutoka sebuleni, mkononi akiwa ameshika kitambulisho chake.

"Mammaaaaaa kitimu timu kimeanza sasa ataweza kweli kupigana na hizi njemba zote yeye peke yake au ana plani nyingine hebu nione?" Nilijisemea kimoyomoyo na kukaa kimya nitazame mtanange.
Je itakuwaje sasa? Hakikisha una kulike na kucomenti fanya ku share kabisa mnasemaje wadau💥 ili usipitwe na kipande kinachofuata maana mambo ni balaa
..ITAENDELEA......


Endelea

Sehemu ya Nne

"Jumatatu kuna meli ya mizigo inatakiwa tukaiteke baharini, tutawaua manahodha wote kisha tutaigeuza meli na kuipeleka nchi za magharibi ambapo tutaenda kuuza hiyo mizigo, najua hatuwezi kukosa maokoto ya kutosha kwasababu kwenye hiyo meli kuna makontena ya watu walioagiza mizigo kutoka china, kuna makontena yenye matirial ya viwandani, kuna makontena yenye vinywaji vya gharama kutoka nje sasa tutakosaje pesa kwa mfano🤔?" Aliongea yule njemba huku watu wote tukiwa tumekaa kimya kumsikiliza. Mara nikashangaa Mr. Michael ama kichaa mpelelezi akitoka chumbani huku akiwa ameshika kitambulisho chake mkononi kisha akasimama mbele yetu na kusema. "Jamani na mimi naombeni nimege sehemu ya muda wenu kuna jambo nataka kuteta na nyie" alisema Mr. Michael Miguel.

"Haaa😂 haya jamani nyamazeni tumpe chizi maiki naye aongee huenda atakachosema tutamuelewa maana pombe ni nusu ya ukichaa, kwahiyo tumsikilizineni maana tayar tushafanana naye" alisema Clara kwa dharau. Mimi nikanyanyuka ili nitokee nnje maana nilijua kitakachofuata "Na wewe unaenda wapi?" Aliniuliza Mr. Michael. "Naenda haja kidogo" Nilidanganya kwasababu sikutaka damu zinirukie nikaamua kujiweka pembeni, basi nikatoka nje na kusimamaa dirishani ili nichungulie kinachoendelea ndani. "Mimi naitwa Mr. Michael Miguel natokea jimbo la Calfonia nchini marekani, mimi ni askari kitengo cha upelelezi na nimekuwa nikiwafuatilia kwa muda mrefu yapata miaka minne sasa hatimaye leo nimewapata sina mengi ya kuongea zaidi ya kusema mjisalimishe maana mpo chini ya ulinzi" Wakati Mr. Michael anaongea Clara na rafiki yake walikuwa wanacheka mpaka kukaukiwa waliona kama utani.

"Hebu tutokee hapa usituchurie na kututia minuksi kwenye kazi yetu ya jumatatu tukakamatwa bure, askari wa Calfonia afanane hivyo ulivyo pumbafu huenda uchizi wako unaanza kukolea kichwani tutokee hapa mchuro mkubwa wewe" Clara alimwambia Michael lakini njemba mmoja akamstopisha Clara. "Sister hebu muache kwanza nimuhoji mwenyewe, wewe Michael kitambulisho chako kiko wapi?" Yule njemba aliomba kitambulisho" Mr. Michael akatoa kitambulisho na kumpatia. Pale dirishani mie mwili wote ulikuwa unanisisimka mpaka nywele maana kitambulisho kile kilikuwa ni orginal sasa nikawa nasubiri nini kitafuata baada ya yule njemba kupata ukweli kukota kwenye kitambulisho.

Akawa anakisoma huku ametoa macho😳 mithili ya mtu aliyekutana na simba katikati ya njia iendayo msituni kushoto pori, kulia pori hajui akimbilie wapi. Ghafla yule njemba alitupa kitambulisho chini na kurusha ngumi moja kali akiwa amesimama, mr Michael alinama ngumi ile ikapita hewa na kwa wepesi wa hali ya juu Mr Michael alimjaza yule Chemba ngumi ya maeneo ya tumbo, sijui alimpiga maeneo gani maana kwa jinsi lile njemba lilivyojazia sikutarajia litadondoka chini na kuanza kushindwa kusimama, aisee askari wana mbinu za kupiga.
Wenzake walipoona vile wakaingia kwa pamoja, Mr Michael aliruka mateke ya dabo dabo moja lilimpata njemba mmoja usoni na lingine likampata Chemba mwingine kifuani, chini waliondoka. Clara na mwenzake walipoona vile wakaona ule mziki mnene hauhitaji vita vya damu na nyama haraka wakakimbilia chumbani nadhani walikimbilia zile silaha kali za kivita ili wa muangamize Mr. Michael lakini Mr Michael akawa mjanja hakutaka kungoja walioanguka chini wanyanyuke haraka akatoka nje.na kuwafungia mlango kwa nje.

Kwa vile alikuwa hajaniona nikakimbia na kujibana sehemu nichungulie atafanya nini? Nilikimbia kwasababu kwa jinsi alivyokua anahema kwa hasira nilihisi atanichanganya na mimi kwenye kipigo. Basi nikamuona amesimama pale mlangoni anapiga simu. "Mpo wapi?" Aliuliza kwenye simu. "Tayari tushafika" nilisikia akijibiwa na punde niliwaona watu ka kumi na kitu hivi wakiruka ukuta na kuingia ndani, watano walizungunga nyumba na wengine walijipanga maeneo ya mbele kama vile watu wanavyomzunguka paka mwizi ili wamuue. Sasa ikawa ni majibizano ya risasi, vigogo vyote vya madirisha vilivunjwa na risasi zilizotokea ndani, nje wakitupa ndani wanajibu.

Mimi nikajibanza kimya kuangalia msala ule kwamba nani ataibuka mshindi! Maana tayari nimehamishia vita ya marekani nyumbani kwangu bila mwenyewe kupenda. Nyieee! Hakikisheni tu mnalike na kukoment ili msije mkapitwa na uhondo huu uliowajaza wengi mate mdomoni kama vile wameona embe bichi😂
Majibizano ya kushambuliana kwa risasi yaliendelea dhidi ya kundi la Clara ambalo lilikuwa ndani na kuni la Mr. Michael yani kichaa mpelelezi ambalo lilikuwa nje. Walimiminiana sana risasi lakini kila mmoja wao alikuwa bingwa wa kuzikwepa, risasi nyingi ziliishia kwenye nyumba na ndani muda mfupi nyuma yangu nzuri ikabadilika na kuwa kama gofu, bado waliendelea kushambuliana kwa kuviziana ghafla maaskari😳 wawili wa kundi la Mr. Michael wakatunguliwa risasi na kuanguka chini huku wakiugulia maumivu makali, hali hiyo ikawapandisha hasira kundi la Mr. Michael wakaamua kujisogeza karibu na nyumba kwa kuvizia ili wawaone vizuri maadui, weeee kundi la Clara lilikuwa vizuri katika mashambulizi ya kutumia silaha kwani ile wanajisogeza tu hatua moja walimiminiwa risasi na kuanguka mmoja mmoja hali ambayo ilisababisha Mr Michael ambaye alikuwa amejibanza nyuma ya mti huku akishambulia kwa kuvizia abaki pekee yake wenzake wote waliuwawa..

Sijakaa sawa ile tu Mr. Michael anajitoa sehemu ya ubavu mmoja ili afyatue risasi kuelekea ndani walipo kina Clara, ghafla😳 nikashtukia amepoligwa risasi ya paja lakini ajabu alishika tumbo na kutupa bunduki kisha akadondoka chini, "mh Inamaana amekufa?" Nikajiuliza lakini nikakumbuka jambo kutoka kwa Mr. Michael, aliwahi kunifundisha mbinu za kijeshi kwamba unapokuwa vitani halafu unaona umezidiwa ghafla ukapigwa risasi aidha ya kiuno, wewe unatakiwa ushike zile sehemu nyeti ambazo adui anadhani akikufyatulia risasi sehemu hizo lazima ufe, ukishashika moja ya sehemu hizo jidondoshe chini kisha jinyooshe na jifanye kwamba umekufa hata kwa kuigia, hiyo ni mbinu ya kumpoteza adui maboya. Basi mimi nikajua tu Mr, Michael hajafa kwasababu alipigwa risasi ya paja yeye akainama na kushika tumbo kisha akajibwaga chini, licha ya kwamba damu nyingi zilitapakaa pale alipokuwa amelala.

Clara na kundi lake walikaa ndani kwa dakika kadhaa wakisikilizia kwamba maadui zao wataamka ama laa walipoona kimya wakatoka nje, "Hawa wameshakufa fanyeni mpango tuondoke mapema pengine wana wenzao wengine wanakuja maana wanajeshi wana tabia ya kutuma vikosi kwa awamu, ili kusaidia kikosi kilichotangulia" Alisema njemba mmoja ghafla nikamsikia mmoja wao akisema😳mbona pale kwenye kona kuna mtu kama kasimama hamuoni kivuli kile" Nilikuwa ni mimi kumbe sehemu niliyosimama kivuli changu kilionekana kupitia mwanga wa umeme. "Hebu nipe bastola" Clara alitoa amri. Haraka nikajitokeza "Clara usininiue ni mimi Brighton" Nilipaza sauti. "Alaa unaleta mchezo nitakumwaga utumbo shauri yako kwanza kwanini ulijificha" aliniuliza kwa kufoka "Hapana sio kwa nia Mbaya ila nilivyoenda msalani nikiwa huko msalani kabla sijaamua kwenda haja ghafla nikasikia milio ya risasi, ikabidi nijifiche kwasababu sikuwa na silaha au ulitaka nife ili unikose mpenzi?" Nilianza kumrubuni Clara kwa maneno matamu kwasababu nilijua wanawake wanapenda maneno matamu hata awe mbabe vipi lazima atulie.

"Oky tuachane na hayo ulikuwa unajua kwamba Michael ni mpelelezi?" Aliniuliza, "Hapana na ndio maana kila siku nilikuwa namuhoji ili nimjue kiundani." Nilimwambia, mara njemba mmoja akadakia "Bwana nyie hakuna muda wa kubishana hapa tuondokeni" alisema njemba mmoja. Clara akatoa amri "Wapigeni sachi hawa maadui tuliowaua kisha mchukue simu na vitu vilivyopo mifukoni mwao mimi naenda ndani kukusanya silaha ili tuondoke. Haraka mimi niliwahi kumpiga sachi Mr. Michael nilipohakikisha simu yake ipo mfukoni mwake nilimwachia.

Basi Clara akakusanya silaha zote za kivita hadi zile za wanajeshi wa kundi la Clara walizokuja nazo akazipakia garini na sisi tukapakia garini pamoja hatimaye tukaondoka, "Jamani hapa tunaenda kulala kwenye hoteli iliyopo karibu na bandari, tutapumzika kesho ili siku ya jumatatu tuvamie meli ya mizigo bandarini kama tulivyokubaliana" Njemba mmoja akatoa ratiba, wote tukakubaliana gari likaondoka. Ndani ya gari kila mmoja alikuwa Bize kuchati kasoro mimi na dereva ambaye alikuwa Bize kwenye usukani. Mara ikaingia meseji kwenye simu yangu alikuwa ni Mr. Michael "umefanya vizuri kuondoka na hao wapuuzi maana wangeondoka wenyewe nisingewapata tena ila na imani kwasababu upo nao nitawapata tu kwa muongozo ambao wewe utanipa pia kuna mbinu nataka nitumie kwasababu Clara ameshakremu sura yangu, nataka niende marekani nikatibu kwanza jeraha la risasi kwenye paja langu kisha nitapitia uturuki kufanya sajari ya kubadilisha sura, sasa kabla ya hapo nataka ufanye hivi, najua Clara anakupenda ila ukikaa naye faragha jaribu kumuuliza mahusiano yake ya nyuma naamini alishawahi kumpenda mtu huyo mtu akamtenda angali yeye bado anampenda, mpelelele kuhusu picha za huyo mtu naamini hatakosa hata kwenye mitandao ya kijamii ya huyo mtu ambaye alimpenda sana lakini ikawa ndio hivyo, Ukipata picha ya huyo mtu nitumie ili nikaifanyie sajari Uturuki iwe sura yangu halafu kazi itabaki sasa kwako wewe kunielekeza maeneo mnayoelekea kisha mimi nitawatangulia kwa mbele naamini akikutana na mimi ugenini lazima atanishobokea na hapo mitaanza tena kumtongoza kwa gharama yoyote hakika hataweza kupindua meza hata kama yupo na wewe kimapenzi na hapo ataingia mtegoni kirahisi fanya hivyo" alisema Mr. Michael kwa njia ya Sms. "Sawa mkuu niamini sitakuangusha" Nilimjibu.

Basi kesho yake ilikuwa siku ya mapumziko kama tulivyopanga, tulipumzika kwenye hoteli moja ya kifahari maeneo ya bandarinj, zile njemba zilinunua makahaba ili ziinjoi nao kwa siku hiyo, rafiki yake Clara aitwaye Emmy naye alikuwa na mtu wake, mimi na Clara tulikua eneo la swiming pool Clara akiwa amevaa bikini tu na mimi nikiwa nimevalia kiboxer, baada ya kumaliza kuogelea tulikaa kwenye viti vilivyopo eneo lile na hapo nilianza kumuhoji Clara kuhusu mahusiano yake ya nyuma " Hivi Clara ulishawahi kumpenda mtu au kuwa na mtu kwenye mahusiano akakuacha ghafla ile hali bado wewe unamuhitaji" Nilimuuliza Clara, akanitazama machoni kwa sekunde kadhaa mara nikashangaa macho yake yanatoa machozi😭 moyoni nikasema yes, huenda hapa kuna mkasa mzito yani mpaka jambazi sugu analia sio poa, Clara akaanza kusimulia. "Yani Brighton usinikumbushe maana unanitonesha vidonda ambavyo vilishaanza kukauka, mimi kuna kaka wa kiitaliano nilimpenda sana sana na ndiye alikuwa mwanaume wa ndoto zangu yani mpaka nilikuwa nathubutu kumuhonga lakini alipokuja kugundua mimi ni jambazi alinipiga chini akawa na mwanamke mwingine na kuniacha nikiwa bado nampenda" alisema Clara huku akilia😭 "pengine una namba yake au picha yake labda?" Nikamuuliza. "Hapana" alijibu. "Je account zake za facebook" nilizidi kumpeleleza "mimi aliniblock simuoni hebu such kwenye simu yako Gabriel Agastino" alisema Clara na mara moja tukapata picha za huyo Gabriel, "Ndio huyo sasa yani nilimpenda sana huyu kaka lakini hakupendeka" alisema Clara. "Aaa usijali mpenzi sahau kuhusu yeye kusudi la Mungu lilikuwa ni ukutane na mimi" nilimwambia kwa mahaba zaidi, akanibusu 😘 kwa hisia kali bila kujua kwamba alikuwa mtegoni. Baada muda mfupi Clara alirudi tena ndani ya Swiming pool kuogelea na kuniacha nikiwa nimekaa kwenye kiti, hapo nikapata mwanya wa kumtumia Michael picha za X wa CLara. Michael alifurahi sana Nakwambia safari hii na kwa mbinu hii huyo nyamera hatoboi tena amejiongezea makosa ameua wanajeshi wangu na kuchukua tena silaha zao yani atakamatika kirahisi kama njiwa aliyetegewa pombe" alisema Mr. Michael.

Nyieee.....
Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumatatu, mchana tulilala ili usiku tuingie baharini kuteka meli ya mizigo iliyokuwa inatoka jiji la Hong kong nchini china kuja Tanzania. Wakati Clara akiwa amelala anakoroma, mimi nilikuwa bize kuchati na Mr. Michael, aliniambia serikali ya Marekani kwa walituma watu waje kuchukua miili ya wanajeshi waliouwawa na Clara, serikali ya Marekani hawakutaka kutoa taarifa kwa serikali ya Tanzania kuhofia kwamba Clara akisikia taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba anatafutwa atazidi kujificha zaidi, hivyo walikuja na helcopter za jeshi la Marekani wakachukua miili ya marehemu waliouwawa kimya kimya wakaondoka nayo huku wakijiapiza kwamba siku Clara atapatikana adhabu yake itakuwa zaidi ya yale mateso ya yesu kristo aliyopewa na wayahudi na kuangikwa msalabani.

Tulichati sana na Mr. Michael akaniambia kesho yake anaenda Marekani hivyo nimpe namba ya ndugu yangu yeyote ili amkabidhi nyumba, nilimpa namba ya mdogo wangu aongee naye, kiufupi kwa muda mfupi tu Mr. Michael tayari alishakuwa kama ndugu na mimi niliapa nitasaidiana naye katika kazi yake ya upelelezi kama vile ninavyosaidiana na ndugu zangu katika majukumu yao. Basi usiku tuliamshwa, tukala vizuri baada ya hapo njemba mmoja kati ya wale watatu akatoa Muongozo. "Nimeshawasiliana na mtu ambaye yupo china, ameniambia meli ya mizigo tayari imeshatoa nchini china, hivyo sasa hivi tuelekeeni baharini tukakodi bodi ili tukakutane na meli katikati ya bahari." Basi tukatoka pale hotelini ambapo tuliacha gari letu sehemu ya parking ambayo tuliilipia mwezi mzima kwa ajili ya ulinzi wa gari kisha tukachukua mabegi yetu yenye silaha za kivita kisha tukaelekea baharini.

Pale baharini tulimkuta bwana mmoja mwenye boti injini, pia ina taa, tulimkodi bwana huyo kwa kumdanganya kwamba kuna meli yetu ndogo imezama wakati ikiwa inakaribia kufika bandarini hivyo atupeleke tukafanye uokozi, bwana yule alikubali kwa kututajia dau kubwa la pesa ili tushindwe maana alionekana hataki kuingia kwenye maji usiku ule hivyo akashindwa kusema haendi bali akatutajia dau kubwa la pesa," mtanipa milioni tatu" alisema bwana yule mwenye asili ya kiarabu. "Sawa" alijibu njemba mmoja kisha akamuhesabia yule bwana pesa yake keshi palepale, wala yule bwana hata hakushtuka kwanini hawa watu hawaombi punguzo, yeye akadhani amekutana na mafogo.

Akazichukua zile pesa na kumkabidhi bosi wake kisha akamuita mwenzake mmoja waongozane naye, tulipanda kwenye boti na safari ya kwenye maji ilianza .Tulitembea kwa muda wa masaa mawili, yule bwana tuliemkodi akacheza na machale, "Jamani mbona safari imekuwa ndefu kiasi hiki hatufiki" Yule bwana alianza kulalamika, ghafla😳 njemba mmoja alimrukia kwenye usukani na kumtwanga vichwa vitatu wakati huo bodi ikiendelea kuyumba yumba maana walikuwa wanagombania usukani, sasa yule mwenzake aliyemsindikiza akataka kuingilia, Clara alimparaza ngumi moja ya uso😮 iliyomtupa kijana yule ndani ya maji, bado boti ilikuwa inayumba yumba kwani yule bwana tuliyemkodi boti aling'ang'ana kwenye usukani kwa damu na jasho hakuta kuachia. Emmmy rafiki yake Clara akatoa sindano ambayo sijui hata ilikuwa na sumu ya nini akamdunga yule bwana mgongoni, yani kitendo cha sekunde tu yule bwana akaangukia ndani ya maji tukafanikiwa kupora boti.
Tuliondoka huku wanacheka😁 "hii ni sumu ya mamba bwana mtu akidungwa sindano yenye sumu hii akichukua dakika mbili bado yupo hai basi huyo si binadamu wa kawaida ni jini" aliongea Emmy huku wakicheka na kujisifu.

Mimi nilikaa kimya tu nikiangalia mambo yanavyoenda, mara kwa mbali sana tena sana tukaona mwanga mkubwa wa taa, yani umbali wa kama lisaa limoja hivi, "Jamani meli yenyewe ndio ile kulee acha niongeze speed tuifikie"alisema yule njemba aliyeshika usukani, lakini ghafla😳 boti ikaanza kushtuka shtuka kama inakata mafuta, kumbe yule bwana tuliyemkodi alikadiria mafuta yake, kwamba sehemu anayoenda yatamtosha kwenda na kurudi salama, mara bosi ikasimama ikawa inaelea tu juu ya maji, mawimbi ya bahari yakaanza kuchanganya, boti inayumbishwa kwamba itaangushwa, wakati huo moyo wangu unapiga kite balaa, kwani nilihofia tukiangukia ndani ya maji naweza kuliwa na samaki wakubwa wa baharini maana nilikuwa sijawahi kuogelea kwenye bahari bali ni kwenye mabwawa, swimming pool na mito, sikuhofia simu kwasababu tuliziweka kwenye mifuko ya plastiki ambayo ilikuwa Ndani ya mabegi, ghafla😳 boti ikazidiwa na mawimbi. "Jamanieee kila mmoja ajiokoe mwenyewe mpaka tuifikie ile meli kule, mtu akifa hakuna mtu kugeuka nyuma" alisema njemba aliyepo kwenye usukani baada ya kuona anazidiwa. Moyoni nikasema "maweeee sasa nimeyakanyaga rasmi"Wakati naendelea kutetemeka kwa woga ghafla😳.........
Nyiee

"Jamanieee kila mmoja aangalie namna ya kujiokoa mwenyewe maana boti imezidiwa nguvu inaelekea kuzama" Alisema yule njemba aliyekuwepo kwenye usukani. Ghafla boti lilianza kuzama, nikaona wenzangu wanaanza kujirusha ndani ya maji mithili ya watoto wa vyura ambao walikuja nchi kavu kutalii, " Mh nani afe?" Nilijisemea kimoyomoyo kisha na mimi nikajitosa ndani ya maji, mara ghafla nikashangaa😳 naanza kuzama wakati huo wenzangu wanapiga mbizi balaa kama vile wapo kwenye mashindano ya kuogelea. Kila nikijitahidi kusogea mbele siendi zaidi sana nazidi kuzama, nikiangalia mbele wenzangu wananicha, niliachia ukelele mmoja wa hatari, "Yuuuwiiii nakufa nakufaaa " Nilizidi kupiga kelele "Jamani twendeni tukamuokoe mwenzetu anakufa" Clara aliongea. "Achana naye bwana kila mmoja ajipambanie mpaka tuifikie ile meli ya mizigo kule mbele" Njemba mmoja alimwambia wakati huo Clara alikuwa ananifuata, "Sasa nitamuachaje wakati yeye ndiye kabeba begi dogo la mgongoni lenye simu zetu wote" alisema Clara. "Kamnyang'ange begi umzamishe ndani ya maji afie huko maana tukienda naye mbeleni atatutesa kama hajui kuogelea" alisema njemba mwingine, Clara alinifuata, tayari nilishaanza kunywa maji alinivuta juu na kutaka kuninyang'anya begi.

"Letu begi huko mimi naachwa, usituletee mambo ya watoto wa mama, hapa mwanaume gani umeishi dar miaka yote hiyo hujui kuogelea" alisema Clara huku aking'ang'ania kunipora begi. "Jamani Clara😭 sio wewe ulisema utakuwa na mimi kwenye shida na raha niokoe mwenzio" Nililia kama mtoto huku nikimng'ang'ania Clara mwili wake ili nisizame kwenye maji, naye alijitahidi kunipora begi mgongoni, akafanikiwa kisha akanisukumia kwenye maji, akaendelea na safari, yani ni kudra tu za mwenyezi Mungu muda huohuo alionisukumia kwenye maji ikapita meli ndogo ya abiria nikajitahidi kwa juhudi zote nikaidandia ile meli na kukaa sehemu ya nyuma yenye uwazi huku nikitapika maji na kukohoa balaa" Meli isisogea mbele tu kidogo Clara naye akadandia na kukaa sehemu ile ile niliyokaa mimi, "Umejitahidiee huo ndio uanaume sasa sio unaleta utoto wa mama hapa" aliniambia Clara kisha akanisindikiza na tusi nzito akinitukania mama yangu.

Kwa kweli kuanzia hapo nikayaamini maneno ya babu yangu aliyoniambia "daima usiyaamini maneno, mwanamke ni kiumbe hatari sana wewe unaweza kuona anakupenda lakini anaweza kukubadilika mara moja na usiweze kuamini maisha yako yote hivyo ukiwa naye ishi naye kwa akili" nilikaa kimya nikiendelea kuyatafakari maneno ya babu yangu na Clara naye alikaa kimya akitafakari yake. Hatukufika hata mbali wale njemba watatu nao walidandia kwenye ile meli kasoro Emmy rafiki yake Clara, "Emmy yupo wapi" Clara aliwauliza. "Kazidiwa na maji kazama" alijibu njemba mmoja "acha atangulie kuzimu dhambi alizofanya zimeshatosha" alijibu Clara wala hakuonekana kuguswa na tukio la kuzama kwa rafiki yake, yani ni ubabe ubabe, nilimwangalia Clara usoni kwakweli nilishindwa kuamini mwanamke mzuri kiasi kile, mrembo ana roho ngumu kama chuma? Nikajisemea kimoyomoyo "looo! huyu ni dada yake shetani si bure"

Meli ilizidi kwenda hatimaye tukaikaribia ile meli kubwa ya mizigo, "Jamani kama unajiona wewe bado ni mtoto wa mama bora usifuatane na sisi, tunataka mtu ambaye yupo shapu na anayejituma lasi hivyo tutakuulia kwenye maji" alisema njemba mmoja hapo nikabaini wananisema mimi, nikakaa kimya, tayari nilishaanza kumuogopa Clara na kundi lake maana si lelemama. "Sasa tukiikaribia hiyo meli kubwa wote tunairukia kwa madirishani na kuzama ndani na hapo tutanza kazi ya kuteka rasmi" alisema Njemba mmoja.

Moyoni nikasema "hapo sasa kazi imeanza" basi tulipoikaribia Clara alianza kujirusha kama kipanga akashika dirisha la mbele la nahodha. Wengine nao wakajirusha kwenye madirisha ya nyuma na mimi nikajitupa kwa akili na tageti nusura nijikose kose kudaka chuma la dirisha la mwisho kabisa lakini nilijitahidi kunyoosha mkono vidole vyangu vikadaka chuma na hapo nikajitahidi mpaka nikaingia ndani ya meli kupitia dirisha. Humo ndani sasa ni ngumi tu zilikuwa zinaendelea, nilipoangalia mbele kwa nahodha Clara ndiye alikuwa ameushika usukani anaendesha meli wakati huo huku nyuma wahudumu wa meli ya mizigo wakichezea kipondo kutoka kwa zile njemba tatu na kutupiwa baharini kupitia dirisha, sijakaa sawa na mimi akanijia muhudumu mmoja wa meli, akarusha ngumi nikaikwepa kisha nikawa shapu kumbandika ngumi moja matata ya mdomo alitema damu pamoja na meno yote ya sebuleni, nikamkamata kwa nguvu sana na kumtoa nje ya meli kupitia dirisha la meli na kumtupa baharini akiwa hai, hatimaye tukabaki wenyewe sasa ndani ya meli, kila mmoja alichukua simu yake kwenye begi la simu lakini ajabu😳 Clara akanizuia mimi nisichukue yangu. Nikashangaa sana na kumuuliza kwanini. "Wewe nimekusukumia ndani ya maji kwasababu nimeona hutaweza kuendelea na safari maana huwezi kuogelea, ajabu nakukuta juu ya meli ndogo ya abiria, uliwezaje kutoka kwenye maji mpaka ukapanda kwenye ile meli inamaanisha wewe ni mafia ila unatutega, sasa nahisi kuna watu unashirikiana nao maana hata siku ile pale nyumbani kwako tunapambana na kina Michael mwishoni kabisa wa mapambano tulikukuta nje umejificha, sasa ili sisi tuwe na amani tukimaliza kazi zetu kabla hatujagawana pesa tutakagua simu yako ili tujue wewe ni mwenzetu ama ni mmoja wa maadui tuyayetembea naye pasipo kujua" alisema Clara tena bila mzaha. Hakika nilihisi kuchanganyikiwa kama si kupagawa kwani kwenye simu yangu meseji zote nilizokuwa na nachati na Mr . Michael zilikuwepo na nilisahau kufuta.

Jamani Nyieee .....Nyieee nahisi ungekuwa ni wewe ungeshajinyea palepale Clara alipokuwa anaongea lakini mimi nilikaa kimya huku nikitafakari nifanye nini? Je itakuwaje? Usipite bila kulike na kukomeniti fanya ku share kabisa ili sehemu inayofuata isikukose maana ndiyo sehemu balaaa🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
..ITAENDELEA...... Vb

Muendelezo soma: Sikujua kichaa anayelala nje ya jengo langu ni mpelelezi anayemtafuta gaidi wa Kizungu niliyemuoa bila mimi kujua ni gaidi
 
Sehemu ya Tano

Kimya kilitawala ndani ya meli kila mmoja alikuwa Bize na lake, Clara alikuwa bize kwenye usukani, wale manjemba watatu walikuwa bize na simu zao, mimi nilikuwa nimekaa pembeni ya Clara huku nikiwa nimeinamisha kichwa chini kama kobe nikitunga sheria😞 nitumie mbinu gani ili Clara asikague simu yangu maana kama atafanikiwa kufanya hivyo atakutana na jumbe za njama tulizokuwa tunapanga mimi na Mr. Michael dhidi yake sijui angenifanya kitu gani baada ya kukuta jumbe hizo,niliendelea kuwaza bila kupata majibu kamili, hatimaye kukaanza kupambanzuka, kwa mbali tuliona mji mzuri sana. "Brighton ulishawahi kufika kwenye ule mji" aliniuliza Clara. "Hapana ndio mara yangu ya kwanza" Nilimjibu. " Pale ni Muscut Oman uarabuni ukisikia Oman ndio pale sasa" alisema Clara. "Inamaana hadi huku unapafahamu?" Nilimuuliza "Ndio nimeshafanya sana biashara ya kuuza silaha za kivita kwa waarabu wa hapa Muscut kwahiyo mimi ni mwenyeji" alisema Clara, "Waooo ni pazuri sana hebu simu nipige angalau picha ya ukumbusho maana mandhari yake ukiwa kwa mbali inavutia sana" Nilimzuga Clara nione atasemaje, nikashangaa anaingiza mkono wake kwenye begi na kunitolea simu yangu ili nipige picha, sasa sijui ni zile stori zilimchanganya mpaka akasau kwamba aliniambia hatonipa simu mpaka aikague, nadhani alijisahau.
Nikaipokea ile simu na kuanza kuzuga kama naupiga ule mji wa Oman picha 😀 kumbe nilikuwa bize kufuta jumbe zote za siri nilizokuwa nachati na Mr. Michael mpaka nikamaliza kufuta zote wakati huo Clara alikuwa bize kwenye usukani, nilipomaliza kuzifuta ikabidi nishushe pumzi na kumshukuru Mungu kimoyomoyo maana niliona kama vile ametuma muujiza wake ili roho yangu iliyokuwa inaweweseka kwa hofu bila kutulia itulie. Moyo wangu ulipotulia na kurejesha amani yake ambayo ilipotea, sasa nikaendelea na zoezi la kupiga picha ule mji wa Oman, nikamuonyesha Clara zile picha " Waooo ni nzuri sana" alisema Clara kuonyesha anafurahishwa na picha zile, kiufupi alijisahau kabisa mpaka nikaiweka simu yangu mfukoni tukaendelea na stori za hapa na pale mpaka tukaingia bandarini kwenye mji wa Muscut Oman, Punde tu meli ilipotia nanga pale bandarini vishoka pamoja na madalali wa pale bandarini wakaizunguka meli baada ya kugundua ni ya mizigo. Tulishuka kwenye meli pamoja na wale manjemba watatu huku tukiwa tumebeba mabegi yetu yenye silaha kali za kivita.
"Nifuateni" Clara akatoa amri. tukamfuata nyuma na kuingia kwenye ofisi kuu za pale bandarini, Clara aliongea na mkurugenzi wa pale bandarini, kwa jinsi walivyokuwa wanaongea Clara alionekana kufahamiana na yule mkurugenzi "una uhakika meli hii ya awamu hii haina shida? Maana ile uliyoniletea kipindi kile haikumaliza hata mwaka ikaharibika" alisema yule mkurugenzi akimwambia Clara, "mh ama kweli hili ni jambazi la kimataifa kumbe sio mara yake ya kwanza kuiba meli" nilijisemea kimoyomoyo huku nikiendelea kusikiliza maongezi yao. "Hii haina shida mkuu isitoshe hii ni ya mizigo ile ilikuwa ya abiria" alisema Clara. "Kwa hiyo si ina mizigo ndani yake?" Mkurugenzi aliuliza. "Ndio ina mizigo?" Alijibu Clara. "Kwa hiyo unaniuzia meli yenyewe au na mizigo" mkurugenzi akauliza. Niwewe tu ukitaka na mizigo sawa" alisema Clara, "basi sawa twendeni tukathaminishe mizigo pamoja na meli niwape pesa yenu halafu leoleo naenda kuibadilisha kabla wenyewe hawajaanza kuifuatilia" alisema Mkurugenzi tukatoka ofisini na kwenda kuthaminisha mizigo pamoja na meli, alitulipa pesa ambazo ni sawa na bilioni 10 za kitanzania, hakutoa keshi bali ziliwekwa kwenye account ya Clara.
Mpaka kufikia saa tisa jioni tulikamilisha zoezi la kuuza meli sasa tukaelekea hotelini kupumzika "Jamani kazi tuliyofanya ni kubwa itabidi tupumzike japo mwezi mmoja hapa Oman tule Bata maana kama ni pesa tunazo kwahiyo tupumzishe miili yetu wakati tukitafuta chaka lingine la kuvamia" aliongea Clara kama mkuu wa kundi, hakuna aliyempinga wote tukakubaliana naye, hakika kilikuwa ni kikao kizito kwani walifikia mpaka hatua ya kukagua simu yangu lakini hawakuweza kuambulia chochote maana kama ni meseji nilishafuta, basi tukakodi vyumba hotelini na kulipia mwezi mzima kabisa, yani ilikuwa ni mwendo wa Bata tu. Hata hivyo siku zilianza kusogea na mimi nikiendelea kuwasiliana na Mr Michael kwa siri sana, akaniambia tayari ameshatoka uturuki na amekwisha fanya sajari yani amebadilisha sura yake na kuwa sura ya Gabriel Agustino ambaye alikuwa ni X wa Clara lakini akamtema Clara na kumuacha hali ya kuwa Clara bado alikuwa anampenda. Cha kufurahisha ni kwamba kwa muonekano wa picha huyo Gabriel Agustino alionekana kulingana kimo kabisa Mr. Michael mpaka wembamba.
Hatimaye siku mbili zikapita Mr. Michael akanipa taarifa kwamba tayari ameshatua Oman maana nilikuwa nikimpa taarifa mpaka sehemu ambayo tupo, naye Mr Michael akaja maeneo hayo na kunitaarifu kwamba amechukua chumba kwenye hoteli iliyopo karibu na maeneo ambayo tupo, basi jioni moja Mr. Michael ama Gabriel feki, akanijulisha bar ambayo yupo kisha akanisisitiza nifanye hima niende na Clara ili tuone baada ya Clara kumuona itakuwaje.
Nyieee😂 nyieee acheni tu yani Clara anaingia mtegoni kiulaini mithili ng'ombe anayepelekwa machinjioni. Unajua ilikuwaje baada ya Clara kukutana na Gabriel feki? Acha Nicheke kwanza😂 Usipite bila kulike na kukomeniti fanya ku share kabisa ili sehemu inayofuata isikukose maana ndiyo sehemu balaaa
..ITAENDELEA......
 
"Enhee🤔nipe kaifa huyo nyamera anasemaje?" Aliwahi na swali. "Aah unajua lile begi la slaa ambazo ulikuwa unasema ni za kambi ya jeshi la Marekani lipo ndani...."
Zile silaha za bilioni 10 ndiyo zilikua kwenye bag ndani? Ziliibwa kwenye kambi nchini Marekani au Kambi nje ya Marekani au ni mzigo uliporwa wakati unasafirishwa ukawa redirected?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom