Lile lishangazi lilinifanya nijiingize kwenye umarioo, sitasahau

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,788
52,747
LILE LISHANGAZI LILINIFANYA NIJIINGIZE KWENYE UMARIOO, SITASAHAU

Na, Robert Heriel
Mtibeli

Hivi ndivyo ilivyokuwa, kama ilivyosemwa na watu wa kale yakuwa shida haina adabu. Ndivyo ilivyotokea kwangu.

Haya sasa tulieni niwasimulie, tena mtege masikio yenu msikie habari hii ya aibu niliyoifanya wala sikutegemea kuwa siku moja nitafanya haya. Lakini ndivyo nilivyotumbukia katika shimo baya la umarioo. Looh! Taikon leo kageuka Marioo wa Dar es Salaam.

Maisha tayari yalishafikia hitimisho lake kunishinda. Yalisubiri kutia muhuri wa jeuri kuwa nirudishe mpira kwa kipa. Nirudi Kijijini, huko nilipotoka, huko nilipozaliwa, nikasoma na sasa nikawa mtu miongoni mwa watu ingawaje sikuwa mvaa viatu bali mwenye roho ya utu.

Kila kona nilizungukwa na majeshi ya vita yaliyobeba silaha za kutisha, upande huu nilidaiwa kodi ya chumba kidogo nilichokuwa nimepangisha, upande huu nilikuwa nadaiwa elfu themanini na Mangi lilipoduka; hapo nilikopa vitu vya kula tokea mwezi uliopita. Upande mwingine nilizingirwa na pesa ya usafi na umeme ambayo wapangaji wenzangu walikuwa wakinisimanga kila wakumbukapo.

Tumboni njaa nayo haikuniacha nipumue. Jamani njaa ya siku zile ilikuwa kama njaa ya siku ya mwisho wa dunia. Iliniuma jamani! Nilikonda jamani! Nilipauka jamani! Nilitia huruma jamani! Nilipiga miayo jamani mpaka nikachoka. Na iliujue nilichoka kupiga miayo ni vile nilivyokuwa naipiga hiyo miayo. Unajua miayo inaraha yake hasa pale ukiwa umeshiba na sasa unasikia kusinzia; Miayo yenye raha ni ile ukiipiga unafumba macho na uso wote unalegea kwa raha bila karaha. Lakini miayo ya njaa kali haipo hivyo ndugu zangu, miayo ya njaa kali hutoka huku macho yakitoka nje na misuli ya uso ikikaza. Hakika nilipata shida wala sitanii.

Basi nikawaza moyoni niuze vitu vyangu vya ndani, ikiwemo Feni, kitanda, godoro, na sofa ili walau nipate nauli ya kurudi nyumbani. Wazo hilo likanipendeza. Nikaamka ili nikatafute wateja. Basi nikazunguka, mimi na barabara. Mimi na kivuli changu, mimi na matope kwani ilikuwa kipindi cha mvua. Nikazama mtaa mmoja na kuibukia mtaa mwingine. Kila kijiwe nikitafuta wateja wa vitu vyangu vya ndani, kwani jiji lile lilishanichosha kwa maudhi na karaha zake; Sisemi sikuwa nalipenda bali ni kuwa gharama zake za maisha zilikuwa juu kama nini.

Tafuta mteja wapi, saka madalali wapi, jamani sikuwahi kuona pesa ikilaumiwa kiasi kile. Kila mmoja alinambia hela ngumu. Basi nikarudi tena ghettoo kupumzika. Nilipifika tuu nililakiwa na sauti za wanawake waliokuwa tunakaa nao. Mmoja akanirushia maneno "Leta pesa ya maji" mwingine akadakia akisema: Pesa ya Umeme tunataka, mwanaume suruali wewe, mwanaume mlegezo"

Looh! Jamani.... jamani kumbe maneno makali ya mwanamke huweza kuizima njaa. Maneno ya wanawake wale yaliiyeyusha njaa iliyokuwa inanitafuna tumboni. Sikuwajibu; nikazama ndani na kufunga mlango. Looh!

Nikawasha Redio ya simu; Oooh! Zilikuwa ni habari za Corona. Ati wagonjwa wamefikia kumi. Hapo hapo nikamsikia kiongozi mmoja akiruhusu watu watumie hata barakoa za kushonwa na mafundi wa nguo. Hapo nikaona kuna fursa.

Nikatoka nje, kwa Fundi Maiko, siyo yule maiko wa Morogoro ambaye ni maarufu huku mitandaoni. Nikamwambia anishonee barakoa alafu mimi nitakuwa natembeza. Akanambia nitafute kitambaa alafu anishonee kwa mia tano alafu mimi niwe nauza elfu moja au elfu mbili.

Masikini Taikon, nitapata wapi kitambaa cha kushonea barakoa. Sina pesa wala nini. Hapo nikakumbuka jambo. Nikaondoka kwenda nyumbani(Ghetto), nikachukua shuka langu. Lilikuwa la rangi ya Samawati wengi huiita Bluu bahari. Nikakata vipande vinne nikavilite kwa Fundi Maiko anishonee Barakoa. Muda huo njaa ilikuwa ipo mapumzikoni nadhani kelele za wale wanawake ziliifubaza.

Sasa nilishona barakoa zaidi ya hamsini. Na nilikuwa nauza elfu mbili mbili.

Agizo la kila mmoja avae Barakoa lilifanya Barakoa zangu zinunuliwe kwa upesi mno.

Nilikuwa nikiimba maneno haya:

"Vaa Barakoa, Barakoa Barakoa,

Linda afya yako, usijeukapotea,

Linda na wenzako, pale unapokohoa,

Vaa Barakoa, Buku mbili tuu itakuokoa."

Nilirudia wimbo huo mara kwa mara kila nilipokuwa nakatiza mitaa. Labda ungependa kujua jinsi nilivyokuwa nimevalia. Ngoja nikuambie sasa: Nilikuwa nimevalia Tisheti nyeusi isiyo na maandishi, suruali ya Jeans nyeusi mpauko na Raba kali huku usoni nikiwa nimevaa Barakoa iliyofunika uso wote mithili ya Spiderman. Hii ilifanya kila nilipopita watu kunishangaa. Ungesema wanashangaa nini, ningekujib; pengine ni jinsi nilivyovalia hiyo barakoa usoni.

Basi nikiwa nakatiza Mtaa wa Makumbusho nilishtushwa na maji machafu yaliyonirukia na kunilowanisha mwili mzima. Looh! Lilikuwa ni gari lililonirushia maji yaliyokuwa yametuama kwenye madimbwi yaliyosababishwa na mvua.

Nililowa mimi na Barakao zangu, lile gari likasimama kwa mbele. Kisha mlango ukafunguka; punde akatoka Mama wa makamo hivi, nadhani umri wake ulicheza kwenye miaka arobaini na mbili hivi.

Akanifuata akiwa na wasiwasi mwingi huku akiniomba radhi kila mara. Hatimaye aliniomba nipande gari lake ili anipeleke kwangu. Sikuwa na jinsi, sikuwa fungua mdomo zaidi ya kufuatana naye mpaka mahali lilipokuwa limesimama gari. Tukapanda tukaondoka. Jamani! Jamani! Kitendo cha kumwagiwa yale maji kuliamsha rasmi njaa yangu yapata mida ya saa tisa jioni. Nilianza kutetemeka kama mgonjwa wa degedege. Kumbuka bado hajaona sura yangu, wala hajasikia sauti yangu.

Mara kwa mara alikuwa akinichungulia kwenye kioo cha gari kilichopo mule ndani. Alitamani kuifahamu sura yangu.

Yule mama wa makamo akafungua kinywa chake:

" Samahani kwa kukumwagia maji machafu. I'm very sorry. Naitwa Mama Debora, Sijui unaitwa nani"

Niligeuza uso wangu ukamuelekea. Hapo akawa ananitazama huku akiangalia mbele kule gari lilipokuwa linaelekea.

" Naitwa Taikon, Muuzaji mashuhuri wa Barakoa katika jiji la Dar es Salaam. Hivyo tuu"

Nilimjibu kwa sauti ya uchovu ambayo mtu yeyote angejua kuwa nilikuwa nina njaa kali.

" Okey Taikon, Umenisamehe kwa jambo hili?"

Yule Mama aliniuliza. Lakini sikumjibu niligeukia mbele kwenye kioo cha mbele cha gari. Hali hiyo ilisababisha ukimya kwa kitambo. Lakini Yule Mama alifukuza tena ukimya mule ndani ya gari.

" Unakaa wapi? Mimi ninakaa Goba, ningeonelea nikupeleke nyumbani kwangu alafu baadaye nitakupeleka kwako . Sawa?"

Sikujibu kitu, ningejibu nini wakati nilikuwa na njaa kali. Yote yalikuwa ni sawa, mfukoni nilikuwa nimeshapata elfu arobaini za kuuza Barakoa.

Tulifika nyumbani kwake, ilikuwa nyumba kubwa ya kisasa yenye kila sifa ya kuitwa nyumba ya kifahari. Alikuwepo Mlinzi peke yake, sikujua wengine walikuwa wapi. Hata hivyo hilo halikunihusu, kilichonihusu muda ule ni chakula tuu.

Nifungua Barakoa yangu, hapo akashangaa kuuona uso wangu. Ulikuwa uso uliolegea kwa njaa, macho yangu yalikuwa yamechoka sana, midomo yangu ilishaanza kupasuka. Basi akanipa juisi na ndizi rosti kisha akanielekeza lilipo bafu; nikaenda kuoga Looh! Nilifurahia mno.

Nilirudi baada ya kutoka kuoga nikiwa nimevaa tuu taulo, nikamkuta kakaa sebuleni anatazama muziki kwenye luninga. Akanikaribisha nikae kwenye sofa alilokaa yeye lakini mimi nikaenda kukaa kwenye sofa jingine.

Basi akaanza kuongea:

" Umenisamehe kwa kukumwagia machafu Taikon?"

" Ndio nimekusamehe" Nikamjibu.

" Nafurahi kukutana na kijana Mzuri kama wewe?"

Yule mama alisema huku akichukua Chupa ya pombe na kuibwia. Mimi nilikuwa kimya nikimtazama.

Punde mlango uligongwa, Yule Mama akamruhusu aliyekuwa anagonga. Alikuwa ni Mlinzi, aliingia akiwa kabeba mfuko akamkabidhi yule mama. Mlinzi akanikata jicho la husda, sikujua ni kwa nini. Yule Mama alimuamuru aondoke kisha akatuacha sisi wenyewe kama awali.

Yule Mama akaingiza mkono kwenye ule mfuko na kutoa nguo mpya. Zilikuwa suruali mbili za jinsi, tishti tatu na viatu jozi mbili.

" Embu zijaribu mara moja tuone kama zitakutosha"

Yule Mama aliongea huku akinitupia usoni zile nguo. Nilifurahi moyoni lakini usoni niliificha furaha yangu.

Nikamuaga kuwa niende kujaribu zile nguo bafuni lakini yeye akacheka na kuniambia nijaribu pale pale kwani nini naogopa. Basi huo ndio ulikuwa mwanzo wa ganda la ndizi kulikanyaga, huo ndio mwanzo wa kuserereka kama kwa Sadala, lakini zaidi kama sio kushuka kitonga basi sijui niseme nini.

Nakumbuka siku ile nililala na yule Mama, wala sio kwa nguvu, bali kwa tamaa zangu mwenyewe kwani yule Mama alikuwa anavutia licha ya umri kumtupa mkono lakini alijaliwa mali na uzuri ambao wanawake wengi hawakuwa nao. Sio lengo langu kumsifia lakini ikiwa ipo haja acha nisema sifa zake za mwonekano. Alikuwa Mama mwenye Rangi ya maji ya kunde iliyoivaa, mwenye umbo namba nane linalotamanisha wanaume wote wenye uhai, macho makubwa kiasi yaliyoficha aibu na madeko, mwenye midomo mikubwa kiasi. Looh! Niishie tuu hapa maana picha yake naiona inakuja kabisa kichwani.

Basi Taikon, ndiye mimi Muuza Barakoa nikaingia Rasmi kwenye enzi ya Umarioo. Nikilelewa kama mtoto asiye na miguu wala mikono. Nikiangaliwa kama mgonjwa mahututi, Hata kuogeshwa nilikuwa naogeshwa kwa tahadhari mithili kidonda cha Saratani.

Ukibebwa ubebeke wahenga waliniasa. Basi na mimi nikaona nijikakamue kumuonyesha manjonjo yule Mama mtekaji wa Taikon.

Mwezi wa tatu wote uliishia kwa huyo Mama nikila raha Mustarehe. Nikiyala maisha pasipo kubakiza mifupa yake.Looh! Taikon nilinenepa jamani jamani!

Basi siku isiyo na jina, siku ya mkosi ilikuja, siku ya jinamizi. Wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha. Hata mjusi ana mkia, hata dunia ina kiama, basi mwisho wa raha zangu na Mama Debora ulikuja, tena ulikuja kwa jeuri na kiburi.

Kumbe sikujua, lakini nilizembea kutokujua. Mama Debora alikuwa muuzaji wa Madawa ya Kulevya. Hilo nililitambua siku Polisi wa nne walipokuja pale nyumbani kwa Mama Debora. Polisi wawili walikuwa wamevalia kiraia na wengine wawili walivalia sare za Polisi. Hapo wakatuchukua licha ya Mamam Debora kujaribu kuwapa rushwa ya milioni mia mbili. Lakini wale polisi walikuwa wagumu kama Almasi ya kukatia vioo vigumu.

Nilijaribu kujitetea kuwa mimi sihusiki na biashara hiyo lakini hiyo haikuwa pona yangu. Tulichukuliwa na kwenda kulazwa lockup ya Mabatini.

Kesi ikasomwa, hukumu ikatolewa. Nikafungwa miaka saba jela, huku Mama Debora akifungwa miaka kumi na tano jela.

Hiyo ilikuwa mwezi wa nne mwisho.

Nilianza maisha mapya ya Jela, nikawa Taikon Mjela jela. Maisha ya kulala saa tisa, maisha ya ubabe na utabe. Huko jela nikakutana na watu wengi watukutu kama Majuto ambaye sikuzote ni Mjukuu.

Lakini kilichonimaliza zaidi ni kuugua kwa ghafla, hali iliyosababishwa kwenda kulazwa hospitali ya mwananyamala. Nilipopimwa majibu yalitoka Nina HIV Positive. Jamani UKIMWI nimeukwaa Kwa Mama Debora. Tamaa ndio kichwa na mkia wake ni Mauti naam Tamaa mbele mauti nyuma.

Siku ile nililia sana, nilijuta kujiingiza kwenye tabia za umarioo. Barakoa zimeniponza, noop! sio Barakoa bali ni tamaa zangu.

Basi nikapelekwa kwenye wodi ya wagonjwa wa UKIMWI, huko nikaona kundi kubwa la watu, wakike kwa wakiume, wakubwa kwa watoto. Lakini wale watoto walinitoa machozi kwani niliwaona kuwa hawakuwa na hatia yoyote kama mimi niliyemuasherati.

Basi wakanyanyuka kwenye vitanda vyao wakanitazama kisha wakaanza kuimba:

" Bado tunatumaini, kuishi kwa kujilinda

Vyakula kwa yetu mwili, tusisahau matunda,

Mazoezi ndio kiini, ya mwili kuutunza

UKIMWI sio Kifo, nafasi bado ingalipo."

Basi wimbo huo uliimba huku macho yakinitoka, niliumia maumivu ya mwisho kabisa. Ona bado kijana mdogo, bado hata sijafikisha miaka thelasini lakini nimeingia ukanda wa mauti. Ona sasa.

Basi hayo ndiyo matokeo niliyokutana nayo nilipopenda ganda la ndizi lililonitelezesha kwenye shimo la tewa.

Barakoa ya Marioo nimeivaa usoni.

Taikon Nimemaliza, mwenye swali ruksa kuuliza.

Robert Heriel

Taikon wa Fasihi

Kwa sasa Dar es salaam
 
Wewe mtoto unajua sana , wacha nipime ngoma maana sikukuu za mwisho wa mwaka nimeruka sana

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo mwamba umeukwaa kwa mama kubwa,

Dah Mungu atulinde vijana tusipende vya bure tufanye kazi
 
Ukimwi unaenda Kwa Kasi hivi sasa, ni kama vijana wameuchukulia kawaida.

Asante Kwa ujumbe mzuri ewe muuza barakoa aina ya shuka used.
 
Pole , huko jela umetumikia miaka yote saba tiyari au bado upo kifungoni, au uliachiwa huru?
 
Back
Top Bottom