Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Screenshot_20230804_001109.jpg


Kunahitajika PROGRAMU ya dharura kuliokoa hili jiji.

Sina maana ya kusema vijana wote wa Arusha ni wahuni na waalifu ama kusema Arusha si salama kabisa, La Hasha! ni kwamba uhuni ni kama umefumbiwa macho usambae mithiri ya kansa ya kidole inavyosambaa mwilini kwahio sio jambo la kufumbia macho kwamba eti kwasababu sio wote basi wapuuziwe, kumbuka hata mayai machache yaliyooza yatazidi kuozesha mengine hatua zisipochukuliwa, kwa wale tuliosoma soma nadhani tunajua kitu kinaitwa compounding.

Vijana wengi ni waliozaliwa na kukulia hapa hapa ni jamii za wazawa wenye asili ya Arusha kama Wameru na Waarusha pamoja na jamii za wenyeji ambao walihamia na wapo kwa muda mrefu kama Warangi, Wachaga, Wambulu, Wanyaturu.


Huu utamaduni wa kutukuza uhuni sijui ulifika vipi huu mkoa lakini unazidi kuleta athari kubwa, ulianza kidogo ila unazidi kukuzwa na kufanywa na vijana wengi wa sasa walioukuta tangu wakiwa wadogo, Mazingira ya jamii inayowazunguka na Mifumo ya malezi imekuwa mstari wa mbele kuwa kichocheo.

Kijana akiwa mhuni ama muhalifu ni jambo analoweza kujisifia na kupewa heshima, akienda jela ni kama cheo kabisa kisicho na shaka kwamba aliwahi kupiga tukio.

mapikipiki haya yanakimbizwa vibaya mno ili tu kupata sifa, vijana wanapoteza maisha kwa sifa za muda mfupi, tena sikuhizi kumezuka makundi ya kuendesha kwa kuinua tairi, Mbaya zaidi hawavai uniform za kujilinda ama kutumia pikipiki maalum za michezo, wanatumia bodaboda hizi za kichina za kubebea abiria na hapo hana jaketi gumu, hana kiatu kigumu kirefu, hana begi la sponji kulinda mgongo, hajavaa gloves za mikono, hana guard za viwiko na makoti, hana hata helmet kavaa mzula wa baridi ila anadiriki kuendesha kwa kasi ama / na kunyanyua tairi la pikipiki isiyo ya michezo, ajali hizi za kujitakia zipo nyingi vijana wanazikwa kama kumbikumbi, wengine wamejaa mount Meru na nkoaranga hospital wamevunjika vunjika....

vijana wanazidi kuutukuza ulevi wa hayo ma k-vant na bangi, sina shida na matumizi ya vilevi hata mimi ni mdau ila nafata misingi,tatizo makundi yanaponza sana na kuchangia abuse (abnormal use), wanatumia kwa kuigana au ile kutaka kuonekana wamepinda ili kupata uhakiki kutoka wenzao kwamba ni wajanja, na ndio hapa mtu ananasa kwenye uraibu.

Kuna Umakundi makundi wa kihuni huni wanaoishi bila future,

Suala la kupigana beto (visu) nalo halipo nyuma, Sime na visu vimekuwa vitu ambavyo vinazidi kuzoeleka kutumika sio tu kwenye uporaji bali hata kwenye ugomvi , niliwahi shuhudia live kwa macho yangu pale karibu na stendi ugomvi niliodhani watu watachapana ngumi niliona mtu anapigwa kisu damu inamwagika, hata wasanii wa huko kina Lord Eyes na Fido Vato wamewahi kupigwa visu,Marehemu Father Nelly wa kundi la X Plastaz aliuliwa kwa visu.

Wizi nao hauna dalili ya kupungua, watu wanaporwa kikatili sana inabidi utii amri lasivyo utavurugwa maini na beto, bodaboda wanaibiwa pikipiki mpaka kuuwawa, ujambazi nao upo wa kuvamia matajiri, kwa ufupi kuna famjlia zinajulikana kabisa wanaishi mjini kwa shughuli hizo lakini ndio wanapewa heshima maana uhuni unaonekana ujanja.

Suala la maadili nalo limepungua sana na hii imechangia sana hata makanisani na misikitini kuwepo na upungufu mkubwa sana wa vijana,
Kuna msiba vijana wameshiriki mazishi ya mwenzao mara wakataka mchapa mchungaji kisa mchungaji aliwapa maneno ya kweli wakachukua maiti kwenda kuizika wenyewe, kuongea hovyo hata mbele ya camera mpaka hivi sasa imekuwa kama jadi yao, mavazi wanayoona yanayomwakilisha mwana arusha original ni kuvaa mashati marefu mpaka magotini pamoja na miviatu mikubwa kuliko size za miguu.

Ajabu ni kwamba hata polisi ni kama vile wamefumbia jicho ama jitihada wanazofanya ni ndogo sana, ni kama vile wamezila na kujikatia tamaa wamewaacha wenye mji wafanye watachojua wao with little interference
 
Mimi mwanzo ilikuwa inanipa shida sana mpaka kuja kukaa sawa na kuwaelewa style ya maisha yao. Nilikuwa nashangaa mtoto anaweza kukupita tu na anakutazama na wala hakusalimii, sio mtoto unakuta hata mtu mzima.

Ila baada ya kuwaelewa jinsi gani wanaishi maisha yao na ID yao wala sikupata tabu tena kuhusu Wachugga, na mimi nawapita tu...!
 
Vijana wengi wahuni ni wazawa wa hapa hapa Arusha na matokeo ya kuukuta utamaduni wa kutukuza uhuni tangu wakiwa wadogo, imeshakuwa ndani ya mfumo wa maisha wa vijana wengi kwamba ili uonekane mjanja basi uwe mhuni wa kunywa pombe kali, kuvuta bangi ama uwe mhalifu.

mapikipiki haya ya Toyo wanakimbiza vibaya mno, ajali kila siku, wamejaa mount Meru na nkoaranga hospital wamevunjika vunjika miguu, kwenye magrouo yao haya ya kudandia pikipiki kuna rip nyingi sana.

vijana wanazidi kuutukuza ulevi wa hayo ma k-vant na bangi imekua fashen Yan Arusha haifai.

Wizi nao unashamiri sana, wezi wa bodaboda, tatumzuka, majambazi, n.k.
Ndio maana hayati Nyerere alidai uhuru kwa kuanza kuwahusisha watu wa pwani ,kati ,kusini na nyanda za juu....

Hapa kuna siri kubwa mno....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom