Ni kuhusu lile Jambazi la Arusha .....

WanaJF,
Lile jambazi sugu lililoua polisi constable mmoja na kumjeruhi mkuu wa upelelezi kituo cha USA nalo limeuawa usiku wa kuamkia leo maeneo ya Monduli ambako lilikuwa limejificha. Kwa habari zaidi naomba mtulie nafuatilia tukio hilo kwa undani ili ikiwezekana nipate picha!!!

Video hiyo kwa hisani ya KibopaMchachuaji, picha nitaweka baadae kidogo.

 
Last edited by a moderator:
Tuwe wakweli jamani pamoja na tuhuma nyiingi kwa huyo zombie ambazo am sure kuna ukweli nadani yake ila huyu bwana hakuua wale wafanyabiashara wala hakuawepo maeneo ya ule msitu kabsaa, tutoe tuhuma kisomi zaidi ili wana JF waelewe sheria ikoje. Ndio mana jaji aliwaachia kwa kosa hilo, kosa la kuua ni mpaka ushiriki mwenyewe physically na sio eti oooooh alitoa amri au alishauri tuue! hapo utashtakiwa kwa kosa lingine sio la kuua, na ndio mana DPP aliwafungulia kina zombie mashataka ya kimagumashi akijua fika watatoka tuu kwa vile wote hao ni wale wale!
 
Police wa bongo wanajuana na majambazi na wezi wa aina zote! Wanawakamataga only ikitokea kusalitiana au kuhatarisha kazi zao kama issue itaenda kombo!
Hebu fikiria hii; Siku moja tulikuwa Lumumba Street kuremba gari, kwa bahati mbaya mwenzangu akahisi kaibiwa bastola kumbe aliisahau kwenye gari ingine nyumbani, tilipanic ikabidi tuwaulize wale vijana kama wameiona wakakataa, uamuzi ukawa kwenda msimbazi police!
Kufika pale tukaeleza shida yetu then wakamtia ndani jamaa kwa uzembe which i think it was correct!
Bt cha ajabu baada ya muda walinirudia mm wakanambia hio bastola haijaibiwa bwana mtakua lazima mmeisahau mahali hebu pigeni simu nyumabani wapekue kila kona inawezekana ipo huko.
Kwa haraka niliwaza hawa jamaa wanauhakika gani kama haijaibiwa wakati cc ndio wahusika na imeibiwa Lumumba?
Ukichunguza sana utagundua kwamba hawa watu wanamtandao mitaani ya wahalifu kila kona, na kitu kikiibiwa smwhere lazima watajua haraka hata kabla ya kutoa mguu ofisini, mitandao yao hii ndio pia ni informers wa matukio yote ya uhalifu.
Hata gari tuliibiwa pia police walijua fika lipo kimara na linabadilishwa no na rangi, wakasema tukate kitu kidogo wakalifuatilie tukakata mara ya kwanza, ya pili tukaona wanatufanya ATM tukawaambia watupe ripoti tu tuka claim bima vile ubabaishaji ulizidi.
Hii ndio bongo mtu anakula mahali pa kazi , tatizo tu hawa ndugu zetu kazi yao ni muhimu na nyeti kuliko kula kwa kuuza twiga huko ngorongoro.

nyie inaonekana ni wazembe tena wa kupindukia,kitu kama silaha (bastola) eti mliiacha kwenye gari wakati watu wanaremba gari,alafu tukaripoti tukawekwa ndani,,,,,,,kumbe bastola tuliisau nyumbani,si ajabu ata huko nyumbani mliisau sebuleni au jikoni, eti police wkatuweka ndani mlitaka waweke nje?nyie ni wazembe mmesikiaaaa,na mnastaili mnyan'nganywe,
 
Wakuu nimefanikiwa kupata picha la jambazi hilo pamoja na video clip moja. Picha nitaweka mua si mrefu ila video itabidi nipate mdau ambaye atai up load ile mambo yawe shwari.
 
Wakuu nimefanikiwa kupata picha la jambazi hilo pamoja na video clip moja. Picha nitaweka mua si mrefu ila video itabidi nipate mdau ambaye atai up load ile mambo yawe shwari.

Mkuu ahsante kwa taarifa,

Tunasubiri hizo picha na ikiwezekana maelezo ya tukio zima la kuuawawa kwake.
 
kama wanaweza kwanini wasimkamate akiwa hai, ili haki itendeke na tusikie ana yepi ya kusema.
My take: Jamaa watakuwa wameua raia mwema, ili kujisafisha kwenye umma, urongo? Why, kila jambazi sugu liuwawe ilhali wahalifu wengine wanakamatwa. I smell something fishy...

Mwanafunzi wa chuo kikuu Mtanzania?
 
Isije ikawa mambo kama yale ya Rhino wa serengeti aliponyofolewa pembe,zikatoka taarifa za uongo! Fanya tafiti kwanza then ndo uje uweke bandiko lako humu,mkuu.
 
Mwanafunzi wa chuo kikuu Mtanzania?

si nishasema nimesimamishwa?
Hiyo imeathiri maujuzi yangu katika lugha, ukizingatia ndo shahada niliyokuwa nasomea. Anyways, hayo si ya leo. Jadili mada ya polisi kupambana na jambazi sugu kisha kuliulia mbali.
 
Wakuu nimefanikiwa kupata picha la jambazi hilo pamoja na video clip moja. Picha nitaweka mua si mrefu ila video itabidi nipate mdau ambaye atai up load ile mambo yawe shwari.

Tunakutegemea!

Na bila shaka ni hii ni habari njema kwa police na hata raia na mali zao hapa Arusha mjini na hata vitongoji vyake!
 
Kuwakamata mafisadi kwa nchi ya Tanzania ni ndoto.

Achana na neno MAFISADI BADO HALIJAINGIZWA KWENYE KATIBA YA NCHI KAMA KOSA NA ADHABU YAKE KUAINISHWA. SUBIRI KAMA KATIBA MPYA ITALIINGIZA HILO NENO NA KUELEZA MAANA YAKE NA KAMA NI KOSA NA ADHABU YAKE. POLENI SANA MNAOFIKIRI KUITWA FISADI NI KOSA KISHERIA, KWA SASA BADO.
 
Ngeleja keshafanya vitu vyake hivyo wadau muwe na subira kidogo akifurahi Ngeleja kila kitu kitakuwa hewani.
 
Ni rahisi sana kwangu kutoa pole kwa jeshi la Polisi na familia ya askari aliyeuwa wakati ule, lakini ni ngumu na haiwezekani kabisa kwangu kuwapongeza au kuamini kuwa wameua jambazi hawana, utashi,sura,maadili wala maumbile ya kuaminiwa.
Kuna askari mmoja wa upelelezi na wenzake , naendelea kufuatilia taarifa zake, kuwa kila anapohamishiwa baada ya muda kuna kikundi cha vijana 'wake' hufuata, vijana hao hufanya shughuli za utekaji magari ili kuibia abiria na uhalifu mwingine wa kiporaji kwa kutumia silaha au wa kuaminika.
 
Mimi Nadhan Kama aliyeuwawa ni Yule aliyeuwa polisi basi Watakuwa na Connection Nzuri na huyu Jambazi katika biashara zao za kukwapua!! Sasa polisi huwa wanakuwa so smart kwenye Kutunza siri na njia pekee ni Kumuua mshukiwa ili kupoteza ushahidi!! Sasa kama polisi wangekuwa Watu Waadilifu si wangemkamata huyu Jambazi akiwa Hai!! Hii ingesaidia kupata Taarifa muhimu za Kiintelijinsia!!
 
Back
Top Bottom