Ni Kosa Gani La Kawaida • Ambalo Watu Wanalo Kuhusu Wewe?"

Nyafwili

JF-Expert Member
Nov 27, 2023
2,774
6,885
Habari wana JF, Poleni na pilika pilika za hapa na pale 🤝, Binadamu mara nyingine wanaweza kuwa na tabia ya kutoa hisia au sifa za kibinadamu kwa vitu ambavyo havina hisia wala ukweli wowote, yani utakuta mtu au watu wanajiuliza maswali ya namna hii kuhusu wewe:-

• Watu wengi wanapata ugumu kuamini ukiwaambia kuwa huna uhusiano wa kimapenzi(upo single) , labda kwa sababu ya muonekano wako, wanakwambia "Mtu mzuri kama wewe unakosaje mchumba."

• Marafiki wanafikiri una utajiri, na unaposhindwa kutoa pesa, au mchango fulani wanakuona kama mkatili vile, au mchoyo usiye na ushirikiano kijamii.

• Watu Wengi wanakuchukulia kama mtu mgumu na mkaidi, labda kutokana na jinsi unavyojieleza au muonekano wako, ingawa kuna baadhi ya marafiki wa karibu wanaweza kuona kwa upande mwingine upo sahihi unachofanya.

...……. Jamii inayokuzunguka inasemaje kuhusu wewe 😐.
 
Back
Top Bottom