Ni kitu gani ambacho licha ya usomi wako bado kinakusumbua?

Kama yupo mwingine ambaye saa ya mshare ni changamoto kama mimi yaani akiangalia anaanza kuhesabu na kutofautisha mshare mrefu na mfupi; tuko pamoja!!
 
Mambo ni mengi ambayo hatujui/hatuwezi licha ya umri wetu au level zetu za elimu au kipato. Licha ya ukweli huu kuna watu kwenye huu uzi wanaona kuwa wako perfect zaidi ya rula.
 
Mimi hesabu za hasi na chanya nimekuja kujua juzi kati tu hapo

Kingine, kufunga tai, hii ndo imenishinda kabisa
 
HIVI KWELI DUNIA NI DUARA .??

KAMA NDIYO NI NCHI GANI ZIPO KWENYE NCHA YA DUARA .

PIA KUNA UHUSIANO GANI KATI YA MWAKA NA MIEZI KUMI NA MBILI ?? AU WIKI NA SIKU SABA ..??

PIA NI KWELI AKILI ZIPO KICHWANI TU ??
 
Najaribu ku figure out inakuwaje nchi kama Korea ambayo ilianza from scratch baada ya vita ya peninsula miaka ya 1950s ambayo ni almost sawa na sisi tulipopata uhuru (hakuna tofauti ya miaka 10).

Wao wanawaza kufanya expeditions huko kwenye space wakati sisi tunajaribu kuhamasishana na kuelimishana juu ya uchimbaji wa vyoo.

CCM ni cancer iliyojichimbia hata kwa chemotherapy hatupati ahueni.
😂😂😂 Sisi tunajaribu kuhamasishana na kuelimishana juu ya uchimbaji wa vyoo
 
Nashindwa kuacha pombe,makampuni mengi yananihitaji kutokana na taaluma yangu lakini kikwazo pombe

Huwa najaribu kuacha,lakini sijawahi kumaliza siku mbili,eti nisipige nyagi

Yaani nikikosa kwa muda wa siku mbili Basi mwili unawasha nitajikuna mpaka Basi

Nilishawahi kuita wachungaji nyumbani waje kuniombea lakini ilishindikana

Kuna siku tulipanga tukutane siku ya jumamosi saa nane mchana

Basi siku hiyo licha ya kuwa na kiu ya hayo maji nilijikaza Sana ili ule muda wa maombi unikute Niko na akili timamu,

Chaajabu sijui ilikuaje,wakati timu ya watu sita akiwemo pastor inaingia sebuleni Mimi tayari nilikuwa na simirnof mezani,ikabidi tuahirishe suala la maombi
 
HIVI KWELI DUNIA NI DUARA .??

KAMA NDIYO NI NCHI GANI ZIPO KWENYE NCHA YA DUARA .

PIA KUNA UHUSIANO GANI KATI YA MWAKA NA MIEZI KUMI NA MBILI ?? AU WIKI NA SIKU SABA ..??

PIA NI KWELI AKILI ZIPO KICHWANI TU ??
Bangi unayovuta Ni ya wapi
 
Back
Top Bottom