Hakuna kitu kinaleta Stress kama kuota Mvi au upara halafu bado hujajipata

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
Kwema Wakuu!

Ni Stress hapa!
Ni sonona hapa! Kihoro kinakaba kama pumu huku. Yaani hapa mambo sio mambo.

Kuna Watu wanakuambia umri ni number tuu lakini huko ni kufarijiana tuu!
Hakuna kitu kinauma na kuleta mfadhaiko na mtagusano kulinafsi kama kuona jua lile linazama halafu wewe mambo bilabila.

Nywele kunyonyoka kama mbwakoko mzee. Alafu ukicheki huna mbele wala nyuma sio Pouwa Washikaji.
Mvi kukuota wakati unaishi chumba kimoja sio lelemama ndugu zangu.

Fikiria mvi hizi hapa alafu huna hata mke wala mtoto. Kiumri ni miaka labda 35 hivi. Shida ni kuwa mpaka muda moja na mbili haikai.
Kila ukikumbuka ile kauli ya kusema nikiwa mkubwa nitafanya bla! Blah! Blah! Unapiga ngumi ukutani.
Nani akutake na mvi zako Budah! Yaani huna pesa alafu umejaza mvi kichwani. Ni binti gani yupo tayari kukubali kuwa nawe?
Binti gani atakubali kuwa na wewe na kipara chako na hauna Maisha.

wanasema vijana ndio huona maono bwashee! Wazee wenye mvi na vipara huota ndoto tuu. Yaani kila unaloliwaza kuna asilimia 70 kuwa ni ndoto uotayo ya alinacha.

Kipara sio shida. Shida ni pale huna mbele wala nyuma. Nyie ni mateso bila chuki. Hujui tawi gani ushike.
Yaani Upara na mvi vinakukuta ni Jobless mamaaaa! Hujui ufanye nini unafikiri Daah!

Unakipara chako kinamea polepole, au unamvi zako alafu huna pesa mbona lazima uwe introvert tuu. Yaani ndio ile unajikita mkimya maana nini sasa utaongea. Na hawa vijana wa 2000 hawana salia mtume, hawajui la muhazini wala mnadi Swala. Watakuona Babu yao ilhali hata miaka 40 huijui.
Utani utani wa kijinga na maneno ya kukutania vitazidi kushamiri.
Automatically kijiweni utaanza kupotea na utakuwa mtu wa kuwa bize for nothing.

Usiombe hiyo hali ikukute mazee! Kwanza hata ukienda vibaruani lazima uzinguliwe na matajiri kwa sababu wanajua huna chaguo, alafu mbaya zaidi lazima wakuzungushe kwenye malipo. Alafu ukijaribu kuwa mshari wanakuambia hayo mambo waachiw vijana ilhali wewe mwenyewe ndio kwanza upo miaka 35. Kudadadeki! Innalilah wainalilah Rajuun!

Chochote ukitaka kukifanya ukiwa kipara au mvi tena kwa mtaji mdogo lazima kikutie unyonge, Watu watakuwa wanakuona kama Budah fulani hivi.

Napendekeza, ukiwa below miaka 30 na umetoka familia maskini, kisha bado hauna ramani kivile.
Miaka 20- 30 ndio umri wako wa kujaribu kufanya kazi zózote na kujiweka sawa. Ndio umri wa kutafuta Pisikali moja uzae nayo yaani uanzishe familia ukiwa bado unamuonekano mzuri.

Usibeti kuwa ngoja utafute pesa Kwanza, huko ni kubet Ndugu yangu. Unaweza ukapata pesa au usipate. Lakini kwa umri wa miaka 20-30 huwezi kukosa Mwanamke mzuri wa kuanza naye familia akuzalie watoto angalàu mmoja au wawili.

Ili hata mambo yakibuma na mkeo akakuzingua uwe unafaida ya mtoto au watoto.
Lakini umechelewa kuanzisha familia kwa kubet kuwa unatafuta pesa Kwanza. Alafu umri umesogea, kipara na mvi zile alafu pesa hujapata. Ndugu yangu umekwisha!

This is Africa. Kanuni za huku ni za kipekee. Fanya kile ambacho unauhakika nacho kwa sasa na sio kubet kuwa unatafuta pesa kwanza kama vile uko Ulaya.

Elewa, huku Afrika unaweza ukawa na Juhudi, bidii na akili lakini bado maisha yakakupasua tuu. Lakini kwa Ulaya hilo haliwezekani.
Usijidanganye hapo na vishughuli vyako vya kujitafutia ambavyo vinakuingizia mia mbili mia tatu na kujipa moyo kuwa mambo yakikaa vizuri ndio utaanzisha familia. My friend, unajidanganya. Kwa Afrika labda uwe umeajiriwa tena serikalini ndio unaweza kufikiri kwa namna hiyo.

Biashara inabadilika muda wowote. Ni bora ibadilike ulishapata watoto tena na mke mzuri ambaye hata mkiachana haitalalia upande wako.

Uzee unatísha wazee! Uzee ambao haujajipata sio pouwa ndugu zanguni. Wanaosema Fainali uzeeni wanajua wanasema nini ndugu zanguni.

Tuombe Mungu atupe akili ya kutumia baraka zake lakini pia atupe uwezo wa kufanya mambo kwa wakati ili tusijetaabika.

Mwenye mvi nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Formula ya Bongo kujipata ni miaka 50 msidanganyike, kinyume cha hapo hayo ni majizi tu.

Vijana msikate tamaa, hakuna tajiri yoyote Africa ambaye ni self made millionaire ambaye yuko under 50, hakuna.

Hiyo betting ni mbaya sana. Fikiria kijana anapiga mzigo na kutafuta maisha mpaka miaka 50 alafu bilabila. Ndio atake kuanzia familia. Binti wa nani atakuwa tayari kumkubali?
 
Sijazungumzia swala la familia, nazungumzia uhalisia wa kujipata Bongo ngoma inakwenda 50.

Cha Kwanza Bongo hakuna muendelezo kwenye kumiliki uchumi, ndio maana si ajabu kukuta mtu ambaye 2015 alikuwa njema lakini Leo 2024 kachoka Vibaya hali mbaya na biashara zote zimekwenda kombo.
 
Formula ya Bongo kujipata ni miaka 50 msidanganyike, kinyume cha hapo hayo ni majizi tu.

Vijana msikate tamaa, hakuna tajiri yoyote Africa ambaye ni self made millionaire ambaye yuko under 50, hakuna.
Wengi tunaangalia outliers. Majority ya watoto kutoka familia masikini watajenga @ the age of between 35-50. Na wengine watamalizia kwa pension kama waliajiriwa na wengi hawatajenga kabisa.

Wengine mafanikio yao makubwa watawapitisha watoto wao shule. Just the hustle ya kutafuta Ada, na kuwalisha watamalizia maisha na nguvu zao hapo.

Mlinganyo wa maisha ya kijana wa kitanzania ni Mgumu sana jitahidi usiongeze stress maana utaugua na Hela ya kufurahia kidogo uzeeni na mama mtaipeleka Kairuki.

Tuliza kichwa, macho yako weka kwenye sahani yako.
 
Tatizo lenu mnajicompare na watu wengine
Uwezo wa kung'amua mazingira yako ni muhimu sana kutiliwa mkazo katika malezi ya watoto. Unakuta mtu yeye ndio first generation educated kwenye ukoo na uzao wa kwanza kuishi mjini... Anajilinganisha kimafanikio na watu ambao Babu zao walizaliwa mijini, na biashara aliamza Babu yake Babu.... Kujitafutia stress tuu
 
Jifunzeni Kwa wakurya, miaka 18 u meshaoa, una watoto wawili ndipo unaendelea na utafutaji.

Maisha ni Kupambana, muhimu Uzima,

Hakuna stress kubwa kama Binti wa 12 yrs kujazwa mimba.

Mwanaume hapati mimba!!

Hivyo Kwa sie wanaume hakuna kitu inaitwa stress, tupambane.
 
Kwa hii mindset yako mleta mada, niseme tu; umekwisha.

Hata unaposema bora kukimbilia kuanzisha familia mapema kabla hujajipata, hao watoto wataishije? au ndio unamzalia bibi yao? sasa huo kwako ndio ujanja?! Hapana, huo sio ujanja, hapo simply unaambukiza umaskini wako kwa wengine.

Unatakiwa kubadilisha the way you think kuhusu maisha yako, kama ukiendelea kuamini hizi porojo ulizoandika hapa, utaishia kujitundika.

Ukumbuke tu, kila mmoja amepangiwa namna yake ya kutoboa kwenye haya maisha, haijalishi umri, usilazimishe kutengeneza formula ya kufanikiwa maishani kama ulivyoandika hapa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kwema Wakuu!

Ni Stress hapa!
Ni sonona hapa! Kihoro kinakaba kama pumu huku. Yaani hapa mambo sio mambo.

Kuna Watu wanakuambia umri ni number tuu lakini huko ni kufarijiana tuu!
Hakuna kitu kinauma na kuleta mfadhaiko na mtagusano kulinafsi kama kuona jua lile linazama halafu wewe mambo bilabila.

Nywele kunyonyoka kama mbwakoko mzee. Alafu ukicheki huna mbele wala nyuma sio Pouwa Washikaji.
Mvi kukuota wakati unaishi chumba kimoja sio lelemama ndugu zangu.

Fikiria mvi hizi hapa alafu huna hata mke wala mtoto. Kiumri ni miaka labda 35 hivi. Shida ni kuwa mpaka muda moja na mbili haikai.
Kila ukikumbuka ile kauli ya kusema nikiwa mkubwa nitafanya bla! Blah! Blah! Unapiga ngumi ukutani.
Nani akutake na mvi zako Budah! Yaani huna pesa alafu umejaza mvi kichwani. Ni binti gani yupo tayari kukubali kuwa nawe?
Binti gani atakubali kuwa na wewe na kipara chako na hauna Maisha.

wanasema vijana ndio huona maono bwashee! Wazee wenye mvi na vipara huota ndoto tuu. Yaani kila unaloliwaza kuna asilimia 70 kuwa ni ndoto uotayo ya alinacha.

Kipara sio shida. Shida ni pale huna mbele wala nyuma. Nyie ni mateso bila chuki. Hujui tawi gani ushike.
Yaani Upara na mvi vinakukuta ni Jobless mamaaaa! Hujui ufanye nini unafikiri Daah!

Unakipara chako kinamea polepole, au unamvi zako alafu huna pesa mbona lazima uwe introvert tuu. Yaani ndio ile unajikita mkimya maana nini sasa utaongea. Na hawa vijana wa 2000 hawana salia mtume, hawajui la muhazini wala mnadi Swala. Watakuona Babu yao ilhali hata miaka 40 huijui.
Utani utani wa kijinga na maneno ya kukutania vitazidi kushamiri.
Automatically kijiweni utaanza kupotea na utakuwa mtu wa kuwa bize for nothing.

Usiombe hiyo hali ikukute mazee! Kwanza hata ukienda vibaruani lazima uzinguliwe na matajiri kwa sababu wanajua huna chaguo, alafu mbaya zaidi lazima wakuzungushe kwenye malipo. Alafu ukijaribu kuwa mshari wanakuambia hayo mambo waachiw vijana ilhali wewe mwenyewe ndio kwanza upo miaka 35. Kudadadeki! Innalilah wainalilah Rajuun!

Chochote ukitaka kukifanya ukiwa kipara au mvi tena kwa mtaji mdogo lazima kikutie unyonge, Watu watakuwa wanakuona kama Budah fulani hivi.

Napendekeza, ukiwa below miaka 30 na umetoka familia maskini, kisha bado hauna ramani kivile.
Miaka 20- 30 ndio umri wako wa kujaribu kufanya kazi zózote na kujiweka sawa. Ndio umri wa kutafuta Pisikali moja uzae nayo yaani uanzishe familia ukiwa bado unamuonekano mzuri.

Usibeti kuwa ngoja utafute pesa Kwanza, huko ni kubet Ndugu yangu. Unaweza ukapata pesa au usipate. Lakini kwa umri wa miaka 20-30 huwezi kukosa Mwanamke mzuri wa kuanza naye familia akuzalie watoto angalàu mmoja au wawili.

Ili hata mambo yakibuma na mkeo akakuzingua uwe unafaida ya mtoto au watoto.
Lakini umechelewa kuanzisha familia kwa kubet kuwa unatafuta pesa Kwanza. Alafu umri umesogea, kipara na mvi zile alafu pesa hujapata. Ndugu yangu umekwisha!

This is Africa. Kanuni za huku ni za kipekee. Fanya kile ambacho unauhakika nacho kwa sasa na sio kubet kuwa unatafuta pesa kwanza kama vile uko Ulaya.

Elewa, huku Afrika unaweza ukawa na Juhudi, bidii na akili lakini bado maisha yakakupasua tuu. Lakini kwa Ulaya hilo haliwezekani.
Usijidanganye hapo na vishughuli vyako vya kujitafutia ambavyo vinakuingizia mia mbili mia tatu na kujipa moyo kuwa mambo yakikaa vizuri ndio utaanzisha familia. My friend, unajidanganya. Kwa Afrika labda uwe umeajiriwa tena serikalini ndio unaweza kufikiri kwa namna hiyo.

Biashara inabadilika muda wowote. Ni bora ibadilike ulishapata watoto tena na mke mzuri ambaye hata mkiachana haitalalia upande wako.

Uzee unatísha wazee! Uzee ambao haujajipata sio pouwa ndugu zanguni. Wanaosema Fainali uzeeni wanajua wanasema nini ndugu zanguni.

Tuombe Mungu atupe akili ya kutumia baraka zake lakini pia atupe uwezo wa kufanya mambo kwa wakati ili tusijetaabika.

Mwenye mvi nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
kuota mvi, kuwa upara baadae unashangaa nywele za kifuani nazo zinakuwa nyeupe aisee ni srtess juu ya stress
Hata kama umejipata vinashtua, utajikuta unapaka black kifuani 😆 😆 😆
 
Maisha ya kiafrika hayana formula kabisa.
Unaweza pambana sana na usitoboe mpaka unakufa.

Kosa kubwa ni kuishi kwa kujifananisha na walio fanikiwa badala ya kujifunza kutoka kwao .
Matokeo yake ni kupata depression na matatizo ya afya ya akili.

Muombe MUNGU sana, fanya kazi kwa bidii, focus on your goals, live simple and enjoy life.
 
Kipara na mvi ni swala la genetic and not about being broke or jobless and other related stuffs.

Maisha hayana kuwahi wala kuchelewa kitu muhimu ambacho MTU anabidi kukipigania to all his lifetime ni kuhakikisha unakuwa sober all the time Kwa kukubali kujifunza kila siku, kujizuia na aina yoyote ya uraibu Kama Pombe, madawa, ngono and etc.

Ukijifunza hivi vitu

Movement vs progress
Speed vs direction.

Watz tupo katika movement Ila hatuna progress we live fucking life paycheck to paycheck and hand to mouth life.

As well tuna speed ya kuharakia mambo Ila hatuna direction yoyote Kuwa wapi tinahitaji kufika na nini tunataka katika MAISHA yetu.

Ikiwa MTU atapata stress Kwa kupata kipara na mvi basi huyo MTU atakuwa hajitambui na hajui anahitaji nini katika aya Maisha .

Na unfortunately Africans wanaishi Kwa kuongozwa na macho ya watu na sio kutoka ndani and this is problem why we are still broke day to day.
 
Back
Top Bottom