Ni ipi siri ya Wachaga kuwa kabila lililoyaacha makabila mengine mbali mno kwenye mafanikio?

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Licha ya umasikini wetu wa taifa hapakosekani kundi la watu wenye nafuu, hata kwenye ukoo masikini wale wenye magari hutokea koo maskini ila wao kama wao wapo mbali kuzidi wenzao, Tukigusia makabila yenye asili ya hapa kwetu, wachaga wapo mbali mno, yapo makabila yanayofatia ila ni gepu refu mno.

1.Elimu: Hawa watu wamesoma sana na shule zipo huko kwao tangu zamani sana, shule zipo nyingi zimejengwa vizuri hakuna mambo ya wanafunzi kurundikana madarasan ama kukaa chini, walishamaliza haya matatizo tangu zamani. Mwamko huu wa elimu umepelekea kuwepo shule nyingi za kimataifa Moshi na Arusha, matajiri wanapeleka watoto shule hizi hawaoni shida kulipia ada milioni 40, shule hizi ni kama international school of Moshi, Braeburn, Kennedy house, St Constantine, n.k. ni shule zenye mfumo moja duniani na hata matajiri na wanasiasa wa nchi za ulaya husomeshea watoto, kuna comnections nzito na expoosure,.... hapa kwenye elimu wanaokaribia labda wahaya lakini tatizo wahaya wanakomaa kusoma tu Ila mchaga anasoma, anatafuta pesa, hasahau kwao na hata akipata hajigambi wala kuridhika.

Biashara - Ni wakongwe katika hii sekta, biashara ipo ndani ya damu, hata walioishia darasa la saba wanafanya makubwa, wasomi nao maarufu tumeona wakileta makampuni ya ndege, media house, kampuni za kuwachota pesa wazungu waje kutalii, n.k. ukicheki hata soko la hisa DSE watanzania wa asili wapo wachache ila wachaga ndio wengi. sikuhizi naona kuna makabila mengine yamepata mwamko kama wakinga, waha, wasukuma n.k ila kwakweli bado gepu ni refu, wameachwa mbali sana na wachaga.

siasa - Siasa pia ipo ndani ya damu, nikueleze tu ya kwamba hata vyama vingi maarufu vya upinzani vilianzia huko, TLP, NCCR, CHADEMA, n.k.

kuendeleza na kujenga vijijini kwao hawana mpinzani, Ni sehemu yenye vijiji vyenye makazi bora ya nyumba nzuri na za kisasa, wengi wakistaafu hurudi kuishi huku bila shida. maji Safi ya bomba yapo, barabara zipo, hospitali zipo, umeme upo, n.k. Kama ilivyo kwa Moshi kuwa mojawapo ya miji Safi miaka n'a miaka, vijijin pia makazi yamepamgiliwa vizuri kwa usafi wa hali ya juu. nimeona makabila mengine wanajaribu lakini tatizo unakuta hata mtu akijenga kijijini kwao, nyumba nzuri bado inaweza kuwa moja ama zinahesabika kijiji kizima, na hapo kuna shida ya maji inabidi wachimbe kisima, umeme watumie jenereta, barabara mbovu, n.k. Hali hii hupelekea hata waliojenga vijijini wakistaafu wanabaki mjini, ila pia wengi huogopa kujenga ama hata wakijenga wanasita kwenda kuishi vijijini kwasababu ya uchawi, Nina rafiki yangu wa Geita huko wazazi wake walikataa awajengee nyumba ya kisasa kwa kuogopa kuwatia ndugu na majirani zao wivu wasije wakarogwa ama wamroge mtoto wao, mtu anaweza kujenga huko kibishi lakini ni ile ijulikane tu kajenga kwao ila hapendi kukaa huko labda itokee msiba ama dharura.

Kwenye hizi nafasi za Teuzi hawajajaa sana maana hizi nafasi kwa kiasi kikubwa ni Raisi anateua watu wake ila ukija huku kwenye ajira za ofisini wamejaa, mashirika ya uma na kimataifa wapo.

kuridhika kwa wachaga ni ngumu sana, mtu alieridhika mara nyingi huonyesha majigambo, ujivuni, kiburi, sifa, n.k. anaona ndio ashafika, ataanza kuiita laki si pesa hadharani, dharau, sifa za kutaka attention watu wajue ana hela, n.k kwa wachaga mtu anaweza kuwa na pesa kibao ila hizi tabia hawaendekezi.

Ni nadra sana kusikia mambo ya uchawi uchagani kama ilivyo umasaini na ukuryani, simaanishi kwamba haupo kabisaaaa ila ni kwa kiwango kidogo sana, si jambo la kusumbua sana jamii kwamba flani kamtupia jini jirani kisa kapata kazi, kurogana kisa mtu kanunua baiskeli, kutupiana mabusha, malimbwata, kuwanga usiku, n.k. ukisikia mganga mchaga, mmasai au mkurya kimbia, huyo tapeli tu, huku mtu akitaka uchawi afunge safari kwenda kununua kwengine, sehem ya karibu upareni.

Wanaheshimu mila na desturi zao: kifupi wanajua wapi wametoka na wapi wanaenda, wachaga ikifika december kuna mtu asiejua balaa lao ? huwa ni kama waisrael wa nchi mbali mbali wanarudi kwao, Kama ilivyo utamaduni wa kila kabila matambiko hayawezi kukosekana kwa zile koo za kichifu.
..........................
 
20230714_183713.jpg
20230711_164912.jpg
 
Tukigusia makabjla yenye asili ya hapa kwetu, jamaa wapo mbali mno.

Kunaweza kuwa na kabila linalowafatia ila gepu ni kubwa sana.

Iwe ni elimu, iwe ni biashara, iwe nk siasa, iwe ni kuendeleza kwao, iwe ni kujaa kwenye system, jamaa wapo mbali mno.

Kwa wengir unaweza kukuta kwenye elimu wapo ila kwengine zero

wengine unaweza kuta wanajitahidi biashara ila huko kwao hakutamaniki na elim bado sana

n.k.
Pamoja na baadhi ya wachaga kuwa wezi

Lakin jamaa wapo very smart

Nmefanya nao kazi sehemu tofauti tofauti

Sio wanawake wala wanaume
Wako smart
 
Wachaga nimefanya nao biashara ni watu smart sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haswa mkuu
Wako vizuri na wakipata fursa hawaachii

Nakumbuka miaka ya nyuma sana wakati jeans walikuwa wanavaa ndugu za mabaharia tu ila cha ajabu nilikuwa nasoma wilaya moja tajiri pale alikuwa mchaga mwenye duka kubwa kuliko yote

Alikuwa anauza Jeans na Yale mashati ya cowboy yenye miraba
Saa za omax, omega, citizen na Oris pia

Alikuwa anatoa Kenya ila jamaa alikuwa smart sana
Jeans ya kwanza mzee alininunulia kwake
 
Elimu! Elimu! Elimu!
Hii ndo siri kuu ya wachaga. Wakati uhuru unapatikana tayari wachaga walikuwa mbali sana kielimu. Shule za msingi na sekondari za kutosha. Kingine pia ni kujali mila na tamaduni zao. Kwa Afrika mashariki, kati na kusini hakuna kabila lenye maendeleo kuwazidi wachaga.
 
Tukigusia makabjla yenye asili ya hapa kwetu, jamaa wapo mbali mno.

Kunaweza kuwa na kabila linalowafatia ila gepu ni kubwa sana.

Elimu, wapo njema,

Biashara - wanaofata ni waha na wakinga ila wamepigwa gepu refu sana

siasa - ccm wamo na kila chama pinzani kuanzia tlp, nccr, chadema vina asili ya wachaga

kuendeleza na kujenga kwao hawana moinzani, nimeona wengine wanajenga nyu.ba nzuro vijijini kwao ila unakuja kijiji kizima nyumba nzuri zinahesabika.

kujaa kwenye system, vyeo kama majaji, wakurugenzi, wahandisi, madaktari, wapo kibao.

Kwa wengir unaweza kukuta kwenye elimu wapo ila kwengine zero

wengine unaweza kuta wanajitahidi biashara ila huko kwao hakutamaniki na elim bado sana

n.k.
Wachaga ni lile kabila kati ya 12 la Israel lililopotea (Lost tribe of Israel).

Kwa kifupi wachaga ni wayahudi wa Africa.

Tafiti za DNA zimethibisha kabisa.
 
siri iko hapa,

wajerumani walitawala maeneo ya kilimanjaro mapema sana kuanzia 1885, hivyo wachaga walikua ni moja kati ya makabila ya kwanza kabisa kuchangamana na watu weupe tanzania bara....

shughuli la kiuchumi na ile elimu ya kikoloni kwa wale wachaga wa tabaka la juu ndo ikapelekea wao kujanjaruka haraka kuliko makabila mengine....
 
Back
Top Bottom