sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
- Kijijini kwetu huwa tunarudi wote kwa pamoja kukiwa na msiba tu, nje ya hapo kila mtu huwa anarudi kimpango wake, kuna ambao hawarudigi kabisa.
- Tunaoishi mijini hatujawazoesha watoto warudi kwao, wakiwa wakubwa wanashindwa hata kurudi kwao kwasababu hawajapazoea, Nina marafiki wengi waliokulia mjini wamewahi kwenda kwao mara tatu tu, wamekuwa watu wazima hawajawahi kwenda kwasababu hawakuzoeshwa kurudi, mtoto inabidi azoeshwe kurudi kwao kila mwaka hata akiwa mtu mzima awe anarudi mwenyewe.
- Huku mijini ndugu tunakutana wenye nafuu ya maendeleo wapo wenye biashara zao, kazi nzuri, n.k. tunaishi vizuri mjini lakini huko vijijini maendeleo ni duni, wapo wanaoendeleza kwao lakini unakuta kijiji kizima nyumba za kisasa ni asilimia 2 tu, hizo ndio huwa zinapigwa picha kudanganya kwamba kijiji kina maendeleo.
- Imani za kishirikina nazo zinachangia watu wasirudi, Sikatai kwamba kuna matambiko na hakuna kabila lisilo na tambiko lake, hata wachaga kuna koo zenye historia za kichifu lazima watambike. Tatizo huku kwetu makabila mengi mambo ya uchawi yamesahamiri tunaogopa kurudi vijijini, stori kibao zipo vijijini watu kupigana vipapai kisa tu mtu kanunua pikipiki, kutupiana magonjwa, kutupiana majini, n.k.