Hannah
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 10,247
- 42,004
Unaona sasa?Unesema vyema, nakumbuka nilikwenda Shinyanga vijijini kwenye outreach fulani ilikua imeandaliwa na UNDP, na ilikua ni kipindi cha uchaguzi na lengo ilikua ni kutoa hamasa na awareness kwa wananchi ili wajue haki na wajibu wao wa kuopiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka
Wanawake wengi walilalamika wakasema waume zao wameshikilia kadi zao za kura na hawaruhusiwi kwenda kupiga kura, na wakati mwingine wenyeviti wa vijiji wanakusanya kadi za kura za wanawake wote na wanapohoji wanaambiwa kwamba viongozi wanachaguliea na wanaume tu, kwa hiyo wanaume ndio wataamua hizo kadi zimpe nani kura, asilimia 90 ya wanawake walikua na lalamiko moja katika maeneo yote tuliyopita
Wengine walisema unapokua na itikadi tofauti na ya mume, basi ujue hutapata matunzo wala unyumba, tulipopata nafasi ya kuzungumza na wanaume, wengi wao walikua wabishi tena wasukuma ni wabishi balaa yani walituambia nyie wanawake hamna mamlaka ya kuzungumza na sisi, asimame mwanaume mwenzetu azungumze
Kwenye kijiji fulani, mwenyekiti wa kijiji alikua ni mwanamke, alitukaribisha vizuri na alitueleza changamoto nyingi lakini pia alitukutanisha na mwanamke mmoja mwenye watoto watatu wote wa kike, huyu mwanamke naweza sema umri wake ulikua kati ya miaka 19-21, mwanamke huyu alikua amejeruhiwa kila mahali na alikua amefika ofisi ya serikali ya kijiji kulalamika, watoto wake wote watatu walikua wametendewa ukatili na baba mdogo yaani mdogo wa mume, na hao watoto wote ni chini ta miaka mitano, mwanamke alitoa taatifa kituo cha polisi na baba mdogo alikamatwa ila mume wake alimpiga na kumjeruhi kwa kosa la kutoa taarifa kituo cha polisi na akaenda mbali zaidi akamfukuza nyumbani pamoja na watoto wenye majeraha ya kubakwa
Hii ni mifano michache ambayo inaumiza na ni dhahiri kwamba bado tunahitaji sana kuwasaidia wanawake especially kwenye maeneo ambayo bado wana mila kandamizi kwa wanawake na watoto wa kike
Kama mwanamke hatafundishwa ataona ni haki yake kupigwa, hata watoto wakifanyiwa ukatili hawataona ni vibaya wataona ni haki yao kufanyiwa hivo.
Ndio maana kuna jambo lililetwa humu baba anabaka watoto wake, mama wa watoto alivyogundua hajashitaki popote akaondoka akaachana na mume wake. Kuondoka aliacha watoto , yule baba akaendelea kubaka mtoto na majirani wakajua ila hawakufanya chochote hadi mwisho wa siku mtoto ana ujauzito wa baba ndio unaona wanasema ni jambo la siku nyingi sana, hata mama yao aliamua kuondoka baada ya kugundua hilo.
Sasa hapa utagundua mwanamke anahitaji elimu ya kujitambua na kujua kitendo kibaya kikifanyika anatakiwa asikae kimya apaze sauti hadi apate msaada. Na watoto pia.
Leo hii mtu anakuambia hizi elimu zinapotosha wanawake hazisaidii kitu.