Ni ipi maana halisi ya kumkomboa Mwanamke?

Hivi unajua kuna mila ambazo hadi leo zinakeketa wanawake?
Unajua kuna maeneo hadi leo mwanamke ruhusiwi kusoma na anaozwa akiwa na miaka 6 kwa lizee la miaka 50?
Unajua kuwa wanawake wangapi wapo kwenye ndoa lakini wananyanyasika? Mume haachi matumizi akirudi kalewa anapiga kwanzia mke hadi watoto?

Hayo ni machache, msiwe mnajadili mambo ambayo hamyajui .
Hili naungana na wewe. Bahati nzuri mimi natembea sana maeneo tofauti tofauti kutokana na shughuli zangu hivyo nimejionea kwa macho sio kusimuliwa.

Binafsi ni muumini wa haki sawa na sijawahi pata shida yoyote kwwnye familia yangu.
 
Unajua kuna maeneo hadi leo mwanamke ruhusiwi kusoma na anaozwa akiwa na miaka 6 kwa lizee la miaka 50?
Mwanamke ana haki ya kusoma, kwani tunahitaji matabibu wanawake na mfano wa hayo. Shida baada ya kusoma hufata nini na hali huwaje ? Yaani baada ya kujenga huwa mnabomoa.

Muwe mnapata muda wa kuyafikiria haya mambo katika uhalisia wake, tazama fikra za wanawake wote walio soma yaani za kijinga sana. Wamekuwa mishumaa.
 
Ajabu ipo wapi kuwa zaidi ya mwanaume? Kama uwezo anao kumzidi mwanaume kuwa mpole
Hili nishakujibu katika uzi mwingine, nashangaa unarudia rudia kuuliza mambo uliyo jibiwa.

Unajuaje haki fulani dhidi ya mwingine ?

Ipi nafasi ya faida na hasara katika kusimamia au haki ?

Uwezo tu si sababu ya kumfanya mtu afanye jambo fulani endapo kufanyika jambo hili kutaleta hasara kubwa kuliko faida. Namaanisha nini ? Leo hii tunajua uwezo wa kuiba watu wanao, uwezo wa kuzini watu wanao lakini kwanini hatutakiwi tuibe au tuzini ? Sababu mambo haya yana hasara kubwa mno kuliko faida. Hali iko hivyo hivyo Wanawake wenye uwezo wapo,walikuwepo na wataendelea kuwepo bali hata katika Qur'aan wapo wanawake waliobeba dhamiri ya kiume, lakini uwezo wa huo waliutumia katika yale yakiyozidi kuwapa heshima zaidi na katu hawakushindana na wanaume katika majukumu.

Sasa usihoji kitoto na kutumia kivuli cha uwezo wakati hili suala dogo sana na linajulikana tangu zamani, huko tulishatoka miaka na mikaka, tuko katika kuangalia faida na hasara kwa mwanamke, mwanamke, kizazi na jamii kwa ujumla. Ndiyo maana huwa nakuweka katika kundi la watu sio yafikiria mambo kiundani.

Mwanamke alishapewa hadhi na heshima kubwa na Mola wake na hakuna mwanadamu atakaye weza kumpa hadhi na heshima mwanamke kuzidi ile aliyopewa na Mola wake zaidi ya kumshusha na kumfanya bidhaa kama tuonavyo leo hii.
 
Ni kumpa kibri ambacho kitampa ulimbukeni ambao mwisho wa siku atajiona anayaweza yote she is complete kimahusiano kipesa na kijamii hlf moyoni unamuua na stress za upweke na vidonda vya tumbo..

Wadhungu wameshusha thamani wanwake zetu.
 
Mwanamke anakombolewa kutoka mfumo dume na wa kijima uliohodhi karibu kila njia za fursa za kimaisha na kuweka vigingi kwa kwenye njia hizo ambazo mwanamke angezitumia kufikia fursa za elimu, uchumi, uongozi n.k
Angalia haya.
1.Katika jamii nyingi watoto wa kike wanahudhuria shule mara chache zaidi kuliko wenzao wa kiume.Kwa sababu ya hedhi! na kazi nyingine za nyumbani zinawapa muda mdogo wa kusoma na kucheza kama wenzao wa kiume.
2.Watoto wa kike wanakatizwa masomo na wanaume,wakati mwingine walimu, kwa sababu ya kupewa mimba
3.Kuna watoto wa kike wanaozeshwa mapema na familia zao.
4.Wanafunzi wa kike wanaombwa rushwa za ngono vyuoni.
5.Mabinti wanaoomba kazi wanaombwa rushwa za ngono na waajiri.
6.Wanaweka wanapigwa na wanaume zao, wanajeruhiwa
7.Wanaume vibuyu ni rahisi zaidi kuchaguliwa na kuteuliwa katika nafasi za utawala dhidi ya wanawake smart.
9.Wanawake wengine wamefanywa mashine za kuzaa tu za waume zao, na hata hao wanaume wanaishia kuzitelekeza familia zao
10.Wanawake ndio wanatembe maili nyingi kuchota maji, kutafuta kuni, kupeleka watoto clinic/hospitali,...
11.

Kabla ya kuuliza faida ya kuibadilisha hii hali wewe. Jiulize ungejisikiaje kuishi katika jamii inayotoa haki na fursa sawa kwa kila mtu bila kujali dini yake, chama chake, kabila lake au jinsia yake.

Hakuna hasara yoyote ya kumkomboa mwanamke kutoka madhila ya kimfumo anayotwishwa yanayotokana na tamaduni za binadamu.Hili sio suala la feminism, ni suala la haki kwa takribani nusu ya binadamu wenzetu.

Naamini wanawake wanayo 'potential' kubwa ya kuchangia kuondokana na umaskini na udikteta ulioshindwa kuondolewa na wanaume katika bara hili kwa nusu zaidi ya karne sasa.
 
Kwahiyo majibu ya kumtoa katika huu mtihani ndiyo kumfundisha ajilinganishe na sisi ?

Hivi una uelewa wa kuelewa vitu? Ni kwamba hauelewi kabisa au jeuri tu?
Umeng'ang'ana kujilinganisha na sisi kujilinganisha na sisi? Nani amesema anataka kujilinganisha na nyie?

Mnajikuta special sana kwamba wanawake wanataka kuwa kama nyie wakati kila siku mnatoga masikio mnavaa hereni mnajipaka podaa ili mfanane na sisi na lip bulm. Wanaume siku hizi mmekuwa na tabia za kike hata kutuzidi halafu bla bla bla tunataka kujilinganisha na nyie. Kwa lipi?

Nimekuambia kwanzia mwazo kwanini hizi harakati zipo na hamna nilipotaja kujilinganisha na mwanaume.
Kama wewe unawafuatilia slay kwini wa Instagram huko waliojificha nyuma ya kivuli cha uharakati badilika anza kufuatilia watu wa maana , problem solved.
 
Hivi una uelewa wa kuelewa vitu? Ni kwamba hauelewi kabisa au jeuri tu?
Umeng'ang'ana kujilinganisha na sisi kujilinganisha na sisi? Nani amesema anataka kujilinganisha na nyie?
Kujadiliana na watoto wa kike huwa shida sana, na kunataka uvumilivu mno.

Ulichokisema ninakielewa vizuri na ninaweza kukuelekeza pia,ndio maana huwa nakariri kwa kusema haya mnayoyadai ni vivuli tu ila mwisho wa siku msingi wenu ni kufanana na sisi. Sasa wewe ndiyo ulitakiwa au hao viongozi wenu waweke wazi juu ya hili, siyo mnadanganywa kwamba mnataka haki sawa na huku si haki sawa bali kufanana kwa haki. Yaani leo hii mkiona mwanaume ni konda wa dala dala na wewe uwe konda au mfano wake, huu ni mfano wa hitimisho lenu na harakati zenu, yaani wakubwa zenu wanatumia madhaifu na makosa fulani ambayo yanajulikana ili kuwaleta katika ushindani na sisi, hivi hamuwezi kutetea haki zenu bila kutuweka sisi kama marejeo, yaani "mbona wanaume wanafanya kadha? "

Hayo mengine uliyo yaandika yanarejea katika haya niliyo yaandika. Sasa kama hujaelewa hiki nilichokiandika,hiyo tena si kazi yangu, na kwa kukupa faida soma historia ya hizi harakati na ujue sababu ni ipi na ilikuwaje, hizi zikianza karne ya 19 kuja 20 huko umagharibi kisha Ufaransa, Marekani mkaletewa nyinyi huku.

Nisikuchoshe bibie, kazi yangu mimi nimemaliza.
 
Yaan kwa kifupi ni kwamba mwanamke pia alizaliwa kwa kusudi la Mungu na ana ndoto zake za kutimiza maishani, aachwe atomize ndoto zake hata ziwe kubwa vipi asiwekewe vikwazo kama vilivyopo sasa hiv kwenye jamii kwa ujumla
Heshima kwa mume mke anayo tuuu akiwa Hana chochote na zaidi anayo Sana akiwa ana mume anayesupport kutimiza ndoto zake.

Maisha yanakua matamu mnooo. Sio mume akiona mke anauwezo anapambana kumgandamiza kwa madai hatakiwi kuwa na uwezo ohh kisa wewe ni mwanaume, uwezo wa mke hauwi limited na uwezo wa mume.
Nafikiri katika kufundishana hizo harakati mngefundishana na somo la hekima na busara ..Maana bila hivyo mtazidi kubomoa jamii kuliko kuijenga.

Focus imewekwa kwenye competition zaidi kuliko kupinga uonevu.
 
Swadakta, halafu wanatoa mifano ya kawaida sana, suala ls kukeketwa ubaya wake uko wazi, lakini wao ndiyo wanaona hoja, kadhalika shule.

Ukiwabana wanaanza "oooh wewe huelewi mara kadha... "
 
Kujadiliana na watoto wa kike huwa shida sana, na kunataka uvumilivu mno.

Ulichokisema ninakielewa vizuri na ninaweza kukuelekeza pia,ndio maana huwa nakariri kwa kusema haya mnayoyadai ni vivuli tu ila mwisho wa siku msingi wenu ni kufanana na sisi. Sasa wewe ndiyo ulitakiwa au hao viongozi wenu waweke wazi juu ya hili, siyo mnadanganywa kwamba mnataka haki sawa na huku si haki sawa bali kufanana kwa haki. Yaani leo hii mkiona mwanaume ni konda wa dala dala na wewe uwe konda au mfano wake, huu ni mfano wa hitimisho lenu na harakati zenu, yaani wakubwa zenu wanatumia madhaifu na makosa fulani ambayo yanajulikana ili kuwaleta katika ushindani na sisi, hivi hamuwezi kutetea haki zenu bila kutuweka sisi kama marejeo, yaani "mbona wanaume wanafanya kadha? "

Hayo mengine uliyo yaandika yanarejea katika haya niliyo yaandika. Sasa kama hujaelewa hiki nilichokiandika,hiyo tena si kazi yangu, na kwa kukupa faida soma historia ya hizi harakati na ujue sababu ni ipi na ilikuwaje, hizi zikianza karne ya 19 kuja 20 huko umagharibi kisha Ufaransa, Marekani mkaletewa nyinyi huku.

Nisikuchoshe bibie, kazi yangu mimi nimemaliza.
Nyie mnatahiriwa sio?
Mbona sisi tunapinga kukeketwa kama dhumuni letu ni kufanana na nyie?
 
Nani amesema anataka kuwa kama mwanaume?
Huenda wewe una mtazamo tofauti ila kinachoonekana kwenye Campaigns za ukombozi wa mwanamke ni kama revenge plans.

Kwamba kundi la sasa la wanawake wawe empowered ili nao wawe kama wanaume meaning wawe equipped kielimu na kichumi ili wachague either kutii mamlaka ya mume au kupuuza.

Kuna msemo niliona kuna mdada kapost kwenye status yake unasomeka,,,"The more i can pay my own bills the more that i find a man more useless"...
Utaona kwa picha halisi kuwa kadri mwanamke anavyopata mamlaka ndio kadri ambavyo anakua na mentallity ya kumchukulia poa mwanaume..Mtajenga familia gani hapo?
 
Kujadiliana na watoto wa kike huwa shida sana, na kunataka uvumilivu mno.

Ulichokisema ninakielewa vizuri na ninaweza kukuelekeza pia,ndio maana huwa nakariri kwa kusema haya mnayoyadai ni vivuli tu ila mwisho wa siku msingi wenu ni kufanana na sisi. Sasa wewe ndiyo ulitakiwa au hao viongozi wenu waweke wazi juu ya hili, siyo mnadanganywa kwamba mnataka haki sawa na huku si haki sawa bali kufanana kwa haki. Yaani leo hii mkiona mwanaume ni konda wa dala dala na wewe uwe konda au mfano wake, huu ni mfano wa hitimisho lenu na harakati zenu, yaani wakubwa zenu wanatumia madhaifu na makosa fulani ambayo yanajulikana ili kuwaleta katika ushindani na sisi, hivi hamuwezi kutetea haki zenu bila kutuweka sisi kama marejeo, yaani "mbona wanaume wanafanya kadha? "

Hayo mengine uliyo yaandika yanarejea katika haya niliyo yaandika. Sasa kama hujaelewa hiki nilichokiandika,hiyo tena si kazi yangu, na kwa kukupa faida soma historia ya hizi harakati na ujue sababu ni ipi na ilikuwaje, hizi zikianza karne ya 19 kuja 20 huko umagharibi kisha Ufaransa, Marekani mkaletewa nyinyi huku.

Nisikuchoshe bibie, kazi yangu mimi nimemaliza.
Asilimia kadhaa ya waliozaliwa wanaume wamefanya transition kuwa na mwonekano wa kike. Hawa wanaitwa Trans women. Ukikutana nao utadhani wanawake kabisa.

Lakni watu kama nyie mna lalamika ni sisi tunataka kujifananisha na nyie. Haya hamyaoni?
 
Usifananishe jamii za mashwaini wa ulaya na purebreed Afrikanus!
Huo ushenzi umebarikiwa na watu hao hao ambao wanajiita watetezi wa haki za binaadamu. Those guys are Evil!
 
Swadakta, halafu wanatoa mifano ya kawaida sana, suala ls kukeketwa ubaya wake uko wazi, lakini wao ndiyo wanaona hoja, kadhalika shule.

Ukiwabana wanaanza "oooh wewe huelewi mara kadha... "
hiki kitu kilikuwa na negative impact ulaya, wakaona wakilete na Africa ili kuvuruga jamii zetu na utamaduni imara tuliokuwa nao.
 
Huenda wewe una mtazamo tofauti ila kinachoonekana kwenye Campaigns za ukombozi wa mwanamke ni kama revenge plans.

Kwamba kundi la sasa la wanawake wawe empowered ili nao wawe kama wanaume meaning wawe equipped kielimu na kichumi ili wachague either kutii mamlaka ya mume au kupuuza.

Kuna msemo niliona kuna mdada kapost kwenye status yake unasomeka,,,"The more i can pay my own bills the more that i find a man more useless"...
Utaona kwa picha halisi kuwa kadri mwanamke anavyopata mamlaka ndio kadri ambavyo anakua na mentallity ya kumchukulia poa mwanaume..Mtajenga familia gani hapo?
Jambo lolote linaanzaga vizuri lakini hawakosekani watu wa kulitumia kwa maslahi yao.
Sasa kama nyie mnajikita kuangalia hao watu wanayoyatumia kwa maslahi yao na hamuoni wale wengine hilo ni tatizo la nani?
Kwa hiyo kitu kifutwe kwa sababu baadhi ya watu wanaenda kinyume na muongozo wa hizo harakati?
Chagueni watu sahihi wa kuwafuatilia. Wanufaikaji wa hizi harakati wengi hata smartphone hawana.
 
Lengo laweza kuwa jema kwa walioanzisha. Lakini kuna wabinafsi flani wa kike wanatumia kama kichaka. Nikitegemea hizi harakati zisimbae huko vijijini ndani ndani ambako hata boda boda kupita ni shida. Ila kwa uvivu wao wanazifanya huku mijini hata wale wasiokuwa hata na redio ambao ndio walengwa haziwafikii.
 
Usifananishe jamii za mashwaini wa ulaya na purebreed Afrikanus!
Huo ushenzi umebarikiwa na watu hao hao ambao wanajiita watetezi wa haki za binaadamu. Those guys are Evil!
Ha ha ha ha ha ha ha.
Haki za binadamu na wanaume wanataka haki ya kuwa kama wanawake[emoji23][emoji23]. Halafu mnatusingizia sisi tunataka kuwa kama nyie.
 
Wanaume gani hao? Maana hapa bongo sijawaona bado!
 
Lengo laweza kuwa jema kwa walioanzisha. Lakini kuna wabinafsi flani wa kike wanatumia kama kichaka. Nikitegemea hizi harakati zisimbae huko vijijini ndani ndani ambako hata boda boda kupita ni shida. Ila kwa uvivu wao wanazifanya huku mijini hata wale wasiokuwa hata na redio ambao ndio walengwa haziwafikii.
Upo sahihi kabisa.

Ila hizi kampeni zinafanyika vijijini sema haionekani kwa sababu hawana smartphone wa post.

Kijijini kwetu hizi semina zilikuwa zinafika sana, hata nakumbuka kipindi nipo primary walikuwa wanakuja hadi shuleni wasichana wote tunaitwa tunafundishwa mambo kuhusu kukataa kufanyiwa vitendo vibaya kama kukeketwa, kubakwa na kukaa kimya(maana mabinti wengine wanabakwa hadi na baba zao na hawajui kama ni vibaya kufanyiwa hivyo), ukifanyiwa kitendo kama hicho inabidi useme nk.

Kwahiyo zinafanyika ni vile hazifanywi na watu maarufu ambao watakuja kupost kwenye pages zao za instagram watu waone. Ila zinafanyika sana na kwa asilimia kubwa wamefanikiwa.
 
Back
Top Bottom